Simba vs Tiger

Simba vs Tiger

Huyu ndie Alligator ambaye wana JF wanasema Tiger anaweza akamchukua kutoka majini na kusepa nae.
15070461f026b88be61d362cf6bef628.jpeg
918d6b1e3fcbafbc9fa6824a7e665f2a.jpeg
4ac3aff95fa33f2a11711714bbc2303b.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jidanganye na stori za mtaani eti simba dime hajui kuwinda, siku ukiingia kwenye 18 zake ndo utajuta
Simba dume hajui kuwinda na sio kwamba kwasababu hajui kuwinda basi hajui kujilinda pindi atapoona alama ya hatari mbele yake

Anaweza kumshambulia mtu kama self defense tu katika harakati za kujiokoa yeye na sio kwamba kumshambulia kama ni mpango wake wa kuwinda
 
Kwa mimi naona tiger is better

Huyu tiger anauwezo wa kuingia kwenye mto na kumchukua mamba akiwa mle mle kwenye maji jambo ambalo sio rahisi ukizingatia na kwamba nguvu ya mamba ni maji lakini si kwa chui

Halafu hata skills za uwindaji chui yuko vizuri zaidi, kama silaha basi naweza kumfananisha na AK47 wakati simba namfananisha na gobole

Action za chui ni noma hadi ndege anawinda, yani anajiviringa juu huko huko aliko ndege kisha anamdaka kwa mikono kama mtu

Simba dume ndo kabisa hata kuwinda halijui lenyewe kula kulala tu kazi zote limemuachia shemu
nyie ndo kwenye essay tunasema umeenda op kila kitu hahahah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba sio mkubwa kama Tiger

Kiasili Tiger wanapatikana Asia na Ulaya Mashariki ambayo ni Russia na Tiger wakubwa kbsa wanapatikana Siberia
Tofauti na wa india na kadhalika

Kwenye sifa za kuwinda

Simba ndio paka ambao wanawinda kwa ushirikiano tofauti na jamii nyingine ya paka

Kwenye kupiga simba Tiger wa umri mmoja

Kwanini simba atashinda na Tiger atashindwa

Simba anapigana kwa kutumia mguu mmoja wa mbele na kusimama kwa mitatu iliyobaki wakati Tiger yeye anapigana kwa miwili kwa wakati mmoja na miwili ya nyuma anasimamia
Simba kwenye mapigano anamoyo wakupigana mpaka kifo atakama anajua anashindwa lakini Tiger hanauwezo huo wakupigana kwa muda mrefu

Simba dume ana mane nywele za pale shingoni ile nisilaha tosha kwake inamkinga zidi ya Adui wakati Tiger hana hizo

Simba kwa kimkakati anauwezo mkubwa sana wakumpiga Tiger kuliko mikakati ya Tiger kwakuwa Tiger sio mvumilivu kama simba
Ukitaka kujua Roho ngumu ya simba ..Dume moja la simba lipo tayari kupigana na madume manne akijua kbsa hanauwezo ila analinda Heshima yake mpaka umauti unamkuta ,kwa hiyo simba amepewa sifa za ziada ambazo nitofauti na paka wengine

Pia tambua simba anaona usiku mara nane ya binamu kwa usiku

Tambua kuwa simba Dume anapounguruma sauti yake inasikika mile 8

Tambua pia simba nipaka wanaoishi kaya ambapo wapo mashangazi mabibi mama na watoto mabinamu na Baba zao na ni mwiko mwanaume kumpanda Mama au Dada yake tofauti na paka wengine

Pia tambua simba ndio paka pekee ambao wakiamua leo wale mnyama wanayemtaka wanafanya hivyo mfano tembo twiga nk

Simba jike watoto wao wanaruhusiwa kunyonya kwa mama yoyote wakaya yao na mtoto analindwa na kina mama wote atakama sio wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante Sana mkuu, hapo kwny kupambana mpaka tone la mwisho NAMKUBALI SANA SIMBA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimependa maelezo haya. Yamechambua vizuri nguvu na udhaifu wa kila mmoja katika aina hizi za paka. Ni kweli Simba hana mzaha linapokuja suala la kupambana. Huwezi ukamtoa nduki kama unavyoweza kufanya kwa Tiger and the like. Utamuua akijilinda huku akitafuta uwezekano wa kukumaliza na wewe

Ila nina swali moja mkuu. Umesema Simba ndio mnyama wa aina ya paka anaewinda kwa pamoja. Je mbwa mwitu hawako kwenye kundi hili maana wao haswaa ndio wawindaji kwa group
Mbwa mwitu sio paka mkuu, we mwenyewe ushasema "mbwa" sa anakuaje paka, mengine Google tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mamba ni tishio kwa wavuvi na wanyama wazembe wazembe kama simba

Unapozungumzia tiger ni mnyama mwingine kabisa mwenye special skills katika mission zake
Huyo tiger hana ishu yoyote ni kubwa jinga, jitu zembe kama nini, japo lina mwili mkubwa!

Huyo tiger mlete mto ruaha asozege pua yake,wala asiingie majini ajilengeshe hata pembeni ya mto aone shughuli yake!..atachapwa mkia mmoja, kwisha habari yake huyo tiger wako unayemsifia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mimi naona tiger is better

Huyu tiger anauwezo wa kuingia kwenye mto na kumchukua mamba akiwa mle mle kwenye maji jambo ambalo sio rahisi ukizingatia na kwamba nguvu ya mamba ni maji lakini si kwa chui

Halafu hata skills za uwindaji chui yuko vizuri zaidi, kama silaha basi naweza kumfananisha na AK47 wakati simba namfananisha na gobole

Action za chui ni noma hadi ndege anawinda, yani anajiviringa juu huko huko aliko ndege kisha anamdaka kwa mikono kama mtu

Simba dume ndo kabisa hata kuwinda halijui lenyewe kula kulala tu kazi zote limemuachia shemu
Mkuu,hapa umechanganya madesa, umezungumzia tiger,leopard na jaguar.
Tiger hawindi kwenye maji, Yule mnyama unaona anawinda kwenye maji na jaguar,Kuna tofauti Kati ya jaguar na leopard, pia yule unaenuona anawindwa anafanana na mamba, sio mamba anaitwa caiman, Kuna tofauti Kati ya croc na caiman.
 
Huyo tiger hana ishu yoyote ni kubwa jinga, jitu zembe kama nini, japo lina mwili mkubwa!

Huyo tiger mlete mto ruaha asozege pua yake,wala asiingie majini ajilengeshe hata pembeni ya mto aone shughuli yake!..atachapwa mkia mmoja, kwisha habari yake huyo tiger wako unayemsifia

Sent using Jamii Forums mobile app
Tiger utamfananisha na huyo simba anayelelewa na demu wake ambaye ni mzee wa kula kulala?

Uhatari wa simba uko midomoni mwa watu kwa namna ambavyo mnamkuza ila kiuhalisia ni useless kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom