Single mums and dads come this way

Single mums and dads come this way

daaah! hii thread imefanya nihairishe mpango wangu wa kuwa single mom! tatzo men wenyewe chenga tupu. mnaweza mkawa wote ila mwanamke ndio ukalea mtoto mwanzo mwisho lenyewe lipo tu kimwili.
 
Ni kweli! Badala ya kuyafanyia kazi eti ooh wanawake wengine wabaya wanawajaza maneno watoto! Shame on you hivi mnadhani watoto wajinga si wanaona mambo yanavyokwenda! Una kipato kizuri hutaki kumsidia. akumatambua tu. Ukizeeka au ukaona ana kipao kizuri ndi unamfuata. Akikutolea nje hukawii kuanza oo watoto wa kulelewana na mma wana tabia mbaya Shame on you all mliofanyau mnaotarajiwa kufanya hivy. Be responsible make sure hupati watoto hovyo, kw wanaume hebu jiulize una uwezo waupata watoto wangapi maishani mwako? Chukua tahadhari!
 
Niliwahi kuwa na mate chuoni
Mama na baba yake hawakuoana
Sijui detail zilizosababisha yote hayo
Ila baba yake alikuwa happily married na mwanamke mwingine

Huyu binti hakuwa na connection na baba yake ile ya baba na mtoto
Kibaya sasa (ambacho sijajua kama wamama wote hufanya kwa kujua au bila kujua), binti amefuata nyayo za mama yake

Kwanza mama yake alizaa watoto wengine na wanaume tofauti tofauti
Na akawa anamwambia mtoto wake hataki kumsikia anamwambia swala la nimepata mchumba
Mume wake ni elimu; mama yake huyu alikuwa secretary, hajasoma sana

Nilichogundua ni kuwa alikuwa anataka kurekebisha makosa yake kupitia mwanae...

Huyu binti kwa kuwa tulikuwa close (rum mate chuo) alikuwa ananisimulia huku analaani tabia ya mama yake
Kwani alikuwa na kijana anampenda sana alipompeleka kwao mama yake kamfurumusha naye...

Saa hivi kweli binti kasoma sana tu, lakini ana mtoto mmoja na nyepesi nyepesi ni kuwa amezaa na mfanyakazi mwenzao ambaye ni mume wa mtu...

Mama yake alikuwa very protective na mtoto alikuwa anaona kuwa si sawa na alikuwa hataki kuwa kama mama yake...
Lakini piga ua mama ana nguvu sana...maneno alokuwa anamjaza naona yalimwingia kidogo kidogo...

Na mama yake bado yuko proud na mwanae...nilikutana nae ananambia NK fulani siku hizi ana maisha mazuri sana na ana mtoto wake....roho yake iko tuli maana hakutaka mwanae awe chini ya control ya mwanaume yeyote...

Kuwa single mother kunataka busara sana; ili uwe mama na baba at the same time...
Napenda sana kitabu cha Ben Carson...Gifted Hands...
Pamoja na huyu mama kuwa single mother kwanza alikuwa na hofu ya Mungu
Aliwalea watoto wake kwa maadili ya hali ya juu si kuwa spoil (kwanza hakuwa na hiyo ela ya kuwa spoil)
Alikuwa mkali na aliweka sheria za hali ya juu kwa wanae...

Watoto hawakuwa wanamtania tania kisa ni mama tu

That is why Ben Carson made it ....
 
everthing happens for reasons
uzinzi upo na utaendelea kuwepo
wapo watu wameolewa na wametelekezwa pia
ngoja nkupe mf:mama angu mkubwa alikataliwa na baba wa mtoto 28years ago
miaka 20 iliyopita mamkubwa amefariki mtoto kalelew a na mama zetu wakubwa na mama angu mzazi na mamdogo tu
baba anajiweza na alimkataa mtoto
kasoma kwa shida sana leo ana kazi nzuri sana
miezi3iliyopita mamdogo kamuita yule binti akamwambia babako yupo na anahitaji kuongea na wewe
on the spot!!!akamwambia mamdogo sina baba leo ndo anajua km ana mtoto simtaki simtaki na sina haja nae
kumbe yule mzee hana mtoto mwingine na ni mtu mzima
so ndgu yangu mtu km huyo mzee akiitwa jibwa kuna ubaya
amekaaa miaka yote leo analeta kende zake kutaka mtoto kisa kule kungine hajazaa means angezaa asingemkumbuka
yaani alimfanya reserve
ila sie km ndg tumemwambia the choice is yours kumkubali au kukataa
amesema sina baba na sitaki hata kumuona
Of coz case kama hizi zipo ila pia hujatuambia kwa nini alimkataa. Kwa sababu kukataa mtoto aliyezaliwa na mtu unayemwita mke wangu sio rahisi kama unavyodhani. Tupe mkanda mzima sio hii ya upande mmoja tu.
 
Wadau habari zenu,kwa akina kim na wengineo haijalishi umeumizwa kiasi gani na muzazi mwenzako jitahidi umwambie au kumuonyesha mwanao baba yake maana kwa badaye maumivu atakayo yapata mtoto ni zaidi ya yako x 3.nimetumia neno kuumizwa maana kama hukuwa ktk msuguano hakika ni lazima ungetamani mwanao amjue baba yake labda kama baba alifariki. mtoto akiwa mdogo.pia kutokana na mimi mwenyewe kuwa case study kwa story yangu nitakayo kuja kuitoa hapa nilifanya ka utafiti kidogo kujua kwa nini wazazi wa kike hasa hawa single mumy hawataki kuwambia watoto wao baba zao.niligundua kuwa wengi wa mama hawa alimpenda mtu sana badaye akamtelekeza,kumuacha sababu flani ambayo hakuijua pindi alipokuwa naye(alimdanganya),amegundua kitu ktk familia /ukoo wa mwenza una matatizo fulani au mwenza wake amebadilika na kuwa mtu mwenya tabia ambazo yeye hazipendi.pia kwa kupitia kusoma sehemu mbalimbali niligundua ni rahisi kwa watoto wa kike kukubaliana na sababu za mama kwa kutokuhoji zaidi kuhusu baba yake hivyo wengi huridhika na kuwa na mzazi moja
 
Mwanzoni nilipo anza kusoma post zenu hasa ya kim nilianza kutokwa na machozi.Binafsi hadi sasa nina miaka 25 nimemaliza chuo kikuu sijawahi kumuona baba yangu hata ktk picha ila ninasikia kutoka kwa ndugu zangu kuwa yupo.mama yangu ni mkirya na katika ukoo wake ni watu wakali kupindukia(wenye asira sana) hasa mama yangu ndugu zake wa tumbo 1 na wengine wa ukoo nao huwa wanamuogopa kutokana na asira zake hawapendi kabisa kumwambia jambo hilo kuhusu mimi kujua baba yangu.
Kila mara nikianza kumuuliza huwa tuna korifishana kabisa,zengwe lilianza toka nipo form 1 kwa kuwa nilikuwa bado mdogo sikutilia manani sana,mara nilipo fika form 4 nilidhamiria kwa kweli mpaka nimjue lakini niliishia patupu na kukorofishana sana.nilipo maliza form 6 nikasema sasa nimekuwa na mama atanielewa kwa nini nasisitiza hakika mambo yalikuwa bado magumu ndugu yangu moja alinitosa kisiri lakini naye alikuwa hana uhakika hivyo nilizungumza na mama akanisikiliza kwa umakini sana jibu alilo nipa sita sahau aliniambia aliye beba mimba ni mimi au wao? Nilikosa majibu.
Nina mpenda sana mama yangu ,Nilipo anza chuo kikuu sikuta kabisa kuongelea jambo hilo lakini moyoni iliniuma sana maana yeye ndo alikuwa kila kitu kwangu nilikuwa sina mtu atakaye nisomesha chuo kama atazira maana nilikuwa sina mkopo hata zero% kwa kuwa nilipa dvsn 3 form 6 na sikusoma ualimu na kozi nimechagua ambayo yeye hakutaka kabisa maana kutokana na yeye alitaka nisome ualimu ili nipate mkopo.yeye ni mwl.wa primary kipato chake ni kidogo nikileta haya mambo ata zira kabsa hvyo nikauchuna.
Baada ya kumaliza chuo ngoma ikawa vilevile na visingizio vingi mara unanisumbua ikabidi niache maada hiyo maana huwa sipendi nimkwaze kabisa.mwaka jana kuna ndugu (mtt wa mama yangu mkubwa) akanitonya kuhusu baba yangu.itaendelea
 
Naye sikutaka kumwamini nikawauliza ndugu zangu ambao ni mkubwa wake na wadogo zake mama (wa tumbo mmoja) nao wakaniambia kama ndugu wa kwanza alivyo niambia jina na mahali alipo baba yangu,nilifurahi niliwasiliana nae kwa simu na akakubali ni kweli lakini nilitaka nipate uhakika kutoka kwa mama wala hata sikumuandaa nilimshutukiza siku moja.nilimuingia mama kisoma na kumuomba ni kuwa ni mda sasa aniambie tuliongea badaye akaniambia yupo sehemu flani na akanipa mawasiliano yake hapo hapo baada ya dakika 2 nilimpigia na akakubali cha ajabu yule niliye ambiwa na ndugu na aliye niambia mama ni watu 2 tofauti hakika nili butwa kwa muda,siku iliyo fuata nikamuuliza tena akasema kwani yeye umeongea naye amekuambiaje amekataa au? Nikamwambia hamna ila nikamuuliza vipi fulani ambaye niliwahi kukuuliza akarudia kauli yake walio beba mimba ni mimi au wao.itaendelea
 
Nikapatwa tena na mshangao wa ajabu.Hadi hapa ninapo andika sijawahi kumuona hata moja wao kingine cha ajabu ndugu wanasema nina fanana sana na huyo baba yangu wamjuao wao hata kwa tabia mama nae kwa upande wake ananiuliza kama huwa naongea na baba yangu (anayemsema yeye) kama mara 4 namsikia anasema yani wewe kama baba yako tabia yako ata ukiongea naye! mambo yake kama wewe ,ww mwenyewe si huwa unamsikia?ananiuliza mm namjibu huwa siongei naye ananiuliza kwa nn? Kabla sijatoa sababu anajitetea kwa nini hakuniambia mapema na kuniomba niache hasira.wandugu nina subiri nipate kazi nipate hela nikawatembelee wote wawili niangalie kwa macho yangu na nipime D.N.A nimjue baba yangu ni yupi.nina shauku sana nimuone
 
Kwa kweli moyoni mwangu huwa nahuzuni sana i wish baba yangu na mama yangu wangeishi pamoja hata kama ni masikini kiasi gani. nimekuwa na baba wa kambo 2 maishani mwangu moja aliza wadogo zangu wawili huyu moja wa ukubwani nilie ishi naye amezaa mdogo wangu anayenifata hakika hamna raha hata kidogo kuongea naye hata nilipo kuwa naishi nyumba 1 ni shida salamu mpaka kesho tena salaamu.
Madhara ni makubwa kwa mtoto kwanza kutomjua baba yako hasa ukiwa mkubwa unaona ni kama una upungufu fulani hivi ni bora umjue afu uwe unajua sababu ya kutoishi naye.
Pili ukoo wa mtoto unakuwa mfinyu mfano mimi ninajua ndugu wa upande wa mama yangu tu simjui shangazi,ba mkubwa au ba mdogo na wengineo upande wa baba ukihitaji msaada wowote kama upande wa mama hawawezi basi ndo imisha toka.
Tatu,najua si vizuri kumchukulia mama yangu kama case study ila naomba nifanye hivyo labda itasaidia baadhi yenu kuwa na watoto na kila mtoto ana baba yake si vizuri hata kidogo nina waombeni kwa hilo ni mbaya kwa watoto tena sana.utawatesa wanao hata kama utawapatia kila kitu mfano una wtt wa 3 kila mtto na baba yake akaishi na baba wa mtt A hakika hawa 2 au 1 hata kuwa na raha /upendo kamili.asanteni Hope mtajifunza kitu ni story ambayo sijawahi kumwambia mtu yoyote maishani mwangu lakini nashangaa leo nimeweza isema kwa watu wengi ni moyo wangu ulijisikia kuandika tu ili wngne nao wajifunze.nina amini kuna wengi kama mimi na kuna wengi wenye kesi kama za kim na wengine humu humu lakini hawajaweza fanya hivi kuna ugumu wake katika hili.
 
To be a single is a challenge. I stayed with a man for six good years in a relationship. Fortunately I fell pregnant to him. He told me to abort. Aisee niligoma. Jamaa alikua mbogo na alinitolea maneno mengi sana ya kashfa. Alinitesa sana kipindi cha ujauzito. Kuna wakati usiku nilikua naugua sana but nilikua nahangaika peke yangu usiku kucha yy akiwa kalala pembeni. Kwa neema ya Mungu nilijifungua salama.
Jamaa alinikimbia na kuniacha na mtoto mchanga wa wiki tatu hata arobaini nilikua sijafichikisha. By that time nilikua sina hata kazi masikini ya Mungu. Kula shida,kodi ya nyumba sina. Nakumbuka nilikuja kufukuzwa ninayoishi nikapewa masaa 24 niwe nimehama kama ntakua sijalipa kodi. Nilimweleza mwenzangu akaniambia kopa ukianza kazi utakuja kulipa ila kwa sasa mi sina hela.
Sitasahau jinsi nilivyoumia coz sikuwa na kwa kwenda na mwanamgu. Bahati nzuri kuna rafiki yangu alinikopesha na nilikuja kumlipa baadae nilipopata kazi. Nilimbatiza mwanangu nikiwa sina hata shilingi kumi. Gauni la ubatizo alinunuliwa na rafiki yangu na wasimamizi wa mwanangu ndio walioniandalia chakula. Yy hakutoa hata senti kumi na wala hajui mwanae alivaa nn siku ya kubatizwa.
Ni mengi mno niliyoyapitia lakn kwa neema ya Mungu nimeweza kusimama imara. Binti yangu kwa sasa yuko darasa la pili na nimekua nikimueleza unyama alioufanya baba yake ili atambue kuwa baba ake ni mtu wa aina gani. Sijutii kumweleza ukweli kwan hata akimuuliza baba ake sijali kwan ndiyo aliyoyafanya kwake na kwangu.
Nikimwangalia binti yangu alivyo faraja kwangu huwa nakumbuka mbali sana.
 
so sad.... thats y I promised my self sintakaa nimuache mtoto wangu alelewe na single parent..........by the way huyo kubwa jinga mpotezee tuuu hana msaada wowote sanasana ukijaribu kumtafuta atazidi kukuumiza na kukudharua onyesha kama hana msaada wowote kwenye maisha yako

I speak through experience (nililelewa na mana tuu)huyu kubwa jinga they call him my dad pu.mbavu zake alimuachisha mama masomo mzumbe university (second year) mama akapata kazi benki baadae ikaja sera ya kupunguza watu maofisini mama akapunguzwa lile kubwa jinga likamkimbia and mama had nothing alikuwa ajui aanzie wapi I can't recall asking my lovely mum about that big a.ss ladba nikiwa mdogo sijielewi huyo mwanao akikuwa atazoea tuu na hatakusumbua cha muhimu usionyeshe unamchukia huyo kubwa jinga (mama yangu hajawai kumsema vibaya huyu kiazi) na hata pale alipotaka kuniona hakunizuia

unachotakiwa ni kukubali uhalisia ukiendelea kuukataa utaumia sana na utapoteza muda wako kwenye vitu visivyo na maana yoyote jipange kumlea mwanao kwa nguvu zako zote sometimes we (children) are stubborn lakini usife moyo jitahidi kumpatia mwanao kila kitu asihisi utofauti wowote (my lovely mum gave me everything I needed)

mama hakuniambia ni kwanini huyu pi.mbi alisepa hata hivyo wala sitaki kujua lakini alishawai kuniambia "alikuacha ukiwa na miaka mitano" dada yangu hawa mbuzi hawabadiliki kama mtu alikana kiumbe chake usitegemee ipo siku ata jirekebisha remember I speak through experience huyu big a.s.s alikuja kunitafuta nikiwa 20 years nilimpa golden chance yule mzee a tegeneze makosa yake (wanasema watoto tulioleewa na mama tuu tuna huruma sana)hakuonyesha kujali alishindwa hata kumpokea kijiti my lovely mum kunisomesha na uwezo anao nikambull shit tupa kule nimekuwa na maisha yangu na vijisenti vimeanza kuja kanajipendekeza ipo siku nitamtoa miguu....

good newz ni kuwa watoto walio lelewa na single mum wana bahati sana most of them they achieve very well in life (obama & co hata viongozi wengi wa taifa hili walilelewa na single mom)

.......hope u will get something. .........

Umeongea kwa uchungu kilaza. I feel you. Nna rafiki yangu nimeongea nae juzi. Yy ni binti na baba alimpa ujauzito mama ake akiwa anasomea unesi shule ya masista. Yule mama alifukuzwa shule kwa kosa la kupata mimba. Akarudi kijijini kuzaa then baadae akatafuta shule pengne akasoma. Kalea mwanae peke yake.
Big ass kiazi kama unavyomwita alikuja kumtafuta mwanae baada ya kujua kachaguliwa kwenda kusomea udaktari. Huwez amini yule dada alimfukuza baba yake na hata wakikutana barabarani ni shikamoo marahaba no story. Yule dada kwa sasa ni daktari na kaolewa ana watoto wawili. Mzed hata siku ya harusi hakukaribishwa na analalamika wamemuoza binti yake bila kumshirikisha. Watoto wanaokataliwa huwa Mungu anawainua sana baadae.
 
Umeongea kwa uchungu kilaza. I feel you. Nna rafiki yangu nimeongea nae juzi. Yy ni binti na baba alimpa ujauzito mama ake akiwa anasomea unesi shule ya masista. Yule mama alifukuzwa shule kwa kosa la kupata mimba. Akarudi kijijini kuzaa then baadae akatafuta shule pengne akasoma. Kalea mwanae peke yake.
Big ass kiazi kama unavyomwita alikuja kumtafuta mwanae baada ya kujua kachaguliwa kwenda kusomea udaktari. Huwez amini yule dada alimfukuza baba yake na hata wakikutana barabarani ni shikamoo marahaba no story. Yule dada kwa sasa ni daktari na kaolewa ana watoto wawili. Mzed hata siku ya harusi hakukaribishwa na analalamika wamemuoza binti yake bila kumshirikisha. Watoto wanaokataliwa huwa Mungu anawainua sana baadae.

Pole kwa majaribu ya dunia...

Ila hapo pa kuanza kumwambia mwanao wa darasa la pili mabaya ya baba yake sidhani kama ni jambo jema;

Nikiangalia mwanangu wa darasa la pili alivyo mdogo afu nianze kumsimulia matatizo yangu naona kama siyo fair...

Watoto wana haki ya ku enjoy utoto wao
 
mmh Mungu tusaidie.
Inauma sana sanaaaaaaaa!
Imagine mtoto kunasiku akiamua anakuita Fadher na siku nyingine mother.
Ukifikiria babayake ulivyomwambia uko na ujauzito wake alikuambia toa haraka iwezekanavyo
Uko sahihi ndugu yangu hata mimi ilinitokea hivyo aliniambia nitoe but nilikataa na mapenzi yakaisha tangu mimba mpaka sasa mtoto ana miaka mitano hajui anachokula anachovaa wala matibabu na anajua kama ana mtoto natamani nicngemwambia kama ni mtoto wake hataki hata kumuona nimemuongopea mpaka sasa nimeamua kumwambia ukweli baba yako hakutaki
 
Mke wangu tumeish nae kwa miaka kumi na kupata watoto wawil wa kiume,aliamua kuondoka na watoto wote na kurudi kwao.Baada ya mda mfup alipata kaz na kupanga chumba.Alipopanga ni karibu namm ninapoishi.Watoto wangu walikua wanaishi maisha magumu kwan walikua wanakuja kwangu na kunieleza.Baada ya takriban miez sita niligundua kuwa rafiki yangu wa karibu na kama ndg yangu ndie alie mpangashia chumba,kumtafutia kaz napia anawalisha adi wazaz wa mke wangu.Ilinibidi nikashtaki ofsin icho kitendo il jamaa ahamishwe,cha ajabu familia ya mke wangu na mke wangu wote wakanifungulia kes kuwa nawatishia.Mtoto wangu mkubwa aliekua ananipa siri wakamfukuza.Mpaka sasa naish nae.Napata changamoto nyingi sana kumlea kwan ni mdogo yupo darasa la nne na mimi kaz zinanibana.Akimaliza mtihan wa taifa tampeleka akaish na wazaz wangu.Mwanamke kaniudh na jamaa yangu ameniuzi sana.
 
Emotions zilivyotapakaa kwenye hii post? Anyway sikumaanisha kumuumiza yeyote, bali kuwa objective.

Why do gays come out?And why straight people don't come out?

Kuna some sort ya kutafuta acceptance kwa wale wa kwanza. Na kwa nini watafute acceptance kama wanaona wako normal?

Ulishawahi kuongea na mwanamke aliyebakwa? Anakuwa emotional over small things.

Kama uko okay for real huwezi kuwa emotional kiasi hiki, sababu kuzaa bila mwenza si ulemavu.

Kongosho amesema anayotaka kusema na mimi nimesema ninayotaka kusema sasa kama ww umeamua kuwa mshenga wake thats your business...And point of correction I AM AN OPENMINDED PERSON na nina uhuru wa kusema nikitakacho!kuna watu wengi tu wametoa udhaifu wa Miss Kim ukiachia mbali huyo mshenga wako na kwa busara sana tu!
 
Last edited by a moderator:
Bitterness.

Weakness ya wamama wengi, anahamishia uchungu wa mahusiano yake kwa watoto, bila kujua in the process anamuumiza mtoto wake.

Hivi kuna faida gani ku ruin mahusiano ya baba na mwanae kisa alikuumiza?

Maana ukute mzazi yeye alikuwa na nafasi ya kuhusiana na baba yake, leo yeye anaharibu ya mtoto wake na baba yake.
Pole kwa majaribu ya dunia...

Ila hapo pa kuanza kumwambia mwanao wa darasa la pili mabaya ya baba yake sidhani kama ni jambo jema;

Nikiangalia mwanangu wa darasa la pili alivyo mdogo afu nianze kumsimulia matatizo yangu naona kama siyo fair...

Watoto wana haki ya ku enjoy utoto wao
 
Kwa kweli moyoni mwangu huwa nahuzuni sana i wish baba yangu na mama yangu wangeishi pamoja hata kama ni masikini kiasi gani. nimekuwa na baba wa kambo 2 maishani mwangu moja aliza wadogo zangu wawili huyu moja wa ukubwani nilie ishi naye amezaa mdogo wangu anayenifata hakika hamna raha hata kidogo kuongea naye hata nilipo kuwa naishi nyumba 1 ni shida salamu mpaka kesho tena salaamu.
Madhara ni makubwa kwa mtoto kwanza kutomjua baba yako hasa ukiwa mkubwa unaona ni kama una upungufu fulani hivi ni bora umjue afu uwe unajua sababu ya kutoishi naye.
Pili ukoo wa mtoto unakuwa mfinyu mfano mimi ninajua ndugu wa upande wa mama yangu tu simjui shangazi,ba mkubwa au ba mdogo na wengineo upande wa baba ukihitaji msaada wowote kama upande wa mama hawawezi basi ndo imisha toka.
Tatu,najua si vizuri kumchukulia mama yangu kama case study ila naomba nifanye hivyo labda itasaidia baadhi yenu kuwa na watoto na kila mtoto ana baba yake si vizuri hata kidogo nina waombeni kwa hilo ni mbaya kwa watoto tena sana.utawatesa wanao hata kama utawapatia kila kitu mfano una wtt wa 3 kila mtto na baba yake akaishi na baba wa mtt A hakika hawa 2 au 1 hata kuwa na raha /upendo kamili.asanteni Hope mtajifunza kitu ni story ambayo sijawahi kumwambia mtu yoyote maishani mwangu lakini nashangaa leo nimeweza isema kwa watu wengi ni moyo wangu ulijisikia kuandika tu ili wngne nao wajifunze.nina amini kuna wengi kama mimi na kuna wengi wenye kesi kama za kim na wengine humu humu lakini hawajaweza fanya hivi kuna ugumu wake katika hili.

Econometrician pole sana mdau,
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom