Moja kati ya mambo yaliyowachanganya wengi ni kumuita Mhe Queen Mama wa Taifa, lakini kupitia ADC hasa baada ya chama kujiridhisha na tafiti mbalimbali tuliamini kupitia ushujaa wa Mwanamke katika dhana ya Uongozi kunzia mama alivyohifadhi kiumbe chake miezi 9 tumboni na hatimaye mtoto mpaka malezi.
Hatua iliyofuta baada ya hapo (kutoka kwenye mikono ya mama) ni baadhi yetu kuwa ma Profesa, Daktari, Walimu n.k.
Nikirejea katika hoja yangu ni kuwa kuna baadhi ya Watanzania walidiriki kusema Nchi haiwezi kuongozwa na Mwanamke, ni hivi juzi tumetoka kuwa na kumbukumbu ya Siku ya Mwanamke, kwa macho yetu tumeona ubora wa viongozi Wanawake wakiongoza vitengo muhimu na vikubwa.
Wanawake hao wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wameoesha kuwa wanaweza kuwa viongozi sio tu tukiwa wadogo bali hata kuongoza watu wazima.
Namtaja Queen kwa kuwa namjua na nimemfuatilia, ni mmoja wa viongoni wenye weledi mkubwa, ni msikivu na ndio maana licha ya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa mara kadhaa lakini Queen amebaki, najua hii si kwa bahati mbaya bali kwa kuwa anatenda kazi.
Ushauri wangu ni kuwa Queen hatakiwi kubweteka na kuona tayari amemaliza kazi, kwa uwezo wake ninavyomjua anatakiwa kukaza zaidi ya hapo kwa kuwa namuona mbali.
Achana na sifa za uchapakazi wake na kuwa kama kioo au mfano kwa baadhi ya Viongozi, nikiwa katika Shughuli zangu binafsi nimefika Manyara ambapo kwa sasa yeye ni Mkuu wa Mkoa nimeona na nimesikia kuhusu sifa zake bado ni zilezile ninazozijuwa mimi za Uwajibikaji rafiki wa Maendeleo, dhana hiyo ya utendaji wake inayosukumwa na uwajibikaji imekuwa rafiki wa maendeleo kila aendapo, ukiondowa Manyara Queen amehudumu kama Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Rukwa na sasa Manyara,
Kote huko ametatuwa migogoro ya Wananchi wa ngazi ya chini, angalia jinsi halivyo shughulika na tatizo la maafa yaliyotokana na maporomoko kule Manyara, hakika Queen anastahili tuzo ya kitaifa.
Pamoja na yote Queen anastahili kuitwa RC wa Taifa, anamsaidia ipasavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kutekeleza yale aliyoyakusudia kwa Wananchi wa Tanzania hususani katika nafasi yake ya ukuu wa Mkoa.
Hongera sana RC wa Taifa, Uwajibikaji rafiki wa Maendeleo.
By Ombe Kilonzo mdau wa maendeleo Mwananchi wa kawaida.