HUO NI MRADI WA MWAKIPESILE NA MULLA KULA FEDHA YA EPA
Steven wa BOT hawezi hata kushinda uchaguzi wa uenyekiti wa kijiji cha Mwakaleli! Wengi tunamfahamu hapa Mbeya, ni mdebwedo kama Tom Mwang'onda na hafahamiki kiasi hicho hata kama magazeti ya Rostam yataendelea kumwandika kila siku. Tatizo la Mkoa wa Mbeya ni ushamba na ulimbukeni wa watu wa Mbeya.
Watu wa Mbeya hawana aibu, wanatumiwa na watu walio nje ya mkoa kukomoana wao wenyewe! Ujinga huu huwezi kuuona Kilimanjaro au Mwanza, ni ujinga maalum wa watu wa Mbeya! Tom Mwang'onda alichochewa na akina Lowassa kumg'oa Mpesya, akaishia yeye mwenyewe kung'oka meno pamoja na baba yake kumalizia ushushushu wake wote na fedha ya EPA kwenye uchaguzi huo!
Tom Mwang'onda huyo huyo akachochewa na akina Rostam, Lowassa na Makamba kumg'oa Mwandosya kwenye NEC, akaishia tena kung'oka meno mengi zaidi pamoja na kusaidiwa na vyombo vya dola, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wote wa Wilaya, Makamba, watendaji wote wa CCM na baba yake! Sasa, akina Rostam, Lowassa, Makamba na Kingunge wameona Tom hafai, atafutwe mtu mwingine wa kutumwa.
Kama kawaida yake, korokoroni wao Mbeya - Mwakipesile, akamtafuta Steven na anamwandaa ati kupambana na Mwandosya! Mwakipesile si mjinga, anajua kuwa Steven hawezi! Lakini anajua kuwa huo ni mradi wa kula fedha ya EPA! Steven ni mradi wa Mwakipesile na Mulla kutafuna vizuri fedha ya EPA aliyonayo Rostam. Hata mimi nimekaa mkao wa kula kumshabikia Steven ili nipate mgao wangu wa EPA! Hii Bongoland bwana!
Mimi nina taarifa kuwa hata Dk. Mwakyembe katafutiwa mtu wa kupambana naye! Mtu mwenyewe ni dereva wa malori anaitwa Elias Mwanjala! Huo ni mradi mwingine wa Mwakipesile wa kula hela ya EPA. Wabunge wengine machachari Zambi, Dk. Siame na Victor Mwambalaswa ati nao wametafutiwa wagombea.
YOTE HII NI MIRADI YA KINA MWAKIPESILE NA JANGILI MULLA KULA FEDHA YA EPA!
Lazarosmtindi,
Inaelekea unawajua vizuri hao waheshimiwa. Nikuulize swali, je huyo Mwanjala si ndiye aliongoza kampeni za Dr. Mwakyembe mwaka 2005? Ndiye aliyetoa baadhi ya magari yaliyokuwa yanabeba wajumbe kwenda kuwaficha kule Tukuyu kabla ya uchaguzi. Je kumetokea nini leo kawa upande wa Mwakipesile?
Kama nilivyowahi kuandika huko nyuma Dr. Mwakyembe na Mwakipesile wanahusika kwa njia moja ama nyingine na kukwamisha maendeleo ya wilaya Kyela kwa kuendeleza ugomvi wa kisiasa badala ya kuchapa kazi.
Mwaka 2010 hauko mbali na waambieni waache ujinga wao huo vinginevyo wote wawili wajiandae kuwajibika 2010.
Uchaguzi uliisha mwaka 2005 na Mwakipesile wananchi walimkataa, inatakiwa akubali hilo na kusonga mbele. Lakini pia Dr. Mwakyembe hawezi kuchukia anapoona mwana Kyela mwenzake anapewa nafasi. Ni ujinga kushangilia kuona mwana Kyela mwingine anakuwa chini na kula vumbi. Sisi tunaamini ng'ombe akiumia malishoni hujikokota zizini kusaidiwa. Mwakipesile aliumia vibaya mwaka 2005 na ilitakiwa apewe pole na sio kuendeleza vijembe hata baada ya uchaguzi.
Mtu hachagui jirani yake, hivyo hivyo huwezi kuchagua mtu wa kufanya naye kazi. Inatakiwa hawa mafahari wawili wakae pamoja na kuacha kusikia maneno ya watu ambao sio wa Kyela ya kuwachonganisha na kuwagombanisha kwa cost ya Kyela.
Mwakipesile alikuwa na miaka 10 ya kuitumikia Kyela, hakufanya lolote la maana, wana Kyela wanajua hilo. Sio rahisi kwake kurudi wala sio rahisi kwake kuwa Nyerere wa Kyela. Ashukuru nafasi hiyo aliyopewa na kuitumia vizuri kuendeleza mkoa wake. Ni wachache sana ambao wanapewa nafasi za kutumikia mikoa yao. Inatakiwa ashukuru mungu kwa hilo na sio kutumia hicho cheo kupinga viongozi waliochaguliwa na wananchi.
Kyela haiwezi kutumika kama uwanja wa JK na prof. kupambana. Wote wako kwenye baraza la mawaziri na kama wana ugomvi wapambane huko.
Kama Steven anataka kugombea Rungwe, mwache afanye hivyo na ni haki yake, vile vile Mwanjala kama naye anataka kujitosa Kyela mwache afanye hivyo na ni haki yake sawa na raia mwingine yeyote. Ushauri wangu tu ni kwamba waende huko kutokana na dhamira zao na wala sio kutumwa na watu wa mbali. hatutaki Mamluki Kyela.
Kuna umaskini wa kutisha Kyela, badala kuhangaika kuwasaidia hao wananchi, wao kila siku ni kuongelea migogoro tu. Wakati Rungwe wanasonga mbele, Kyela iko pale pale pamoja na resources nyingi na pia kuwa mpakani.
Mnaowachochea hawa mafahari wawili acheni kwa faida ya Kyela. 2010 itafika na mtakuwa na uwezo wa kupiga siasa kadri muwezavyo. Kwasasa tuongelee namna ya kuisogeza wilaya mbele.
Mimi nawajua vizuri sana hawa waheshimiwa wawili, najua uzuri na matatizo yao. Ila kwa faida ya Kyela nitakuwa neutral na sitaki kujiingiza kwenye ugomvi wao.