Shibuda out

Shibuda out

Hicho chama cha peoples power kinasitaajabisha sana, kwanza katiba yake bora katiba iliyopo inayopingwa hata sijui mandati ya kudai katiba mpya wanaitoa wapi?

Katiba gani hiyo inayotumika, watu wa shinyanga wamechagua kiongozi wao, harafu kiongozi wa watu wa shinyanga anakataliwa na kakikundi ka wahuni wachache kutoka kaskazini.

Makamu Mwenyekiti enzi hizo (CHACHA) amechaguliwa na wanachama wengi wa Taifa zima eti kakikundi haka ka wahuni kanaamuwa kuwaamulia wananchi wote. Kakikundi haka kana nguvu za AJABU. Harafu, wakitoka hapo watakwambia nguvu za rais ni kubwa, watakwambia peoples power. THIS IS CRAZY.

Na tena watakwambia maamuzi ya bunge ama bunge siyo sahihi maana yanalinda interest ya wahuni wachache. Na tena watakwenda mbali kuhubiria kwamba bunge lisiamue hoja ipelekwe kwa wananchi ikapigiwe kura. Well, na haka ka group ka thugs , the so called kamati kwanini kasipeleke hoja kwa wananchi husika wakaamue mwakilishi wao? Watanganyika nani aliyewaloga?

hahahahaahha umefanya uchambuzi mzuri hiyo ni Demokrasia version CHADEMA
wao Demokrasia ni maamuzi ya Mbowe au Dr. Slaa (kamati)
nakumbuka wale wanawake viti maalumu - kamati ilifuta uchaguzi kutoka kwa wanachama ikaweka vipengele na ikachagua yenyewe hahahhaha
 
Chama cha peoples power hicho. Teh teh teh, hata uchaguzi wa vijana mwaka ule ulishindikana hii kamati ikakaa ikawatimua akina Kafulila, pia hata kwenye uchaguzi wa mwenyekiti taifa haukuwezekana mpaka hii kamati ilipomwengua zitto kwa kumshinikiza ajitoe. Peoples powder
 
wanaJF

kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) iliyokutana tarehe 30/4/2011 imeamua kumtoa shibuda kwenye nafasi ya kukaimu nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa shinyanga, lakini kwnye kikao hicho nusura zichapwe kati ya lema na zitto baada ya lema, kumjia juu zitto ya kuwa mambo yote hayo ya shibuda kayasababisha yeye pale shinyanga kwa kuwaambia baraza la uongozi la mkoa kumteua shibuda kuwa kaimu mwenyekiti wakati katiba ya chama inasema kaimu mwenyekiti anapaswa kutokana na baraza la uongozi la mkoa,

huku shibuda akiwa si mjumbe wa baraza hilo, ndipo aliposimama zitto na kupinga kauli hizo ndipo wabunge na wajumbe wa kamati kuu walipo kuja juu na kumkumbusha zitto juu ya shibuda ya kuwa aliwatukana wabunge na akaambiwa aombe radhi akakataa na mpaka sasa hajaomba kwanini zitto unamtetea huyu jamaa, aliuza mjumbe huyo ambaye ni swahiba wa zitto bwana Msafiri mtemelwa

Nimeridhika, safi sana.Infact anafaa kufukuzwa CDM.Shibuda ni kibaraka wa wazi kabisa wa CCM.Yeye na Zitto hawa-deserve kabisa kuwa CDM.
 
Habari kama hizi zinawafanya wananchi waone CHADEMA haijakomaa inavyotakiwa kuendesha nchi.

Wanachi wanatakiwa kuelewa hakuna chama kinaweza kukomaa bila kupitia hatua kama hizi. CCM yenyewe imekomaa lakini unaona inajuvua magamba.

Nimeridhika, safi sana.Infact anafaa kufukuzwa CDM.Shibuda ni kibaraka wa wazi kabisa wa CCM.Yeye na Zitto hawa-deserve kabisa kuwa CDM.

Yaani wewe unataka watu warudi enzi zile za nyerere akisema watu wote ndio. wenye mawazo mbadala wawe supreesed. Nadnahi watu mnaongelea demomkrasia bila kujua maana ya demokrasia

BTN
Nadhani watu inabidi wawatumbue hulka na tabia za watu tofauti mfano ni hawa kina wenje, lema zitto na hata kina myika, regia Kila mtu anastyle yake ya kudili na mambo na watu.

Huwezi kutaka zitto awe kama myika au Lema awe Kama tindu lissu .Lakini vile vile tusitee tu kwa vile mbunge fulani yuko CDM lakini angekuwa CCM kwa kitendo kile kile tugemuita muhuni.

Habari kama hizi zinawafanya wananchi waone CHADEMA haijakomaa inavyotakiwa kuendesha nchi.
Very true mkuu

Tuna safari ndefu sana kuelekea demokrasia kamili, tatizo kubwa kwangu ni pia namna ambavyo tunaadress frustrations zetu kwenye hizi democracies... we also become very undemocratic in the process

tuko selfish and self centred sana

Utakuta tunalaumu CDM kwa kumsikiliza Mbowe au \slaa pekee, lakini tunakubali mtu atukane na kushurutisha wengine waamini asemayo au atakayo, tuko tayari kukubali kwamba CCM can just decide, or |Slaa can do what he wants au Lema can shout with rage au hata mtu akichangia chama wacha we na nguvu zaidi...... LONG WAY TO GO
 
the more i read this post the more i think jenifa anaumwa

nadhani tuache kuchangia kishabiki. Inafaa tujuzwe katiba ya cdm inasemaje ktk hili: Je baraza la mkoa linapaswa kutea kaimu ndani ya muda gani kujaza nafasi baada ya kiongozi husika kufariki? 2. Zitto kama kiongozi wa kitaifa alikuwa sahihi kusimamia kikao kile kutokana na cheo chake? 3. Je kulikuwa ng uharaka kufanya hivyo bearing in mind that the bereaved family was still mourning? Siku 3 za kutandua msiba zilikuwa zimekwisha? If we can answer those qns sincerely then we can be able to judge.
 
Tatizo nafikiri ni kuwa sote bado hatujajua nini kilipelekea huyu bwana kusimamishwqa kwani hatujapata inside story ya kilichojiri, leo nimejaribu kuwasiliana ila bado wapo kwenye kikao cha baraza kuu kwa hiyo nafikiri aliyeleta mada atupe inside story kama ambavyo siku nyingine huwa tunapata ndipo tuweze kuchangia kikamilifu.
 
nadhani tuache kuchangia kishabiki. Inafaa tujuzwe katiba ya cdm inasemaje ktk hili: Je baraza la mkoa linapaswa kutea kaimu ndani ya muda gani kujaza nafasi baada ya kiongozi husika kufariki? 2. Zitto kama kiongozi wa kitaifa alikuwa sahihi kusimamia kikao kile kutokana na cheo chake? 3. Je kulikuwa ng uharaka kufanya hivyo bearing in mind that the bereaved family was still mourning? Siku 3 za kutandua msiba zilikuwa zimekwisha? If we can answer those qns sincerely then we can be able to judge.

Kama Zitto alikuwepo nafikiri anaielewa katiba ya chedema vizuri. Pia swala la kukaimu japo sijui huko chadema likoje lakini kwa kawaida huwa halisubiri nini wala nini, kama wewe ni kiongozi wa kakampuni kadogo tu ukisafiri hata siku moja lazima uache mtu wa kukaimu.

Ndiyo maana kwa vyama vya ukweli, ama taasisi huwa vime-define kabisa ikitokea hiki, anayekaimu ni huyu mpaka pale uchaguzi ama uteuzi utakapofanyika.
 
majungu,majungu,majungu...kila siku zitto,zitto,zitto..kuna ajenda gani? hivi kutofaitiana mawazo ndo kununuliwa?maana ya kikao nini? mtu mmoja afikiri kwa niaba ya wengine?
Lema ana strangle za kitoto sana,hata bungeni alisha wahi kushauri milango ifungwe ili wabunge wapigane..huyu mtu ni hatari na ni mamluki mkubwa,kidogo auzee jimbo huyu lema,hana lolote kila siku kuhama vyama,mara CCM,TLP, Ghafla chadema,sijui hata ataenda wapi....
 
Ujana maji ya moto!!!!!!!

Mbona hawa vijana hawana simile! Zipigwe mbele ya kikao hii ni aibu wanapaswa kujirekebisha bwana! Kwa hilo siwezi kuwaunga mkono.
 
Hivi Shibuda ku-kaimu tu imekuwa nongwa? Hawa jamaa wana bifu nae kwenye issue nyingine, na hivi siri za vikao zinavuja kabla ya hata vikao vyenyewe kwisha tutasikia mengi!
 
Kama CDM watakuwa bado wana feelings za U-kaskazini basi litakuwa kosa kubwa muno ambalo halitazaa mafanikio maana ilivyo sasa hivi wana nguvu kwa sababu tu kimefika kona nyingi za nchi.

Lakini pia lazima wajilinde na uvamizi na misimamo ya watu wasioeleleweka. Hao akina Shibuda. Bila kujali hata kama atakuwa ni Zitto au Slaa akionyesha unafiki na usaliti lazima aachiwe adondoke.

Huyu Zitto kila wakati analaumiwa kwa kukisaliti chama. Kwake yeye ni hatari na 2005 alionekana kama kivutio cha vijana, leo hii sioni tena hali hiyo sifa ambayo ilimponyoka pale alipoanza kuhangaikia mambo ya Tanesco. Sijui yeye anajifunza nini au anafanikiwa nini kwa kutimiza hayo! Au anatumiwa kama toilet paper?
 
Nafikiri mnapotosha ukweli.
Zitto aliacha kuwa kipenzi chenu baada ya kuwania uenyekiti, na hako ka ukweli kadogo tu unaamua kukapindisha? mhhhh
 
hahahahaahha umefanya uchambuzi mzuri hiyo ni Demokrasia version CHADEMA
wao Demokrasia ni maamuzi ya Mbowe au Dr. Slaa (kamati)
nakumbuka wale wanawake viti maalumu - kamati ilifuta uchaguzi kutoka kwa wanachama ikaweka vipengele na ikachagua yenyewe hahahhaha

Tusishangae. Sehemu kubwa ya hao tuwaitao wanasiasa ni watafuta ajira. Bahati mbaya iwe CDM, CCM, CUF, nk wote wanajipendekeza. Tena huko CCM ndo kabisa! Ukikosana na M/kiti wao tu, ujue wote wamekuacha.

Hivi huko CCM siku hizi hakuna fikra sahihi za M/kiti nini? Au anakwenda kimya kimya?
Akisema tuvue magamba woote safi! Akisita kidogo wote sasa wamesita.

Bora hii ya CDM ya 'papo kwa papo' maana CCM imekwenda na Makamba bila kuridhika naye miaka yooote hiyo. Hakuna aliyeweza kusema hatukutaki maana M/kiti alikuwa hajasema.
 
Nafikiri mnapotosha ukweli.
Zitto aliacha kuwa kipenzi chenu baada ya kuwania uenyekiti, na hako ka ukweli kadogo tu unaamua kukapindisha? mhhhh

Sidhani,
Anagombea uenyekiti wakati magazeti yalisha anza kukosana na maoni yake juu ya Tanesco. Na siamini kama hayo mambo yake ni suala la CDM ni suala la wa-TZ wote walivyoona anavyoelekea kugeuza msimamo juu ya mambo ambayo yalishaeleweka kwamba ni ufisadi ndani ya Tanesco.

Lakini hata hivyo si bora CDM kuliko CCM walioweka 'wanted' kwa yeyote atakayegombea nafasi ya Urais against Kikwete? AU!

BTW; Huyu Mkama /Mukama, katibu wa CCM ni nduguyo? Mbona leo alikaa high table wakati ni sherehe za Wafanyakazi? tena akiwa na jezi ya CCM au hajafahamu mipaka ya wadhifa wake? Nieleweshe kana unaweza.
 
Nafikiri mnapotosha ukweli.
Zitto aliacha kuwa kipenzi chenu baada ya kuwania uenyekiti, na hako ka ukweli kadogo tu unaamua kukapindisha? mhhhh
Acha uzandiki wewe...Zitto hakuwa kipenzi cha wanachadema wengi tangu alipoingia kwenye kamati ya muungwana ya madini. Kuanzia pale Zitto alibadilika kabisa. Hata Slaa na yeye akikaa ki-CCM CCM tutamchana tu
 
Hivi Shibuda ku-kaimu tu imekuwa nongwa? Hawa jamaa wana bifu nae kwenye issue nyingine, na hivi siri za vikao zinavuja kabla ya hata vikao vyenyewe kwisha tutasikia mengi!

Fanya homework yako vizuri usije ukawa mpiga propaganda wa NCCR-MANUNUZI
 
Back
Top Bottom