Sielewi kwanini mtu aliyechakachua msaada wa serikali na kujimilikisha enzi za Kikwete, akaondolewa leo anateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa

Ukosefu wa demokrasia miaka 5 ya muovu dikteta jiwe haikutoa fursa kwa wanasiasa wapya kuonesha vipaji vyao. Ndiyo maana watu wanaojulikana vipaji vyao ni wale wa enzi ya Kikwete.

Madhara ya kuongozwa na mwendazake ndiyo tunayaona
Bila ya kumtetea huyo 'dikteta', uozo mwingi umeenea ndani ya chama chenyewe, na hata katika jamii nzima sasa.
 
Hivi sisi waswahili tuna tatizo gani lakini? kwa nini tunaona kwamba kuna watu fulani wanastahili kupewa fursa za uongozi hata wafanye madhambi ya ajabu kiasi gani? Ina maana hapa nchini suala la uongozi kuna watu wanaostahili na wengine wasiostahili?

Mtu anafanya makosa makubwa katika nafasi fulani, anaondolewa, anapumzishwa na baada ya muda fulani anateuliwa tena katika nafasi nyingine ya uongozi. Au utakuta mtu anaharibu sana katika sehemu moja, badala ya kuwajibishwa anahamishiwa sehemu nyingine.

Imekuwa kawaida sasa kusikia Raisi, au Waziri Mkuu au Waziri wakisema kwamba mtu fulani ameharibu sana hapa. Arudishwe wizarani akapangiwe kazi nyingine. Au Raisi kamtumbua mtu fulani, atapangiwa kazi nyingine. Ina maana apewe nafasi ya kuharibu sehemu nyingine? Hivi ina maana kuna watu ambao wanapewa hati miliki za uongozi? Na wengine hawastahili?

Kwa mfano, watu walilalamika kuhusu tabia za baadhi ya wakuu wa mikoa, kuhusu dharau zao, lugha zao, pamoja na Chalamila, lakini hawakusikilizwa. Kweli ilibidi Raisi Samia asubiri hadi na yeye awe mhanga wa lugha zisizofaa ndio achukue hatua? Kwa nini alipoambiwa hakutaka kusikiliza?

Kuna mkuu wa mkoa mwingine ambae alichakachua msaada wa seikali, Jakaya Kikwete akakasirika na kumwondoa kwenye nafasi yake. Leo Raisi Samia anaamua kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa. Hatuna watu wengine Tanzania wanaoweza kuwa wakuu wa mkoa bali yeye tu?
Very strange!
 
Bila ya kumtetea huyo 'dikteta', uozo mwingi umeenea ndani ya chama chenyewe, na hata katika jamii nzima sasa.
Acha uongo. Si tunachotaka maendeleo na si maneno, Period! Eti wanasiasa wa Kikwete wapi hao wapiga maneno au. Hebu eleza kipi kikubwa alichokifanya!
 
Nikujibu kwa kifupi mkuu 'Philipo Bukililo'.

Mimi sioni 'strategy' (mkakati) wowote katika teuzi hizi.

Kama ni kumfurahisha Kikwete ndiyo 'strategy', basi hapo nitakuwa nimepoteza dira katika uoni wangu.

Mimi nadhani sasa inaonekana mama anajipigia tu, mradi liende, na siku zisonge.
Yaani kwa kweli hata sielewi tunakoelekea kwa kweli!
 
Kiini cha matatizo yote ya nchi hii kinaeleweka...unafiki na kulindana ambazo ndizo nguzo kuu za chama tawala CCM. Kumtafuta kiongozi msafi ndani ya CCM ni sawa na kutafuta nguo safi ndani ya dampo la taka. CCM wanajuana...kila moja anajua uchafu wa mwenzie na uoga wa kufichuana ndio msingi mkuu wa kulindana.

Usemi wa you scratch my back, and I’ll scratch yours (nikune mgongo na mimi nikukune) ndiyo falsafa kuu katika chama hicho kikongwe na zipo sababu nzito zinazozuia makada fulani kuadhibiwa...wanajua mengi! Kama tukifanya kosa tupeni adhabu ndogo ili nasi tuje tuwape adhabu ndogo makosa yenu yatakapofichuliwa!
Kiongozi msafi tulimpata kwa ni tuliona matendo yake! Sasa tunalala!
 
Acha uongo. Si tunachotaka maendeleo na si maneno, Period! Eti wanasiasa wa Kikwete wapi hao wapiga maneno au. Hebu eleza kipi kikubwa alichokifanya!
Wewe hata kuandika tu vizuri ueleweke ni shida; sasa utaanzia wapi kuelewa kilichoandikwa!
 
Tupunguze sana ' Nongwa ' zetu ambazo nahisi zingine ni ama zinasababishwa tu na Wivu wetu kama ' Waswahili ' au huwa hatupendi kutafuta Ukweli wa Jambo husika.

Kwa Mfano leo tuko hapa tunapiga hii ' Nongwa ' kumhusu Batilda Buriani ila tukiacha ' Unafiki ' wetu ' Uliotukomaa ' Watanzania ( Waswahili ) ni nani ana Ushahidi kamili ( wa kutosha ) kuhusu hizi ' Shutuma ' ambazo tunazielekeza Kwake kutokana na ' Mihemko ' yetu Sisi wana Mitandao?

Halafu ni nani aliyewadanganyeni Watanzania ( Waswahili ) kuwa ukifanya ' Blunder ' sehemu fulani ndiyo huwezi tena kuwa na ' Ufanisi ' wa Kiutendaji sehemu nyingine? Kwani Mtu akiwa amekosea hawezi ' Kujirudi ' na baadae akawa Mtu mzuri tena hata kuliko waliopo au alivyokuwa huko awali?

Tambueni wengine wana Nyota zao pia.
Gentamycine, hii post uliyotoa hapa haifanani na wewe kabisa. Kama unasema kuna nongwa ya Batilda, halafu unauliza ni nani ana ushahidi kamili, unajuaje watu wanaooingelea hawana ushahidi? Yaani mtu akitaja kitu kwenye post lazima aweke ushahidi wote? Na usikimbilie kuwaambia watu wanatoa maoni yao kwa ajili ya wivu na unafiki wakati hujajua wako karibu kiasi gani na watajwa waliohusika. Kwa mfano, mimi naweza kuwa ndani ya wizara inayohusika na watu waliofanya matukio fulani, na ninajua ukweli wote. Sasa kwa kuwa sijafanya photocopy ya huo ukweli na kuupaste hapa mtandaoni usiwe na haraka kusema ninachosema msingi wake ni wivu na unafiki.

Hapa hatuko ku-present document ya mashitaka, bali kupresent context, na anapotajwa mtu inakuwa na namna fulani ya mfano kutokana na matukio halisi ambayo watu walisikia au kusoma kwenye vyombo vya habari. Sasa usisome kila comment humu ndani with the eyes of a lawyer. Huko ni kuwa na expectation kwamba kila mwana JF awe a learned lawyer.

Nimemuuliza mtu mmoja aliyetoa maneno kama yako, kwamba ina maana nikikuandika humu ndani umefanya mchoro fulani ambao uliipiga serikali ukafanikiwa, utakata shauri kwamba mimi ni mtu wa majungu, au nafanya hivyo kwa ajili ya wivu na unafiki? Labda pia na wewe nikuulize swali kama hilo. Je wewe ni aina ya Watanzania ambao nikipewa uwaziri wa ujenzi utaniambia nimeukata sana lakini nikipewa uwaziri wa utamaduni na michezo utaniona sijapata kitu?
 
Ukosefu wa demokrasia miaka 5 ya muovu dikteta jiwe haikutoa fursa kwa wanasiasa wapya kuonesha vipaji vyao. Ndiyo maana watu wanaojulikana vipaji vyao ni wale wa enzi ya Kikwete.

Madhara ya kuongozwa na mwendazake ndiyo tunayaona
Jiwe aliteua watu ambao aliona wakiwa na PhD kama yeye au maprofessor basi wataweza kuwa viongozi wazuri. Alikuwa na mentality ya ajabu sana huyu mtu.
 
Kuna mwingine alikuwa waziri wakati wa JK akavurunda , akapewa ubalozi Japan akavurunda , Jiwe akampa ubalozi Kenya akavurunda , Mama kampa uRAS kwa wiki moja na kumpandisha kuwa mkuu wa mkoa .
Hebu fikiria sasa, mtu kama huyo ana nini cha maana ambacho Watanzania wengine hawana, hadi unaendelea kumng'ang'ania wakati anaharibu?
 
Angalau weka code ya mkoa ili tuweze kuchangia vizuri
Hapana Mkuu, changieni tabia ya viongozi wetu kuteua watu waliofanya makosa au skendo na kuondolewa kisha kurudishwa, sio kuchangia kumsema mtu fulani.
 
Sajo, nimekusoma mkuu.

Haya uliyoandika hapa ndicho kitendawili kikuu cha nchi yetu. Nchi imekuwa ya watawala, sisi wengine tumekuwa wasindikizaji tusiokuwa na sauti yoyote katika mambo yanayotuhusu!

Kwa nini iwe hivyo?

Kwa nini tunakosa uwezo wa kuibadilisha hali hiyo?
Ni kwa sababu tunategemea kupata viongozi wa nchi tuwatakao kwa kupitia sanduku la kura.

Hali hii itabadilika pindi tutakapopata kiongozi asiyetokana na chama cha siasa wala asiyetokana na boksi la kura.
 
Mwanasiasa akikwambia toka nje kuna mvua, usikimbilie kumuazima mwamvuli bali jiongeze uhakikishe kweli kuna mvua!, vinginevyo unapigwa.
 
Ni kwa sababu tunategemea kupata viongozi wa nchi tuwatakao kwa kupitia sanduku la kura.

Hali hii itabadilika pindi tutakapopata kiongozi asiyetokana na chama cha siasa wala asiyetokana na boksi la kura.
Ninaweza kukubaliana nawe nikielewa atapatikana vipi/kwa njia zipi kiongozi huyo.

Lakini pia kuna njia nyingine ambayo sijui kwa nini inawawia vigumu waTanzania kuitumia njia hii rahisi, lakini wanakubali kuendelea tu na ulaghai wanaopewa miaka yote.

Labda niseme tu kwamba, pengine ni kukosa mtu/watu (wachache wanaowaamini kuwaongoza) ili wasimamie mabadiliko wanayoweza kuyafanya waTanzania wenyewe kwa umoja wao.
 
Back
Top Bottom