Siasa za Mbeya 2005-2010

Siasa za Mbeya 2005-2010

Enginner,
Kazi za mbunge ni

  1. Kutunga sheria;
  2. Kuisimamia serikali; na
  3. Kuwakilisha wananchi.
Kipimo cha ufanisi wa mbunge wakati wa muhula wake sharti kiendane na kazi zake kama inavyotajwa hapo juu.
Ni makosa kwa wananchi kudhani mbunge anatakiwa kujenga shule, vituo vya afya, barabara, visima vya maji na kadhalika. shughuli hizi pamoja na nyinginezo zianzofanana na hizo ni wajibu wa serikali. Lakini iwapo serikali itakuwa imetekwa na mafisadi haiwezi kuwa na rasilimali za kutosha kugharimia shughuli za maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi. Kyela haina shule, barabara, vituo vya afya au miundombinu ya huduma nyingine, ambavyo ni hafifu, basi kelele za Mbunge wenu Mwakyembe dhidi ya mafisadi ndio mahali pake; anaisimamia serikali ipasavyo. Shukuruni Mwenyezi Mungu kwa maana mnaye mbunge mahili anayefanya kazi zake kwa ipaswavyo.
Mtu yeyote anayejinadi kujendga visima vya maji, kujenga barabara, kununulia watoto sare za shule na kadhalika sharti atambulike kuwa ni mtu asiyefaa kuwa mbunge, kwa sabau, ama hana uelewa na kazi za mbunge au ni malaghai. Je, Kyela mnataka kulaghaiwa?
Ni juu yenu kusuka au kunyoa!
wakhtanabahu
Ndugu yangu,

Kama kazi za mbunge ni hizo tu unazozisema wewe, basi hatuhitaji kuwa na wabunge wa majimbo. Tuanzishe wabunge wa kuchaguliwa kufuatana na kura za chama kama zinavyofanya baadhi ya nchi.

Pesa nyingi sasa ziko kwenye halmashauri ya wilaya na hata mipango mingi ya maendeleo inaamuliwa huko na sijui kwa kazi za mbunge kama ulivyoandika, nini wajibu wa mbunge kwenye halmashauri ya wilaya yake?

Nakuhakikishia, kazi ya mbunge ni zaidi ya ulizozitaja. Maendeleo sehemu kubwa kwasasa hayaletwi na serikali peke yake. Sehemu kubwa wananchi wanachangia na Mbunge hapo ni kiungo muhimu mno.
 
Injinia ebu nielezee kidogo sifa za mwakyembe (LOL). najua huwezi!!!

Ugomvi - Kakosana karibu na kila kiongozi Kyela
Majigambo - Anadharau madiwani hawajasoma huku anaongoza wilaya ambayo zaidi ya asilimia 99 ya wananchi wake hawajafika chuo kikuu.

Uwongo - Sisi huku tunasema NTUNGULU FIJO. Dr kuzua jambo kwake sio kitu kigumu

USANII - Ukimsikia mikutano yake utacheka. Kuna sehemu anaulizwa tatizo la barabara, anasema wacha niongee na mhandisi, anapiga simu na kujadiliana na Mhandisi kwamba aache huko anakojenga barabara, aje Kyela maana wananchi wake wanateseka. Huo kama si usanii ni nini? Hizo simu huwa anwapigia wapambe wake. Mfano huo huo anaurudia kwenye vijiji vingine akiongelea mabomba ya maji. Anasahau huko nyuma huyo mhandisi alikuwa wa barabara, sasa kageuka wa maji.

Sifa zake:
Huku wanasema NKIFU maana yake Jasiri wa kuongea
Pia alifanya kazi nzuri Richmond.

Sisi tulimbeba Dr 2005 na kusukuma gari lake, ila sasa simtaki kabisa na wala hilo sifichi. Jamaa hata kuongoza mukutano tu kunamshinda, yeye ni manguvu tu na majigambo kwamba yeye kasoma, hajui hata wengine ni Wahandisi bwana!

Wewe dogo soma maana ukija huku Kyela na elimu ndogo ndogo, Mwakyembe atakunyanyasa sana.
 
Alipoulizwa kiini cha mgogoro kati yake na Bw. Mwakipesile unasababishwa na nini, Dkt. Mwakyembe alisema kuwa yeye hana mgogoro wowote na mkuu huyo wa mkoa, bali yeye RC huyo anayekwamisha maendeleo ya mkoa huo kutokana na muda wote kukaa Kyela kwa lengo la kumwondoa mbunge mwaka 2010.

Familia ya Mwakipesile iko Kyela muda wote. Ratiba ya kawaida ya RC ni kuondoka Jumapili jioni kwenda Mbeya ambako anakaa na kurudi Kyela Ijumaa usiku. Hiyo ratiba ni ya miaka yote toka awe RC.

Kama kuna kazi muhimu basi huwa anabaki weekend Mbeya.

Ni uwongo kusema RC muda wote anashinda Kyela. Kwa mwaka huu wote RC amefanya ziara moja tu ya kikazi wilayani Kyela.

Itafaa mbunge akieleza wazi wazi RC anakwamisha hayo maendeleo kivipi? Na atoe mifano ili wananchi tujue hili limeshindikana kwasababu RC kakwamisha.
 
wewe engineer nina wasiwasi nawe kuwa mpiga bede tu wa mwakilinga,hoja zako mmh ndogo sana,naomba nkufahamishe kuwa Mwakyembe anafanyia kazi Taifa,so anahitajika sana,so hata mkimletea majungu huko mbeya si haba tz tunae atapanda tu.kwanza seems hampendi wasomi huko, Mwandosya nae hayo hayo na huyo huyo mwakipesile,may be mnataka wachawi ndo wawaongoze,mkipata wacha Mungu mnakuwa ngiri na mbogo!! nimediscover hilo pia!!
 
huu uchafu wa mwakyembe na mwakipesile unaniudhi kweli.ngoja nakuja kugombea ubunge kyela kwa tiketi ya nanii!mizee mizima inashambuliana kwenye vyombo vya habari.Haki ya nani yaani basi tu
 
Lakini hata tukisema tusubiri 2010 wapiga kura ni sisi na hata kama wameronga tunawapa kura hapa sipati picha
 
huu uchafu wa mwakyembe na mwakipesile unaniudhi kweli.ngoja nakuja kugombea ubunge kyela kwa tiketi ya nanii!mizee mizima inashambuliana kwenye vyombo vya habari.Haki ya nani yaani basi tu

Mama,

Njoo tu, kama sera zako nzuri, vijana tutakupigia debe tu. Tunataka mabadiliko na wala sio hizi ngonjera za kila siku Mafisadi huku vijana wetu wanaendelea kusota kwa elimu mbovu.

Nikiona unafaa zaidi ya Mwakalinga basi nitahamia kwako, vinginevyo nitakushauri tuungane pamoja kumng'oa msanii.

Mimi nataka waje wagombea wengine wengi tu. Ila huyo msanii akisikia, jiandae kuitwa fisadi.
 
huu uchafu wa mwakyembe na mwakipesile unaniudhi kweli.ngoja nakuja kugombea ubunge kyela kwa tiketi ya nanii!mizee mizima inashambuliana kwenye vyombo vya habari.Haki ya nani yaani basi tu

Mapambano ya hwa jamaa kwenye vyombo vya habari inaeleka havina mshindi.
Mimi nataka kufadhili pambano la NDONDI KAVU KAVU kati ya Mwakyembe na Mwakipesile.
Sisi tunataka tujue nani zaidi.
Wengine kina Engineer na wapambe wa pande zote tafuteni washabiki ili mufurahishe roho zenu.
 
Mi naona mwakipesile ana chuki na Mwakyembe sababu ndie aliyemtoa katika ulaji wa Ubunge.

JK alifanya kosa la mwaka kumchagua Mwakipesile kuwa RC mbeya sababu yeye alipigwa chini na wana Kyela sasa anawakomoa wanakyela na kuhakikisha Mwakyembe nae anashindwa.

Unajuwa Mwakipesile alikuwa mbunge wa kyela for more than 15 yrs
 
Ndugu yangu,

Kama kazi za mbunge ni hizo tu unazozisema wewe, basi hatuhitaji kuwa na wabunge wa majimbo. Tuanzishe wabunge wa kuchaguliwa kufuatana na kura za chama kama zinavyofanya baadhi ya nchi.

Pesa nyingi sasa ziko kwenye halmashauri ya wilaya na hata mipango mingi ya maendeleo inaamuliwa huko na sijui kwa kazi za mbunge kama ulivyoandika, nini wajibu wa mbunge kwenye halmashauri ya wilaya yake?

Nakuhakikishia, kazi ya mbunge ni zaidi ya ulizozitaja. Maendeleo sehemu kubwa kwasasa hayaletwi na serikali peke yake. Sehemu kubwa wananchi wanachangia na Mbunge hapo ni kiungo muhimu mno.

Kazi zote anazofanya mbunge zimegawanyika katika makundi hayo matatu. Aidha ni bora kufahamu kuwa mbunge ni mjumbe wa halmashauri ya wilaya lilimo jimbo lake, na hivyo kumpatia nafasi ya 'kuisimamia serikali' vilivyo kupitia ujumbe wake katika haulashauri husika. Aidha ni bora kufahamu kuwa kama ilivyo kwa mipango ya maendeleo, majukumu yote ya mbunge hufuata sheria, ikiwa ni pamja na kuisimamia serikali. Ni pale tu sheria zinapokiukwa mbunge hui-task serikali-kuu au ya mitaa.
Ni hayo tu kwa leo.
 
Ndugu yangu,

Kama kazi za mbunge ni hizo tu unazozisema wewe, basi hatuhitaji kuwa na wabunge wa majimbo. Tuanzishe wabunge wa kuchaguliwa kufuatana na kura za chama kama zinavyofanya baadhi ya nchi.

Pesa nyingi sasa ziko kwenye halmashauri ya wilaya na hata mipango mingi ya maendeleo inaamuliwa huko na sijui kwa kazi za mbunge kama ulivyoandika, nini wajibu wa mbunge kwenye halmashauri ya wilaya yake?

Nakuhakikishia, kazi ya mbunge ni zaidi ya ulizozitaja. Maendeleo sehemu kubwa kwasasa hayaletwi na serikali peke yake. Sehemu kubwa wananchi wanachangia na Mbunge hapo ni kiungo muhimu mno.

Mkuu Halmashauri za Wilaya ndizo serikali yenyewe pamoja na serikali kuu! Hivyo inaposemwa kusimamia utendaji na utekelezaji wa kazi za serikali maana yake Halmashauri za Wilaya!
Zilizotajwa ndizo kazi za Mbunge hayo ya kujenga shule, kununua uniform n.k. kama sio serikali basi wewe ni Mfadhili/Mhisani na sio lazima uchaguliwe UBUNGE ndio uwe Mhisani/Mfadhili!
 
Nashukuru mungu ktk sakata hili la kyembe na kipesile pumba zote zimeanza taratibu kujitenga.....ndio maana hata mh jm kikwete aliwahi kusema vita dhidi ya mafisadi ni ngumu sana na haitaki papara....ugumu mmoja wapo ndio huo kwamba unavyokuwa unapigana vita hii unaweza ukajikuta unapigana hadi na baba yako mkwe.
 
mwee tubhuke nkughala ubwalwa iwikiendi jifikile bha kana nongi
 
Ili kuwa fair, ni vema Muungwana akampiga chini mwakipesile na wanakyela nao wakampiga chini huyo mwakyembe.Tumechoka kila siku kusikia kelele zisizoisha juu ya ugomvi wao ambao hauwasaidii wananchi zaidi ya kuwaacha maskini wa kutupwa.
 
Weka Pamba masikioni!
 
Hii kitu nadhani hata JK anahusika. Amebadilisha Wakuu wa Mikoa yote akamwacha Mwakipesile pale pale. Kweli Mbeya watapata Maendeleo kwa staili hii?? MC.

Ah,
Kwani RC aliwahi kuleta maendeleo gani, na wapi?
Kazi anayoifanya Mwakipesile ndiyo hasa kazi ya RC.
 
Ugomvi - Kakosana karibu na kila kiongozi Kyela
Majigambo - Anadharau madiwani hawajasoma huku anaongoza wilaya ambayo zaidi ya asilimia 99 ya wananchi wake hawajafika chuo kikuu.

Uwongo - Sisi huku tunasema NTUNGULU FIJO. Dr kuzua jambo kwake sio kitu kigumu

USANII - Ukimsikia mikutano yake utacheka. Kuna sehemu anaulizwa tatizo la barabara, anasema wacha niongee na mhandisi, anapiga simu na kujadiliana na Mhandisi kwamba aache huko anakojenga barabara, aje Kyela maana wananchi wake wanateseka. Huo kama si usanii ni nini? Hizo simu huwa anwapigia wapambe wake. Mfano huo huo anaurudia kwenye vijiji vingine akiongelea mabomba ya maji. Anasahau huko nyuma huyo mhandisi alikuwa wa barabara, sasa kageuka wa maji.

Sifa zake:
Huku wanasema NKIFU maana yake Jasiri wa kuongea
Pia alifanya kazi nzuri Richmond.

Sisi tulimbeba Dr 2005 na kusukuma gari lake, ila sasa simtaki kabisa na wala hilo sifichi. Jamaa hata kuongoza mukutano tu kunamshinda, yeye ni manguvu tu na majigambo kwamba yeye kasoma, hajui hata wengine ni Wahandisi bwana!

Hizi habari zinanishtua sana. nimewahi sikia watu wanamwita prof J. kwa hizi sifa ninahisi mwakyembe wa 2005 sio wa leo sasa ngoja nifanye utafiti na kukusanya data hapo kyela ili niprove. lakini mimi sikumsukuma kabisa. pole kwa kumsukuma. uongo ni muongo hilo siwezi kataa. kwa kunipa sifa zake ambazo ni positive na negative inabidi nifanye utafiti mpya. lakini kuna diwani hapo hata mimi silidhiki na utendaji wake wa kazi hususani wa hapo mjini. nitakuja baada ya utafiti mkubwa kidogo. maana hii imenishtua sana.
 
Mapambano ya hwa jamaa kwenye vyombo vya habari inaeleka havina mshindi.
Mimi nataka kufadhili pambano la NDONDI KAVU KAVU kati ya Mwakyembe na Mwakipesile.
Sisi tunataka tujue nani zaidi.
Wengine kina Engineer na wapambe wa pande zote tafuteni washabiki ili mufurahishe roho zenu.
Kaka Lole,

Mimi naweza kukusanya mtaa mzima kama hilo pambano litapangwa. Mtu lazima atolewe knock-out siku hiyo.

Hata mimi hawa wakubwa wamenichosha na hizi kelele zao kupitia magazetini. Wakipatanishwa wanashikana mikono, kesho yake wanaanza kugombana tena.
 
Hizi habari zinanishtua sana. nimewahi sikia watu wanamwita prof J. kwa hizi sifa ninahisi mwakyembe wa 2005 sio wa leo sasa ngoja nifanye utafiti na kukusanya data hapo kyela ili niprove. lakini mimi sikumsukuma kabisa. pole kwa kumsukuma. uongo ni muongo hilo siwezi kataa. kwa kunipa sifa zake ambazo ni positive na negative inabidi nifanye utafiti mpya. lakini kuna diwani hapo hata mimi silidhiki na utendaji wake wa kazi hususani wa hapo mjini. nitakuja baada ya utafiti mkubwa kidogo. maana hii imenishtua sana.

[/QUOTE]

We dogo
Tunasubiri utafiti wako.
 
Back
Top Bottom