Sielewi kwanini mtu aliyechakachua msaada wa serikali na kujimilikisha enzi za Kikwete, akaondolewa leo anateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa

Tupunguze sana ' Nongwa ' zetu ambazo nahisi zingine ni ama zinasababishwa tu na Wivu wetu kama ' Waswahili ' au huwa hatupendi kutafuta Ukweli wa Jambo husika.

Kwa Mfano leo tuko hapa tunapiga hii ' Nongwa ' kumhusu Batilda Buriani ila tukiacha ' Unafiki ' wetu ' Uliotukomaa ' Watanzania ( Waswahili ) ni nani ana Ushahidi kamili ( wa kutosha ) kuhusu hizi ' Shutuma ' ambazo tunazielekeza Kwake kutokana na ' Mihemko ' yetu Sisi wana Mitandao?

Halafu ni nani aliyewadanganyeni Watanzania ( Waswahili ) kuwa ukifanya ' Blunder ' sehemu fulani ndiyo huwezi tena kuwa na ' Ufanisi ' wa Kiutendaji sehemu nyingine? Kwani Mtu akiwa amekosea hawezi ' Kujirudi ' na baadae akawa Mtu mzuri tena hata kuliko waliopo au alivyokuwa huko awali?

Tambueni wengine wana Nyota zao pia.
 
Mkuu walengwa wa hii thread wanaelewa. Unapotaja majina una-risk moderators kuifuta thread yako maana nao hupewa sana shinikizo. Nikitaja majina inabidi nieleze kisa chote, jinsi walivyoomba msaada wa magari kwa niaba ya serikali, wakapewa, kisha wao na watu wa wizara ya Mambo ya Nje wakaamua kujimilikisha. Haikugundulika hadi wahisani walipoongelea huo msaada kwa JK, wakakuta JK anashangaa, msaada upi wa magari mlitupa, mbona haukufika!!!
Nchi yetu inauzwa kwa pesa za kijinga.. Watu mafisadi kama vijana wafungwe na wafanye kazi ngumu.. Kama ni wazee wauliwe na mali zao zote zitaifishwe na majina yao yakashifiwe kiasi kwamba hata watoto wao wawachukie
 
Team JK imerudi kwa kasi, lakini matumaini ni kwamba hao wanaorudishwa hawatarudi na madudu ya awamu ile.

Matumaini ni Rais Samia kuwa na sauti, maana inakuwa haina faida kwa taifa kama wanarudishwa wanamtandao halafu wakarudi na akili zile zile za wakati ule.
Mama wa kazi iendele naomba astaafu 2025 ni utani mtupu
 
Ndiyo maana mnapowaitaga wazungu Ni mabeberu nawaonaga kuwa Ni wapumbavu wakubwa.
Kwani wazungu sio mabeberu na magaidi... Ushamba wa mzungu unakubali nchi yako iuzwe.. Nahisi unatamani uzaliwe mzungu
 
Rostam alipokelewa Ikulu na Magufuli mama akiwa makamu.
Kumuweka kibaraka wa Rostam , wewe unamjua Rostam Azizi wewe, unamjua vyema JK! Acha kuongea mambo ya vijiweni! Unaijua Boys to Men! Acha tu, mama amebanwa mbavu
 
Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
Defence ikizidi tutaanza mgeuka hata tunaomsupport.
Aachwe kivipi? Challenge ni lazima.
Mlisema jiwe aachwe - yaliyotokea wote tunayajua. Hii kuachwa,,, hapana,, akitoka kwenye mstari lazima akumbushwe. La sivyo tutatengeneza dikteta mwingine soon.
 
Kulikua na ulazima wa kutuletea MTU kama Batilda Buriani kweli??

Au mkuu wa mkoa wa Dar??

Hii recycling ya viongozi wale wale Kila awamu mpaka lini

Watuweke wazi tu kuwa kuna Tabaka la watawala na watawaliwa.
Kabisa mkuu.... Hakukuwa na sababu ya kuturudishia hawa watu... Kwa teuzi hizi mi mwenyewe nilishangaa sana...
 
Pamoja na kuhoji kutokutaja jina la mhusika, sehemu pana ya mada iliyowasilishwa ina mantiki sana.

Hawa wateuwaji, hivi wanakosa watu wa kuwateuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi, kiasi kwamba watu wale wale, tena walio na rekodi mbaya katika utumishi wao ndio waendelee kuteuliwa?

Tatizo kubwa tulilonalo ni hilo la watu kutuhumiwa, halafu uchunguzi haufanyiki kuhusu wanayotuhumiwa juu yake; wanapumzishwa au wanapangiwa kwingine. Hili ndilo tatizo la msingi. Kwa nini iendelee kuwa hivi?
Ni kama tunajidanganya kuwa nchi hii ni yetu (watanzania) wote. Ukiangalia kwa kina utaona sisi wengine (achana na wanaostahili teuzi na kuhamahama nafasi) ni kama wahamiaji ila tu hatuitwi haramu. Hatustahili kupata nafasi yoyote ya kimaamuzi zaidi ya kupangiwa utaratibu wa maisha na tabaka lilelile la miaka na miaka. Keki ya Taifa si ya wote, ni sisi tu ndio tunaoambiwa kuwa tujiulize tumeifanyia nini nchi yetu, sasa hili swali linastahili kusomwa kimasikitiko, hivi tumeifanyia nini nchi yetu mpaka tunapuuzwa hivi?
 
Umesema kweli na mifano iko mingi, si ya kutafuta wala kutajiwa. Wanasiasa wa kitanzania wote wanaunganishwa na kitu kimoja: maslahi binafsi. Haya mengine ya kusema sijui kutumikia wananchi ni bla bla tu. Ni sahihi kusema kabisa kuwa ni kama kikundi cha matapeli au wahalifu. Hawatupani.
Hakika kabisa. Juzi nlicheka sana wakati hotuba ya bajeti ikisomwa. Zilipokuwa zinatajwa posho za madiwani kuliibuka shangwe hadi spika akawa anashadadia waziri kurudia hiyo statement.
 
Hivi sisi waswahili tuna tatizo gani lakini? kwa nini tunaona kwamba kuna watu fulani wanastahili kupewa fursa za uongozi hata wafanye madhambi ya ajabu kiasi gani? Ina maana hapa nchini suala la uongozi kuna watu wanaostahili na wengine wasiostahili?

Mtu anafanya makosa makubwa katika nafasi fulani, anaondolewa, anapumzishwa na baada ya muda fulani anateuliwa tena katika nafasi nyingine ya uongozi. Au utakuta mtu anaharibu sana katika sehemu moja, badala ya kuwajibishwa anahamishiwa sehemu nyingine.

Imekuwa kawaida sasa kusikia Raisi, au Waziri Mkuu au Waziri wakisema kwamba mtu fulani ameharibu sana hapa. Arudishwe wizarani akapangiwe kazi nyingine. Au Raisi kamtumbua mtu fulani, atapangiwa kazi nyingine. Ina maana apewe nafasi ya kuharibu sehemu nyingine? Hivi ina maana kuna watu ambao wanapewa hati miliki za uongozi? Na wengine hawastahili?

Kwa mfano, watu walilalamika kuhusu tabia za baadhi ya wakuu wa mikoa, kuhusu dharau zao, lugha zao, pamoja na Chalamila, lakini hawakusikilizwa. Kweli ilibidi Raisi Samia asubiri hadi na yeye awe mhanga wa lugha zisizofaa ndio achukue hatua? Kwa nini alipoambiwa hakutaka kusikiliza?

Kuna mkuu wa mkoa mwingine ambae alichakachua msaada wa seikali, Jakaya Kikwete akakasirika na kumwondoa kwenye nafasi yake. Leo Raisi Samia anaamua kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa. Hatuna watu wengine Tanzania wanaoweza kuwa wakuu wa mkoa bali yeye tu?
CCM kumebaki makapi tupu ndo maana Serikalini hata Bungeni utakuta majina yaleyale ya waliopita na waliopo toka mababu hadi wajukuu. Mfano nzuri wa wakati ni Waziri mmoja kuteuliwa mara tatu na Rais mmoja kushika Wizara tatu tofauti ndani ya kipindi kimoja na kuteuliwa tena na Rais mwingine kushika Wizara ya nne. Sifa zilizoshuhudiwa zikitolewa kwa mteuaji kwa dakika 20 ni maandalizi ya yajayo maana kizazi bado kingalipo. Masikini Kibajaji anapitwa tu ingawa ni mjukuu!
 
You are so stupid my beloved friend! I know them pretty well dogo! Kaa kimya. Bahati mbaya hujui nini JK alikuwa akisema 2015 wakati anakaribia kung’atutaka.

Kwa faida yako alikuwa akisema ‘Shafii yenu mbao Aki serikalini mie najiendea msoga, hayanihusu’ na vingapi aliharibu? Ndiyo maana JPM alimbamiza kisawasawa na sasa ni zamu yake ya mwisho kuikwangua Tanzania ila mungu yupo after Samia atatokea wa kusawazisha. Niachie hapo
Hii ndio kawaida mnapokosa hoja. Whenever you see people speculating about others, just know they are small minds. Haihitaji kuambiwa, wewe jua tu kwamba you are a loser!

How can you start discussing people?? You are talking about Batilda na boys to men as if you know them. Discuss idea, stop discussing people as haisaidii. Mama Batilda is now RC Tabora na wewe na kumjadili kwako haitomfanya now asiwe RC. Mheshimiwa Rais kamteua kamuamini na atafanya kazi aliotumwa. Nyinyi endeleeni kuuliza maswali.

Mmekaa kwa wivu na fitna na majungu mnaombea watu mabaya. Eti Mungu yupo, ni lini Mungu alikuwa hayupo?? Halafu mnafanya kama Mungu ni wenu peke yenu. Losers! Mungu ni wa Mama Samia na Madam Batilda pia.

Na just so you know, kazi inaendelea wewe endelea kulalama.
 
Tupunguze sana ' Nongwa ' zetu ambazo nahisi zingine ni ama zinasababishwa tu na Wivu wetu kama ' Waswahili ' au huwa hatupendi kutafuta Ukweli wa Jambo husika.

Kwa Mfano leo tuko hapa tunapiga hii ' Nongwa ' kumhusu Batilda Buriani ila tukiacha ' Unafiki ' wetu ' Uliotukomaa ' Watanzania ( Waswahili ) ni nani ana Ushahidi kamili ( wa kutosha ) kuhusu hizi ' Shutuma ' ambazo tunazielekeza Kwake kutokana na ' Mihemko ' yetu Sisi wana Mitandao?

Halafu ni nani aliyewadanganyeni Watanzania ( Waswahili ) kuwa ukifanya ' Blunder ' sehemu fulani ndiyo huwezi tena kuwa na ' Ufanisi ' wa Kiutendaji sehemu nyingine? Kwani Mtu akiwa amekosea hawezi ' Kujirudi ' na baadae akawa Mtu mzuri tena hata kuliko waliopo au alivyokuwa huko awali?

Tambueni wengine wana Nyota zao pia.
cc stupid kolola
 
Back
Top Bottom