bambumbile
Senior Member
- Aug 30, 2009
- 109
- 0
hizi post za wanakyela na mwakyembe zimenikumbusha wimbo wa sikunyingi wa bongofleva uliimbwa na GWM[gangstars with matatizo] ulikokuwa unasema''kila kukicha kwa visavisa duhh''hivi majimbo mengine kuko shwari au kwakuwa hakuna waandishi wa habari?au huyu mwakyembe ni tishio sana mpaka watu wanakosa usingizi au yeye ndiye anaenyimwa usingizi na mgombea anaemuona ni kiboko yake?
kwanini kyela tuuuuuuuu?????
Tatizo la Kyela ni waandishi wa habari wa MENGI na hasa huyo Mwanakatwe ambaye anashinda na Dr. Mwakyembe kila siku na kuandika kila aina ya upuuzi kiasi cha kufanya watu wengi wafikirie Kyela kuna vurugu au hakukaliki. Ukweli ni kwamba kama mbunge hayupo jimboni, Kyela inakuwa imetulia na kuendelea na shughuli zake.
Ukichunguza habari nyingi kutoka magazetini hapa JF ni zile zinazotka upande wa Mwakyembe.
Ni kweli Mwakipesile naye ana matatizo yake lakini mbona hatuoni habari magazetini za prof. Mwandosya au Mwakyusa wakilalamika?
Yule mbunge wa Mbeya mjini ana upinzani mkubwa kutoka kwa mtoto wa Mwang'onda ambaye unaweza kabisa kusema anaungwa mkono na mafisadi, lakini mbona hatuoni akilia lia kila siku gazetini?
Tatizo ninaloliona mimi Kyela ni kwamba Dr. Mwakyembe aliwekeza muda wake mwingi kwenye siasa za kitaifa na kusahau kabisa matatizo ya jimboni kwake. Wajanja wameona huo mwanya na wamemkamata pabaya; sasa anatumia kila njia kujiokoa hata kuzua madai ambayo mpaka mtu unajiuliza hivi kuna tatizo gani?