Nguvu za kumfanya mtoto wako awe mtu bora zipo kwako

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
Wazazi daima tuna jukumu kubwa sana la kusisitiza maadili kwa kubwa kwa watoto wao hawa katika kipindi wanapokua na kuchunguza ulimwengu unaowazunguka, lakini lengo la msingi linaweza kuwa sio hilo bali ni kuwatengenezea msingi mzuri wa Maisha hapo mbeleni hata tukiwa hatupo karibu yao.

Ingawa kufundisha maadili kama upendo, uaminifu au heshima inaweza kuoneakana ni kazi rahisi sana kwa mtoto mdogo, ila ni suala zito sana endapo mzazi am mlezi asipokuwa makini. Masomo haya yanaweza kufundishwa hatua kwa hatua kupitia nyakati ndogo lakini kwa kuwa na umakini mkubwa sana kwa mtoto wako.

Usije kuruhusu mtu mwingine akulele mtoto Watoto, hata kama mtoto yupo shule ya bweni basi jiwekee mazingira Rafiki ya kujua mtoto wako amekula nini, na anaishi namna gani kila siku akiwa shuleni, usiwe busy hata siku moja kwa mtoto wako.

Acha kufuata mkumbo wa kuwaiga baadhi ya marafiki zako wa karibu na baadhi ya wanafamilia ambao wamefanya Maisha ya watoto wao wa bweni kuwa mikononi mwa walimu na walezi tu.
1702478057996.png

Nikifikiria haya yote, nilitaka mtoto wangu awe na Upendo na Uhuru wa kujieleza, najiuliza je kweli shule anapata nafasi ya kujifunza yote haya, ama ndo kukariri kuwa Periodic Table ina elements ngapi?

Sina nia mbaya ya kupondea mfumo wa elimu ila je elimu malezi ipo shuleni kweli au ndo Kuchapa kitabu mwanzo mwisho? Mnaweza kutazama tofauti kati ya mtoto aliyekulia bweni na kutwa, nadhani mtaona utofauti mkubwa sana.

Ni jukumu la mzazi na mlezi kumlea mtoto ukweli ndo huo ila kila mzazi na mlezi ana mtindo wake wa kipekee wa malezi ambao unaweza kutegemea mambo kadhaa, mitindo inatofautiana kwenye misingi ya lugha, mawasiliano, makatazo na mengine ambayo yote yanaweza kumjenga mtoto ama kumbomoa kabsa, lakini licha ya tofauti hizi, kuna mambo machache muhimu ambayo mimi na wewe kama wazazi na walezi tunaweza kukubaliana.

Kama kweli, unataka mtoto wenye maadili bora: haswa katika kuendeleza misingi iliyo bora zaidi kwa watoto wako katika nyanja mbalimbali za ukuaji, ikiwa ni pamoja na ustawi wa kiakili wa mtoto wako.​

Mambo nane ya kuwafundisha watoto wako kabla hawajafikisha miaka 18

1. Shukrani:
Mioyo iliojaa shukrani inaendelea kuwa adimu katika ulimwengu huu. Biblia imeonesha wazi kuhusu shukrani, unaweza kusoma vifungu hivi, Luka 17:11-19, pamoja na Wathesalonike wa kwanza 5: 16-18, kwa Waislamu wao wanaelekezwa kupitia kitabu kitakatifu cha Quran, 16:114 pamoja na 34:15. Tuwafundishe sana Watoto wetu kuwa na mioyo ya shukrani, tuwafundishe kushukuru kabla na baada ya kula chakula, kiwe kingi ama kidogo, shukrani ni muhimu sana.
1702477247598.png
Utajisikiaje kama ukimpa zawadi mtoto wa chekechea na kukimbia mbio ndefu bila hata kukushukuru? Utajisikia vibaya ila akikupa asante, utajisikia vizuri sana.

Ni mara ngapi umewahi kupewa shukrani ukiwa kazini au kwenye sehemu ya biashara yako? Wengine hata neno asante ni adimu masikioni mwenu.

Haigharimu mtu hata senti kutoa neon la shukrani ukipata bidhaa au huduma lakini inatoa tabasamu kwenye uso wa mt una ukifanya hivyo mbele ya Watoto wako inawapatia Imani kuwa ni jambo jema kutoa shukrani kwa watu.

Kutoa shukrani na kuthamini ni matokeo makubwa zaidi unayoweza kumzawadia mtu! Kuwa mkarimu katika kufanya hivyo, hii ndiyo jambo kubwa zaidi ninalotaka mtoto wangu akue nalo Maishani mwake.

"Shukrani inaweza kubadilisha siku za kawaida kuwa za shukrani, kugeuza kazi za kawaida kuwa furaha, na kubadilisha fursa za kawaida kuwa baraka" - William Arthur Ward.

2. Adabu:

Ni jambo la ajabu ila ndo ukweli kuwa hali ya kuwa na adabu inatoa hali ya utulivu katika maisha ya mtu. Kuzungumza kwa staha na adabu hata ukiwana hasira kunampatia mtoto uwezo wa kuishi katika fikra hizo pia, kukaa kwa adabu na utulivu sio suala ya kuzungumza tu bali ni suala ya vitendo kamili.

Daima itawahimiza watu kuwa na mwelekeo zaidi kwako na kila wakati utakuwa na watu wazuri kando katika kila awamu ya maisha. Kuwa na tabia njema hazigharimu chochote, na wala haimfanyi mtu aonekane mnyonge.

1702477305598.png

Ni jambo la kipekee sana na ni busara ambayo pengine tunakumbuka kufundishwa tukiwa watoto, na wale ambao sasa ni wazazi huenda wanatkiwa kuwa wameanza kuwafundisha watoto wao.

Tuwafundishe Watoto wetu kuishi na dhana kama vile kusema tafadhali naomba jambo Fulani au asante kwa zawadi hii, nimeipenda sana, kusikiliza kwa makini bila kumkatisha mtu kauli, na kutazamana macho na watu wakiwa kwenye mazungumzo.

3. Ushirikiano:
Buddha aliwahi kusema kuwa - "Maelfu ya mishumaa inaweza kuwashwa kutoka kwa mshumaa mmoja, na maisha ya mshumaa hayatafupishwa. Furaha yako haipungui kamwe kwa kumpatia mwingine furaha”.

Nimekuwa nikishangaa wakati nikitazama suala la "Kushiriki" kwa watu. Mtoto wangu anamiliki vitu vyake binafsi na mara nyingi hataki vishikwe na mtu yeyote, haswa na watoto wa rika lake na wakati mwingine hata ndugu zake, utasikia mdoli wangu huu sitaki ashikwe. Niliona kwamba watoto wengi katika umri huu mdogo hawaoni umuhimu wa kushirikiana.

Ni jambo la ajabu ila ndo hatari kubwa ambayo hata mtaani nilipata kuiona, kunatokea msiba basi wanapuliza pembe na kuwaomba vijana wote twende kuandaa nyumba ya milele ya marehemu, ila ajabu ni kwamba ushiriki wa vijana unakuwa ni mdogo kuliko kipimo cha vijana wanaoishi kwenye eneo husika. Mtaa wenye vijana zaidi ya 30 sio ajabu kukutana na vijana watano tu makaburini.
1702477354799.png

Mtoto hawezi kamwe kufanya kile anachofundishwa mara moja tu, na wengine wanatazama kile ambacho jamii inafanya, sio suala la kushangaa kuona mtoto akikataa kushiriki jambo Fulani na kuweka kabsa neon kuwa “Mbona kaka Fulani huwa hafanyi kwanini mnaniambia mimi?

Nilichojifunza ni kwamba, sifa na ishara nzuri zinahitaji kuelezwa kwao mara kwa mara, pamoja na uzoefu wa vitendo, kwa kuwaonyesha jinsi ushirikiano una umuhimu wake, taratibu wanapoona wanajifunza na kuingiza sifa hizi katika maisha yao.

4. Upendo:
Ndiyo, kila mtoto anatakiwa kuwa na upendo kwa marafiki zake, familia, wanyama na kila kitu katika ulimwengu huu. Lakini hili sio suala jepesi hata kidogo kwa upande wa vitendo kwani hata mimi siwezi kuwa na upendo kwa wote, lakini basi, kutoka moyoni, ninajaribu kumfundisha kuwa mtu mwenye upendo kwa wote.

Kutakuwa na matukio fulani yasiyofaa, lakini badala ya kuiumiza akili ndani yake na kuhisi mipango hasi, kwa nini asiyaache hapo na kuelekeza nguvu zako katika kitu cha ubunifu na chenye ubora kiakili.
1702477412463.png

Wazazi wote wanatamani furaha iwe ndani ya watoto wao kwa kuwaongoza, wakati mwingine wazazi huwa na tabia ya kusahau jambo muhimu zaidi ambalo linahitaji kutolewa kwa watoto ni kuwaonesha upendo kuonesha vitendo vya upendo, ni ngumu sana kwa mtoto kuelewa somo hili kama nyumba ya wazazi wake ni ukanda wa Bakhmut katika mgogoro wa Urusi na Ukraine, aoneshe upendo kwa kuwapenda wanafamilia wako, na wao watajifunza upendo.

Upendo huwasaidia sana watoto kujihisi salama bila kujali mafanikio gani, moja kwa moja jambo hili huwajengea katika kujiamini na kujithamini.

5. Uwajibikaji:
Uwajibikaji ni thamani muhimu kwa mtoto kujifunza kutoka kwa wazazi na walezi, kuwajibika huweka matarajio ya namna anavyopaswa kutenda katika maisha yao ya kila siku, ukiwa karibu n ahata ukiwa mbali.

Ni muhimu sana watoto kujua kabla ya kutenda jambo lolote kuwa kuna sheria ambazo wanavunja, na kutakuwa na matokeo, Uwajibikaji hukita mizizi yake katika uhusiano wa mzazi na mtoto, mzazi na mlezi ajenge utayari wa kuwa na maadili ya kuwafundisha watoto kuhusu matarajio ya mema na mabaya baada ya kutenda jambo fulani.
1702477476887.png

Kuwajibika kwa watoto ni zawadi watakayoishi nayo katika maisha yao yote, hata ukiwa haupo karibu yao, wakiwa wanajitegemea mbali na wewe, au wakiwa na familia zao mbeleni.

Ni suala mtambuka linaloanza na kazi za nyumbani, tengeneza mazingira Rafiki ya watoto kushiriki katika kazi za nyumbani wakiwa na umri mdogo, unaweza kumsaidia kufua nguo zake ila ukampatia vitambaa vyepesi na kibeseni chake pamoja na sabuni kisha mpe nafasi aone namna ya kufanya kazi kwa kukutazama wewe.

Siku nyingine mpatie vivyo hivyo na uondoke ukae pembeni utazame maendeleo yake, mfundishe kutandika kitanda akiwa bado mtoto. Youtube ni nzuri sana ila haina mafunzo yote ya kumjenga mtoto kuwa mwajibikaji bora katika familia na jamii yake mbeleni.

6. Udadisi:
Wazazi wengi wanaweza kuthibitisha kwamba kuwa karibu na mtoto kuanzia akiwa na na umri wa miaka 4 na kuendelea, ni kawaida watoto wao huanza kuuliza maswali makubwa ya "kwa nini".

Nakumbuka mtoto wangu aliwahi kuniuliza “Eti Baba kwanini kila siku tunakula chakula, tena mara mara tatu, asubuhi, mchana, na usiku? Nilishangaa sana udadisi wake, Ingawa wengine huwa na maswali magumu sana kama, "Kwa nini anga lina rangi ya bluu?"

Watoto wengine wanaweza kuwa na mitazamo mikali mapema sana kutokana na mazingira yao mfano kuwa na falsafa, kama vile, “Kwa nini watu huchukiana?” ama “Kwanini Mungu haonekani?”

Tukiwa kama wazazi na walezi ni vyema kufahamu kuwa udadisi ni sehemu muhimu ya kuelewa maadili kikamilifu zaidi na kuwa na utayari wa kufahamu zaidi.

Mtengenezee mtoto wako mazingira ya kuwa mdadisi kwenye vitu vya msingi, mpe nafasi na mazingira ya kudadisi mambo makubwa, sio lazma awe kama Akrit Jaswal, au Jacob Barnett.
1702477516926.png

Jamii yetu inaweza kuwa na familia bora zenye wazazi na watoto ambao wanaweza kutafakari maswali muhimu ya maisha pamoja, kuzungumza lugha moja ya kidadisi, familia ambazo zinaweza kuleta mapinduzi ya kifikra ndani ya jamii.

Mwaka jana nilitembelea kituo cha Watoto Yatma Mkoani Iringa cha Amani Senta, na mtoto mmoja wa darasa la Tatu aliniuliza swali la msingi na lenye udadisi, “Sisi tuna shida kubwa ya Maji ya kunywa na kutumia kwa ajili ya kufua nguo zetu, tunaomba mtusaidie tuwe tunachukua maji ya mvua yanayopotea kila wati, je mnaweza kutusaidia?”

Swali hili liliwaacha watu hoi, tuliona huyu mtoto ni kichwa aisee! Anawezaje kuongea hivi tena akiwa darasa la tatu.
1702477851091.png

Tulijichanga siku hiyo tukanunua bomba kubwa za plastiki na mtoto yule alitupatia malekezo kama vile mkandarasi kiasi kwamba tulimbatiza jina la Engineer.

Nasisitiza kwamba wewe na mtoto wako mnaweza kujifunza mengi kwa kuleta udadisi kwenye meza, kwani unaweza kutoa mtazamo kulingana na uzoefu wako wa maisha, ilhali wanaweza kuona mambo kwa njia iliyo wazi na ya kufikiria zaidi, mpe mtoto nafasi na muda wako wa kuzungumza na wewe.

7. Heshima:
Kujifunza heshima ni thamani muhimu sana ya kumlea mtoto wako akiwa nyumbani. Inahusiana kwa karibu na mazoea kama vile kungoja zamu yake endapo mtu anazungumza na kufuata maelekezo ya mtu mzma.

Heshima inaweza kumtia sana moyo mtoto haswa akiwa anavyosikilizwa kwa hamu maoni anayoyaleta kwako. Wakati swali, "Tunafikiri nini tunatokea tumepochukiana?", kama ni familia yenye misingi ya dini basi msaidie mtoto kupata vifungu vya vitabu husika aidha Biblia ama Quran na mfundishe namna ya kuelezea kwa utaratibu na heshima.

1702477622483.png

Wazazi wote wanataka watoto wao wawe na maadili fulani, lakini ngoja nikwambie kuwa ni muhimu pia kwa watoto kujifunza jinsi ya kuheshimu wale wanaoona ulimwengu kwa njia tofauti kidogo.

Usimlazimishe aamini tu kile ambacho unaona ni sahihi na adharau kile ambacho sio sahihi, kama mtoto amelelewa kwenye msingi wa Kikristo basi ajue kuwa na heshima kwa Imani zote bila taizo vivyo hivyo kwa Imani zingine.

Mfundishe namna ya kutazama na kuzuru ulimwengu pasipo kukariri njia moja tu, na usisahau kumfundisha umuhimu wa kuzingatia kwamba unaweza kuwa na maoni yenye nguvu sana na bado unaweza kukubali kwamba mtu anaweza kuiona kwa njia tofauti sana, na njia yao ya kuiona inaweza pia kuwa ya thamani.

8. Huruma:
Uwezo wa mtoto kuelewa na kuunganishwa na hisia za mtu mwingine husaidia kujenga msingi wa mahusiano imara katika maisha yao. Ndio maana huruma mara nyingi ndio dhamana kuu kwa familia.

Mfundishe kusikitika anapotazama jambo lenye huzuni na asijizuie kuonesha huzuni, mfanye mtoto aelewe kuwa huruma sio udhaifu bali ni kitendo chema cha kuvaa viatu vya mtu mwingine na kufikiria jinsi maisha yanavyoweza kuwa kutoka kwa mtazamo wao, na inajumuisha pia hali zao za kimwili na mazingira pamoja na ulimwengu wao wa ndani wa mawazo, hisia, imani, na tamaa.
1702477711823.png

Uwezo wa kuhurumia hutusaidia kuwa na hamu ya kutaka kujua zaidi kuhusu watu wengine, je wanachofikiri na kuhisi nini, kile wanachopambana nacho na kukitamani, ni nn kinachowakatisha tamaa na kuwatia moyo.

Na kadiri tunavyozidi kuwa na udadisi zaidi kuhusu watu hawa, ndivyo tutakavyojifunza zaidi kuhusu kile wanachotaka hasa na kile kinachowatia motisha, ambayo nayo hutusaidia kutoa suluhisho bora wakati wa matatizo.
1702477737968.png

Hatimaye, kazi ya kufundisha mtoto wako maadili inakuwa ndogo sana ikiwa unaiona kama lengo linaloendelea, ila kama utaliona ni jambo la kumuachia mwalimu basi ni mzigo mkubwa sana.

Mtoto wako ni jukumu lako, Kumbuka atika uzao wa mtoto wako, adiha mjukuu wako ama Kitukuu wako kuna mmoja wao atarithi tabia na mienendo yako.

Amua ni maadili gani ambayo ni muhimu zaidi kumpa mtoto wako. Kisha, tafuta njia za kufundisha na kuzitia nguvu katika maisha yako ya kila siku. Kwa mazoezi ya kutosha, sifa, na kutiwa moyo, maadili ya familia yako yapo kwenye mikono yako mwenyewe.​

Siku Njema Wanajukwaa! Naomba Kuwasilisha
 
Asante kwa Bandiko refu lenye Elimu ndani yake.

UPO SAHIHI MKUU.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Ni kweli kabisa kizazi cha sasa hakina malezi mazuri jukumu limeachwa kwa mwalim, hata wazazi walio wengi muda wa kuwakalisha chini watoto wawaonye au kuwafundisha hayo hawana!

Zamani mtoto alikuwa wa jamii yote hasa inayomzunguka kwa sasa ni jukumu la mzazi au mlezi usishangae kusikia mzazi anakiri kabisa kuwa mtoto amemshinda tabia na mtoto ukimtizama hata 12 years hana.

Niliwahi kwenda msiba sehem 1 Mwanza inaitwa nyashana, vijana wadogo tu let’s say 15-19 years wanakemewa na mwenyekiti kuhusu tabia ya udokozi waiache wafanye kazi wakawa wasema huyu tuanze nae na mbaya zaidi anasema anawafaham hadi makwao.

Wazazi nao wakasema tusaidiwe watoto wana vichwa vigum eti kuna 1 majuzi alimpiga mam’ake kisa hajaachiwa chakula duh! Mwanangu kabisa?

Kwa ujumla niseme hata hizi haki sijui za watoto haki za wanawake zinachangia kuvuruga maadili kwenye jamii zetu!

Tupunguze kupenda watoto kupita kiasi tunashindwa hata kuwakanya, mtoto akichukia eti mzazi ndo anajishusha kum-please (shenzi sana)

Niliona gari 1 limeandikwa
“toto baya zuri kwa mama”
Akina mama acheni kujikosha kwa watoto kwa kuwafichia makosa na kutowaambia ukweli pindi wakikosea, mwisho wa siku mzazi wa kiume ndo unamrushia lawama we uonekano ni mzuri kwa mtoto!

Mwisho niombe wazazi tuwe wakali pindi mtoto akija nyumbani na kitu ambacho unajua kabisa uwezo wake wa kukikipata sio rahisi hivyo (nimeokota/nimepewa)
Huo ndo mwanzo wa udokozi, unyang’anyi ukibaka na mwisho anakuwa jambazi sugu!

Mithali 10:1

Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.

Kwetu ukiwa na tabia mbovu tunasema kapeleka tabia ya ujombani ila ikiwa nzuri basi karithi kwa baba (jokes)

Luka 2:52

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Kiukweli inapendeza unapoambiwa mtoto/watoto wa flani wana tabia nzuri, yaani unatamani na wako wasemwe hivyo

Sio yale mambo ya junior anauliza mgeni umekuja kula kwetu? Yale ni malezi mabovu sio mtoto mtundu kemea kabisa wala hatarudia hilo jambo!

Be blessed tafadhali tufanye iliyo sehem yetu!
 
Wazazi daima tuna jukumu kubwa sana la kusisitiza maadili kwa kubwa kwa watoto wao hawa katika kipindi wanapokua na kuchunguza ulimwengu unaowazunguka, lakini lengo la msingi linaweza kuwa sio hilo bali ni kuwatengenezea msingi mzuri wa Maisha hapo mbeleni hata tukiwa hatupo karibu yao.

Ingawa kufundisha maadili kama upendo, uaminifu au heshima inaweza kuoneakana ni kazi rahisi sana kwa mtoto mdogo, ila ni suala zito sana endapo mzazi am mlezi asipokuwa makini. Masomo haya yanaweza kufundishwa hatua kwa hatua kupitia nyakati ndogo lakini kwa kuwa na umakini mkubwa sana kwa mtoto wako.

Usije kuruhusu mtu mwingine akulele mtoto Watoto, hata kama mtoto yupo shule ya bweni basi jiwekee mazingira Rafiki ya kujua mtoto wako amekula nini, na anaishi namna gani kila siku akiwa shuleni, usiwe busy hata siku moja kwa mtoto wako.

Acha kufuata mkumbo wa kuwaiga baadhi ya marafiki zako wa karibu na baadhi ya wanafamilia ambao wamefanya Maisha ya watoto wao wa bweni kuwa mikononi mwa walimu na walezi tu.

Nikifikiria haya yote, nilitaka mtoto wangu awe na Upendo na Uhuru wa kujieleza, najiuliza je kweli shule anapata nafasi ya kujifunza yote haya, ama ndo kukariri kuwa Periodic Table ina elements ngapi?

Sina nia mbaya ya kupondea mfumo wa elimu ila je elimu malezi ipo shuleni kweli au ndo Kuchapa kitabu mwanzo mwisho? Mnaweza kutazama tofauti kati ya mtoto aliyekulia bweni na kutwa, nadhani mtaona utofauti mkubwa sana.

Ni jukumu la mzazi na mlezi kumlea mtoto ukweli ndo huo ila kila mzazi na mlezi ana mtindo wake wa kipekee wa malezi ambao unaweza kutegemea mambo kadhaa, mitindo inatofautiana kwenye misingi ya lugha, mawasiliano, makatazo na mengine ambayo yote yanaweza kumjenga mtoto ama kumbomoa kabsa, lakini licha ya tofauti hizi, kuna mambo machache muhimu ambayo mimi na wewe kama wazazi na walezi tunaweza kukubaliana.

Kama kweli, unataka mtoto wenye maadili bora: haswa katika kuendeleza misingi iliyo bora zaidi kwa watoto wako katika nyanja mbalimbali za ukuaji, ikiwa ni pamoja na ustawi wa kiakili wa mtoto wako.​

Mambo nane ya kuwafundisha watoto wako kabla hawajafikisha miaka 18

1. Shukrani:
Mioyo iliojaa shukrani inaendelea kuwa adimu katika ulimwengu huu. Biblia imeonesha wazi kuhusu shukrani, unaweza kusoma vifungu hivi, Luka 17:11-19, pamoja na Wathesalonike wa kwanza 5: 16-18, kwa Waislamu wao wanaelekezwa kupitia kitabu kitakatifu cha Quran, 16:114 pamoja na 34:15. Tuwafundishe sana Watoto wetu kuwa na mioyo ya shukrani, tuwafundishe kushukuru kabla na baada ya kula chakula, kiwe kingi ama kidogo, shukrani ni muhimu sana.
Utajisikiaje kama ukimpa zawadi mtoto wa chekechea na kukimbia mbio ndefu bila hata kukushukuru? Utajisikia vibaya ila akikupa asante, utajisikia vizuri sana.

Ni mara ngapi umewahi kupewa shukrani ukiwa kazini au kwenye sehemu ya biashara yako? Wengine hata neno asante ni adimu masikioni mwenu.

Haigharimu mtu hata senti kutoa neon la shukrani ukipata bidhaa au huduma lakini inatoa tabasamu kwenye uso wa mt una ukifanya hivyo mbele ya Watoto wako inawapatia Imani kuwa ni jambo jema kutoa shukrani kwa watu.

Kutoa shukrani na kuthamini ni matokeo makubwa zaidi unayoweza kumzawadia mtu! Kuwa mkarimu katika kufanya hivyo, hii ndiyo jambo kubwa zaidi ninalotaka mtoto wangu akue nalo Maishani mwake.

"Shukrani inaweza kubadilisha siku za kawaida kuwa za shukrani, kugeuza kazi za kawaida kuwa furaha, na kubadilisha fursa za kawaida kuwa baraka" - William Arthur Ward.

2. Adabu:

Ni jambo la ajabu ila ndo ukweli kuwa hali ya kuwa na adabu inatoa hali ya utulivu katika maisha ya mtu. Kuzungumza kwa staha na adabu hata ukiwana hasira kunampatia mtoto uwezo wa kuishi katika fikra hizo pia, kukaa kwa adabu na utulivu sio suala ya kuzungumza tu bali ni suala ya vitendo kamili.

Daima itawahimiza watu kuwa na mwelekeo zaidi kwako na kila wakati utakuwa na watu wazuri kando katika kila awamu ya maisha. Kuwa na tabia njema hazigharimu chochote, na wala haimfanyi mtu aonekane mnyonge.

View attachment 2841529

Ni jambo la kipekee sana na ni busara ambayo pengine tunakumbuka kufundishwa tukiwa watoto, na wale ambao sasa ni wazazi huenda wanatkiwa kuwa wameanza kuwafundisha watoto wao.

Tuwafundishe Watoto wetu kuishi na dhana kama vile kusema tafadhali naomba jambo Fulani au asante kwa zawadi hii, nimeipenda sana, kusikiliza kwa makini bila kumkatisha mtu kauli, na kutazamana macho na watu wakiwa kwenye mazungumzo.

3. Ushirikiano:
Buddha aliwahi kusema kuwa - "Maelfu ya mishumaa inaweza kuwashwa kutoka kwa mshumaa mmoja, na maisha ya mshumaa hayatafupishwa. Furaha yako haipungui kamwe kwa kumpatia mwingine furaha”.

Nimekuwa nikishangaa wakati nikitazama suala la "Kushiriki" kwa watu. Mtoto wangu anamiliki vitu vyake binafsi na mara nyingi hataki vishikwe na mtu yeyote, haswa na watoto wa rika lake na wakati mwingine hata ndugu zake, utasikia mdoli wangu huu sitaki ashikwe. Niliona kwamba watoto wengi katika umri huu mdogo hawaoni umuhimu wa kushirikiana.

Ni jambo la ajabu ila ndo hatari kubwa ambayo hata mtaani nilipata kuiona, kunatokea msiba basi wanapuliza pembe na kuwaomba vijana wote twende kuandaa nyumba ya milele ya marehemu, ila ajabu ni kwamba ushiriki wa vijana unakuwa ni mdogo kuliko kipimo cha vijana wanaoishi kwenye eneo husika. Mtaa wenye vijana zaidi ya 30 sio ajabu kukutana na vijana watano tu makaburini.

Mtoto hawezi kamwe kufanya kile anachofundishwa mara moja tu, na wengine wanatazama kile ambacho jamii inafanya, sio suala la kushangaa kuona mtoto akikataa kushiriki jambo Fulani na kuweka kabsa neon kuwa “Mbona kaka Fulani huwa hafanyi kwanini mnaniambia mimi?

Nilichojifunza ni kwamba, sifa na ishara nzuri zinahitaji kuelezwa kwao mara kwa mara, pamoja na uzoefu wa vitendo, kwa kuwaonyesha jinsi ushirikiano una umuhimu wake, taratibu wanapoona wanajifunza na kuingiza sifa hizi katika maisha yao.

4. Upendo:
Ndiyo, kila mtoto anatakiwa kuwa na upendo kwa marafiki zake, familia, wanyama na kila kitu katika ulimwengu huu. Lakini hili sio suala jepesi hata kidogo kwa upande wa vitendo kwani hata mimi siwezi kuwa na upendo kwa wote, lakini basi, kutoka moyoni, ninajaribu kumfundisha kuwa mtu mwenye upendo kwa wote.

Kutakuwa na matukio fulani yasiyofaa, lakini badala ya kuiumiza akili ndani yake na kuhisi mipango hasi, kwa nini asiyaache hapo na kuelekeza nguvu zako katika kitu cha ubunifu na chenye ubora kiakili.

Wazazi wote wanatamani furaha iwe ndani ya watoto wao kwa kuwaongoza, wakati mwingine wazazi huwa na tabia ya kusahau jambo muhimu zaidi ambalo linahitaji kutolewa kwa watoto ni kuwaonesha upendo kuonesha vitendo vya upendo, ni ngumu sana kwa mtoto kuelewa somo hili kama nyumba ya wazazi wake ni ukanda wa Bakhmut katika mgogoro wa Urusi na Ukraine, aoneshe upendo kwa kuwapenda wanafamilia wako, na wao watajifunza upendo.

Upendo huwasaidia sana watoto kujihisi salama bila kujali mafanikio gani, moja kwa moja jambo hili huwajengea katika kujiamini na kujithamini.

5. Uwajibikaji:
Uwajibikaji ni thamani muhimu kwa mtoto kujifunza kutoka kwa wazazi na walezi, kuwajibika huweka matarajio ya namna anavyopaswa kutenda katika maisha yao ya kila siku, ukiwa karibu n ahata ukiwa mbali.

Ni muhimu sana watoto kujua kabla ya kutenda jambo lolote kuwa kuna sheria ambazo wanavunja, na kutakuwa na matokeo, Uwajibikaji hukita mizizi yake katika uhusiano wa mzazi na mtoto, mzazi na mlezi ajenge utayari wa kuwa na maadili ya kuwafundisha watoto kuhusu matarajio ya mema na mabaya baada ya kutenda jambo fulani.

Kuwajibika kwa watoto ni zawadi watakayoishi nayo katika maisha yao yote, hata ukiwa haupo karibu yao, wakiwa wanajitegemea mbali na wewe, au wakiwa na familia zao mbeleni.

Ni suala mtambuka linaloanza na kazi za nyumbani, tengeneza mazingira Rafiki ya watoto kushiriki katika kazi za nyumbani wakiwa na umri mdogo, unaweza kumsaidia kufua nguo zake ila ukampatia vitambaa vyepesi na kibeseni chake pamoja na sabuni kisha mpe nafasi aone namna ya kufanya kazi kwa kukutazama wewe.

Siku nyingine mpatie vivyo hivyo na uondoke ukae pembeni utazame maendeleo yake, mfundishe kutandika kitanda akiwa bado mtoto. Youtube ni nzuri sana ila haina mafunzo yote ya kumjenga mtoto kuwa mwajibikaji bora katika familia na jamii yake mbeleni.

6. Udadisi:
Wazazi wengi wanaweza kuthibitisha kwamba kuwa karibu na mtoto kuanzia akiwa na na umri wa miaka 4 na kuendelea, ni kawaida watoto wao huanza kuuliza maswali makubwa ya "kwa nini".

Nakumbuka mtoto wangu aliwahi kuniuliza “Eti Baba kwanini kila siku tunakula chakula, tena mara mara tatu, asubuhi, mchana, na usiku? Nilishangaa sana udadisi wake, Ingawa wengine huwa na maswali magumu sana kama, "Kwa nini anga lina rangi ya bluu?"

Watoto wengine wanaweza kuwa na mitazamo mikali mapema sana kutokana na mazingira yao mfano kuwa na falsafa, kama vile, “Kwa nini watu huchukiana?” ama “Kwanini Mungu haonekani?”

Tukiwa kama wazazi na walezi ni vyema kufahamu kuwa udadisi ni sehemu muhimu ya kuelewa maadili kikamilifu zaidi na kuwa na utayari wa kufahamu zaidi.

Mtengenezee mtoto wako mazingira ya kuwa mdadisi kwenye vitu vya msingi, mpe nafasi na mazingira ya kudadisi mambo makubwa, sio lazma awe kama Akrit Jaswal, au Jacob Barnett.

Jamii yetu inaweza kuwa na familia bora zenye wazazi na watoto ambao wanaweza kutafakari maswali muhimu ya maisha pamoja, kuzungumza lugha moja ya kidadisi, familia ambazo zinaweza kuleta mapinduzi ya kifikra ndani ya jamii.

Mwaka jana nilitembelea kituo cha Watoto Yatma Mkoani Iringa cha Amani Senta, na mtoto mmoja wa darasa la Tatu aliniuliza swali la msingi na lenye udadisi, “Sisi tuna shida kubwa ya Maji ya kunywa na kutumia kwa ajili ya kufua nguo zetu, tunaomba mtusaidie tuwe tunachukua maji ya mvua yanayopotea kila wati, je mnaweza kutusaidia?”

Swali hili liliwaacha watu hoi, tuliona huyu mtoto ni kichwa aisee! Anawezaje kuongea hivi tena akiwa darasa la tatu.

Tulijichanga siku hiyo tukanunua bomba kubwa za plastiki na mtoto yule alitupatia malekezo kama vile mkandarasi kiasi kwamba tulimbatiza jina la Engineer.

Nasisitiza kwamba wewe na mtoto wako mnaweza kujifunza mengi kwa kuleta udadisi kwenye meza, kwani unaweza kutoa mtazamo kulingana na uzoefu wako wa maisha, ilhali wanaweza kuona mambo kwa njia iliyo wazi na ya kufikiria zaidi, mpe mtoto nafasi na muda wako wa kuzungumza na wewe.

7. Heshima:
Kujifunza heshima ni thamani muhimu sana ya kumlea mtoto wako akiwa nyumbani. Inahusiana kwa karibu na mazoea kama vile kungoja zamu yake endapo mtu anazungumza na kufuata maelekezo ya mtu mzma.

Heshima inaweza kumtia sana moyo mtoto haswa akiwa anavyosikilizwa kwa hamu maoni anayoyaleta kwako. Wakati swali, "Tunafikiri nini tunatokea tumepochukiana?", kama ni familia yenye misingi ya dini basi msaidie mtoto kupata vifungu vya vitabu husika aidha Biblia ama Quran na mfundishe namna ya kuelezea kwa utaratibu na heshima.

View attachment 2841548

Wazazi wote wanataka watoto wao wawe na maadili fulani, lakini ngoja nikwambie kuwa ni muhimu pia kwa watoto kujifunza jinsi ya kuheshimu wale wanaoona ulimwengu kwa njia tofauti kidogo.

Usimlazimishe aamini tu kile ambacho unaona ni sahihi na adharau kile ambacho sio sahihi, kama mtoto amelelewa kwenye msingi wa Kikristo basi ajue kuwa na heshima kwa Imani zote bila taizo vivyo hivyo kwa Imani zingine.

Mfundishe namna ya kutazama na kuzuru ulimwengu pasipo kukariri njia moja tu, na usisahau kumfundisha umuhimu wa kuzingatia kwamba unaweza kuwa na maoni yenye nguvu sana na bado unaweza kukubali kwamba mtu anaweza kuiona kwa njia tofauti sana, na njia yao ya kuiona inaweza pia kuwa ya thamani.

8. Huruma:
Uwezo wa mtoto kuelewa na kuunganishwa na hisia za mtu mwingine husaidia kujenga msingi wa mahusiano imara katika maisha yao. Ndio maana huruma mara nyingi ndio dhamana kuu kwa familia.

Mfundishe kusikitika anapotazama jambo lenye huzuni na asijizuie kuonesha huzuni, mfanye mtoto aelewe kuwa huruma sio udhaifu bali ni kitendo chema cha kuvaa viatu vya mtu mwingine na kufikiria jinsi maisha yanavyoweza kuwa kutoka kwa mtazamo wao, na inajumuisha pia hali zao za kimwili na mazingira pamoja na ulimwengu wao wa ndani wa mawazo, hisia, imani, na tamaa.
View attachment 2841550

Uwezo wa kuhurumia hutusaidia kuwa na hamu ya kutaka kujua zaidi kuhusu watu wengine, je wanachofikiri na kuhisi nini, kile wanachopambana nacho na kukitamani, ni nn kinachowakatisha tamaa na kuwatia moyo.

Na kadiri tunavyozidi kuwa na udadisi zaidi kuhusu watu hawa, ndivyo tutakavyojifunza zaidi kuhusu kile wanachotaka hasa na kile kinachowatia motisha, ambayo nayo hutusaidia kutoa suluhisho bora wakati wa matatizo.
View attachment 2841553

Hatimaye, kazi ya kufundisha mtoto wako maadili inakuwa ndogo sana ikiwa unaiona kama lengo linaloendelea, ila kama utaliona ni jambo la kumuachia mwalimu basi ni mzigo mkubwa sana.

Mtoto wako ni jukumu lako, Kumbuka atika uzao wa mtoto wako, adiha mjukuu wako ama Kitukuu wako kuna mmoja wao atarithi tabia na mienendo yako.

Amua ni maadili gani ambayo ni muhimu zaidi kumpa mtoto wako. Kisha, tafuta njia za kufundisha na kuzitia nguvu katika maisha yako ya kila siku. Kwa mazoezi ya kutosha, sifa, na kutiwa moyo, maadili ya familia yako yapo kwenye mikono yako mwenyewe.​

Siku Njema Wanajukwaa! Naomba Kuwasilisha
Asante sana kwa elimu hii ya malezi ya mtoto
 
Back
Top Bottom