Shibuda out

Shibuda out

Chama cha peoples power hicho. Teh teh teh, hata uchaguzi wa vijana mwaka ule ulishindikana hii kamati ikakaa ikawatimua akina Kafulila, pia hata kwenye uchaguzi wa mwenyekiti taifa haukuwezekana mpaka hii kamati ilipomwengua zitto kwa kumshinikiza ajitoe. Peoples powder

Hahahaaa..Mkuu umesahau Sofia Simba alitukanana na kutaka kupigana na Mama Kahama kwenye kinyang'anyiro cha Uenyekiti UWT?
na unataka kusema uamuzi uliomhalalisha Masauni agombee Uenyekiti UVCCM haukuwa na misingi ya zengwe?
Au unadhani Nape alienguliwa kihalali?
Fanya analysis vizuri wewe
 
Hicho chama cha peoples power kinasitaajabisha sana, kwanza katiba yake bora katiba iliyopo inayopingwa hata sijui mandati ya kudai katiba mpya wanaitoa wapi?

Katiba gani hiyo inayotumika, watu wa shinyanga wamechagua kiongozi wao, harafu kiongozi wa watu wa shinyanga anakataliwa na kakikundi ka wahuni wachache.

Makamu Mwenyekiti enzi hizo (CHACHA) amechaguliwa na wanachama wengi wa Taifa zima eti kakikundi haka ka wahuni kanaamuwa kuwaamulia wananchi wote. Kakikundi haka kana nguvu za AJABU. Harafu, wakitoka hapo watakwambia nguvu za rais ni kubwa, watakwambia peoples power. THIS IS CRAZY.


Na tena watakwambia maamuzi ya bunge ama bunge siyo sahihi maana yanalinda interest ya wahuni wachache. Na tena watakwenda mbali kuhubiria kwamba bunge lisiamue hoja ipelekwe kwa wananchi ikapigiwe kura. Well, na haka ka group ka thugs , the so called kamati kwanini kasipeleke hoja kwa wananchi husika wakaamue mwakilishi wao? Watanganyika nani aliyewaloga?

Kama Baraza Kuu la Chadema Mkoa litakubaliana na maamuzi haya nitawaona hawanazo, hii sio demokrasia kwa viwango vyovyote na maamuzi kama haya hayapaswi kuendelea kuvumiliwa, kamati kuu ya Chadema iliyojaa wateuliwa wa Mwenyekiti ina nguvu kupita kiasi na inatumika kama chombo cha kuwashughulikia wote wanaopingana na status guo ndani ya chama.

Ilianza kwa Chacha Wangwe, ikaja kwa walioshinda Uchaguzi wa Vijana, ikaendelea kwenye uchaguzi wa kuchagua Wabunge wa Viti Maalumu, Sasa Shibuda na kama hatua stahili hazitachukuliwa list itaendelea to infinity, tunaulea ugonjwa mbaya sana na ambao ni hatari kwa taifa kama Chadema itaingia madarakani kama ilivyo sasa!!

Can you imagine ingekuwa vipi kama former Spika Sitta na Mwakyembe wangekuwa Chadema hii na kutofautiana na chama kama walivyofanya kwenye issue ya Richmond ndani ya CCM?wangeshughulikiwa zamani...!! Nasharia kuwa Chadema inaendeshwa kidikteta kuliko ata chama kikongwe cha CCM, tutauonaje mbadala katika mazingira haya?

Ni Heri CCM walishinda kwenye uchaguzi wa 2010 kwa sababu nasharia ingekuwa ni disaster kwa nchi.
 
Sidhani,
Anagombea uenyekiti wakati magazeti yalisha anza kukosana na maoni yake juu ya Tanesco. Na siamini kama hayo mambo yake ni suala la CDM ni suala la wa-TZ wote walivyoona anavyoelekea kugeuza msimamo juu ya mambo ambayo yalishaeleweka kwamba ni ufisadi ndani ya Tanesco.

Lakini hata hivyo si bora CDM kuliko CCM walioweka 'wanted' kwa yeyote atakayegombea nafasi ya Urais against Kikwete? AU!

BTW; Huyu Mkama /Mukama, katibu wa CCM ni nduguyo? Mbona leo alikaa high table wakati ni sherehe za Wafanyakazi? tena akiwa na jezi ya CCM au hajafahamu mipaka ya wadhifa wake? Nieleweshe kana unaweza.

Ndivyo hivyo,
Kwanza ilianza kula kwa CHACHA baada ya kutaka kuuwania uenyekiti, wakasitisha kwa mda zoezi la uchaguzi walipolileta baada ya CHACHA kuwa kishatoweka wakafanya uchaguzi wakiamini hatatokea mpinzani mara gafra bin vuu Zitto, tangu hapo inakula kwa Zitto. Jaribu kuidanganya akili tu kwamba walianza kabla. Ofcoz ukisema walianza kabla kwenye kipindi cha kampeni hiyo ya kuchukua fomu na kujitoa nitakuelewa.

Mukama na Mkama ni majina mawili tofauti na hata kama kwani una unataka kujenga hoja gani?
 
Hahahaaa..Mkuu umesahau Sofia Simba alitukanana na kutaka kupigana na Mama Kahama kwenye kinyang'anyiro cha Uenyekiti UWT?
na unataka kusema uamuzi uliomhalalisha Masauni agombee Uenyekiti UVCCM haukuwa na misingi ya zengwe?
Au unadhani Nape alienguliwa kihalali?
Fanya analysis vizuri wewe

Kwahiyo na ninyi mnafanya kama ccm sio?
 
wacha habari zako ww,tangu lini zitto ukamfananisha na Dk Slaa??Dk Slaa is next level,ni sawa kifo na usingizi,vision ya Dk Slaa ni infinite. Nadhani U-premium member wako unaniti shaka na usikupe kibri cha Kuhadaa watu hapa jamvini,na ndio maana hujawahi kugongewa thanx hata moja hapa tangu ujiunge,sijui upo kwenye mlengo gani kifikra na kama unamuhusudu zitto hizo ni za kwako na si za jamvi...ebooo!!
hiyo ni kwako wewe sio kwa kila mtu.
 
Nchi hii hakuna chama bali mikusanyiko ya wasaka tonge tu!! Haya jioneeni. CCM wanaparurana na kuvuana magamba huku CHADEMA wanataka kupigana. Mimi ni mshabiki wa LEMA kama LEMA ila si Chama lakini sasa naanza kujiuliza juu ya ukomavu wake kisiasa manane kauli zake zimekuwa za ngumi mbele!!

Ah! Huyo jamaa waovyo sana, wala hajuwi anachofanya ilimradi yeye aseme tu.
 
Vandugu zangu, yatokeayo hapana budi yawe ili kuibua kasoro ndogo ndogo zilizofichika ziweze kufanyiwa kazi. Chadema kinahitaji kukua si kwa kuongeza wanachama tu ila kimuundo systematically ili mfumo wake uweze kuleta ufanisi katika jitihada za kujijenga kuchukua dola. Viongozi ni binadamu ambao wangali na silika na madhaifu, yatokeayo ni kama mirrow itakayowasaidia walipo matongotongo wayaonayo waweze kujisafisha.

Zitto ana kasoro zake, lakini kamati ya maadili ilishawahi kumwita na kumsikia au kumwonya kutokana na yale wanayoona anafanya yasiyofaa kwa chama? Kwa vile hakuna utaratibu kama huo ndio maana Zitto anaendelea na hamsini zake na wale wanaochoshwa na tabia hiyo wanaamua kumtolea uvivu vikaoni na hii inawafumbua macho viongozi.

Misuguano kama hiyo ni yakawaida ila ustaarabu utangulizwe ili kunusuru amani na utulivu ndani ya chama. Mwenye kujali maamuzi ya vikao ni mtume na anania njema ya kujenga chama, na mwenye kupendelea maamuzi ya papo kwa papo bila vikao ni kasoro inayohitaji kufanyiwa kazi, na itakuja siku wataelewa na kutoleana uvivu kwa kujenga umoja wenye nguvu ndani ya Chama.

Kasoro tuzionazo tuziweke wazi ili kuwasaidia maana kushabikia kila kitu kama mtu huna akili timamu vile ni utumwa wa kifikra.

Ningeshauri Chadema wawe na tume ya maadili ya Chama, kama wanayo ni vema na kama bado hawana basi waiunde mara moja. Na tume hiyo iwe huru kupokea maoni ya wapenzi kutokana na wengi kuonekana kufurahishwa na kasi yao. Hilo nalisema kwa vile kuna wengi wanatoa maoni mazuri kuhusu Chadema lakini ni nani anayeratibu maoni hayo? Haiwezekani maoni ya watu yamfikie kiongozi binafsi na kufanyia kazi, ila kuwe na utaratibu mzuri wa kuratibu maoni ya wetu hapo chama kitapata mawazo mengi mazuri ya kujijenga.
 
Mhhhhhh.........

jk%2Bna%2Bkijana%2Bwake.JPG
 
Katiba ya chadema inasemaje? http://www.chadema.or.tz/nyaraka/katiba_2006.pdf

6.3.5 Kuziba Nafasi Wazi za Uongozi
(a) Kamati ya Utendaji ya kila ngazi au Baraza Kuu itaziba kwa muda nafasi yoyote ya
kiongozi aliyechaguliwa na mkutano mkuu wa ngazi husika.
(b) Nafasi wazi za uongozi walioteuliwa zitazibwa na vikao husika kwa kufanya uteuzi
mpya katika muda usiozidi miezi mitatu tangu nafasi kuwa wazi.
(c) Muda wa uongozi wa muda kwa mujibu wa kifungu 6.3.5 (b) hautazidi mwaka
mmoja.
(d) Bila kujali sharti la kifungu 6.3.5 (c) hakutafanyika uchaguzi rasmi wa kuziba
nafasi kama kumebakia miezi sita tu au chini ya hapo kabla ya uchaguzi mkuu wa
kawaida wa Chama unaofuata kufanyika.
 
Katiba ya chadema inasemaje? http://www.chadema.or.tz/nyaraka/katiba_2006.pdf

6.3.5 Kuziba Nafasi Wazi za Uongozi
(a) Kamati ya Utendaji ya kila ngazi au Baraza Kuu itaziba kwa muda nafasi yoyote ya
kiongozi aliyechaguliwa na mkutano mkuu wa ngazi husika.
(b) Nafasi wazi za uongozi walioteuliwa zitazibwa na vikao husika kwa kufanya uteuzi
mpya katika muda usiozidi miezi mitatu tangu nafasi kuwa wazi.
(c) Muda wa uongozi wa muda kwa mujibu wa kifungu 6.3.5 (b) hautazidi mwaka
mmoja.
(d) Bila kujali sharti la kifungu 6.3.5 (c) hakutafanyika uchaguzi rasmi wa kuziba
nafasi kama kumebakia miezi sita tu au chini ya hapo kabla ya uchaguzi mkuu wa
kawaida wa Chama unaofuata kufanyika.

Kama hivyo ndivyo,then Baraza Kuu la Chadema Shinyanga limekosea nini hapa kumteua Kaimu Mwenyekiti?

BARAZA Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Shinyanga limemteua Bw. John Magale Shibuda kuwa mwenyekiti wa muda wa mkoa.

Akitangaza uamuzi huo, Katibu wa Mkoa wa CHADEMA, Bw. Nyangaki Shilungushela alisema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha dharura kilichofanyika juzi jioni.

Bw. Shilungushela alisema, wajumbe wa baraza la mkoa waliketi katika kikao cha dharura na kumteua Bw. Shibuda kuwa mwenyekiti wa muda wa mkoa huo mpaka pale uchaguzi wa kujaza nafasi yake utakapofanyika.

"Mbali ya kumteua Bw. Shibuda kuwa mwenyekiti wa muda wa mkoa, lakini pia wajumbe wa baraza kuu la mkoa walimpendekeza kuwa mlezi wa mkoa wa Shinyanga, na atakaimu nafasi ya uenyekiti mpaka pale utakapofanyika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi iliyoachwa na Bw. Shelembi," alieleza Bw. Shilungushela.
 
Ujumbe wako unachonganisha watu, wabunge, na wana CDM!! hoja haikukaa vizuri. Ungeishia kusema kuwa Kamati kuu imemuengua shibuda na kumuweka fulani kwa sababu fulani; badala ya kuleta malumbano ya vikaoni ambayo hayana tija na hayaendani na hitimisho la hoja yako uliyoleta. Kwa msingi huo, naiona hoja yako imekaa kimajungu majungu tu NA INALENGO LA KUBOMOA CDM!!!

huja tenda haki kwa kujaribu kumshawishi mwandishi afiche mengine!!!!
hivi ingekuwa ni habari inayomuhusu JK na EL ungetoa huo ushawishi?!!!!
forum hii haina chama kwa hiyo maoni yatolewe kwa uwazi bila kuegemea upande wowote!
shibuda ni tatizo tangu siku ile alipojitoa kwenye kinyang'anyiro cha urais!!! mara nyingi mimi hushawishika kuamini kuwa JS katumwa kukisambaratisha chicho chama!!
 
Ujumbe wako unachonganisha watu, wabunge, na wana CDM!! hoja haikukaa vizuri. Ungeishia kusema kuwa Kamati kuu imemuengua shibuda na kumuweka fulani kwa sababu fulani; badala ya kuleta malumbano ya vikaoni ambayo hayana tija na hayaendani na hitimisho la hoja yako uliyoleta. Kwa msingi huo, naiona hoja yako imekaa kimajungu majungu tu NA INALENGO LA KUBOMOA CDM!!!

mwandishi kaweka wazi ili tujue kilichojili kule kikaoni siyo mpaka asubiri siku lema azipige na zitto ndio aanze kuelezea chanzo cha ugomvi wao, kuanzia leo tayari namjua Lema kama si mtu mwema kwa mbunge wangu zitto.asante kwa kutujuza.
 
Niliwahi kusema kuna siku mtakuja tafuta refenrece JF.Jiulize Lema ana cheo gani kitaifa ?.Zitto ni naibu katibu mkuu sauti yake ni sauti ya CHADEMA kitaifa Lema ni mbunge wa Arusha tu naomba kujuzwa na kusahihishwa kama ana wadhifa mwingine zaidiya ubunge?. Lema kaikuta CHADEMA imara baada ya kazi nzuri na kubwa iliyofanywa na Zitto na Dr Slaa.



Mkuu tusije kuwasingizia CCM siku mambo yakienda kombo !.



Mkuu umesahau chama chetu hakifanyi makosa.

kwa wasiomjua Zitto watasema anafanya kazi nzito.alipoanzaa alikuwa kijana mzsuri sana.lakini ulimbukeni umemponza sana,amepoteza sifa zote na hiyo ni kawaida.wanadamu huwa hatuhesabu wema wa mtu bali mabaya mangapi amefanya.kijana huyu amejaa hila kuanzia kichwani mpaka kwenye unyayo.alinikera sana alipouza mkoa wa kigoma kwa NCCr huku akiwadanganya wenzake wa chadema,usiku anafanya yake.
 
wacha habari zako ww,tangu lini zitto ukamfananisha na Dk Slaa??Dk Slaa is next level,ni sawa kifo na usingizi,vision ya Dk Slaa ni infinite. Nadhani U-premium member wako unaniti shaka na usikupe kibri cha Kuhadaa watu hapa jamvini,na ndio maana hujawahi kugongewa thanx hata moja hapa tangu ujiunge,sijui upo kwenye mlengo gani kifikra na kama unamuhusudu zitto hizo ni za kwako na si za jamvi...ebooo!!

Hiko cheo si hela yako tu, hata ukichangia BUKU unakuwa Premier Member!
 
Mi nimefurahi, na nimeipenda kama mnaweza kukaa, kuelezana ukweli, kukosoana ni vizuri kuliko mmekaa kwenye kikao mnakazi ya kusema ndiyo ndiyo alafu mkitoka nje muanza kusema fulani sijui fulani.
ni safi kupeana challenge then mnatafuta conclusion na ndio unakuwa msimamo wa chama nje na ndani ya chama.
 
huyu zitto kama kafanya hivyo ni laana tupu hafai kabisa tusilee litakuwa donda ndugu
 
Back
Top Bottom