Mbona sku nyingi sana JF imekuwa kijiweTAARIFA HII SIO YAKWELI, IPO KICHONGANISHI, haya mambo sio rasmi, tuweni makini. Jf itakuwa sasa kibanda cha kahawa!
Mbona sku nyingi sana JF imekuwa kijiweTAARIFA HII SIO YAKWELI, IPO KICHONGANISHI, haya mambo sio rasmi, tuweni makini. Jf itakuwa sasa kibanda cha kahawa!
nilishasema tangau hapo awali kwamba CDM ni chama kinachowahada watanzani, wanachokiongea sicho wanachokiamin ,uthibitisho ni huu upuuzi wa kutaka kununua magari machakavu wakati huo huo wanapinga serikali kufanya hivyo hii ni aibu kwa chama kinachojiita chama makini
Kwenye RED naomba nisikupinge kwakua nimaoni na mtazamo wako ila kwenye Blue umedhihilisha ukilaza wako samahani naomba nifafanue maana hua mnasema tupinge kwa hoja.
Nina maswali mawili ya msingi ( 1 ):_Naanza na kwenye nyekundu...Unaposema mikusanyiko ya wasaka tonge tu hasa unakua unamaanisha nini? (a) Tofauti ya wasaka tonge na wanaotetea maslahi na ustawi wa inji yao ukoje?
Swali la (2 ) Shabiki wake kwenye nini?nitakuogopa kidogo kama utasema kwenye siasa au chama chake kwakua tayari umejipambanua kua wewe huamini katika hilo(a)kauli zangumi mbele unahisi hatanufaika nazo ila kauli na ndio mzee ndio nakupigiana makofi zinamaslahi kwako?
Hapo kwenye bold ya zambarau sina neno napo mkuu kwa sababu ulikua unaandika kwa jazba.
Naamini utajibu kistaarabu kwakua wewe nimtu mzito bhana hahahahahahahahahaa!!!!!
Hivi hili suala la Shibuda limekaaje? Jamani kama alichaguliwa na wananchi au vikao vya maamuzi ya Shinyanga naomba CDM msivuruge utaratibu maana anakaimu tu na wakati wa uchaguzi basi itajulikana kama alikuwa mchapa kazi au la!!
Epukeni migogoro kwa kutomwondoa Shibuda kinyemela hata kama hafai.
Sunday, 01 May 2011 22:56
NI VITA YA KAMBI ZA MBOWE, ZITTO, SHIBUDA ANGOLEWA KAIMU M/KITI SHY
Ramadhan Semtawa
VITA vya makundi vimezidi kuviandama vyama vikubwa vya siasa nchini, ambapo sasa hali si shwari ndani Chadema, ambako kunadaiwa kuwepo mkakati wa kumng'oa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.
Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, anadaiwa kuponzwa na msimamo wake kupinga ununuzi wa magari mitumba yenye thamani ya Sh480 milioni ya Chadema.
Hali hiyo ilijitokeza katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi juzi Jumamosi chini ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kikao ambacho pia kilimgoa John Shibuda katika nafasi ya kukaimu uenyekiti mkoa wa Shinyanga.Shibuda ambaye ni mbunge wa Maswa Magharibi ameondolewa baada ya kukalia nafasi hiyo takriban kwa siku nne tu tangu ateuliwe, kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Shinyanga Philip Shelembi ambaye alizikwa April 27, 2011.
Chanzo cha mvutano
Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa kikao hicho zinasema kuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, ndiye alianzisha mvutano wa kutaka Zitto ang'olewe kutokana na kupinga wazo la kununua magari chakavu kutoka India.
Chanzo chetu cha uhakika kilidokeza kuwa mashambulizi dhidi ya Zitto yalianza pale alipounga mkono hoja ya Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo ambao walinukuliwa wakisema kwamba, isingekuwa sahihi kwa chama hicho kinachopinga ufisadi kufanya ufisadi kwa kununua magari chakavu wakati wamekuwa wakiibana serikali isifanye hivyo.
Baada ya Zitto kuunga mkono hoja hiyo, vyanzo hivyo nifafanua kuwa ndipo vurugu zilipoanza kwani Lema alianza kumrushia vijembe akisema kwamba Zitto ni tatizo na kwamba amekuwa akimtetea Shibuda.
Habari zinasema baadhi ya wajumbe walisema hoja ya Lema haikuwa na nguvu ya kumshutumu Zitto kwani Shibuda ni mbunge halali wa Chadema.
Duru zaidi za kisiasa kutoka ndani ya kikao hicho zinasema wakati mvutano huo ukiendelea, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alikuwa kimya huku kwa mara ya kwanza Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akiwa mmoja wa wajumbe waliomtetea Zitto.
"Wakati Lema akisema hivyo, Dk Slaa wakati wote alikuwa kimya na hakusema chochote. Mnyika alisimama na kumtetea Zitto kwa mara ya kwanza, na katika utetezi pia alikuwepo Grace Kiwelu," kiliweka bayana chanzo hicho.
Katika majibizano hayo inadaiwa ulifika wakati Zitto alisimama na kumwambia mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwamba mpango mkakati wake huo wa kujenga mtandao utakuja kumgharimu katika siku za usoni."Zitto alimwambia Mbowe mpango wake huo wa kujenga mtandao ungekuja kumletea matatizo hapo baadaye, "kilisema chanzo hicho kikimnukuu Zitto ndani ya kikao.
Kungolewa kwa Shibuda
Mbali ya Zitto, Kamati Kuu hiyo pia iliazimia kutengua nafasi ya Shibuda, kukaimu nafasi ya uenyekiti ya Chadema mkoa wa Shinyanga.Vyanzo hivyo viliongeza kwamba, kabla ya mpango huo genge linalompinga Zitto lilimshutumu kwamba alikwenda Shinyanga na kushirikiana na baadhi ya wanachama kumweka Shibuda ili kutimiza ajenda zao.
Mvutano huo unaondelea ndani ya Chadema unazidi kukiweka chama hicho kinachokua na kuwa na malengo ya kukamata dola katika wakati mgumu kutokana na makundi mawili, huku moja likimuunga mkono Zitto na jingine Mbowe.
Zitto na Shibuda ni viongozi ambao wamekuwa wakikumbwa na misukosuko ndani ya Chadema na mara kadhaa Zitto amenusurika kung'olewa katika nafasi zake za uongozi kutokana na kile kinachodaiwa ni hulka yake ya kutofautina na wenzake hata katika mambo yenye maslahi kwa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Kauli za Zitto, Shibuda
Zitto alipoulizwa na Mwananchi jana jioni kuhusu tafrani hiyo alisema .tafadhali sana, naomba nisiongee chochote kwa sasa, hiki ni kipindi cha kukijenga chama, si kipindi cha kuonyesha umma kwamba Chadema kuna mgogoro.
Pale mwandishi alipomhoji zaidi alisema tafadhali naomba nikupigie baadaye kisha kukata simuKwa upande wake Shibuda alikiri kusikia taarifa hizo na kuongeza kwamba, anasubiri apate taarifa rasmi kwani yeye alipewa heshima hiyo na wanachama wa Shinyanga kupitia vyombo vyao vya maamuzi.
Nilikuwepo kwenye kikao mwanzo hadi mwisho. Mengi yanayoandikiwa hapa ni hisia zinazotokana na mazoea. Tatizo ni kwamba tumezoea siasa za ndiyo mzee, kitu ambacho hakipo CHADEMA. Ndani ya vikao vya CHADEMA tunajadiliana sana, mvutano ni mkubwa, tena wakati mwingine kwa ukali hadi mwafaka unapopatikana. Na mwafaka hupatikana kwa kuzingatia uzito wa hoja na ushahidi wa kutosha. Kwa sababu ya mazoea ya siasa za ki-CCM za funika kombe mwanaharamu apite, watu wakiona CHADEMA wakivutana kihoja wanatafsiri kwamba ni mgogoro au tatizo.
Ukweli ni kwamba kwenye kikao kulikuwa na mjadala mkali juu ya mambo mbalimbali. Mwisho wa siku tumefikia mwafaka na maamuzi yamefanyika kidemokrasia na amani ni tele.
Kuhusu Shinyanga, ni kwamba ukaimishaji haukufuata taratibu na kanuni za Kikatiba. Viongozi wetu wa Shinyanga walikiri kosa lao na wamekubaliana na maamuzi ya kutengua uteuzi huo hadi hapo taratibu zitakapofuatwa. Tofauti ni hio tu, kwamba CHADEMA huchukua hatua madhubuti na mapema, badala ya kufunika kombe mwanaharamu apite.
Hivyo, ndugu zangu wapenzi wa mabadiliko katika nchi hii msinyong'onyee, there is total peace in CHADEMA and the struggle continues.

ujumbe wako unachonganisha watu, wabunge, na wana cdm!! Hoja haikukaa vizuri. Ungeishia kusema kuwa kamati kuu imemuengua shibuda na kumuweka fulani kwa sababu fulani; badala ya kuleta malumbano ya vikaoni ambayo hayana tija na hayaendani na hitimisho la hoja yako uliyoleta. Kwa msingi huo, naiona hoja yako imekaa kimajungu majungu tu na inalengo la kubomoa cdm!!!
Kwa kweli Huyu Zitto haeleweki, kila controversial ya CDM lazima ahusike. Isije ikawa amepandikizwa kuiua CDM.
Wana JF
Kamati kuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana tarehe 30/4/2011 imeamua kumtoa Shibuda kwenye nafasi ya kukaimu nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga. Lakini kwenye kikao hicho nusura zichapwe kati ya Lema na Zitto, baada ya Lema kumjia juu Zitto ya kuwa mambo yote hayo ya Shibuda kayasababisha yeye pale Shinyanga kwa kuwaambia baraza la uongozi la mkoa kumteua Shibuda kuwa Kaimu Mwenyekiti, wakati katiba ya chama inasema Kaimu Mwenyekiti anapaswa kutokana na Baraza la Uongozi la Mkoa,
Huku Shibuda akiwa si mjumbe wa Baraza hilo, ndipo aliposimama Zitto na kupinga kauli hizo, ndipo wabunge na wajumbe wa kamati kuu walipo kuja juu na kumkumbusha Zitto juu ya Shibuda ya kuwa aliwatukana wabunge.
Na akaambiwa aombe radhi akakataa na mpaka sasa hajaomba kwa nini Zitto unamtetea huyu jamaa, aliuliza mjumbe huyo ambaye ni swahiba wa Zitto bwana Msafiri Mtemelwa

Kwa usahihi ni kwamba maamuzi yalishatenguliwa na kamati kuu na baraza kuu lenye sauti ya mwisho tukaridhia pendekezo la kamati kwa kwa sababu hayakufuata desturi ya kitanzania na kanuni za chadema. Sababu za kutengua ni hizi kwa ufupi sana zilizo wasilishwa katika baraza kuu na kamati kuu.si kweli kwa hilo jambo kwa sasa, ninavyomfahamu shibuda akiwa anataka kitu huwa nimnyenyevu sana. Yeye alikuwa anaona aibu tu sabab amekikuta chama kina watu makin, sidhan kama maamuz yanaweza kutenguliwa na kamati kuu wakati katiba ya chama ilifuatwa nadhan bwana shibuda kapewa baraka zote za kuingia cc, baada ya kupewa uongozi bwana shibuda kishatoa mikakati mingi.
Nilikuwepo kwenye kikao mwanzo hadi mwisho. Mengi yanayoandikiwa hapa ni hisia zinazotokana na mazoea. Tatizo ni kwamba tumezoea siasa za ndiyo mzee, kitu ambacho hakipo CHADEMA. Ndani ya vikao vya CHADEMA tunajadiliana sana, mvutano ni mkubwa, tena wakati mwingine kwa ukali hadi mwafaka unapopatikana. Na mwafaka hupatikana kwa kuzingatia uzito wa hoja na ushahidi wa kutosha. Kwa sababu ya mazoea ya siasa za ki-CCM za funika kombe mwanaharamu apite, watu wakiona CHADEMA wakivutana kihoja wanatafsiri kwamba ni mgogoro au tatizo.
Ukweli ni kwamba kwenye kikao kulikuwa na mjadala mkali juu ya mambo mbalimbali. Mwisho wa siku tumefikia mwafaka na maamuzi yamefanyika kidemokrasia na amani ni tele.
Kuhusu Shinyanga, ni kwamba ukaimishaji haukufuata taratibu na kanuni za Kikatiba. Viongozi wetu wa Shinyanga walikiri kosa lao na wamekubaliana na maamuzi ya kutengua uteuzi huo hadi hapo taratibu zitakapofuatwa. Tofauti ni hio tu, kwamba CHADEMA huchukua hatua madhubuti na mapema, badala ya kufunika kombe mwanaharamu apite.
Hivyo, ndugu zangu wapenzi wa mabadiliko katika nchi hii msinyong'onyee, there is total peace in CHADEMA and the struggle continues.
Watu kwa vibweka siku nyingi gani wakati hujamaliza hata mwezi.Mbona sku nyingi sana JF imekuwa kijiwe
- Hii yadhihirisha yale yote niliyokuwa nayasema sana humu jamvini kuwa upendeleo, udini, ukabila na ukanda vitawatafuna sana CHADEMA. Na dhambi hii katu haita waacha
- CD Mina wenyewe, na wenyewe ndio hao walio mng'oa Shibuda na kutaka kumuweka kibaraka wao
- Ubabe wa Lema ( mzee wa funga mlango tupigane) unadhidi kujidhirisha , badala ya kushindwa kuwahudumia wananchi amekuwa mwana masumbwi
With due respect, Dr. Kitilb amekuwa mtetezi mkubwa wa ukandamizaji wa demokrasia ndani ya cdm, tunakumbuka maelezo yake juu ya chaguzi za Vijana, wabunge wa viti maalumu na hata uchaguzi mkuu wa cdm.