Single mums and dads come this way

Single mums and dads come this way

it was a well thought decision which has worked out for the best of everyone

Huo wako unaweza kuwa udikteta , unawezaje kuamua jambo la watu watatu mwenyewe na ukadhani ni best for everyone?
Mm nahisi its best for yourself zaidi.
All in all nakutakia kila la kheri.
 
aisee kwenye hii thread nimejifunza mengi mods hebu iwekeni iwe sticky
 
Dah, kama ukilelewa na single mother unakuwa na matusi namna hii basi kuna tatizo fulani katika malezi. Nimeona single mothers wengi humu ni wajasiri na mashujaa wana determination kuwalea watoto wao vizuri, nashauri wawalee watoto wao wasiwe na hii tabia ya kutoa matusi na kujifanya kijogoo. Mwisho wa siku naona pia kuna character ya kutaka kulipa kisasi au kufidia yale mapungufu ya malezi kwa kujitengenezea mazingira kuwa wewe ni bora zaidi,,, na kuwa kulelewa na single parents ni bora kuliko otherwise,, kitu ambacho kila mtu angependa mtoto alelewe na wazazi wote iwe ndio standard practice.

Hakuna sehemu kafundishwa matusi,tena kilaza kamsifu mamaake kwa kumlea kwenye maadili,kuna watu humu wamelelewa na wazazi wawili lakini wana matusi ajabu,kilaza katukana hapo kwanza?!hayo ni majina tu kayatoa kwa mtu asiyejali familia yake hasa watoto,mi nasema mwanaume kama huyo ni Fisi Maji.Alaa!
 
Miss Kim, usiwe na wasiwasi kuhusu mtoto kumfahamu baba yake;
Kuna umri utafika atamtafuta baba yake tena hata bila ya wewe kujuwa;
Jitahidi tu usiumie sana kutokana na yale baba yake aliyokutendea;
Pia usimfeed mtoto lolote baya kuhusu dad wake, nakuhakikishia siku moja watakutana tuuu.
 
Last edited by a moderator:
Miss Kim, usiwe na wasiwasi kuhusu mtoto kumfahamu baba yake;
Kuna umri utafika atamtafuta baba yake tena hata bila ya wewe kujuwa;
Jitahidi tu usiumie sana kutokana na yale baba yake aliyokutendea;
Pia usimfeed mtoto lolote baya kuhusu dad wake, nakuhakikishia siku moja watakutana tuuu.

Miss Kim, how will you feel?
...nimependa courage yako na maelezo yako ya uhakika from the moment I read your story..!!
 
Last edited by a moderator:
Hakuna sehemu kafundishwa matusi,tena kilaza kamsifu mamaake kwa kumlea kwenye maadili,kuna watu humu wamelelewa na wazazi wawili lakini wana matusi ajabu,kilaza katukana hapo kwanza?!hayo ni majina tu kayatoa kwa mtu asiyejali familia yake hasa watoto,mi nasema mwanaume kama huyo ni Fisi Maji.Alaa!

Ahasnte sana
 
ti

hahahaaaaaaaaaaaa!!!
umepaniki bro!!
calm down!!!
Una-enjoy eeh? Basi kama vipi hao watoto wangu uwalee vizuri, ila nikija tena najua utanipa halafu utakuja humu kulialia au ukishajaa kwa mara nyingine au sio?
 
Kongosho amesema anayotaka kusema na mimi nimesema ninayotaka kusema sasa kama ww umeamua kuwa mshenga wake thats your business...And point of correction I AM AN OPENMINDED PERSON na nina uhuru wa kusema nikitakacho!kuna watu wengi tu wametoa udhaifu wa Miss Kim ukiachia mbali huyo mshenga wako na kwa busara sana tu!
Wewe unajua maana ya mshenga kweli? And by the way just so you know, you are a very CLOSED MINDED PERSON. For one those type of people need not and in fact do not have to pronounce themselves as such. But you wouldn't understand this stuff coz it is way above your level of the so called "open mindedness"!!!
 
Asante Mamndenyi for your concerns but i should make it very clear that i am not worried about my son finding out about his dad na pia mm na mzazi mwenzangu never had a bad ending, tulipendana sana na bado nampenda sana ila kuna mambo ambayo siwezi kuweka bayana hapa ambayo yalipelekea kufikia maamuzi magumu kama hayo.

When the right time comes mm na mwanangu tutakaa chini na kuelezana yaliyomo but as the wise men says "I will only cross the bring when i get to it," so hadi mda ufike i am happy with the way things are.

Miss Kim, usiwe na wasiwasi kuhusu mtoto kumfahamu baba yake;
Kuna umri utafika atamtafuta baba yake tena hata bila ya wewe kujuwa;
Jitahidi tu usiumie sana kutokana na yale baba yake aliyokutendea;
Pia usimfeed mtoto lolote baya kuhusu dad wake, nakuhakikishia siku moja watakutana tuuu.
 
Ok, fine,
Kila la kheri mwaya.
Asante Mamndenyi for your concerns but i should make it very clear that i am not worried about my son finding out about his dad na pia mm na mzazi mwenzangu never had a bad ending, tulipendana sana na bado nampenda sana ila kuna mambo ambayo siwezi kuweka bayana hapa ambayo yalipelekea kufikia maamuzi magumu kama hayo.

When the right time comes mm na mwanangu tutakaa chini na kuelezana yaliyomo but as the wise men says "I will only cross the bring when i get to it," so hadi mda ufike i am happy with the way things are.
 
I am not worried at all! Kuna mambo mtu huwezi kuyaweka hadharani. I have never and will never poison my son against his own father.

Miss Kim, how will you feel?
...nimependa courage yako na maelezo yako ya uhakika from the moment I read your story..!!
 
I am not worried at all! Kuna mambo mtu huwezi kuyaweka hadharani. I have never and will never poison my son against his own father.

Yeah..i understand your point. All the best katika malezi ya big boy..! I've admired you..lol...sio dhambi lakini..teeeeh!
 
Ka swali tu, hivi inawezekana ukamchukia baba wa mtoto na ukawa na mapenzi ya dhati kwa mwanao?

Ukimuona mwanao si unapata reflection ya baba yake? Sasa hakuwagi na regreat kweli, like bila huyu$+p@@ nisingeuwa na huyu mtoto!

Mtoto akileta maudhi kidogo si ndio yale ya m.ji.nga ka baba yako...unachezea chakula ni baba yako kaleta hiki? Baba yako anajua hata bei ya hiyo daftari uliyopoteza..e.t.c

Mtoto kama huyo anakuwa na peace of mind kweli? Atamchukulia vip baba yake?....ila uzuri wa JF "hakuna" wazazi wa hivyo hapa wote wako "perfect" kwenye malazi but in reality hayo ndio yanayotokea huku mtaani! Mara nyingine naonaga JF kama ni "dunia" nyingine hivi....

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Kwa kweli moyoni mwangu huwa nahuzuni sana i wish baba yangu na mama yangu wangeishi pamoja hata kama ni masikini kiasi gani. nimekuwa na baba wa kambo 2 maishani mwangu moja aliza wadogo zangu wawili huyu moja wa ukubwani nilie ishi naye amezaa mdogo wangu anayenifata hakika hamna raha hata kidogo kuongea naye hata nilipo kuwa naishi nyumba 1 ni shida salamu mpaka kesho tena salaamu.
Madhara ni makubwa kwa mtoto kwanza kutomjua baba yako hasa ukiwa mkubwa unaona ni kama una upungufu fulani hivi ni bora umjue afu uwe unajua sababu ya kutoishi naye.
Pili ukoo wa mtoto unakuwa mfinyu mfano mimi ninajua ndugu wa upande wa mama yangu tu simjui shangazi,ba mkubwa au ba mdogo na wengineo upande wa baba ukihitaji msaada wowote kama upande wa mama hawawezi basi ndo imisha toka.
Tatu,najua si vizuri kumchukulia mama yangu kama case study ila naomba nifanye hivyo labda itasaidia baadhi yenu kuwa na watoto na kila mtoto ana baba yake si vizuri hata kidogo nina waombeni kwa hilo ni mbaya kwa watoto tena sana.utawatesa wanao hata kama utawapatia kila kitu mfano una wtt wa 3 kila mtto na baba yake akaishi na baba wa mtt A hakika hawa 2 au 1 hata kuwa na raha /upendo kamili.asanteni Hope mtajifunza kitu ni story ambayo sijawahi kumwambia mtu yoyote maishani mwangu lakini nashangaa leo nimeweza isema kwa watu wengi ni moyo wangu ulijisikia kuandika tu ili wngne nao wajifunze.nina amini kuna wengi kama mimi na kuna wengi wenye kesi kama za kim na wengine humu humu lakini hawajaweza fanya hivi kuna ugumu wake katika hili.

duu! umeongea saaana kwa uchungu. Sasa kama mamako alikuficha kuhusu babako na ulivyomkomalia akakwambia na wewe mwenyewe ukachukua hatua kumfata babako akakutolea nje huoni kama mama yako alikuwa na sababu ya kutokwambia toka mwanzo? Unajuaje kama baba yako alimwambia amkome tangu ukiwa tumboni na ndo maana ulivyomkabili akakutimua? unajitwisha mzigo wa kujionea huruma bure tu eti huna mashangazi sijui ndugu zako ni wachache. Hebu kamuulize prof masalakulangwa pale hubert kairuki anaishije maana yeye aliokotwa akakulia mission - hakuna cha baba, mama wala shangazi. Sijawahi kumhoji lakini huwa nahisi anashukuru kwa yote maana asingetupwa uprofesa wake na baraka zingine alizopewa angezisikia redioni tu. Na sisi wengine tungeikosa huduma yake. Nimesikikitka hata ulivyosema unahangaika upate hela labda babako atakukubali. We kaka wewe! hebu acha kujinyanyapaa bwana. Wasamehe hao wazazi wako, tafuta hela ikusaidie wewe na familia yako. Huna upungufu wowote. Watu tumekulia mazingira kama hayo hayo na tumetoka huko tukiwa washindi. Huku nje ya jf tuna-inspire watu wanaona kuna tumaini kwenye maisha. Haijalishi umetokea wapi. Cha msingi uko hapo ulipo, amua kuishi kwa furaha au kwenye kifungo cha vitimbi vya wazazi. Usijidanganye kuwa ungejikuta ndoani hali ingekuwa tofauti. Kuna wenzio wana baba na mama tena wenye uwezo lakini wameharibikiwa kabisa. Sasa kama mamako aligoma kukwambia kuhusu babako na ulivyomjua babako ukaambulia kutimuliwa, hawa watu wangeoana ungekuwa mtoto wa aina gani? Kawaulize watoto/watu wazima walioishi kwenye paa lenye ndoa aina ya kosovo! Usipoteze muda kwenye kuota maisha uliyotaka yawe. Maisha yashakuleta mpaka hapo chukua hatua kuyaboresha.

Halafu ushauri kuwa wamama/wababa wasizae mtoto zaidi ya mmoja na watu tofauti ni mzuri lakini uzoefu wa aina yako haufanani dunia nzima. Kuna mama namjua ana watoto watatu kila mmoja na babake lakini wanae wanapendana sana na wa kwanza ameshaanza maisha yake ya ndoa, wengine bado wanasoma. Kwa hiyo uzoefu wako si wa wengine.

Halafu naamini kina mama huwa na sababu nzuri tu za kutowaambia watoto kuhusu baba zao mpaka wakati wanapoona mtoto amefikia uwezo wa kuujua ukweli hasa kama ni mzito. Sasa imaggine mamako angekwambia ukiwa mdogo kuwa baba yako alikukataa, si ungeathirika sana? Hapo umemfata babako ukiwa mtu mzima umeishia kulia na kuazimia kutafuta hela ili akukubali. Maadam babako ameshajua kuwa hata we umefata, we muache, endelea na mambo yako. Kwani waliofiwa na baba zao wakiwa tumboni wanaishije? Kwa nini wewe unalikuza sana hili jambo?

Kuna wamama wengine ukiwauliza kuhusu baba unawaumiza tu. Huu mfano ninautoa hapa ni wa kweli, ni wa mtu wa karibu kwangu. Huyu alipewa mimba na baba yake mzazi akiwa na miaka 14. Enzi za zamani na sasa kwa wachache mama akavumilia, mtoto akazaliwa mama akamchukua akamlea kama mtoto wake wa mwisho. Yule mtoto aliyenajisiwa na baba akaondolewa pale nyumbani akaenda kuishi mkoani na ndugu. Yule mtoto aliyezaliwa akawa anamwita mama yake dada, na bibi yake sijui mama mkubwa akawa anamwita mama. Baba tu ndo alipatia. Miaka ikaenda, kwa kuwa lile jambo kimila lilikuwa ni laana, tambiko lilifanyika kwa hiyo kuna wajumbe wa tambiko walishindwa kutunza siri. Kwa hiyo binti akiwa kwenye miaka ya 20 akapata nyuuz kuwa yule mamake si mamake, ila hawakumwambia mama yake ni nani. Mtoto akaenda kuanzisha timbwili nyumbani. Mama wa watu kaishia kupoteza tu fahamu na kulazwa. Ikabidi siri iwekwe hadharani ila wakamsihi binti akienda kwa mama yake mzazi aendelee tu kumwita dada maana ile siri hata mume wa dada yake haijui (wakati huo yule dada-mama alikuwa ameshakaa kwenye zaidi ya miaka 10 na watoto watatu.

Hili jambo lilikuwa zito sana kwa binti. Akaanza kujichukia, akawa kahaba na haikupita miaka mitano akawa ameshaambukizwa VVU akafa. Wakati wa msiba wake ndo shemeji yake ambaye ni babake wa kambo wa kambo anajua ukweli kuwa mkewe alizaa na babake. Ile ndoa mpaka leo ipo inakaribia miaka 30. Nia yangu ni kuonyesha tu kuwa mioyo ya watu ina mengi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom