Siasa za Mbeya 2005-2010

Hivi mkoa gani mwingine ambapo mkuu wa mkoa ni mzaliwa wa mkoa huo?

Mwanakijiji,
Sina hakika kama ni Mbeya tu; lakini kwa ujumla wake, huyu jamaa alipewa U-RC Mbeya kwa kazi maalum, hasa baada ya kujeruhiwa vibaya sana na Mwakyembe kwenye kura za maoni, ndipo mtandao ukampa U-RC ili amshungurikie Mwakyembe kwa upande mmoja na Mwandosya kwa upande mwingine. Na jamaa anawajibika kweli kweli katika katika kumdhibiti Mwakyembe, kwani alishapewa green light na wazee wenyewe. Rejea kamati ya Kinana na matokeo yake pale Mwakyembe alipolalamika kwa JK kwamba Mwakipesile anahujumu juhudi zake.
 
Siyo sahihi kumkataza mzazi kusherekea ujio wa mwanawe aliyeneemesha familia maana hajavunja sheria. Ni kwa sababu hiyo ilikuwa ni halali kwa EL pale Wanamonduli na waliofaidika naye kumpokea. Asha Rose alipopata nafasi UN, serikali ilitayarisha mapokezi makubwa kwa kipindi kifupi na gharama kubwa. Sijui ni kipi Tanzania kama Tanzania inafaidika kuliko mataifa mengine huko UN kwa uwepo wa Migiro, lakini tulikubali kumpa heshima hiyo kwa vile Mtanzania mwenzetu kaukwaa. Iweje leo pawe na vikwazo kwa wanaKyela kumpokea Harrison kwa niaba ya kamati huko kwao tena kwa michango yao binafsi na si pesa kama zile walizotumia mawaziri kupita mikoani wakielezea uzuri wa bajeti.

Ndugu sangu wa Kyela kasaneni, mnatuwakilisha Wanzania wensenu. Mwakyembe na Kamati yake ni wakombozi wetu, Msisahau ibada na sala kwa ajili ya ulinzi juu ya hawa ndugu zetu.

UKIFANYA JEMA UTASIFIWA KWA SHAMGWE NA NDEREMO.
 
Yaani kama Lowassa aliyejiuzulu kwa aibu anaweza kupata mapokezi ya shujaa na Mwakyembe analetewa zengwe tujua politics zinatupeleka pabaya sana.
 
Mwanakijiji,
Sina hakika kama ni Mbeya tu; lakini kwa ujumla wake, huyu jamaa alipewa U-RC Mbeya kwa kazi maalum, hasa baada ya kujeruhiwa vibaya sana na Mwakyembe kwenye kura za maoni, ndipo mtandao ukampa U-RC ili amshungurikie Mwakyembe kwa upande mmoja na Mwandosya kwa upande mwingine. Na jamaa anawajibika kweli kweli katika katika kumdhibiti Mwakyembe, kwani alishapewa green light na wazee wenyewe. Rejea kamati ya Kinana na matokeo yake pale Mwakyembe alipolalamika kwa JK kwamba Mwakipesile anahujumu juhudi zake.
 
Mafuchila,

Hiyo influence ya mtandao kumuweka RC ilitoka kwa Lowassa au JK?

Maana kama ni JK itakuwa contradiction kwa maana Mwakyembe nilifikiri alikuwa karibu sana na JK,au siyo?
 
Mafuchila,Hiyo influence ya mtandao kumuweka RC ilitoka kwa Lowassa au JK?Maana kama ni JK itakuwa contradiction kwa maana Mwakyembe nilifikiri alikuwa karibu sana na JK,au siyo?

Mwakyembe hajawahi kuwa karibu na JK, lakini hajawahi kuwa adui wake. Engine ya mtandao ni EL akifadhiliwa na RA. Yeye EL ndiye mpangaji wa mikakati na mashambulizi kwa wapinzani wa mtandao katika mchakato wa uchaguzi, lakini pia EL ndiye mtoa nishani kwa washirika kulingana na mchango wao.

Hivyo kwa kuwa Mwakyembe hakuunga mkono mtandao adhabu yake ilikuwa ni laana ya mtandao, kwanza kwa kumpa U-RC mpinzani wake, pili kumpa resources Mwakipesile kumdhibiti, tatu ilikuwa ni kumfunga mdomo. Jukumu la kazi hiyo lilifanikiwa mpaka Spika (kwa sababu zake) alipompa arena Mwakyembe kwenye ile kamati, ambayo naye Mwakyembe aliitumia vyema kurudi kwenye game.

Kujibu swali lako, EL ndiye aliyekuwa anajua nani ni nani kwenye mtandao na anastahili mgao gani kutegemea na mchango wake. Mwakyembe hakuwa mmoja wao, hivyo adhabu yake ilishaamuliwa na EL KUNYONGWA (KISIASA) MPAKA AFE.
 
Mwanakijiji,
Sina hakika kama ni Mbeya tu; lakini kwa ujumla wake, huyu jamaa alipewa U-RC Mbeya kwa kazi maalum, hasa baada ya kujeruhiwa vibaya sana na Mwakyembe kwenye kura za maoni, ndipo mtandao ukampa U-RC ili amshungurikie Mwakyembe kwa upande mmoja na Mwandosya kwa upande mwingine. Na jamaa anawajibika kweli kweli katika katika kumdhibiti Mwakyembe, kwani alishapewa green light na wazee wenyewe. Rejea kamati ya Kinana na matokeo yake pale Mwakyembe alipolalamika kwa JK kwamba Mwakipesile anahujumu juhudi zake.

Mafuchila,

Hii case ya Mwakyembe na Mwakipesile kwa mawazo yangu wote wawili wana makosa makubwa sana kwa wana Kyela. Wameruhusu migogoro yao binafsi idumaze shughuli za maendeleo za Kyela.

Mimi nawajua wote wawili kwa karibu na kila mmoja wao ana kosa kwenye hili.

Nafikiri unajua kwamba Mwakyembe alifanya foul kubwa sana kwenye uchaguzi
wa kuteua mgombea wa CCM. Walimzidi speed Mwakipesile kwa kutorosha wajumbe na kwenda kuwalaza Rungwe kabla ya siku ya uchaguzi. Kundi la Mwanyembe waliandaa magari ambayo yaliwafuata wajumbe na kuwaambia wametumwa na Mwakipesile kwenda kuwachukua na kwamba watakaa hotelini mpaka kesho yake ambapo uchaguzi ulikuwa ufanyike. Walivyopakiwa, kituo cha kwanza kikawa kwenye hizo Guest houses huku Rungwe. Mwakipesile alivyogundua akachanganyikiwa. Haijulikani nini kilitokea huko, lakini Mwakyembe akashinda huo uchaguzi.

Pamoja na kwamba mimi nilikuwa nimechoshwa na Mwakipesile na nilikuwa namuunga mkono Mwakyembe, lakini sikufurahia hiyo njia waliyotumia. Ilikuwa ni rushwa na uvunjaji wa sheria wa hali ya juu.

Baada ya uchaguzi Mwakyembe na kundi lake walikuwa wanarusha vijembe vingi mno dhidi ya Mwakipesile kiasi cha yule mzee kukosa raha pale Kyela. Mimi niliwahi kumshauri Mwakyembe akutane na Mwakipesile waongee na kuyamaliza maana ule ulikuwa uchaguzi. Hofu yangu ilikuwa ni Kyela kugeuka kama Zanzibar ya Hamad na Komandoo. Kundi la Mwakyembe walipuuza na kusema amekwisha huyo.

Baada ya muda baraza la mawaziri likatangazwa na Mwakyembe hakuwemo. Kulikuwa na uvumi mkubwa Kyela kuonyesha kwamba Mwakyembe alienda kugombea ubunge kwa kuamini kwamba atapata uwaziri. Watu wa Mwakipesile wakafanya sherehe kushangilia Mwakyembe kutokuwa waziri.

Haikupita muda Mwakipesile akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa. Mwakipesile baada ya kuapishwa tu safari ya kwanza Kyela kwenda kutamba na gari lake la ukuu wa mkoa. Pia akaanza kupinga mipango mbalimbali ya maendeleo ambayo Mwakyembe alikuwa anataka kufanya.

Kama hiyo haitoshi Mwakyembe akaanza kuandika barua kwa PM Lowassa kulalamikia kitendo cha Mwakipesile kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na kwamba hiyo ni dharau kwa wana Kyela. PM akawa anamwonyesha hizo barua Mwakipesile. Kwahiyo ugomvi badala ya kupungua ukawa unaongezeka.

Ukiaangalia maelezo hapo juu utaona wote wawili wana matatizo yao ambayo yanatokana na ubinafsi na hakuna faida kwa Kyela. Mwakipesile inabidi akubali kwamba Mwakyembe kachaguliwa kihalali na wananchi wa Kyela na amsaidie kutimiza majukumu yake. Mwakyembe naye hakuna haja ya kulalamikia mwenzake kupewa cheo. Alitaka sasa mpaka Mwakipesile afe njaa? Kwa wote wawili lazima waweke maslahi ya Kyela mbele kuliko masters wao Dar au chama chao. Vinginevyo wote wawili wataishia kujiangusha machoni mwa wana Kyela.

Kwa uwezo Mwakyembe ana uwezo mkubwa sana na huwezi kumlinganisha na Mwakipesile ila ni too ambitious na hajua kabisa grassroot politics. Wakati huku kitaifa kazi yake inaonekana, kule Kyela hapatikaniki kabisa, sio rahisi kwa wananchi kuonana na mbunge wao. Pia ni msanii, Mwakyembe akikuambia njoo kesho, wewe endelea na safari zako maana hiyo kesho huwezi kumwona.

Kama sasa wanapanga Mwakyembe afike Kyela weekend kwasababu wanajua Mwakipesile weekends zote anakuwa Kyela. Wanataka kumlima vijembe, jambo ambalo sio zuri kabisa. Ilitakiwa Mwakyembe aseme hapana, huo mpango sio mzuri.

Labda sasa ni kumwomba mheshimiwa rais ili amhamishe Mwakipesile kwenda mkoa mwingine. Mimi kama mwana Mbeya ni heshima kuwa na wana Kyela wawili wenye nafasi. Hata siku moja siwezi kuomba Mwakipesile aondolewe kuwa mkuu wa mkoa. Ila kwasababu imeshindikana hao mafahari wawili kukaa pamoja, basi Mwakipesile ahamishiwe mkoa mwingine.

Mwakipesile anaungwa mkono na afisa usalama wa taifa aliyemaliza muda wake, bwana Apson. Pia ana makada wa CCM ambao wanamwunga mkono sana kwasababu yeye kila alichokuwa anapata, alikuwa anagwana nao. Kwa habari ambazo naziamini kwa asilimia kama 90, ni kwamba Mwakipesile hana mpango wa kugombea ubunge tena Kyela. Labda amegundua kwamba hata akigombea atashindwa. Nasema ni tisini kwasababu kwenye siasa lolote linaweza kubadilika. Yeye anasema maadui zake walimtafutia mtu ili amshinde na labda na yeye anamtafuta mtu wa kupambana na Mwakyembe sasa.

Hizo ni za jikoni kabisa kuhusu hawa waheshimiwa wawili.
 
Mafuchila,

Hiyo influence ya mtandao kumuweka RC ilitoka kwa Lowassa au JK?

Maana kama ni JK itakuwa contradiction kwa maana Mwakyembe nilifikiri alikuwa karibu sana na JK,au siyo?

Pundit,

Mwakyembe sio mtu wa JK. Ila JK huwa hasemi tu na wala haonyeshi kirahisi kama anamchukia mtu au la.

Mwakyembe alifanya kosa kama la Msekwa. Alienda kuwambia JK kwamba anataka kuacha bunge la EA ili akagombee Kyela. JK akasema sawa, Mwakyembe akachukulia kama ni green light wakati JK alikuwa na yake.

Ilipofika uwaziri, Mwakyembe akaachwa nje.

Mwakyembe ndiye alikuwa mpiga debe namba moja wa prof. Mwandosya kwahiyo
hakukuwa na uwezekano wa kuwa kitu kimoja na JK.

JK na Lowassa mtu wao kule Mbeya ni Mwakipesile. Pia Mwakipesile ndiye anaungwa mkono na vigogo wengi kutoka mkoa wa Mbeya. Mwakyembe anaungwa mkono na Prof. mwandosya.
 
Hivi ni vitugani ambavyo hawa watu wawili wamevifanya huko kwao kyela ktk kuchochea maendelea ambayo watu wa huko kwao yamewanufaisha japo kidogo.
 
Sasa naanza kupata picha ya Lowasa na Kamati na Spika kumweka Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa kamati .Nina anza sasa ku recall maneno ya Lowasa na madaha makubwa toka kwa Mwakyembe siku ya kusoma report .Hii ngoma tunasema Lowasa kaenda lakini CCM wana kaangana na ndiyo maana leo haya tunawaona kama wanalikuwa wamoja naamini Lowasa na report vyote vingaliweza kumalizika kimya kimya .So again JK is not real for my rich country but tunaitwa watu masikini .Maskini weeeeeeeeeee
 
Pundit,
JK na Lowassa mtu wao kule Mbeya ni Mwakipesile. Pia Mwakipesile ndiye anaungwa mkono na vigogo wengi kutoka mkoa wa Mbeya. Mwakyembe anaungwa mkono na Prof. mwandosya.

Kama ni kweli1 Haya mambo ya wakubwa kuwa na watu wao majimboni ndiyo yanayosababisha wananchi kuhongwa kanga na Tshirts na kisha kutochagua mtu anayewafaa. Ningekuwa Mwakipesile ningekubali kuwa Wanakyela wameamua kubadili mbunge na kama kweli analipenda jimbo lake angeshirikiana kijana Mwakyembe walete maendeleo na siyo hujuma. Kwani aliambiwa yeye ni mbunge wa kudumu?

Kuhusu Mwakyembe kuwania uwaziri, sidhani kama pana mtu anayeweza kuthibitisha hilo.

Kumweleza JK nadhani ilikuwa ktk taratibu za kikazi Mwakyembe hakutoka from nowhere, nadhani nafasi zake za awali zilikuwa zinakidhi haja zake, hili la ubunge nafikiri ni moyo wa utaifa uliomvuta na kama ilivyo kwa wabunge wengi wananchi uwaomba watu wagombee kwa sababu kuona watafanya vema kuliko yule aliyepo.
 
Mkulu Mtanzania,

Saafi sana, dataz nzito hizo na ni streeo tupu, je vipi Mwakyusa nini hatima yake kwenye this whole mess?

FMES,

Huyu mkuu alikuwa anakula huku na huku. Yeye na Mwakipesile walikuwa wanahudhuria vikao vyote vya kumuuza Prof. Mwandosya kwenye urais lakini
huku chini chini walikuwa mtandao.

Kuna watu wanasema Prof. Mwakyusa hakuwa mtandao, nafikiri hawaelewi vizuri politics za Mbeya.

JK aliliingia kundi la Mwandosya mno bila wao kujua. Walipokuja kujua tayari wakawa wamefungwa goli.

Kwa wabunge, nafikiri ni Mwakyembe tu ambaye alikuwa mtu wa prof. Mwandosya kwa asilimia 100.

Huyo prof. Mwakyusa, mwaka 2010 nafikiri atakuwa na kazi ngumu kweli kweli kule Rungwe.
 
Mtanzania,

Kweli unaijua Mbeya! Uliyoongea sina la kuongeza sema tu kama utagombea ubunge kule ili tukupigie debe!

Taabu yaangu mimi nilipenda demu mmoja kule Mbeya na alinitesa sana --yaani sina hamu na watu wa Mbeya!
 
Kuhusu Mwakyembe kuwania uwaziri, sidhani kama pana mtu anayeweza kuthibitisha hilo. Kumweleza JK nadhani ilikuwa ktk taratibu za kikazi Mwakyembe hakutoka from nowhere, nadhani nafasi zake za awali zilikuwa zinakidhi haja zake, hili la ubunge nafikiri ni moyo wa utaifa uliomvuta na kama ilivyo kwa wabunge wengi wananchi uwaomba watu wagombee kwa sababu kuona watafanya vema kuliko yule aliyepo.

Msavila,

Sio rahisi mtu kuthibitisha kwa hard copies kwamba mheshimiwa alikuwa anataka uwaziri. Ukiniuliza mimi nitasema kwa jinsi nilivyoongea naye, alikuwa anategemea awe waziri.

Moyo wa utaifa inawezekana, lakini si pia angeweza kuendeleza utaifa kule kwenye bunge la East Afrika? Utendaji wake kule pia nasikia ulikuwa mzuri sana.

Hii ya kuombwa kugombea ni geresha tu ya wanasiasa. Sitaki kuandika mambo mengi ya hawa waheshimiwa hapa, ukitaka naweza kukupa facts kibao zingine ambazo zinaweza kuonyesha tofauti.
 
Mtanzania,

Kweli unaijua Mbeya! Uliyoongea sina la kuongeza sema tu kama utagombea ubunge kule ili tukupigie debe!

Taabu yaangu mimi nilipenda demu mmoja kule Mbeya na alinitesa sana --yaani sina hamu na watu wa Mbeya!

Mzalendohalisi,

Kwi kwi kwi!!!! hata mimi nimewakimbia hao dada zetu. Nasikia hata makonde huwa wanatembeza. Kuna haja ya kumwuliza mzee wetu TingaTinga, vipi yeye hakuwahi kuchukua mkono? (utani)
 
Mwanakijiji,
Sina hakika kama ni Mbeya tu; lakini kwa ujumla wake, huyu jamaa alipewa U-RC Mbeya kwa kazi maalum, hasa baada ya kujeruhiwa vibaya sana na Mwakyembe kwenye kura za maoni, ndipo mtandao ukampa U-RC ili amshungurikie Mwakyembe kwa upande mmoja na Mwandosya kwa upande mwingine. Na jamaa anawajibika kweli kweli katika katika kumdhibiti Mwakyembe, kwani alishapewa green light na wazee wenyewe. Rejea kamati ya Kinana na matokeo yake pale Mwakyembe alipolalamika kwa JK kwamba Mwakipesile anahujumu juhudi zake.

Mkuu Msavila,
Hili vurumai linaendelea mpaka kesho. Mshike mshike huu ulioanza mwaka 2005 walipelekana nao hadi kwenye uchaguzi wa NEC mwaka jana, yaani mpaka misibani ilikuwa ni habari za vurugu hii tu. We jiulize, kwa nini JK hajakanyaga Mbeya hadi dakika hii tangu aingie madarakani mwaka 2005? Kilichowakutanisha Mwakipesile na Mwakyembe mwaka jana ni ziara ya Lowassa katika kufafanua kale kasungura kake na ndege yake aliyosema inapaa, kwani alizungukia kila jimbo na ilibidi mbunge wa jimbo awepo wakati wa wizara pamoja na mkuu wa mkoa, lakini kila mmoja alikuwa na yake moyoni!
Ngoma bado mbichi sana hii.
Ya sisiemu tuwaachie wenyewe!

Mafuchila,

Hiyo influence ya mtandao kumuweka RC ilitoka kwa Lowassa au JK?

Maana kama ni JK itakuwa contradiction kwa maana Mwakyembe nilifikiri alikuwa karibu sana na JK,au siyo?

Hii ni ifnluence ya mtandao. Lengo lao walitaka Mwakipesile afagie njia ya mtandao kushinda chaguzi za NEC mwaka jana na pia ku-deal na Mwakyembe na Mwandosya. Walishindwa kumng'oa Mwandosya katika NEC baada ya kumpandikiza yule kijana wa Mwang'onda kugombea, akabwagwa.
Ngoma inaendelea. Mbeya mwisho!

Hivi ni vitugani ambavyo hawa watu wawili wamevifanya huko kwao kyela ktk kuchochea maendelea ambayo watu wa huko kwao yamewanufaisha japo kidogo.

Kwa kweli binafsi sijaona mengi kule wilayani Kyela. Nimepita Kyela mnamo mwezi Juni mwaka 2005 (nilikuwa naenda kazini vijiji vya Ikombe, Lumbila, Ikolo, Ipinda na Matema) sikuona maendeleo yoyote ya maana. Barabara ya kutoka Kyela kwenda Matema haipitiki kirahisi. Na hii ni kati ya wilaya mbili za mkoa wa Mbeya ambazo ziko nyuma kimaendeleo, hasa elimu, ikiwemo na Ileje. Kyela ina rasilimali nyingi sana za kuweza kuliletea jimbo lile maendeleo lakini naona hazijatumiwa ipaswavyo ili kukwamua uchumi wake. Ina ziwa Nyasa (uvuvi), ina korosho, ina chikichi, ina mpunga bora, ina kakao, ina hiliki, ina minazi, iko mpakani na nchi ya Malawi kibiashara nk, sasa nashindwa kuelewa shida ni nini hasa inayofanya wilaya ile iwe vile ilivyo, ukilinganisha na wilaya jirani ya akina Mwandosya (Rungwe)!
Mtanzania tupe mchanganuo hapa, maana wewe wapafahamu vyema!

Sasa naanza kupata picha ya Lowasa na Kamati na Spika kumweka Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa kamati .Nina anza sasa ku recall maneno ya Lowasa na madaha makubwa toka kwa Mwakyembe siku ya kusoma report .Hii ngoma tunasema Lowasa kaenda lakini CCM wana kaangana na ndiyo maana leo haya tunawaona kama wanalikuwa wamoja naamini Lowasa na report vyote vingaliweza kumalizika kimya kimya .So again JK is not real for my rich country but tunaitwa watu masikini .Maskini weeeeeeeeeee

Ndiyo maana yake! Wahenga wanasema "Tikiti Bovu liko Shambani mwako" ama " Kikulacho Ki Nguoni Mwako" Atakayevunja sisiemu ni sisiemu wenyewe, kama siasa ni za namna hii!
Nawasilisha
 
FMES,

Huyu mkuu alikuwa anakula huku na huku. Yeye na Mwakipesile walikuwa wanahudhuria vikao vyote vya kumuuza Prof. Mwandosya kwenye urais lakini
huku chini chini walikuwa mtandao.

Kuna watu wanasema Prof. Mwakyusa hakuwa mtandao, nafikiri hawaelewi vizuri politics za Mbeya.

JK aliliingia kundi la Mwandosya mno bila wao kujua. Walipokuja kujua tayari wakawa wamefungwa goli.

Kwa wabunge, nafikiri ni Mwakyembe tu ambaye alikuwa mtu wa prof. Mwandosya kwa asilimia 100.

Huyo prof. Mwakyusa, mwaka 2010 nafikiri atakuwa na kazi ngumu kweli kweli kule Rungwe.

Mtanzania,
Huo ufafanuzi wako wa chaguzi za Mbeya umetulia sana, kama ule ambao tuliuchambua katika blogu ya Maggid Mjengwa mwaka jana wakati wa chaguzi za NEC!
Sasa basi, huo uharamia wa kuwaficha wajumbe wanaopiga kura ulifanyika hata katika chaguzi za wilaya za Mbeya Mjini na Mbeya Vijijini. Wajumbe walipelekwa mjini Tunduma kwa kutumia Toyota Coaster mbili, usiku wa manane, wakabwagwa hapo wakiwa na "Bahasha" zao na magari hayo yakajirudia Mbeya usiku huo huo kama hakuna kilichotendeka vile! Injinia wa yote hayo alikuwa yule meya wa jiji hilo.
Kilichoendelea baada ya hapo nadhani umekifafanua vyema. Siasa ni mchezo wa kiharamia mno, kama mambo ni yale!
Otherwise nikupe tano kabisa kwa uchambuzi huo murua.
 
Back
Top Bottom