Siasa za Mbeya 2005-2010

Siasa za Mbeya 2005-2010

Huyu kijana jana aliandika huu ujumbe.

Nikawa na hamu leo ya kuelewa nini ataandika leo. Leo nakuta huu ujumbe.

Yaani nikisoma hapo juu nina uhakika kabisa huyu mwaandishi ni nani. Mhandisi na wengine, huyu dogo ni mbishi kama dagaa. Hata mfanyenye hamtamuweza. Sanasana atakuja hapa kwa jina jingine na kuanza kudai mie ana/ni/wafahamu na atamwaga data zangu/zenu hapa.

Kijana anza upya. Fanya homework yako vizuri. Yaani umeshindwa hata kitu kimoja kuandika alichofanya Mwakyembe zaidi ya kuzunguka kichaka. Kama elimu na shule, hizo si shule za Lowassa?

Sitaki kukupa pressure kwa sasa. Ila data za Mwakyembe zipo na zinasubiri muda mwanana ufike. Kama Mwakyembe angelikuwa MKALI kama unavyomsema, kwa nini unahaha sasa? Hivi unafikiri kukiwa na mechi katika ya Taifa Star na Brazil, wachezaji gani hawatalala? Je kama ni final kati ya German na Argentina, nani watalala? Wapambe wa Mwakyembe msiwe na wasiwasi kama mnavyosema ni kweli kuwa Mwakyembe kafanya mengi Kyela. Yeye ni shujaa wa Taifa na Kyela ikiwa sehemu sasa kwa nini mnahema kama MJUSI aliyebanwa mlangoni? Mechi nzito siyo?
NIMEFUATILIA huyu sikonge kwenye mjadala huu na nimeona si mtu wa kyela na hafahamu lolote kuhusu kyela. kwanza katika mjadala huu sikonge ni mshabiki tu. maana ueleweki sana. kwa sasa naona uko biased au una nia ya kaaccelerate mjadala. hujui maswala mengi nafikiri muachie mhandisi niendelee naye. wewe huna jipya zaidi ya kubashiri na kukosa kuwa na mjadala wa maana. mambo yanayofanyika kyela ni mengi sana ambayo wanaoweza kuyaona ni wale wanaoifahamu kyela. lakini hawa vijana wa kuja hawajui lolote? sisi tunajadili hapa ni kwa kujua tunakwenda wapi? tuna dira inayotuongoza, tuifahamu kyela ya enzi ya shule tatu za sekondari ipinda, kyela day na itope. tunakumbuka mwakyembe alivyoleta msaada wa karabai kwa ajili ya kusomea pale itope akiwa si mbunge kipindi hicho kyela haina umeme. kabla ya hapo tulikuwa tunasomea vibatari pale itope. Bila misaada ya mwakyembe kyela mimi nisingeweza kufika hapa na kuaccess jf. pengine ningekuwa mkulima wa mpunga kyela. leo tunajua kyela imekuwa ikiwa ya pili au ya kwanza kimkoa kwa kufaulu matokeo ya darasa la saba. tunajua zawadi anazotoa kwa watoto hawa jinsi zinavyoamsha hali ya kusoma na kujisomea kwa watoto hawa. haya yote tunaongea kwa hisia tunayafahamu. sasa mpango uliopo ni kujenga shule ya advance na jitihada za kuanzisha advance pale kyela day tunaziona. huyu mtu yuko siliasi sana. jitihada za kujenga soko la kimataifa zipo wafadhili wameonyesha nia na maongezi bado yanaendelea.ni maendeleo mengi ambayo yako kwenye progress kuendelea kuyanadi hapa ni sawa na kuwapa nafasi ya kuyabeza tu. halafu umekosa kutoa mifano halisi ya kyela. kifupi umejibu juu juu mno. sasa kwa mhandisi anaonyesha uhalisia lakini si wewe.inawezekana kwamba ni kweli hajajua. lakini wewe ni mtu ambaye unapambanisha tu. hoja zako ni nyepesi mno kwa kweli ebu jaribu tena. kama hauko huko kyela na hujui lolote bora uulize kuliko kuja kichwakichwa. wengi wanataka kupata neutral point. tumesikia ya huku ebu tusikilize kote halafu tupime. mimi ninayoyaongea nayafahamu na ninashiriki kuijenga kyela. ninatoa michango na ninaona matatizo yanayokabili maendeleo ya kyela. na ninafahamu hata jitihada zinazofanywa. ukweli hata mimi kama mwakyembe angevulunda ningekuwa wa kwanza kumpinga lakini kwa sasa hakuna haja. japo mapambano yanajibiwa kwa uzito mkubwa lakini ukweli ni kuwa hata mwakyembe angekaa kimya mwakalinga hafurukuti, lakini hatujui nani yupo nyuma yake. kwa sasa inatakiwa kupambana nae bila kujali maana unaweza ukafikiri ni yeye kumbe katumwa. kama kweli huyu angekuwa na nia ya kuendeleza kyela sidhani kama angegombea kipindi hiki ambacho kinajulikana kabisa kuwa mwakyembe sasa yuko juu sana., na ndio maana kuna uwezekano mkubwa kuwa kuna watu nyuma yake. huwezi kubeza maendeleo ya mwakyembe leo katutoa mbali.
 
Mwakyembe anapotoshwa na wapambe-Mwakipesile http://www.majira.co.tz/index.php?v...esile&format=pdf&option=com_content&Itemid=57http://www.majira.co.tz/index.php?v...nt&print=1&page=&option=com_content&Itemid=57http://www.majira.co.tz/index.php?o...pbGUmb3B0aW9uPWNvbV9jb250ZW50Jkl0ZW1pZD01Nw==Wednesday, 23 September 2009 16:52 Asema hana tatizo naye, walisuluhishwa na JK
Akana kuwaomba wazee wa Mbeya wawapatanishe

Na Gladness Mboma

Majira

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Bw. John Mwakipesile amesema Mbunge wa Kyela Dkt. Harrison Mwakyembe anapotoshwa na wapambe wake kwa kumpa taarifa za uongo bila yeye kuzipima na kujua ukweli wake.

Vile vile alisema kuwa hana tatizo na mbunge huyo kwa kuwa tofauti zao zilisuluhishwa kupitia tume iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete iliyoongozwa na Bw. Abdulhman Kinana.

Bw. Mwakipesile alitoa ufafanuzi huo jana alipozungumza na gazeti ili ikiwa ni siku chache tangu Dkt. Mwakyembe adai kwenye vyombo vya habari kuwa anatishiwa kuuawa na hivyo kumfanya ashindwe kukaa kwa amani.

"Ninashangazwa sana na kauli zinazotolewa na Dkt. Mwakyembe za kudai kuwa anatishiwa maisha, mara anataka kuuawa mpaka anashindwa kukaa kwenye nyumba yake na kumfanya ahamehame, wapambe wake wanampa taarifa za uongo ambazo hazifanyii kazi," alisema.

Alisema kuwa tangu waliposuluhishwa mgogoro wao na kushikana mikono, yeye hana tatizo lolote na Dkt. Makyembe, lakini anashindwa kuelewa chochoko nyingine zinatokea wapi.

"Nimeshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni kuandika habari kuwa eti mimi niliwaomba wazee wa Mbeya watusuluhishe mimi na Dkt. Makyembe, kwa kosa gani wakati tulikwishasuluhishwa na yakaisha?" alihoji.

Alisema kuwa kauli hizo za kuuawa kwa Dkt. Mwakyembe amekuwa akizitoa kwenye mikutano kwa wapiga kura wake, taarifa ambazo anadai kuwa anapewa na wapambe wake bila ya kuzifanyia kazi.

"Mimi ndiye mtawala wa Mkoa wa Mbeya sina tatizo na Mbunge yoyote yule, nashindwa kuelewa haya mambo ya kizushi yanatoka wapi, tangu tulipopatanishwa sijawahi kuzungumza lolote kuhusu Dkt. Mwakyembe, hivyo ninashangazwa na kauli zake za mara kwa mara kuhusu kutishiwa kuuawa," alisema.

Alisema kuwa alipokutana na Baraza la Wazee mkoani Mbeya hivi karibuni walimuuliza swali kuhusiana na mgogoro wake na Dkt. Mwakyembe ambapo yeye aliwaeleza kwamba ulikwishaisha baada ya rais kuunda tume wakasamehana, lakini cha kushangaza baadhi ya vyombo vya habari viligeuza maneno na kudai kuwa mimi niliwaomba wazee watupatanishe, jambo ambalo siyo kweli.

Bw. Mwakipesile alisema kuwa hakuna mwenye muda wa kutaka kumuua Dkt. Mwakyembe kama ambavyo anadai na na kusisitiza kwamba hana tatizo lolote na yeye kama ambavyo inadaiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na kumtaka kabla ya kupokea taarifa kutoka kwa wapambe wake akae chini kwanza na kupembua taarifa hizo kabla ya kuzitoa kwa wapiga kura wake au katika vyombo vya habari.

"Muulizeni Dkt. Mwakyembe mwenyewe labda bado ana tatizo na mimi, atawaeleza, lakini mimi nasisitiza kwamba sina tatizo lolote na yeye yalikikwishasuluhishwa yakaisha," alisema.

Mgogoro kati ya Dkt. Mwakyembe na Bw. Mwakipesile umedumu kwa muda mrefu, ambapo Dkt. Mwakyembe amekuwa akidai kutishiwa maisha mara kwa mara za kutaka kuuawa na watu wasiojulikana kwa kumtumia ujumbe mfupi katika simu yake ya mkononi (MSG).

Naye Dkt. Mwamkyembe alipoulizwa juu ya mgogoro huo kati yake na Bw. Mwakipesile alidai kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari za uzushi na kumtaka mwandishi wa habari hizi ampigie simu jioni baada ya kusoma kilichoandikwa kwenye magazeti lakini alipotafutwa simu yake haikupatikana.

Mgogoro kati ya wanasiasa hao ni majeraha ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 walipokuwa wanawania uteuzi wa kugombea katika Jimbo la Kyela na Mwakyembe akaibuka mshindi.
 
NIMEFUATILIA huyu sikonge kwenye mjadala huu na nimeona si mtu wa kyela na hafahamu lolote kuhusu kyela. kwanza katika mjadala huu sikonge ni mshabiki tu. maana ueleweki sana. kwa sasa naona uko biased au una nia ya kaaccelerate mjadala. hujui maswala mengi nafikiri muachie mhandisi niendelee naye. wewe huna jipya zaidi ya kubashiri na kukosa kuwa na mjadala wa maana. mambo yanayofanyika kyela ni mengi sana ambayo wanaoweza kuyaona ni wale wanaoifahamu kyela. lakini hawa vijana wa kuja hawajui lolote? sisi tunajadili hapa ni kwa kujua tunakwenda wapi? tuna dira inayotuongoza, tuifahamu kyela ya enzi ya shule tatu za sekondari ipinda, kyela day na itope. tunakumbuka mwakyembe alivyoleta msaada wa karabai kwa ajili ya kusomea pale itope akiwa si mbunge kipindi hicho kyela haina umeme. kabla ya hapo tulikuwa tunasomea vibatari pale itope. Bila misaada ya mwakyembe kyela mimi nisingeweza kufika hapa na kuaccess jf. pengine ningekuwa mkulima wa mpunga kyela. leo tunajua kyela imekuwa ikiwa ya pili au ya kwanza kimkoa kwa kufaulu matokeo ya darasa la saba. tunajua zawadi anazotoa kwa watoto hawa jinsi zinavyoamsha hali ya kusoma na kujisomea kwa watoto hawa. haya yote tunaongea kwa hisia tunayafahamu. sasa mpango uliopo ni kujenga shule ya advance na jitihada za kuanzisha advance pale kyela day tunaziona. huyu mtu yuko siliasi sana. jitihada za kujenga soko la kimataifa zipo wafadhili wameonyesha nia na maongezi bado yanaendelea.ni maendeleo mengi ambayo yako kwenye progress kuendelea kuyanadi hapa ni sawa na kuwapa nafasi ya kuyabeza tu. halafu umekosa kutoa mifano halisi ya kyela. kifupi umejibu juu juu mno. sasa kwa mhandisi anaonyesha uhalisia lakini si wewe.inawezekana kwamba ni kweli hajajua. lakini wewe ni mtu ambaye unapambanisha tu. hoja zako ni nyepesi mno kwa kweli ebu jaribu tena. kama hauko huko kyela na hujui lolote bora uulize kuliko kuja kichwakichwa. wengi wanataka kupata neutral point. tumesikia ya huku ebu tusikilize kote halafu tupime. mimi ninayoyaongea nayafahamu na ninashiriki kuijenga kyela. ninatoa michango na ninaona matatizo yanayokabili maendeleo ya kyela. na ninafahamu hata jitihada zinazofanywa. ukweli hata mimi kama mwakyembe angevulunda ningekuwa wa kwanza kumpinga lakini kwa sasa hakuna haja. japo mapambano yanajibiwa kwa uzito mkubwa lakini ukweli ni kuwa hata mwakyembe angekaa kimya mwakalinga hafurukuti, lakini hatujui nani yupo nyuma yake. kwa sasa inatakiwa kupambana nae bila kujali maana unaweza ukafikiri ni yeye kumbe katumwa. kama kweli huyu angekuwa na nia ya kuendeleza kyela sidhani kama angegombea kipindi hiki ambacho kinajulikana kabisa kuwa mwakyembe sasa yuko juu sana., na ndio maana kuna uwezekano mkubwa kuwa kuna watu nyuma yake. huwezi kubeza maendeleo ya mwakyembe leo katutoa mbali.

Yaani kujua kuwa mie ni mtu wa Sikonge imebidi hadi uchunguze? Kwi kwi kwiiiiii. Yaani na kujiita Sikonge, bado unafanya uchunguzi kufahamu kama mie si wa Kyela? Kwani wapi nimesema mie wa Kyela? Hata Kyela kwenyewe sijawahi kufika. Ila hiyo haimaanishi kuwa sifahamu lolote kuhusu Kyela. Na wewe hata kama unatoka Kyela (nafahamu watoka Rungwe) haimaanishi unafahamu yote ya Kyela. Kama wafahamu yote hebu niambie kama mke wa Mbunge wa Kyela anavaa G-STRING au HAVAI.

Kama misaada ya Mwakyembe imesomesha mtu kama wewe, basi nampa sana hongera Mwakyembe. Mtu anayechunguza kama Sikonge anatoka Kyela? Kweli umesoma kwenye karabai ya Mwakyembe. Na kama sikosei hizo karabai alipewa na Rostam Azziz wakati wakijadili mradi wa umeme wa upepo kabla ya Rostam Azziz hajamzunguka Mwakyembe na wakagombana hadi leo.

Mwisho nilifahamu tu kuwa ukija na majibu hapa, MAJIBU YAKO YATAKUWA YAMEENDA SHULE YA KARABAI YA MWAKYEMBE.
 
AH JAMANI ETI KUNA MTU ANAROPOKA MWAKYEMBE KASOMA IJMC, mwakyembe mwanasheria jamani wa administrative law...msiwe mnaropoka kifalafala ndani hum mnashusha hadhi ya JF
 
AH JAMANI ETI KUNA MTU ANAROPOKA MWAKYEMBE KASOMA IJMC, mwakyembe mwanasheria jamani wa administrative law...msiwe mnaropoka kifalafala ndani hum mnashusha hadhi ya JF

Angalia isije ikawa wewe ndiye unayeropoka kifalafala.....pitia CV ya mwakyembe vizuri kwanza kabla ya kuanza kushutumu wenzako

omarilyas
 
AH JAMANI ETI KUNA MTU ANAROPOKA MWAKYEMBE KASOMA IJMC, mwakyembe mwanasheria jamani wa administrative law...msiwe mnaropoka kifalafala ndani hum mnashusha hadhi ya JF

Mkuu Semenya,
Upande mmoja uko sawa na upande si sawa. Inategemea unamaanisha nini. Hebu angalia hapa:

The School of Journalism and Mass Communication is a teaching , and research School of the University of Dar es Salaam. The School owes its origin to the former Tanzania School of Journalism (TSJ) which later got transformed into the Institute of Journalism and Mass Communication on 1st 2003 under the University Act, No.2 of 1972

Sasa ukiingia kwenye www ya bunge utakuta kwamba Mwakyembe amesoma (TSJ Tanzania School of Journalism - DIploma in Journalism - 1975-1977 DIPLOMA).

Hiki Chuo miaka hiyo kama ukisoma maelezo yenye rangi nyekundu hakikuwa chini ya UDSM. Hiyo imefanyika mwaka 2003. Hivyo Mwakyembe hajasomea uandishi wa habari UDSM ila TSJ.
Aliandika hivyo bwana mdogo Kasyabone Tall anayedai anamfahamu sana Mwakalinga na Mwakyembe na huku akituonyesha kuwa hafahamu chochote. Um-mezee tu kijana wetu kwani mambo mengi hayafahamu bado na au yanampiga chenga. Na utashangaa anajisifu kuwa anafahamu Mwakalinga ali-disco SUA wakati miaka hiyo hata ya 80 mwishoni, kijana alikuwa ndiyo kwanza anabadilishwa nepi.

Shule ya Mwakyembe ni hii hapa : http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcv.php?PTerm=2005-2010&vpkey=395
 
Mkuu Omarilyas, polepole. Mkuu Semenya yuko sawa kwa upande fulani.
Sawa na mimi leo siwezi kusema kwa kuwa nilisoma Mazengo basi niseme nimesoma Chuo kikuu cha Waanglican.
Kama CV ya Mwakyembe wote tumeisoma. Mwakyembe kasoma TSJ na siyo IJMC. Wakati Mwakyembe anasoma, hakikuwa chini ya UDSM.

Sasa hapa nani anaropoka Kifalafala????????

Mambo yalianzia huku na majibu yakafuata. Ndipo Semenya akaandika hivyo. Kasyabone ni MKURUPUKAJI na hapa wote waone.

Mbona huyo mbunge wako aliyekutuma uje ubwabwaje hapa alichemsha form six akaishia kwenda chuo cha uandishi wa habari badala ya UDSM? Je mafanikio yake ya elimu kwasasa tuyapuuze kwasababu tu hakufanya vizuri form six?

Tupe data katika hili hivi ni kweli kuwa Dr harison mwakyembe aliishia chuo cha uandishi wa habari badala ya UDSM? Hivi ndivyo mnavyodanganya watu huko, kwa kifupi mwakyembe amesoma chuo cha uandishi wa habari ambacho ni chuo kikuu cha dar es salaam, (IJMC). Sasa mzee hivi kuna haja ya kuendelea maana hapa inaonekana hujui hata IJMC kuwa ni sehemu ya UDSM. Uzuri wa jf ni pamoja na watu kupata elimu daka hilo halafu uwafundishe na wenzio.
Kijana kaishia yeye KUPEWA ELIMU, haya daka somo hapo juu.
 
Kasyabone,

Na wewe bora ukae kimya tu. Yaani unashindwa hata kujua Dr. Mwakyembe kasoma wapi wakati taarifa zote ziko website ya bunge?

Mwakyembe alisoma diploma TSJ kwanza kabla ya kuingia UDSM kwenda kusoma bachelor. Wakati huo TSJ ilikuwa chuo kidogo sawa tu na vyuo vingi vingine vya diploma wala haikuwa chini ya UDSM kama unavyodanganya hapa.

Naona hata kujadiliana na wewe ni kupoteza muda kama alivyosema Sikonge maana inaelekea hata uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana.

Kyela yenyewe huijui na wala hutoki Kyela na ndio maana hata hoja zako zinayumba.
 
Kazi ipo hapa nilijua wengi wale wa kukurupuka watakuja kama mlivyokuja sikonge (mzee wa kubashiri). mhandisi wa kule kyela wote si makosa bali ndio kufikiri huko. kuna jamaa kaja vizuri na citation lakini kaja kuhalibu mwishoni sana wakati anaconclude. sasa TSJ ukiongelea wakati huu ni IJMC ambacho kipo chini ya UDSM. sasa ningesema TSJ iko chini ya UDSM hapo ningekuwa nimekosea. SAsa hata kusema IJMC iko chini Ya UDSM bado haieleweki?
Wakati huo hakukuwa na chuo kinachotoa degree ya uandishi wa habari. kwa wakati huo TSJ ndio kulikuwa chuo kikubwa cha uandishi wa habari. sasa ingekuwa leo huyu mtu anayetaka kusomea uandishi wa habari basi angesoma IJMC ambayo ndio chuo kinachotoa elimu ya ngazi ya juu kwa uandishi wa habari hapa tanzania. sasa kufikiri ni muhimu, wakati mwingine kulinganisha nyakati.
unapoongelea TSJ inategemea unaongelea wakati gani.(nasisitiza).LEO hio TSJ haipo ni historia wakati huu ukiongelea TSJ basi UNAongelea IJMC nafikiri hapo mmenipata. NILItegemea kupata majibu makubwa sasa mtu unasoma halafu unaoverlook ni kustiki hapo. nafikiri kwa sasa hoja zimekwisha.
kama utasema KUwa TSJ ilikuwa sawa na vyuo vidogo tu kwa wakati huo, hapo unakosea. hiki wakati huo kilikuwa ndio chuo kinachotoa ngazi kubwa ya elimu ya uandishi wa habari tanzania. sasa hapo kama bado mjanipata basi kunajitihada za kueleweshana vizuri. Singonge unayejifanya mkubwa sana hupo? na wewe inginia upo?
 
Wewe dogo acha kudanganya watu hapa. Soma ujumbe wako wa jana na ghafla leo umebadilika kama Kinyonga na kuandika kitu tofauti.

Kuwa mwandishi wa habari sio lazima usomee chuo cha uandishi wa habari. Angalia hata waandishi wa habari wengi wa maana TZ wala hawakusoma chuo cha uandishi wa habari.

Pia Mwakyembe kusoma TSJ ilikuwa njia ya kwenda chuo kikuuu na wala sio kwasababu alitaka kuwa mwandishi wa habari.

Watu wote ambao walikuwa hawawi na points za kutosha kuingia chuo kikuu moja kwa moja walikuwa wanatumia njia hiyo. Wala hakuna ubaya kwenye hilo, ila nilitaka kukuonyesha tu kwamba kwa mfano mtu kutokufaulu vizuri form six haina maana hata mafanikio yake ya mbele yadhalauliwe.

Wewe soma tu shule yako na acha kupoteza muda wako kujadili mambo ambayo hata huyajui.
Kazi ipo hapa nilijua wengi wale wa kukurupuka watakuja kama mlivyokuja sikonge (mzee wa kubashiri). mhandisi wa kule kyela wote si makosa bali ndio kufikiri huko. kuna jamaa kaja vizuri na citation lakini kaja kuhalibu mwishoni sana wakati anaconclude. sasa TSJ ukiongelea wakati huu ni IJMC ambacho kipo chini ya UDSM. sasa ningesema TSJ iko chini ya UDSM hapo ningekuwa nimekosea. SAsa hata kusema IJMC iko chini Ya UDSM bado haieleweki?
Wakati huo hakukuwa na chuo kinachotoa degree ya uandishi wa habari. kwa wakati huo TSJ ndio kulikuwa chuo kikubwa cha uandishi wa habari. sasa ingekuwa leo huyu mtu anayetaka kusomea uandishi wa habari basi angesoma IJMC ambayo ndio chuo kinachotoa elimu ya ngazi ya juu kwa uandishi wa habari hapa tanzania. sasa kufikiri ni muhimu, wakati mwingine kulinganisha nyakati.
unapoongelea TSJ inategemea unaongelea wakati gani.(nasisitiza).LEO hio TSJ haipo ni historia wakati huu ukiongelea TSJ basi UNAongelea IJMC nafikiri hapo mmenipata. NILItegemea kupata majibu makubwa sasa mtu unasoma halafu unaoverlook ni kustiki hapo. nafikiri kwa sasa hoja zimekwisha.
 
Mwakyembe awa mbogo
Atoboa siri ya ugomvi wake na Mwakipesile
Adai kiongozi huyo anafanya kazi ya mafisadi
Ataka atambue kwamba yeye ni RC na siyo MC

Na Gladness Mboma

MBUNGE wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa tatizo analoliona kati yake na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. John Mwakipesile ni harakati zake za kutaka kumng'oa katika jimbo la Kyela, jambo ambalo hataweza.

Alisema kuwa kazi anayoifanya Bw. Mwakipesile katika jimbo lake ni sawa na kuuza kofia za polisi ambazo hazinunuliki na kwamba anajisumbua, anajidhalilisha na kujifedhehesha licha ya kutumwa na mafisadi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Dkt. Mwakyembe alitoa kauli hizo za kejeli alipozungumza na gazeti hili kujibu hoja za Bw. Mwakipesile kuwa mbunge huyo anapotoshwa na wapambe wake wanaompa taarifa za uongo na kwamba hajawahi kuwaomba wazee wa Mbeya ili wawapatanishe.

"Ni lazima Bw. Mwakipesile atambue kuwa yeye ni RC na siyo MC kwa maana ya msema chochote. Mkuu wa mkoa mmoja kati ya wakuu wa mikoa 21 kuzungumza magazetini kila siku akiwarukia wabunge wanaopambana na ufisadi ni dalili ya kuweweseka.

"Ninalazimika kusema kuwa mwenzetu anahitaji ushauri nasaha, waandishi mchunguzeni Bw. Mwakipesile ili kujua anapatana na mbunge gani mkoani Mbeya?" alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe aliongeza kuwa, kila mtu anatambua kuwa Bw. Mwakipesile anashinda Kyela kufanya kampeni za kuhakikisha kuwa, anamuondoa mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu na kwamba Serikali inatambua jambo hilo.

"Hili tatizo halinipi tabu hata kidogo kwa sababu kazi anayofanya ni kama kuuza kofia za polisi mali ambazo hazinunuliki anajisumbua, anajidhalilisha na kujifedhehesha," alisema.

Dkt. Mwakyembe alisema kuwa alipata kura asilimia 93 katika uchaguzi mkuu mwaka 2005, lakini anashangazwa na kauli aliyoitoa Bw. Mwakipesile katika gazeti hili kwamba wapambe ndio wanaompotosha na kumtaka atambue kuwa wapambe hao ni wananchi wote wa Kyela.

"Tatizo la Bw. Mwakipesile anadanganywa sana na mafisadi ambao wanamtumia kama wakala, hiyo kazi waliyompa kwa Kyela ni ngumu kwelikweli, ni sawa na kuuza kofia za polisi kwa wananchi hivyo ni lazima atambue kuwa mimi ni mti mkavu usiochimbwa dawa," alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Alisema kuwa yeye alikuwa nje ya nchi na amerudi juzi ndipo alipomkuta mwenzake akiongea hovyo katika vyombo vya habari huku akitoa malalamiko kwamba yeye ndiye anayekwamisha maendeleo ya Mkoa wa Mbeya.

Alipoulizwa kiini cha mgogoro kati yake na Bw. Mwakipesile unasababishwa na nini, Dkt. Mwakyembe alisema kuwa yeye hana mgogoro wowote na mkuu huyo wa mkoa, bali yeye RC huyo anayekwamisha maendeleo ya mkoa huo kutokana na muda wote kukaa Kyela kwa lengo la kumwondoa mbunge mwaka 2010.

Akizungumzia madai ya kutaka kuuawa alisema kuwa huo ni uongo na kwamba anaokoteza maneno barabarani na kuyafanyia kazi.
 
Nyani haoni kundule, kama Mwakipesile hapatikani na mbunge yeyote wa mkoa wa Mbeya, je yeye Dr. Mwakyembe mbona na yeye hapatani na diwani yeyote wa wilaya ya Kyela? Mbona hapatani na kiongozi yetyote wa CCM wa wilaya ya Kyela. Hawa jamaa wote wawili wanaturudisha nyuma shauri ya ujinga wao usio na mwisho.

Baada ya kuitangazia dunia yote kwamba alitaka kuuwa, sasa anaanza kuruka na kusema ni uwongo? Amejua polisi wamegundua nini na anaanza kujiandaa kabla ya report. Kama ni uongo kwanini alienda kununua kisu na kuwapa wapambe ili wakitumie kama ushahidi wa kutaka kuuwa kwa kisu? Mbona alitumia magazeti ya MENGI kuitangazia dunia nzima kwamba alitaka kuuwa?
 
Hii kitu nadhani hata JK anahusika. Amebadilisha Wakuu wa Mikoa yote akamwacha Mwakipesile pale pale. Kweli Mbeya watapata Maendeleo kwa staili hii?? MC.
 
Hii issue nadhani hata JK anahusika, amebadilisha Wakuu wote wa Mikoa lakini Mwakipesile akamwacha pale pale. Kweli Mbeya watapata maendeleo?
 
Dkt. Mwakyembe alisema kuwa alipata kura asilimia 93 katika uchaguzi mkuu mwaka 2005.

Wanasiasa kwa propaganda ndio wenyewe. Dr. Mwakyembe alipata asilimia 93 pale aliposhindanishwa ni kivuli kwasababu hakukuwa na upinzani Kyela kwenye uchaguzi mkuu.

Ushindani ulikuwa kwenye uchaguzi wa CCM ambako yeye alishinda kwa asilimia zaidi kidogo ya 50.

Yeyote ambaye angeshinda kutokea CCM, angeweza kupata asilimia nyingi kwenye uchaguzi mkuu.

It doesn't matter really kama umeshinda kwa asilimia 50 au asilimia 100. Muhimu ni ushindi, nashangaa anaporudia mara nyingi hiyo ya ushindi wa asilimia 93 huku anajua ukweli kwamba hata CCM wangemsimamisha kichaa kwa Kyela bado angeshinda kwa asilimia kubwa kwa mwaka 2005.

Ndio yale yale ya akina Saddam kushinda kwa asilimia 99.
 
Wewe dogo acha kudanganya watu hapa. Soma ujumbe wako wa jana na ghafla leo umebadilika kama Kinyonga na kuandika kitu tofauti.

Kuwa mwandishi wa habari sio lazima usomee chuo cha uandishi wa habari. Angalia hata waandishi wa habari wengi wa maana TZ wala hawakusoma chuo cha uandishi wa habari.

Pia Mwakyembe kusoma TSJ ilikuwa njia ya kwenda chuo kikuuu na wala sio kwasababu alitaka kuwa mwandishi wa habari.

Watu wote ambao walikuwa hawawi na points za kutosha kuingia chuo kikuu moja kwa moja walikuwa wanatumia njia hiyo. Wala hakuna ubaya kwenye hilo, ila nilitaka kukuonyesha tu kwamba kwa mfano mtu kutokufaulu vizuri form six haina maana hata mafanikio yake ya mbele yadhalauliwe.

Wewe soma tu shule yako na acha kupoteza muda wako kujadili mambo ambayo hata huyajui.
mwakyembe amesoma chuo cha uandishi wa habari ambacho ni chuo kikuu cha dar es salaam, (IJMC). hii ndio kauli yangu ya jana. labda nianze na kiswahili kilichotumika.
amesoma kitenzi kinachoonyesha wakali uliopo timilifu.
 
Nyani haoni kundule, kama Mwakipesile hapatikani na mbunge yeyote wa mkoa wa Mbeya, je yeye Dr. Mwakyembe mbona na yeye hapatani na diwani yeyote wa wilaya ya Kyela? Mbona hapatani na kiongozi yetyote wa CCM wa wilaya ya Kyela. Hawa jamaa wote wawili wanaturudisha nyuma shauri ya ujinga wao usio na mwisho.
QUOTE]

Dr. anasema 2005 alipata 93% inamaana hata hao madiwani walimpigia kura!

Dr. huyu ni Mbunge wa Taifa siyo Kyera pekee watu wa Mbeya sijui kwanini hawaelewi.
 
hizi post za wanakyela na mwakyembe zimenikumbusha wimbo wa sikunyingi wa bongofleva uliimbwa na GWM[gangstars with matatizo] ulikokuwa unasema''kila kukicha kwa visavisa duhh''hivi majimbo mengine kuko shwari au kwakuwa hakuna waandishi wa habari?au huyu mwakyembe ni tishio sana mpaka watu wanakosa usingizi au yeye ndiye anaenyimwa usingizi na mgombea anaemuona ni kiboko yake?

kwanini kyela tuuuuuuuu?????
 
Hii issue nadhani hata JK anahusika, amebadilisha Wakuu wote wa Mikoa lakini Mwakipesile akamwacha pale pale. Kweli Mbeya watapata maendeleo?

Hivi RC anaweza kukwamisha maendeleo ya wilaya yanayoletwa na mbunge?

Labda Dr. Mwakyembe atuambie kwamba alitaka kujenga shule hii lakini RC akakwamisha, au alitaka kujenga kituo cha afya na RC akakwamisha.

Mwakyembe anatoa madai yake hewani tu bila kutaja mahali alipokwamishwa. Ni sawa na avyotoa madai ya ufisadi hewani bila kutoa nushahidi wowote.

Aige mfano wa Dr. Slaa ambaye anawataja mafisadi kwa majina na kutoa ushahidi. Pia pamoja na kwamba ni CHADEMA lakini anafanikisha maendeleo wilayani kwake bila kulalamika na karuhusu hata mkewe awe diwani wa CCM.

Hilo la Dr. kusema alitaka kuuwa naona kafulia kweli. Kuna ushahidi tosha kwamba alihusika kupanga hilo tukio la kutaka kuuwa huku akijua wazi kwamba ilikuwa ni uwongo. Polisi wanapogundua ukweli anaanza kukana.

Hapa Kyela mambo hayatakuwa salama mpaka 2010 ufike.
 
Back
Top Bottom