Simba vs Tiger

Simba vs Tiger

Lazima uelewe kwamba wanyama wanatofautiana tabia zao kulingana na mazingira waliyomo lakini pia kulingana na jinsi walivyo kwa asili yao.

Tiger ni mnyama anayeishi maisha ya upweke. Hivyo, kila anapowinda lazima awe na shabaha ya uhakika ya kukamata windo lake mara moja na kwa ufanisi bila kuchelewa maana hana kampani ya kumpa msaada.

Tabia hiyo ya kuwinda mwenyewe, imemfanya kuwa mnyama mwenye ufanisi na maguvu mengi kama matokeo ya natural evolution.

Ni mnyama ambaye ameundwa kuua na kupambana na adui kwa nguvu na kwa ufanisi uliotukuka. It is a killing machine. Akikushambulia ujue ndani ya dakika mbili ameshakutoa roho.

Simba ni mnyama aliyeundwa kwa mapigano. Ni mnyama anayefurahia bifu, kutawala na kuvamia himaya za wengine. Ni mnyama anayependa ubabe tu na udikteta japo hana ukatili wa kufanya mauaji ya haraka.


Ndio maana tiger na simba wakiwa wanapigana, yule tiger atamvamia simba kwa kasi kwa nia ya kutaka kummaliza kwa kichapo cha fasta fasta, lakini bahati mbaya simba anahimili na kurudisha mapigo bila kuchoka au kusalimu amri.

Tiger akishaona anapigana na adui ambaye hafi kwa urahisi, lazima aondoke maana hajaundwa kwa mapambano. Ameundwa kuua haraka na kujificha kwa sababu ni solitary hunter anahitaji kujilinda dhidi ya majeraha yoyote kwa kadiri inavyowezekana.

Tiger akipata jeraha anakufa njaa mana hana sapoti ya kuwindiwa na wenzake. Ni mnyama aliyeundwa kuua chap chap na kwa tahadhari ya hali ya juu kuepuka kujeruhiwa.

Hivyo anapopigana na simba anatoa dozi nzito kweli kweli za mwanzoni lakini anachoka na kukacha pambano maana simba harudi nyuma hata apigwe vipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asiyekuelewa atakuwa na matatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hello,habari za majukumu wadau,bila shaka mtakuwa mko vyema na mnaendelea kuchukua hatua na tahadhari dhidi ya hili gonjwa dharimu la Covid-19 linalosababishwa na virus hatari wa corona,Mungu awabariki sana!.

Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kuna mjadala mahali fulani nimekutana nao kuhusu mnyama SIMBA na TIGER (Chui milia).

Kiukweli kama mnavyofahamu mijadala mizito mara nyingi huwa ina vuta nkuvute,kulingana na tafiti mbalimbali pamoja na Historia kadha wa kadha!,sasa kuna wengine waliosema ya kwamba SIMBA ni hatari zaidi ya Tiger na kuna wengine waliosema Tiger ni hatari zaidi ya Simba,na huo uhatari wao ni pale wanapokutana wao kwa wao.

Wapo waliosema SIMBA kwa uwezo wa nguvu,uwindaji,mapigano basi akikutana na Tiger atapokea kipondo kikali,lakini pia wapo vilevile waliosema kwamba Tiger kwa uwezo,minguvu,uwindaji na mapigano basi akikutana na Simba atampiga mpaka achakae kabisa,na si kuchakaa tu bali pia kuua kabisa.

Mtazamo wako wewe ni upi hapa,hebu lete facts za uhalisia,kiroho na kimwili pia unaweza kuhusisha!!

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..
Shabiki wa Yanga hapa watafata upepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mimi naona tiger is better

Huyu tiger anauwezo wa kuingia kwenye mto na kumchukua mamba akiwa mle mle kwenye maji jambo ambalo sio rahisi ukizingatia na kwamba nguvu ya mamba ni maji lakini si kwa chui

Halafu hata skills za uwindaji chui yuko vizuri zaidi, kama silaha basi naweza kumfananisha na AK47 wakati simba namfananisha na gobole

Action za chui ni noma hadi ndege anawinda, yani anajiviringa juu huko huko aliko ndege kisha anamdaka kwa mikono kama mtu

Simba dume ndo kabisa hata kuwinda halijui lenyewe kula kulala tu kazi zote limemuachia shemu

Umenichekesha eti anamuachia shem haaa haaa haaaaaaa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sidhani kama uko sahihi huyo unaemsema wewe anaitwa jaguar anapatikana marekani ya kusini huyo unaemuita mamba ni alligator ... tiger kwa asili anapatikana Asia ... na kwa taarifa tu hakuna mnyama anaeweza kufanya huo upumbavu wa kuwinda mamba mtoni ( the strongest bite on earth ) Hakuna mnyama anaeweza kuwinda hawa jamaa nile crocodile au salt crocodile labda alligator they’re more like lizards than mazafaka crocs
Mzee unajua, 100%



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba sio mkubwa kama Tiger

Kiasili Tiger wanapatikana Asia na Ulaya Mashariki ambayo ni Russia na Tiger wakubwa kbsa wanapatikana Siberia
Tofauti na wa india na kadhalika

Kwenye sifa za kuwinda

Simba ndio paka ambao wanawinda kwa ushirikiano tofauti na jamii nyingine ya paka

Kwenye kupiga simba Tiger wa umri mmoja

Kwanini simba atashinda na Tiger atashindwa

Simba anapigana kwa kutumia mguu mmoja wa mbele na kusimama kwa mitatu iliyobaki wakati Tiger yeye anapigana kwa miwili kwa wakati mmoja na miwili ya nyuma anasimamia
Simba kwenye mapigano anamoyo wakupigana mpaka kifo atakama anajua anashindwa lakini Tiger hanauwezo huo wakupigana kwa muda mrefu

Simba dume ana mane nywele za pale shingoni ile nisilaha tosha kwake inamkinga zidi ya Adui wakati Tiger hana hizo

Simba kwa kimkakati anauwezo mkubwa sana wakumpiga Tiger kuliko mikakati ya Tiger kwakuwa Tiger sio mvumilivu kama simba
Ukitaka kujua Roho ngumu ya simba ..Dume moja la simba lipo tayari kupigana na madume manne akijua kbsa hanauwezo ila analinda Heshima yake mpaka umauti unamkuta ,kwa hiyo simba amepewa sifa za ziada ambazo nitofauti na paka wengine

Pia tambua simba anaona usiku mara nane ya binamu kwa usiku

Tambua kuwa simba Dume anapounguruma sauti yake inasikika mile 8

Tambua pia simba nipaka wanaoishi kaya ambapo wapo mashangazi mabibi mama na watoto mabinamu na Baba zao na ni mwiko mwanaume kumpanda Mama au Dada yake tofauti na paka wengine

Pia tambua simba ndio paka pekee ambao wakiamua leo wale mnyama wanayemtaka wanafanya hivyo mfano tembo twiga nk

Simba jike watoto wao wanaruhusiwa kunyonya kwa mama yoyote wakaya yao na mtoto analindwa na kina mama wote atakama sio wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiona una like nyingi ujue umenena,,

Ngoja niendelee kuona mtanange

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishaona battle ya simba vs tiger wakuu sio poa, ilikua hivi wote walikua shimoni sijui waliingia vipi so hakuna aliekua anaweza kutoka yani ulipigwa mkono sio poa ilifikia point tiger alikua hawezi kuamka alikua anapigana kalala chali simba ndo alikua bado yupo active alikua anapigana akiwa bado kasimama ila kajeruhiwa balaa dam zimamwagika. Mwisho wakawa wote wanatazamana. Nilichogundua simba anapumzi kuliko tiger so naweza kusema simba ni habari nyingine anapigana mpaka kufa.
Fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishaona battle ya simba vs tiger wakuu sio poa, ilikua hivi wote walikua shimoni sijui waliingia vipi so hakuna aliekua anaweza kutoka yani ulipigwa mkono sio poa ilifikia point tiger alikua hawezi kuamka alikua anapigana kalala chali simba ndo alikua bado yupo active alikua anapigana akiwa bado kasimama ila kajeruhiwa balaa dam zimamwagika. Mwisho wakawa wote wanatazamana. Nilichogundua simba anapumzi kuliko tiger so naweza kusema simba ni habari nyingine anapigana mpaka kufa.
Mkuu nipe link nikajionee

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom