Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
9,296
7,666
Kheri ya pasaka waungwana!

Ningeanza na kusema kwenye kila jambo kuna pande mbili za shillingi.

Katika pitapita zangu nyingi nimegundua kuna uzi nyingi katika jukwaa hili la MMU zinazowakandamiza na kuwaponda single mothers! Mnasahau kama hao walowatia mimba single mothers nao ni single fathers?

Nakubali katika maisha kuna kukosa na kukosoana lakini ningependa tuwekane sawa katika hili, haimaanishi kwasababu BAADHI ya single mothers hawana msimamo na vigeugeu basi wote wapo hivo.

Na kingine kama mtu ni single mum lazima uelewe kuna sababu ilopelekea hilo sidhani kama kuna mtu anaependa kulea mtoto peke yake bila ya sababu ya msingi.

Au ukiachilia mbali hilo kuna baadhi wanaoamua kulea mwenyewe kwasababu the other part is not the right father figure for their child! Naamini si kila anayeweza kumimbisha mtu anapaswa kuwa baba!

Ningependa tuwekane sawa kuwa kuna single mother wa aina nyingi:

1. Kuna wadada wengi wanaoamua kujizalia tu kwasababu hakuna wanaume wanaoeleweka ambao wanakidhi viwango vyao na umri umeshatupa mkono mtu anaona ajizalie tu apate mrithi, wa aina hii naamini wanaweza kujimudu na kuhudumia watoto wao bila msaada wa mtu na ni watu wanaojielewa.

2. Kuna walopewa mimba ambazo wawili hao walikubaliana kuzaa pamoja na wakatengana kwasababu tofauti. Hawa mara nyingi wapo mguu ndani, mguu nje kwasababu kulikuwa na mapenzi na makubaliano kati yao kwahio ni rahisi kukumbushiana

3. Kuna walobeba ujauzito kibahati mbaya na mwanaume hayupo tayari kubeba majukumu. Wanawake wa kundi hili hawatakagi mahusiano na maex zao kiujumla kwasababu wanakuwa wameumizwa vyakutosha na wakishasonga mbele wamesonga.

4. Kuna walojibebesha mimba kwa matumaini ya kuolewa au kupata mwenza wa maisha au mteremko wa maisha(hawa ni wale ambao wanazaa hata na wanaume za watu). Hawa ni kundi jingine ambalo pia ni mguu ndani, mguu nje yaani anytime anarudiwa na kuachwa madhali yake yanamuendea.

But all in all mwishoni mwa siku kuna mwanaume alihusika katika hili kwa njia moja au nyingine. Kama ni kinga wanapaswa kutumia wote kujikinga na ujauzito usotarajiwa sasa ikiwa wewe unaenda kulala na mwanamke ambaye huna future nae bila kinga yoyote(kondom au uzazi wa mpango) unategemea nini hasa?

Tusihukumu single mothers kama wakosaji ni wao tu na wanaume ndo malaika mbona hamwahukumu single fathers? Au mnataka kusema wao ni tofauti kwasababu hawajabeba ujauzito.

Mtoto siku zote ni wamama ndio maana wamama ndio wanapata jukumu la kulea lakini tukipiga tathimini ya wanaume au ambao wamezaa tu ni single fathers naamini imepiku idadi ya wanawake.

Single fathers pia wanaweza kwenda kwa ex zao na kubinjuana so hakuna tofauti ya kusema ni single mothers tu sio Wife material kwasababu mnahofia wataliwa. Then tunaweza kusema Single fathers nao sio Husband material. This goes both ways kwa jinsia zote.

La muhimu ni kujuana vyema huyo single mum/ dad kabla ya kuanzisha mahusiano naye na mahusiano alokuwa nayo na ex wake lakini sio kuhukumiana!

1619867692321.png

 
Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.

8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.

9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.

10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?

11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.

Yohana 8:7-11
 
Splendid...!!!!
Ni mentality za watu tu kuJudge na kuona ni jambo baya kua Single Father.
Kila mtu na mentality yake na ni ngumu kuchange mentality za watu (walio wengi) wanao ona ni jamba baya.

A hero can't exist in vacuum, there's always has to be a majority so that the person can be recognized as a Hero.
So my statement is pinpointed to the fact that "Hakuna singo Maza bila Singo Faza"

Both haa to be criticised for their doings if it has to be.
Tell me about it.A man kan impregnate 5 different women and thats ok. The same man made 5 women single mothers and a single father of 5. But a woman with one child just one is not good enough and is a whore 🙄
 
Single mother aliyezaa na mwanamme wa mtu huku akijua hastahili huruma,kwani kayataka mwenyewe.

Wengine hao tunaweza kuwa onea hurumia,kwani SOMETIMES sisi wanaume tumekuwa waoga wa kubeba majukumu,kazi yetu kubwa ni kuonyesha ubunifu kitandani.Lakini kutunza kile kitokacho na ubunifu wetu tunaogopa.
 
Andameni na wanaume pia kwani hao wanawake walijitia mimba wenyewe??Muwaseme wote sio upande mmoja alaaa!!

Mimba inakaa kwa mwanaume au kwa mwanamke?

Umalaya kwa mwanamke ni sifa mbaya mrejee Rahabu kahaba
Umalaya wa mwanaume ni urijali mrejee mtume Suleiman

Ubakaji anayefungwa ni mwanaume
Lakini mwanamke akibaka hafungwi, hujiulizi tuu?
 
Ukifanya umavi lazima uandamwe, ungapaswa ujiulize mbona wanawake waliojitunza hawaandamwi?
Watu wengi hua tunawaonea huruma watu amabao tunawafahamu tu lakini tunasahau kuwaonea huruma hata wale ambao hatuwafahamu wala hawapo kwenye mazingira yetu lakini baya zaidi hua tunawaonea huruma wale watu ambao wapo kwenye maumivu makali mfano magonjwa, Umaskini, nk tunasahau kuwaonea huruma pia hata wale ambao wana maishha mazuri. Inatakiwa tuwe na upendo kama wa mama zetu, mama zetuu huwaonea huruma watoto wote bila kujali mtoto Fulani ana afya na hali nzuri na huyu ana afya na hali mbya.

Ni kweliii ukifanya vibaya utaandamwa kiroho na kuna njia ya kudhibiti hilo. Lakini kama kafanya kitu kibaya wewe mwanadamu hupaswi kumuandama mwenzio kwa makosa yake. Kumbuka mwanamke kuzaa ni matokeo ya mahusiao baina ya watu wawili.....Wewe unachotakiwa kufanya ni kusamehe nakusahau. Since there's no anyone worthy and perfect before The Almighty

Kulinganisha mwanaume na mwanamke ni dalili ya upumbavu,
Yes You can... Kiroho
We are all the same from the same originality
Baadaye utauliza mbona mwanaume akikojoa hainami si ndio?
That's an assumption...Just doesn't justify your claim because it's the matter of creation.
 
Single mother aliyezaa na mwanamme wa mtu huku akijua hastahili huruma,kwani kayataka mwenyewe.

Wengine hao tunaweza kuwa hurumia,kwani SOMETIMES sisi hizi na sisi wanaume tumekuwa waoga wa kubeba majukumu,kazi yetu kubwa ni kuonyesha ubunifu kitandani.Lakini kutunza kile kitokacho na ubunifu wetu tunaogopa.
Huyo mwanaume hakujua na yeye kama ana mwanamke wake atumie kinga akifanya ufirauni wake?
 
Single Mother awe na hela yeye. Sio aje kwangu maisha mazuri na katoto kake afaidi mali zangu tu. Mm najijua siwezi nikasomesha wanangu shule nzuri alafu mtoto wake nimpeleke kayumba. Shida hivi vitoto vikikua vinakua na dharau vinakuona wewedingi yake wa kambo kama Sen.ge fulani hivi. So wapambane wenyewe Single Mothers
 
Usihalalishe uzinzi kwa wanaume!Uzinzi ni uzinzi tu!!

Uzinzi ni uzinzi ndio lakini madhara ya uzinzi ni tofauti baina ya mwanamke na mwanaume.

Nimekuuliza anayebeba mimba ni nani kati ya me na ke?
Anayezaa kwa uchungu ni me au ke?

Wanawake wanaandamwa kwa sababu wao ndio wanaoathirika zaidi kuliko wanaume.

Wewe ukipata familia ndio utajua ni kwa nini mtoto wa kike anakuwa chini ya uangalizi zaidi kuliko mtoto wa kiume, hata muda wa kurudi nyumbani mtoto wa kike lazima alimitiwe tofauti na dume
 
Watu wengi hua tunawaonea huruma watu amabao tunawafahamu tu lakini tunasahau kuwaonea huruma hata wale ambao hatuwafahamu wala hawapo kwenye mazingira yetu lakini baya zaidi hua tunawaonea huruma wale watu ambao wapo kwenye maumivu makali mfano magonjwa, Umaskini, nk tunasahau kuwaonea huruma pia hata wale ambao wana maishha mazuri. Inatakiwa tuwe na upendo kama wa mama zetu, mama zetuu huwaonea huruma watoto wote bila kujali mtoto Fulani ana afya na hali nzuri na huyu ana afya na hali mbya.

Ni kweliii ukifanya vibaya utaandamwa kiroho na kuna njia ya kudhibiti hilo. Lakini kama kafanya kitu kibaya wewe mwanadamu hupaswi kumuandama mwenzio kwa makosa yake. Kumbuka mwanamke kuzaa ni matokeo ya mahusiao baina ya watu wawili.....Wewe unachotakiwa kufanya ni kusamehe nakusahau. Since there's no anyone worthy and perfect before The Almighty


Yes You can... Kiroho
We are all the same from the same originality

That's an assumption...Just doesn't justify your claim because it's the matter of creation.

Mkuu sisi ndio watenda makosa na sisi sisi ndio watoa hukumu, mambo mengi yanaishia huku huku duniani, usipolipwa na mimi utalipwa na yule.

Kuwasema tutawasema mpaka mwisho wa maisha yetu
 
Huyo mwanaume hakujua na yeye kama ana mwanamke wake atumie kinga akifanya ufirauni wake?
1.Siku zote yule ambaye maafa yata mkuta zaidi ndiye anaye takiwa kuchukua tahadhari, mwisho wa siku anaye umia ni mwanamke,mwanaume anarudi zake kwa mke wake.

2.Alafu kuingilia ndoa ya mtu mwingine unaweza ukasababisha ndoa kuvunjika na ukamfanya mwanamke mwenzako kuwa single mother.

So kwangu mimi masingle mother wanao zaa na waume za watu huku wakijua wana ndoa zao hawa stahili huruma.
 
Mkuu sisi ndio watenda makosa na sisi sisi ndio watoa hukumu, mambo mengi yanaishia huku huku duniani, usipolipwa na mimi utalipwa na yule.

Kuwasema tutawasema mpaka mwisho wa maisha yetu
Ha ha ha what a coincidence.Nyinyi mmekuwa Mungu sasa??Eti watoa hukumu 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom