Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 50,163
- 123,276
Hata hizo asilimia 30 ulizompa simba nikama umem-bust tu.Mkuu, Simba dume na Tiger dume wakipambana Simba ataipata, Tiger ni mnyama anayeishi Solitary kama chui anavyoishi (yaani ni mnyama anayeishi peke yake), ukiwakuta wawili basi watakuwa ni jike na dume na jike amemfuata dume ili "apigwe mashine" baada ya hapo kila mmoja utafuta ustaarabu wake.
Katika kuwinda Tiger huwinda peke yake, Tiger mmoja peke yake anaweza kumuua AUGUR (aina ya nyati waliopo India) hii ni tofauti na Simba ili aue nyati wanatakiwa wawepo sio chini ya simba wawili. Tiger anayo kasi kubwa, nguvu na uzito kuliko simba na anapowinda asilimia kubwa ni lazima apate tofauti na simba akiwinda peke yake, kifupi Tiger ni mpambanaji peke yake (a lone starring) tofauti na Simba ambao kwa tabia huwinda kwa kundi hasa majike, Tiger anaweza kuogelea na anapopigana na mwenzake huweza kusimama kwa kutumia miguu ya nyuma pekee na kutumia miguu ya mbele kama silaha hii ni tofauti na simba ambaye hawezi kusimama kwa miguu ya nyuma pekee, hivyo ukiwapambanisha simba na Tiger, Tiger anayo nafasi kubwa ya kumpiga simba na hasa simba jike kwani yeye hana manyoya ya kumkinga usoni (mane) kama ilivyo kwa Simba-dume.
Hitimisho langu ni hili; ninampa Tiger 70% ya Ushindi dhidi ya 30% ya ushindi wa Simba.
Japo Simba ni "Baba lao" ,🤣
NB:Tahadhari na Corona vaa barakoa😷
Simba kawa overrated sana