Siasa za Mbeya 2005-2010

Siasa za Mbeya 2005-2010

Kaka Lole,

Mimi naweza kukusanya mtaa mzima kama hilo pambano litapangwa. Mtu lazima atolewe knock-out siku hiyo.

Hata mimi hawa wakubwa wamenichosha na hizi kelele zao kupitia magazetini. Wakipatanishwa wanashikana mikono, kesho yake wanaanza kugombana tena.
injinia japo bado ninaendelea na utafiti na mzee imbombongafu amesema anasubiri sasa inabini nifanye kazi kweli kweli japo ninakusanya data kwa njia ya interview sijafikia kwenye conlusion lakini nikapata wazo nafikiri ni la maana zaidi.
hapa wazee tukiangalia vita vyao athari kubwa ni kwa wanakyela. huyu mwakyembe akuchaguliwa na miti ni watu. na sisi vijana wa kyela tumekuwa wapole mno, na wengi wao hawashiriki hata kupiga kura. lakini tukiacha haya mambo yaendelee na tabia za mbunge zinaonekana zina matatizo. watakao kuja kuumia ni watoto wetu na wajukuu wetu. kwa kuwa viongozi wetu wote hakuna vijana. mimi ninashangaa kama darasa la pili anashika udiwani wakati injinia upo hapo. hapa kuna haja ya kutumia ujana wetu tuikamate kyela.
HIvi huyu mwakyembe mnamuogopa sana? kusubili mpaka uchaguzi ndio kumshughulikia mtu hii imetuumiza sana.( kumbuka enzi za mwakipesile). na uongo kwa hawa wabunge wetu imekuwa ni jadi wakiamini kuwa watu wa kyela hajui lolote.
sasa kuna umuhimu wa ku organize mkutano wa vijana wa kyela na huyu mbunge atueleze kwa kirefu nini kinafanyika. lakini pia asutwe kwa tabia zake mbaya. pia lazima tuwe na vipaumbele sisi kama vijana ili kila mbunge tumwambie tunataka ufanye hiki na kile.hapa tutakuwa tumewashika, la sivyo watakuwa wanatuchezea kama mpira wa kona. kama organisation itakwenda vizuri ni suala la kuwasiliana kwenda ofisini kwa mbunge(kama mnaogopa mimi nitawawakilisha) tumuandikie barua na kumwita. ni vizuri ikawa mwenzi wa kumi na mbili wakati vijana wengi wanakuwepo hapo. lakini ili tuwe na nguvu za kuwaendesha watu hawa ni lazima tujiandikishe kwa wingi na tukipiga kura basi kuwe na effect inayoonekana. hii inawezekana, pia kuongea na vijana ambao wanahitimu vyuo vikuu waje wagombee hata udiwani. hapa hakuna mchezo. vijana wajenge kyela yao kwa manufaa ya watoto na wajukuu wao. hapo injinia kama utaweza kuorganize maana wewe ndio upo hapo na unaweza kukutana na vijana wengi sana tuwasiliane. na wengine ambao mnaaunga mkono hili ebu tuweke network. hii ndio njia pekee ya kuwashughulikia watu hawa. tutamwambia aje, akigoma kuja huyo mbunge sisi tutaunganisha nguvu ya kumuondoa. hawezi kugoma. hapo tumseme waziwazi kama sio kumsuta aache kuhisi kila mwanakyela atakayempinga basi anauhusiano na mafisadi. ajue wanataka mabadiliko, hii vita ya mafisadi isimpe kiburi na kuamini atashinda hata bila ya kuleta maendeleo. hata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mjiandikishe na muweke viongozi wenye dira. hapa tutaikamata kyela na kuindeleza.
 
Last edited:
Kasyabone,

Mheshimiwa Mwakyembe kaingia Kyela jana jioni na akaenda mpaka Ipinda, akakuta wale vijana wa kumshangilia hawapo tena. Baadhi ya vijana wakaanza kuimba mwogopeni huyo, ana mfupa wa Albino, kautoa Tabora.

Mkuu Sikonge, hatukutaki tena Kyela maana inaelekea huko Tabora kumbe mnaua Albino. Yaani siasa za Kyela ni usanii mkubwa. Watu tukacheka kidogo mbavu zipasuke.

Leo kuna mkutano muhimu sana wa vijana kule Ipinda. Lengo ni kupanga mikakati ya kuelemisha wananchi juu ya sifa za madiwani na wabunge kwa ajili ya 2010. Vijana wamepania kutokufanya makosa ya 2005.

Huyo diwani Makete hata kuandika kunampa shida. Ila jamaa ana wajibika mno. Pia sasa wamempa kuwa mwenyekiti wa Wazazi Kyela. Siku moja walishikana shati na mbunge kwenye mkutano. Mbunge kwa kujua Makete hajui kiingereza akaanza kumteta pale pale mbele yake kwa kuongea kiingereza na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya. Makete kumbe kuna maneno anajua bwana! Zogo lililotokea hapo ilikuwa balaa kabisa. Hawa ndio viongozi wetu, kazi kutetana kila sehemu, hayo maendeleo yatatoka wapi?

Mimi siasa siziwezi bwana! sina muda wa kuita mhogo eti karoti. Mtu mjinga mimi namwita mpumbavu, wananchi watanitupa baada ya wiki moja tu. Hata vijana hapa mimi nawatukana tu, walikuwa wanaona mimi najifanya babu kubwa kwasababu ni engineer, ila sasa wengi wamenielewa na tunaanza kuelewana. Tumewasaidia wengi waache kukaa vijiweni na walime kokoa. Tutaendelea kusaidiana kwa mbali lakini siasa sitaki kabisa.

Karibu Kyela, ila desemba naona hapa patajaa na hapatatosha maana Mwakyembe huwa anakuwepo xmas na sasa nimesikia Mwakalinga naye anakuja. Sisi wapambe tutashiba tu. Kulingana na mkwe Malafyale pikipiki yangu haitakosa mafuta. karibu sana Kyela.
 
hio safi sana mzee. kunahabari nimezipata punde eti umefukuzwa Kyela sasa sijui kama ni uzushi au kuna ukweli ndani yake. naomba unihakikishie!!! na kuhusu laptop vipi eti wategemea kupewa na mwakalinga? mimi sijui huyo sikonge kakumbwa na nini maana hupo kimya sana. December lazima nione vituko mzee!!!
 
Kasyabone,

Mheshimiwa Mwakyembe kaingia Kyela jana jioni na akaenda mpaka Ipinda, akakuta wale vijana wa kumshangilia hawapo tena. Baadhi ya vijana wakaanza kuimba mwogopeni huyo, ana mfupa wa Albino, kautoa Tabora.

Mkuu Sikonge, hatukutaki tena Kyela maana inaelekea huko Tabora kumbe mnaua Albino. Yaani siasa za Kyela ni usanii mkubwa. Watu tukacheka kidogo mbavu zipasuke.

Leo kuna mkutano muhimu sana wa vijana kule Ipinda. Lengo ni kupanga mikakati ya kuelemisha wananchi juu ya sifa za madiwani na wabunge kwa ajili ya 2010. Vijana wamepania kutokufanya makosa ya 2005.

Huyo diwani Makete hata kuandika kunampa shida. Ila jamaa ana wajibika mno. Pia sasa wamempa kuwa mwenyekiti wa Wazazi Kyela. Siku moja walishikana shati na mbunge kwenye mkutano. Mbunge kwa kujua Makete hajui kiingereza akaanza kumteta pale pale mbele yake kwa kuongea kiingereza na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya. Makete kumbe kuna maneno anajua bwana! Zogo lililotokea hapo ilikuwa balaa kabisa. Hawa ndio viongozi wetu, kazi kutetana kila sehemu, hayo maendeleo yatatoka wapi?

Mimi siasa siziwezi bwana! sina muda wa kuita mhogo eti karoti. Mtu mjinga mimi namwita mpumbavu, wananchi watanitupa baada ya wiki moja tu. Hata vijana hapa mimi nawatukana tu, walikuwa wanaona mimi najifanya babu kubwa kwasababu ni engineer, ila sasa wengi wamenielewa na tunaanza kuelewana. Tumewasaidia wengi waache kukaa vijiweni na walime kokoa. Tutaendelea kusaidiana kwa mbali lakini siasa sitaki kabisa.

Karibu Kyela, ila desemba naona hapa patajaa na hapatatosha maana Mwakyembe huwa anakuwepo xmas na sasa nimesikia Mwakalinga naye anakuja. Sisi wapambe tutashiba tu. Kulingana na mkwe Malafyale pikipiki yangu haitakosa mafuta. karibu sana Kyela.
hio safi sana mzee. kunahabari nimezipata punde eti umefukuzwa Kyela sasa sijui kama ni uzushi au kuna ukweli ndani yake. naomba unihakikishie!!! na kuhusu laptop vipi eti wategemea kupewa na mwakalinga? mimi sijui huyo sikonge kakumbwa na nini maana hupo kimya sana. December lazima nione vituko mzee!!! hivi wewe unamsapoti mtu yeyote au ni mwakalinga tu?
 
mimi kinachonihudhi ni siasa za ukabila, ukoo, kitongoji na uchafu wote usiostahili,
 
Mapambano ya hwa jamaa kwenye vyombo vya habari inaeleka havina mshindi.
Mimi nataka kufadhili pambano la NDONDI KAVU KAVU kati ya Mwakyembe na Mwakipesile.
Sisi tunataka tujue nani zaidi.
Wengine kina Engineer na wapambe wa pande zote tafuteni washabiki ili mufurahishe roho zenu.

Mshindi nitampatia tiketi ya ndege na pesa ya matumizi siku tatu aende kwenye ile hoteli waliyofikia "akina Mwakipesile"........kuomba kitu kwa kutumia darubini/hadubini.....lol
 
Mabishano na marumbano ya hawa waheshimiwa ni aibu na pia ni upuuzi ambao unabidi ukemewe kwa nguvu zote. Watoto na vijana wanajifunza nini katika hili?.
Hawa waheshimiwa walipaswa kuonesha mfano mzuri, watafute njia mbadala ya kulizungumza na kulitatua tatizo lao kiustaarabu na wala si kutukanana kwenye magazeti. Na hata kama watashindwa kukubaliana basi ni vyema kukubali kutokubaliana, lakini si kubwatuka kama mbwa koko mwenye njaa.

Mwakyembe na Mwakipesile linga mbakolile angubakoma. Muli bakonyofu fijo.
 
RC sasa awashukia waandishi wa habari
Awabwatukia hadharani
MATUKIO ya watendaji kufokewa hovyo kwenye mikutano ya wazi mkoani Mbeya yamezidi kushika kasi hadi kuwafikia wanahabari mkoani humo.
Ilianza kama jambo la kawaida ambapo tukio la kwanza lilimhusu aliyekuwa Mhandisi wa Wilaya ya Kyela, Stanley Mgaya kufokewa na Mkuu wa Mkoa huo, John Mwakipesile kwenye moja ya vikao vya serikali vya mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile

Ilihitaji uvumilivu wa hali ya juu kwa mtumishi yule kuvumilia unyanyasaji aliofanyiwa siku ile mbele ya hadhara.
Haukupita muda mrefu Mgaya akahamishiwa mkoani Mara; huku taarifa za ndani za serikali wilayani Kyela zikibainisha kuwa Mhandisi yule alilazimika kujiepushia shari zaidi kwa "kuwaachia wenye mkoa", na inaelezwa zaidi kuwa hata hivi sasa anaogopa kutembelea mkoa huo akihofu asije kuzushiwa jambo la hatari zaidi.
Aliyefuata kuonja joto ya uongozi wa juu wa Serikali mkoani Mbeya ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Elizabeth Munuo.
Naye huyo, pasipo kuzingatia hata haki za binadamu na ukweli kwamba ukiweka pembeni utumishi wake bado anabaki kuwa mwanadamu; tena mama wa watoto ambao ni watu wazima, alifokewa hadharani.
Alifokewa kwenye moja ya vikao vya mkoa huo kana kwamba ni kiumbe dhalili vile, asiyestahili chembe ya heshima wala staha.
Mama huyo alihukumiwa na uongozi wa juu wa Serikali ya Mkoa wa Mbeya pasipo kufanyika utafiti wa kina kufahamu matatizo halisi yanayoukabili uongozi wa Jiji hilo. Kwa maneno mengine, alifanywa kuwa mbuzi wa kafara na "wenye mkoa".
Kilichofuata ni Mkurugenzi huyo kuhamishiwa jijini Dar es Salaam.
Lakini wakazi wa mkoa wa Mbeya wakiwa bado wanatafakari kuhusu huo utamaduni wa Mkuu wa Mkoa huo, John Mwakipesile kufokea watendaji wa halmashauri za wilaya na jiji mkoani humo, sunami hiyo akaihamishia ofisini kwake.
Safari hii alikuwa si mwingine; bali ni Mshauri wa Majengo wa Mkoa huo, Aidan Ngwada ambaye alifokewa kwenye Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa huo.
Kwa wale tuliomuona Ngwada siku ile mara baada ya kufokewa mithili ya mtoto yatima kwa mama wa kambo jeuri, akiwa amejiinamia kwenye meza, na jinsi alivyoondoka kwenye Ukumbi ule wa Mkapa huku kikao kikiendelea akiwa ameinamisha kichwa chini, ni wazi presha ilikuwa ikipanda na kushuka.
Hata katika mazungumzo yangu na Ngwada mwenyewe siku iliyofuata, nilibaini ugumu wa mazingira aliyokuwa nayo Mhandisi yule siku hiyo.
Alinieleza wazi kuwa hakuwa anaamini kama bado yungali kazini hadi dakika ile.
"Ni Mungu tu ndiye anayejua. Siamini kama bado niko kazini. Hali yangu ya jana ilikuwa mbaya pia kiafya, presha ilikuwa juu. Baada ya kufokewa kule, nilienda moja kwa moja kulala. Yote namwachia Mungu," ndivyo alivyoweza kunieleza Ngwada na hakupenda kuendelea zaidi.
Leo hii ninapoandika makala hii, Mhandisi huyo amesimamishwa kazi kwa madai ya usimamizi mbovu wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
Siyo lengo la makala hii kutetea uozo na utendaji mbovu wa watumishi wa serikali mkoani Mbeya. La hasha, makala hii inahoji umakini wa uongozi huo wa mkoa katika matukio yanayohusu wafanyakazi wake wa chini.
Ninachojaribu kuhoji katika makala hii ni kwamba uongozi wa juu wa mkoa, unashindwa nini kutumia utaratibu wake wa ndani wa kiutumishi katika kuwawajibisha watendaji walio chini yake; badala ya kusubiri kuwafokea kwenye mikutano; tena mbele ya watu wanaowaongoza?
Hebu tujiulize hapa kwamba, kwa hali aliyokuwa nayo Ngwada siku ile, kama (kwa mfano) angepoteza maisha kutokana na mshituko alioupata, hivi Mkuu wa Mkoa, ambaye ndiye aliyeichochea hali ile, angejisikiaje?
Lakini hayo yote ni tisa, kumi ni yaliyojiri kwenye Mkutano wa Mkoa wa Septemba 12, mwaka huu, ulioitishwa rasmi kwa ajili ya kuweka mikakati ya kilimo mkoani Mbeya ikiwa ni kuitikia kauli mbiu ya Kilimo Kwanza.
Pamoja na mkutano kuanza kwa utulivu, ulimalizika ukiwa shubiri kwa wanahabari mkoani humo pale Mkuu wa Mkoa huo alipowafyatukia na kuwafokea akidai kuwa baadhi yao wameapa kumwandika vibaya; hata kama atafanya mambo mazuri.
Hatua ya Mkuu huyo wa Mkoa kuwafokea wanahabari siku hiyo ilifuatia changamoto iliyotolewa na mwasilishaji wa mada ya "Nafasi ya wanahabari katika maendeleo ya kilimo mkoani Mbeya," Jonas Mwasumbi.
Katika changamoto hiyo, Mwasumbi aliishauri Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuondokana na kasumba ya kubagua vyombo vya habari kwa kutoyathamini magazeti, na badala yake kutoa upendeleo zaidi kwenye televisheni na redio; hatua aliyosema itasababisha mchango wa vyombo vya habari kutoonekana kwa mapana yake.
Ni jambo lililokuwa wazi kabisa kwamba changamoto ile haikulenga kuibua malumbano; bali ililenga kuboresha zaidi namna ambavyo vyombo vya habari vinaweza kuchangia kwenye maendeleo ya kilimo mkoani Mbeya.
Lakini tofauti na mategemeo ya wanahabari, walichoambulia kwenye hotuba ya Mkuu wa Mkoa wakati anafunga mkutano huo, ni hasira dhidi ya baadhi yao aliodai wamekuwa wakimwandika vibaya tangu ateuliwe kuwa kiongozi wa juu wa serikali mkoani humo.
Pamoja na kutowataja majina, lakini mkuu wa mkoa huo aliweza kuwabainisha kwa maelezo yake kwamba baadhi ni ndugu wa Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, na wengine alidai wamefukuzwa walikotoka.
Mkuu huyo hakuishia kwenye mkutano ule; bali alienda mbali zaidi siku ya pili yake alipoalikwa na kikundi cha Wazee wa Jiji la Mbeya kuzindua Chama chao cha Akiba na Mikopo (SACCOS) pale alipoyataja kwa majina magazeti ya Mtanzania, Nipashe na Tanzania Daima kwamba anayachukia kwa madai kwamba waandishi wake wanamzushia mambo ya uongo.
Ni wazi kwamba, kwa mtazamo wake, mtu yeyote aliye jasiri wa kumwonyesha upande wake wa pili wa shilingi, hafai, hampendi, na ni mbaya wake. Na kwenye kundi hilo ndimo wanaingia waandishi hao wa habari wasiojipendekeza kwake.
Kwake, mwandishi mzuri na mweledi ni yule atakayeandika; Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amesema hivi.., amesisitiza hivi.., na vifungua sentensi vingi vya aina hiyo.
Inasikitisha kuona kwamba anahitaji waandishi wa habari watakaomsifia kuwa yeye ndiye Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mbeya kuwa karibu na wanahabari na kuwapa uhuru mpana wa kuingia na kuchukua habari ofisini kwake, lakini wakati huo huo wasimweleze mahusiano na ukaribu waliokuwa nao na Basil Mramba wakati akiwa mkuu wa mkoa huo.
Baadhi ya wakazi wa Mbeya sasa wanajiuliza kwamba; kama wale watendaji wa Serikali kina Stanley Mgaya, Mama Elizabeth Munuo na Aidan Ngwada, walihamishwa na mmoja kusimamishwa kazi, atawafanya nini waandishi wa habari wa Mbeya anaowachukulia kuwa ni maadui wake?
Kama ni wale wa magazeti walio kwenye orodha yake ya maadui, hao siyo waajiriwa wa Serikali; kwa hiyo hawezi kuwafukuza kazi au kuwahamisha mkoani humo.
Hofu pekee kubwa waliyonayo waandishi hao wa habari ni kuminywa kwa uhuru wao wa kuandika habari au hata vyombo vyao wanavyofanyia kazi kupigwa marufuku mkoani humo au hata kutungiwa madhambi mengine.
 
Mwakyembe awa mbogo
Atoboa siri ya ugomvi wake na Mwakipesile
Adai kiongozi huyo anafanya kazi ya mafisadi
Ataka atambue kwamba yeye ni RC na siyo MC

Na Gladness Mboma

MBUNGE wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa tatizo analoliona kati yake na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. John Mwakipesile ni harakati zake za kutaka kumng'oa katika jimbo la Kyela, jambo ambalo hataweza.

Alisema kuwa kazi anayoifanya Bw. Mwakipesile katika jimbo lake ni sawa na kuuza kofia za polisi ambazo hazinunuliki na kwamba anajisumbua, anajidhalilisha na kujifedhehesha licha ya kutumwa na mafisadi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Dkt. Mwakyembe alitoa kauli hizo za kejeli alipozungumza na gazeti hili kujibu hoja za Bw. Mwakipesile kuwa mbunge huyo anapotoshwa na wapambe wake wanaompa taarifa za uongo na kwamba hajawahi kuwaomba wazee wa Mbeya ili wawapatanishe.

"Ni lazima Bw. Mwakipesile atambue kuwa yeye ni RC na siyo MC kwa maana ya msema chochote. Mkuu wa mkoa mmoja kati ya wakuu wa mikoa 21 kuzungumza magazetini kila siku akiwarukia wabunge wanaopambana na ufisadi ni dalili ya kuweweseka.

"Ninalazimika kusema kuwa mwenzetu anahitaji ushauri nasaha, waandishi mchunguzeni Bw. Mwakipesile ili kujua anapatana na mbunge gani mkoani Mbeya?" alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe aliongeza kuwa, kila mtu anatambua kuwa Bw. Mwakipesile anashinda Kyela kufanya kampeni za kuhakikisha kuwa, anamuondoa mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu na kwamba Serikali inatambua jambo hilo.

"Hili tatizo halinipi tabu hata kidogo kwa sababu kazi anayofanya ni kama kuuza kofia za polisi mali ambazo hazinunuliki anajisumbua, anajidhalilisha na kujifedhehesha," alisema.

Dkt. Mwakyembe alisema kuwa alipata kura asilimia 93 katika uchaguzi mkuu mwaka 2005, lakini anashangazwa na kauli aliyoitoa Bw. Mwakipesile katika gazeti hili kwamba wapambe ndio wanaompotosha na kumtaka atambue kuwa wapambe hao ni wananchi wote wa Kyela.

"Tatizo la Bw. Mwakipesile anadanganywa sana na mafisadi ambao wanamtumia kama wakala, hiyo kazi waliyompa kwa Kyela ni ngumu kwelikweli, ni sawa na kuuza kofia za polisi kwa wananchi hivyo ni lazima atambue kuwa mimi ni mti mkavu usiochimbwa dawa," alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Alisema kuwa yeye alikuwa nje ya nchi na amerudi juzi ndipo alipomkuta mwenzake akiongea hovyo katika vyombo vya habari huku akitoa malalamiko kwamba yeye ndiye anayekwamisha maendeleo ya Mkoa wa Mbeya.

Alipoulizwa kiini cha mgogoro kati yake na Bw. Mwakipesile unasababishwa na nini, Dkt. Mwakyembe alisema kuwa yeye hana mgogoro wowote na mkuu huyo wa mkoa, bali yeye RC huyo anayekwamisha maendeleo ya mkoa huo kutokana na muda wote kukaa Kyela kwa lengo la kumwondoa mbunge mwaka 2010.

Akizungumzia madai ya kutaka kuuawa alisema kuwa huo ni uongo na kwamba anaokoteza maneno barabarani na kuyafanyia kazi.

.....duuuhh haya ni kweli maneno ya "Dokita".......so weird plus its difficult to comprehend.............
 
Tena Mwakipesile angepewa na kiboko awatandike hao wazembe. Hao Wahandisi wa wilaya za Kyela za Chunya wamesimamia ujenzi wa majengo mabovu ya wakuu wa wilaya na kutoa taarifa za uwongo kwenye vikao. Sababu kubwa ni ufisadi tu.

Wewe ndugu yetu unakuja kutetea watu ambao wanakwamisha maendeleo na kukumbatia uwizi?

Waandishi wa habari nyie mnapoandika habari za kupikwa, mnatakwa muachiwe tu? Huyo Mwanakatwe kweli utamwita mwandishi wa habari au ni mhandisi wa habari?

Tetea mengine labda na huyo mama ambaye mimi simjui vizuri lakini hao Wahandisi wa Kyela na Chunya hawakustahili hata kubaki kazini, inatakiwa wafukuzwe kazi.
 
hio safi sana mzee. kunahabari nimezipata punde eti umefukuzwa Kyela sasa sijui kama ni uzushi au kuna ukweli ndani yake. naomba unihakikishie!!! na kuhusu laptop vipi eti wategemea kupewa na mwakalinga? mimi sijui huyo sikonge kakumbwa na nini maana hupo kimya sana. December lazima nione vituko mzee!!! hivi wewe unamsapoti mtu yeyote au ni mwakalinga tu?

Kasyabone,

Huyu Masanilo nuksi kabisa, mimi engineer mzima eti mpaka laptop nipewe na mtu?

Mimi nipo Kyela tena leo tumewalima wenyeviti watatu wa vijiji. Tulikuwa kuchuja majina ya wagombea wa serikali za mitaa. Hao wenyeviti wa kata za Ipinda na Ikolo wametupwa nje kwasababu waligawa kadi fake kwa wanachama ili wawapigie kura.

Ushahidi uliletwa na katibu wa wilaya akathibitisha ni kweli hizo kadi haziko kwenye daftari lake. Mheshimiwa akajaribu kuwatetea wapambe wake lakini ushahidi ulikuwa mzito, hata mwenyewe akaamua kuondoka na kwenye kikao.

Kasyabone, hata wewe unaweza kuja na sera zako na kama tutaona zinafaa, sisi vijana hatuna noma, tutakuunga mkono. Kwasasa ni wawili tu Mwakyembe vs Mwakalinga. Mimi mpaka sasa namuunga mkono Mwakalinga. Lakini sijawekeana naye mkataba, akija mwenye sera nzuri zaidi mimi nageuka kinoma. Hapendwi mtu mwaka huu, ni sera. Tunataka jogoo linalozalisha kuku, sio jogoo linalojua tu kupiga kokolikoooooooooooo!! asubuhi.

Ogah, kama unashangaa hiyo habari, basi njoo siku moja huku vijijini na umsikilize Dr wakati anahutubia, ukiwa na hasira utachukia na kuondoka, vingine utacheka mpaka mbavu zikupasuke.
 
Nyani haoni kundule, kama Mwakipesile hapatikani na mbunge yeyote wa mkoa wa Mbeya, je yeye Dr. Mwakyembe mbona na yeye hapatani na diwani yeyote wa wilaya ya Kyela? Mbona hapatani na kiongozi yetyote wa CCM wa wilaya ya Kyela. Hawa jamaa wote wawili wanaturudisha nyuma shauri ya ujinga wao usio na mwisho.

Baada ya kuitangazia dunia yote kwamba alitaka kuuwa, sasa anaanza kuruka na kusema ni uwongo? Amejua polisi wamegundua nini na anaanza kujiandaa kabla ya report. Kama ni uongo kwanini alienda kununua kisu na kuwapa wapambe ili wakitumie kama ushahidi wa kutaka kuuwa kwa kisu? Mbona alitumia magazeti ya MENGI kuitangazia dunia nzima kwamba alitaka kuuwa?

mkuu zile milioni 400 vipi hujazimaliza mlizopewa na mwakalinga??
 
Kasyabone,

Huyu Masanilo nuksi kabisa, mimi engineer mzima eti mpaka laptop nipewe na mtu?

Mimi nipo Kyela tena leo tumewalima wenyeviti watatu wa vijiji. Tulikuwa kuchuja majina ya wagombea wa serikali za mitaa. Hao wenyeviti wa kata za Ipinda na Ikolo wametupwa nje kwasababu waligawa kadi fake kwa wanachama ili wawapigie kura.

Ushahidi uliletwa na katibu wa wilaya akathibitisha ni kweli hizo kadi haziko kwenye daftari lake. Mheshimiwa akajaribu kuwatetea wapambe wake lakini ushahidi ulikuwa mzito, hata mwenyewe akaamua kuondoka na kwenye kikao.

Kasyabone, hata wewe unaweza kuja na sera zako na kama tutaona zinafaa, sisi vijana hatuna noma, tutakuunga mkono. Kwasasa ni wawili tu Mwakyembe vs Mwakalinga. Mimi mpaka sasa namuunga mkono Mwakalinga. Lakini sijawekeana naye mkataba, akija mwenye sera nzuri zaidi mimi nageuka kinoma. Hapendwi mtu mwaka huu, ni sera. Tunataka jogoo linalozalisha kuku, sio jogoo linalojua tu kupiga kokolikoooooooooooo!! asubuhi.

Ogah, kama unashangaa hiyo habari, basi njoo siku moja huku vijijini na umsikilize Dr wakati anahutubia, ukiwa na hasira utachukia na kuondoka, vingine utacheka mpaka mbavu zikupasuke.

Nadhani wewe ndo ma engineer wa CCM ambao hata kusoma michoro hamjui. Mhandisi aliye kamilika hawezi kuhongwa vijisenti ili amtumikie mwanansiasa (mwakalinga).
 
Date::9/26/2009Mwakyembe adai vigogo CCM wanaratibu mpango wa kumhujumu
MWAKYEMBE.jpg
Mbunge wa Kyela,Dk Harrison Mwakyembe, amedai vigogo wa CCM, wanaratibu mpango wa kumhujumu kisiasa kwa kutumia pesa za mafisadi.
broken-heart.jpg
*Chiligati asema watalijadili kwenye vikao vya chama

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe ameitupia kombora CCM kwamba, baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho, wameamua kumhujumu kwa kupeleka fedha za rushwa katika jimbo lake ili kumng'oa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, Mwakyembe alisema viongozi hao wamekuwa wakishirikiana na jopo la mafisadi kusambaza fedha hizo kwa wananchi wa Kyela.

Alisema hivi karibuni wabaya wake hao waliingiza mamilioni ya fedha katika jimbo hilo, zilizopelekwa na kiongozi Mwandamizi wa CCM Mkoa wa Mbeya, lakini alipewa taarifa na kuwataka wazee wazipokee na kuzitumia kwa vile ni fedha zao zilizoibwa na mafisadi.

"Mimi nimewashauri wananchi wazipokee fedha hizo na wazitumie kwa sababu ni mali yao iliyoporwa na mafisadi," alisema.

Mwakyembe alisema anashangaa kuona kwamba rushwa inayopelekwa katika jimbo lake na kusambazwa na mafisadi inajulikana na viongozi wa serikali na CCM, lakini hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa mpaka sasa.

"Serikali ina vyombo vya dola inaweza kuchunguza, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa kwa wahusika," alisema.

Alisema njama za watu hao zinafanywa zikiwashirikisha pia baadhi ya viongozi wa serikali waziwazi bila ya kificho, hali ambayo inamfanya aamini kuwa wabaya wake wana baraka na wanayoyafanya.

Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alisema kama taarifa hizo zipo zitazungumzwa kwenye kikao cha ndani cha chama na si nje.

''Kama hilo lipo tutalizungumza kwenye kikao chetu, siwezi kumwaga mchele kwenye kuku wengi, hivyo akiwasilisha madai yake tutayashughulikia,'' alisema Chiligati.

Mbunge huyo ambaye aliongoza kamati ya bunge ya kuchunguza kashfa ya Richmond alijifariji kwamba, atashinda mapambano hayo kwa sababu wananchi wa Kyela bado wana imani naye.

Hata hivyo, habari zilizopatikana kutoka Kyela, zinaeleza kuwa baadhi ya watu waliozipokea fedha hizo walimtaarifu mbunge wao na wakakubaliana kuwa wagawane na nyingine wakanunulia vinywaji.

Mwakyembe ambaye amekuwa katika ugomvi mkubwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile kwa madai kuwa mkuu huyo wa mkoa anamhujumu akitaka kumng'oa katika jimbo hilo, alisema yote hayo anawaachia wananchi wa Kyela kuamua.

Hii ni mara ya kwanza kwa mbunge huyo ambaye yupo katika kundi la wabunge wanaopambana na ufisadi, kuwashutumu baadhi ya viongozi wa juu waandamizi wa CCM kuwa sasa wanashirikiana na wabaya wake kummaliza.

Akizungumzia uhusiano wake na Mwakipesile, mbunge huyo alisema walishasuluhishwa siku nyingi anashangaa kuona bado anaendelea kuzungumzia tofauti yao na akashauri kama hajaridhika ni vyema akalifikisha suala hilo katika ngazi ya CCM.

Hivi karibuni kumeibuka mgawanyiko wa wana CCM wanaopinga ufisadi na wana CCM ambao wako upande wa mafisadi , hali ambayo ina hatarisha uhai wa chama hicho.

Mgawanyiko huo ndani ya chama hicho ndio ambao ulikifanya kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho mjini Dodoma kuunda kamati ya watu watatu wakiongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa na Mwanasiasa Mkongwe nchini, Abdulrahman Kinana kufuatilia uhasama uliopo kati ya wana CCM na wabunge wa chama hicho. Wakati akizungumza na wananchi kwa staili mpya ya kujibu maswali ya papo kwa hapo, Rais Jakaya Kikwete alisema CCM na serikali haijawafunga midomo wabunge wake kuikosoa serikali.
Tuma maoni kwa Mhariri
Facebook
 
Binafsi nakerwa sana na hii tabia ya huyu mheshimiwa kulia lia kila siku kwenye magazeti.

Kama ni kweli kuna pesa zimetumwa Kyela na yeye ana habari, anashindwa nini kutaja majina ya waliyozileta? majina ya waliopewa? Kweli anashindwa kupata hata mtu mmoja ambaye yuko tayari kuongea wazi na kusema mimi nilipewa pesa kiasi fulani na mtu huyu?

Mwakyembe anaiandaa jamii ili akibwagwa hapo mwakani (kitu ambacho sasa ni very possible) awe na sababu ya kutokea. Huenda pia anaandaa mazingira ya kuhamia CHADEMA akishindwa kwenye mchujo wa CCM (hili jambo linaongelewa sana Kyela kwamba ana mpango huo).

Huyu jamaa ni mwansheria, anashindwa kwenda polisi, anashindwa kwenda mahakamani, anashindwa kwenda kushitaki kwenye chama, anashindwa hata kutaja majina kwenye gazeti. Ujasiri wake wote unaishia kwenye kulia lia?

Sio siri Mwakyembe kakamatwa pabaya kule Kyela na sasa joto limepanda. Mtu jasiri kama Mwakyembe anahangaishwa na kijana ambaye yuko miles kama 5000 tokea Kyela, hana uwezo wa kuhutubia mikutano, hana uwezo wa kuongea na wapiga kura. Hii ni aibu sana. Kapoteza miaka minne anashinda Dar, sasa dakika za majeruhi anaona ngoma nzito ndio anaanza kutafuta mchawi?

Mimi nawashauri CCM watume tume huru kwenda kuchunguza madai ya Mwakyembe na nina uhakika watakuta ni upuuzi wake tu.

Mbunge wa Kyela,Dk Harrison Mwakyembe, amedai vigogo wa CCM, wanaratibu mpango wa kumhujumu kisiasa kwa kutumia pesa za mafisadi.

*Chiligati asema watalijadili kwenye vikao vya chama

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Kyela (CCM), Dk Harrison Mwakyembe ameitupia kombora CCM kwamba, baadhi ya viongozi waandamizi wa chama hicho, wameamua kumhujumu kwa kupeleka fedha za rushwa katika jimbo lake ili kumng'oa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, Mwakyembe alisema viongozi hao wamekuwa wakishirikiana na jopo la mafisadi kusambaza fedha hizo kwa wananchi wa Kyela.

Alisema hivi karibuni wabaya wake hao waliingiza mamilioni ya fedha katika jimbo hilo, zilizopelekwa na kiongozi Mwandamizi wa CCM Mkoa wa Mbeya, lakini alipewa taarifa na kuwataka wazee wazipokee na kuzitumia kwa vile ni fedha zao zilizoibwa na mafisadi.

"Mimi nimewashauri wananchi wazipokee fedha hizo na wazitumie kwa sababu ni mali yao iliyoporwa na mafisadi," alisema.

Mwakyembe alisema anashangaa kuona kwamba rushwa inayopelekwa katika jimbo lake na kusambazwa na mafisadi inajulikana na viongozi wa serikali na CCM, lakini hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa mpaka sasa.

"Serikali ina vyombo vya dola inaweza kuchunguza, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa kwa wahusika," alisema.

Alisema njama za watu hao zinafanywa zikiwashirikisha pia baadhi ya viongozi wa serikali waziwazi bila ya kificho, hali ambayo inamfanya aamini kuwa wabaya wake wana baraka na wanayoyafanya.

Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alisema kama taarifa hizo zipo zitazungumzwa kwenye kikao cha ndani cha chama na si nje.

''Kama hilo lipo tutalizungumza kwenye kikao chetu, siwezi kumwaga mchele kwenye kuku wengi, hivyo akiwasilisha madai yake tutayashughulikia,'' alisema Chiligati.

Mbunge huyo ambaye aliongoza kamati ya bunge ya kuchunguza kashfa ya Richmond alijifariji kwamba, atashinda mapambano hayo kwa sababu wananchi wa Kyela bado wana imani naye.

Hata hivyo, habari zilizopatikana kutoka Kyela, zinaeleza kuwa baadhi ya watu waliozipokea fedha hizo walimtaarifu mbunge wao na wakakubaliana kuwa wagawane na nyingine wakanunulia vinywaji.

Mwakyembe ambaye amekuwa katika ugomvi mkubwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile kwa madai kuwa mkuu huyo wa mkoa anamhujumu akitaka kumng'oa katika jimbo hilo, alisema yote hayo anawaachia wananchi wa Kyela kuamua.

Hii ni mara ya kwanza kwa mbunge huyo ambaye yupo katika kundi la wabunge wanaopambana na ufisadi, kuwashutumu baadhi ya viongozi wa juu waandamizi wa CCM kuwa sasa wanashirikiana na wabaya wake kummaliza.

Akizungumzia uhusiano wake na Mwakipesile, mbunge huyo alisema walishasuluhishwa siku nyingi anashangaa kuona bado anaendelea kuzungumzia tofauti yao na akashauri kama hajaridhika ni vyema akalifikisha suala hilo katika ngazi ya CCM.

Hivi karibuni kumeibuka mgawanyiko wa wana CCM wanaopinga ufisadi na wana CCM ambao wako upande wa mafisadi , hali ambayo ina hatarisha uhai wa chama hicho.

Mgawanyiko huo ndani ya chama hicho ndio ambao ulikifanya kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho mjini Dodoma kuunda kamati ya watu watatu wakiongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa na Mwanasiasa Mkongwe nchini, Abdulrahman Kinana kufuatilia uhasama uliopo kati ya wana CCM na wabunge wa chama hicho. Wakati akizungumza na wananchi kwa staili mpya ya kujibu maswali ya papo kwa hapo, Rais Jakaya Kikwete alisema CCM na serikali haijawafunga midomo wabunge wake kuikosoa serikali.
 
Mkuu nimeipenda sana hii,mwakyembe amekuwa analalamika kila mara kuwa anaonewa anawindwa by the way what is so special with him..katuzingua na mambo ya richmond hapa kumbe na yeye ana kampuni yake iliomba zabuni kuzalisha umeme wa dharura.my personal opinion is that Mwakyembe is not as clean as he think ...utulie aone 2010 itakuwaje sio kupiga piga kelele na siasa zake chakavu
 
Yaliyotokea kwenye vikao vya CC na NEC ni ushahidi wa kutosha kabisa kwamba wapiganaji dhidi ya ufisadi wanaandamwa kwa hali na li ili ikiwezekana hata kufukuzwa chamani wakati mafisadi ndani ya CCM akina Lowassa, Mkapa, Rostam na wengineo wakiendelea kupeta. Tuliona na kusikia jinsi walivyokula njama za kuhakikisha Sitta anaondolewa kwenye uspika na hata kufukuzwa CCM kwa sababu yeye ni mamluki.

Baadaye tukaona kauli za fisadi Chiligati na Makamba zilivyobadilika kuhusu wapiganaji dhidi ya ufisadi. Sasa hawakuwa walevi tena wanaoropokaropoka hovyo na hata Makamba akafunga safari mpaka Tabora kwenda kujipendekeza kwa Sitta ili watuzuge kwamba CCM kuna mshikamano.

Masha aliwahi kutamka kwamba uchunguzi dhidi ya wale wanaomtumia vitisho spika utafanyika kufuatia maombi ya Sitta ya kutaka kuongezewa ulinzi dhidi ya vitisho hivyo. Hadi hii leo Masha hajatwambia lolote. Kikwete hata kulizungumzia hili la vitisho dhidi ya Sitta hataki.

Mwakyembe kishapata ajali ambayo ilijaa utata wa hali ya juu na Polisi kujikanyagakanyaga kuhusiana na yaliyojiri katika ajali ile. Mpaka msikie Sitta au Mwakyembe mmoja wao amekufa katika mazingira ya kutatanisha (GoD forbid) labda ndiyo mtaamini kwamba labda kulikuwa na ukweli katika wasiwasi wanaonyesha dhidi ya maisha yao. Mafisadi aka Mafioso wameshika "utamu' ndani ya serikali na CCM na wameshajua hakuna wa kuwababisha ndiyo maana wanatamba huku na kule kuwatisha 'maadui' wao.
Hivi mnafikiri mtu anayetishia maisha yako atajiweka wazi kiasi hicho umjue kwamba anayetishia maisha yangu ni fulani!?

Inakuwaje mtendaji wa juu serikalini kama Spika anatamka kwamba maisha yake yanatishiwa na Serikali yake iko kimyaa bila kusema au kufanya lolote lile.
 
Last edited:
BAK una akili sana, usije owa mzungu huku tunakuhitaji Tanzania yenye mabadiliko!
 
Nimeambiwa Mama Mkapa anawaambia watu wameshandaa fedha za kutosha kumng'oa Kimario kule Moshi. Lisemwalo lipo na mafisadi hawalali.
 
Back
Top Bottom