Sielewi kwanini mtu aliyechakachua msaada wa serikali na kujimilikisha enzi za Kikwete, akaondolewa leo anateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,591
2,000
Hivi sisi waswahili tuna tatizo gani lakini? kwa nini tunaona kwamba kuna watu fulani wanastahili kupewa fursa za uongozi hata wafanye madhambi ya ajabu kiasi gani? Ina maana hapa nchini suala la uongozi kuna watu wanaostahili na wengine wasiostahili?

Mtu anafanya makosa makubwa katika nafasi fulani, anaondolewa, anapumzishwa na baada ya muda fulani anateuliwa tena katika nafasi nyingine ya uongozi. Au utakuta mtu anaharibu sana katika sehemu moja, badala ya kuwajibishwa anahamishiwa sehemu nyingine.

Imekuwa kawaida sasa kusikia Raisi, au Waziri Mkuu au Waziri wakisema kwamba mtu fulani ameharibu sana hapa. Arudishwe wizarani akapangiwe kazi nyingine. Au Raisi kamtumbua mtu fulani, atapangiwa kazi nyingine. Ina maana apewe nafasi ya kuharibu sehemu nyingine? Hivi ina maana kuna watu ambao wanapewa hati miliki za uongozi? Na wengine hawastahili?

Kwa mfano, watu walilalamika kuhusu tabia za baadhi ya wakuu wa mikoa, kuhusu dharau zao, lugha zao, pamoja na Chalamila, lakini hawakusikilizwa. Kweli ilibidi Raisi Samia asubiri hadi na yeye awe mhanga wa lugha zisizofaa ndio achukue hatua? Kwa nini alipoambiwa hakutaka kusikiliza?

Kuna mkuu wa mkoa mwingine ambae alichakachua msaada wa seikali, Jakaya Kikwete akakasirika na kumwondoa kwenye nafasi yake. Leo Raisi Samia anaamua kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa. Hatuna watu wengine Tanzania wanaoweza kuwa wakuu wa mkoa bali yeye tu?
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,591
2,000
Taja jina vinginevyo ni majungu yaliyozoeleka.
Mkuu walengwa wa hii thread wanaelewa. Unapotaja majina una-risk moderators kuifuta thread yako maana nao hupewa sana shinikizo. Nikitaja majina inabidi nieleze kisa chote, jinsi walivyoomba msaada wa magari kwa niaba ya serikali, wakapewa, kisha wao na watu wa wizara ya Mambo ya Nje wakaamua kujimilikisha.

Haikugundulika hadi wahisani walipoongelea huo msaada kwa JK, wakakuta JK anashangaa, msaada upi wa magari mlitupa, mbona haukufika!!!
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,591
2,000
Hata bila UROZI Mkuu wote wachafu hawa na wakati mwingine wanatishana kuhusu uchafu wao. Ukifanya hivi uchafu wako wote tunauanika hadharani kisha tuone nani atakayeathirika sana basi mtu ananywea kwa faida yake si kwa faida ya Tanzania na Watanzania.
Hahaha! Nimwagie ugali wangu nikumwagie mboga yako!
 

TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
2,475
2,000
Mkuu walengwa wa hii thread wanaelewa. Unapotaja majina una-risk moderators kuifuta thread yako maana nao hupewa sana shinikizo. Nikitaja majina inabidi nieleze kisa chote, jinsi walivyoomba msaada wa magari kwa niaba ya serikali, wakapewa, kisha wao na watu wa wizara ya mambo ya nje wakaamua kujimilikisha. Haikugundulika hadi wahisana walipoongelea huo msaada kwa JK, wakakuta JK anashangaa, msaada upi wa magari mlitupa, mbona haukufika!!!
Aya ni majungu tu, maana ujamtaja uyo mtu,Kama Ni Sabaya tayari ananyea ndoo.
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,409
2,000
Mkuu walengwa wa hii thread wanaelewa. Unapotaja majina una-risk moderators kuifuta thread yako maana nao hupewa sana shinikizo. Nikitaja majina inabidi nieleze kisa chote, jinsi walivyoomba msaada wa magari kwa niaba ya serikali, wakapewa, kisha wao na watu wa wizara ya mambo ya nje wakaamua kujimilikisha. Haikugundulika hadi wahisana walipoongelea huo msaada kwa JK, wakakuta JK anashangaa, msaada upi wa magari mlitupa, mbona haukufika!!!
Umesema kweli na mifano iko mingi, si ya kutafuta wala kutajiwa. Wanasiasa wa kitanzania wote wanaunganishwa na kitu kimoja: maslahi binafsi. Haya mengine ya kusema sijui kutumikia wananchi ni bla bla tu. Ni sahihi kusema kabisa kuwa ni kama kikundi cha matapeli au wahalifu. Hawatupani.
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,678
2,000
Team JK imerudi kwa kasi, lakini matumaini ni kwamba hao wanaorudishwa hawatarudi na madudu ya awamu ile.

Matumaini ni Rais Samia kuwa na sauti, maana inakuwa haina faida kwa taifa kama wanarudishwa wanamtandao halafu wakarudi na akili zile zile za wakati ule.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,528
2,000
Taja jina vinginevyo ni majungu yaliyozoeleka.
Pamoja na kuhoji kutokutaja jina la mhusika, sehemu pana ya mada iliyowasilishwa ina mantiki sana.

Hawa wateuwaji, hivi wanakosa watu wa kuwateuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi, kiasi kwamba watu wale wale, tena walio na rekodi mbaya katika utumishi wao ndio waendelee kuteuliwa?

Tatizo kubwa tulilonalo ni hilo la watu kutuhumiwa, halafu uchunguzi haufanyiki kuhusu wanayotuhumiwa juu yake; wanapumzishwa au wanapangiwa kwingine. Hili ndilo tatizo la msingi. Kwa nini iendelee kuwa hivi?
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,528
2,000
Team JK imerudi kwa kasi, lakini matumaini ni kwamba hao wanaorudishwa hawatarudi na madudu ya awamu ile.

Matumaini ni Rais Samia kuwa na sauti, maana inakuwa haina faida kwa taifa kama wanarudishwa wanamtandao halafu wakarudi na akili zile zile za wakati ule.
EeeenHeee, imenibidi nicheke mkuu wangu, baada ya kusoma ulichoandika hapa.

Matumaini yako umeyawekeza kwa huyu mama? Hebu tuonyeshe ishara zinazokupa hayo matumaini ili nasi tuyalee matumaini hayo.
 

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
765
1,000
Nadhani hata kazini kwako wanapata tabu sana na wewe. " majungu, majungu, majungu tu na wivu".

Post yako hii imekaa kimajungu
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,528
2,000
yawezekana wengi mnaohoji hii mada ni either mna umri mdogo au mlikuwa kijijini mnalima.
Kwa hiyo kwa upande wako nyakati zimebaki vilevile, hakuna kilichobadilika toka wakati huo wakati huu, kiasi kwamba yaliyovumiliwa wakati ule ndiyo yavumiliwe wakati huu?
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,678
2,000
EeeenHeee, imenibidi nicheke mkuu wangu, baada ya kusoma ulichoandika hapa.

Matumaini yako umeyawekeza kwa huyu mama? Hebu tuonyeshe ishara zinazokupa hayo matumaini ili nasi tuyalee matumaini hayo.
Mama yupo katika kona ngumu. JK kwake ni kiongozi aliyemtoa Unguja na kumleta bara, alimlea kisiasa hivyo asemalo hawezi kulipinga.

Hivyo hao wanaorudishwa sasa hivi ambao ni watu wa JK ambao Mama aliwakuta baada ya kuja bara wanatakiwa kuwa ni uzalendo badala ya kuanza kurudisha wizi maofisini na magenge ya kitapeli yanayosubiri pesa za bure bure za udalali.

Wanaorudishwa kwa mgongo wa JK wanayo kazi ya kuitazama Tanzania ya sasa na kuwa na ubunifu wa kuongeza tija badala ya kufikiria kuwa wamepata chaka la kutajirikia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom