Janeth Rithe: Siku ya Mtoto wa Kike, Ukatili kwa Wasichana ni Kikwazo

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Siku ya mtoto wa kike, ukatili dhidi ya wasichana ni kikwazo

Leo ni siku ya Kimataifa ya mtoto wa kike Duniani, siku hii ilianzishwa mahususi katika kutambua haki na changamoto wanazopitia watoto wa kike. Hapa nchini Tanzania tunaona bado watoto wa kike wanakabiliwa na changamoto nyingi sana ambazo zinakwamisha ustawi na maendeleo yao.

Changamoto kubwa zinazowakabili watoto wa kike ni kukithiri kwa matukio ya ukatili dhidi yao, kama vile ubakaji, ulawiti na udhalilishaji wa mitandaoni. Vilevile wanakabiliwa na changamoto ya ndoa za utotoni pamoja na mimba za utotoni. Aidha, kutokuwepo kwa mazingira salama shuleni kwa mtoto wa kike kama vile kukosa vifaa vya kujisitiri (taulo za hedhi) na sheria za zinazozuia waathirika wa mimba kuendelea na masomo. Kuendelea kuwepo kwa changamoto hizi kunazuia fursa kwa watoto wa kike kupata haki zao na kutimiza malengo yao katika jamii.

Katika kuadhimisha siku hii, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kuongeza jitihada kwa kuchukua hatua zifuatazo;​
  • Serikali isimamie kupunguza muda wa uendeshaji wa kesi za ukatili dhidi ya watoto na wanawake. Tunataka zipunguzwe hadi kufikia miezi isiozidi miwili kumalizika kwa kesi.​
  • Kuunganisha nguvu katika kupiga vita ndoa za utotoni, mila za ukeketaji na mimba za utotoni.​
  • Serikali iongeze usalama na stadi za maisha kwa watoto mashuleni kwa kupanua na kuanzisha mabaraza ya watoto, klabu za watoto na kwa upekee kabisa kutoa bure vifaa vya kujistiri na hedhi kwa wasichana.​
  • Tunatoa wito kwa Serikali kuboresha madawati ya watoto ili kukomesha ukatili dhidi ya watoto.​
Mwisho, ukatili dhidi ya watoto wa kike bado upo katika jamii zetu. Athari zake za kijamii, kiuchumi na hata kiafya ni kubwa sana. Vilevile, ukatili unapalilia kukosekana kwa usawa katika upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii baina ya mtoto wa kike na wa kiume.
Imetolewa na;
Ndg. Janeth Joel Rithe
Waziri kivuli wa Ustawi na Maendeleo ya Jamaii, wanawake na watoto
ACT Wazalendo.
11 Oktoba 2023.
 
Back
Top Bottom