Shibuda out | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda out

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by never, May 1, 2011.

 1. n

  never JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wana JF

  Kamati kuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyokutana tarehe 30/4/2011 imeamua kumtoa Shibuda kwenye nafasi ya kukaimu nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga. Lakini kwenye kikao hicho nusura zichapwe kati ya Lema na Zitto, baada ya Lema kumjia juu Zitto ya kuwa mambo yote hayo ya Shibuda kayasababisha yeye pale Shinyanga kwa kuwaambia baraza la uongozi la mkoa kumteua Shibuda kuwa Kaimu Mwenyekiti, wakati katiba ya chama inasema Kaimu Mwenyekiti anapaswa kutokana na Baraza la Uongozi la Mkoa,

  Huku Shibuda akiwa si mjumbe wa Baraza hilo, ndipo aliposimama Zitto na kupinga kauli hizo, ndipo wabunge na wajumbe wa kamati kuu walipo kuja juu na kumkumbusha Zitto juu ya Shibuda ya kuwa aliwatukana wabunge.

  Na akaambiwa aombe radhi akakataa na mpaka sasa hajaomba kwa nini Zitto unamtetea huyu jamaa, aliuliza mjumbe huyo ambaye ni swahiba wa Zitto bwana Msafiri Mtemelwa
   
 2. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ili balaa gani kati ya zito na lema,
  duh mbona mapema au mkuu umechakachua hii kitu,
  kuna haja ya kuwa makini na kutumia busara, kama haya yanatokea
  chama kiko hatarini na hekima ya wazee inatakiwa kukinusuru chama,
  na kanuni za chama zinatakiwa kufuatwa, ili zinapokosewa kuna haja ya kuongea kwa kuheshimiana
  ila hii habari yako ninaifanyia uchunguzi kama ina ukweli,
   
 3. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ujumbe wako unachonganisha watu, wabunge, na wana CDM!! hoja haikukaa vizuri. Ungeishia kusema kuwa Kamati kuu imemuengua shibuda na kumuweka fulani kwa sababu fulani; badala ya kuleta malumbano ya vikaoni ambayo hayana tija na hayaendani na hitimisho la hoja yako uliyoleta. Kwa msingi huo, naiona hoja yako imekaa kimajungu majungu tu NA INALENGO LA KUBOMOA CDM!!!
   
 4. R

  Red one Member

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mkuu ni kweli kabisa aliyenena hapo juu yupo sahihi, leo nusura lema na zitto zipigwe pale lema alipo mwambia zitto ukweli kuwa aache kutumiwa na hata kaa afanikiwe kwenye mipango yake hiyo na kuwaacha wajumbe wote midomo wazi kila mmoja akishangaa kijana lema asivyo mumunya maneno na kuamua kumtolea uvivu zitto
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nadhani hii itasaidia viongozi wa Chadema kufanya maamuzi kikatiba badala ya maoni ya mtu kama ilivyozoeleka.
  Wiki iliyopita nilimshauri Dr. Slaa hapa Jamii Forums kwamba ajaribu kutumia vikao vya chama badala ya kufanya maamuzi jukwaani kama ilivyotokea Nzega majuzi. Majibu yake yalionekana kutetea maamuzi yake, lakini ukweli unabaki maamuzi yafanyike katika vikao vya chama na hivyo kama maamuzi yanafanywa kwa uadilifu wa kufuata katiba ya chama hakuna mwenye kumnyoshea kidole fulani na hakuna mwenye kuteleza ulimi kwamba fulani ndiye aliyeamua.

  Haya yatokeayo ni ishara nzuri za kujielewa mapungufu na kuweza kurekebisha kasoro ambazo chama cha Chadema wanazo na wanahtaji kufanya kazi. Kujenga chama kiwe imara si kazi ya siku moja.

  Wapenzi wa Chadema acheni kushabikia tu hata viongozi wanapoteleza vinginevyo hawatajisahihisha makosa.
  Ukomavu ndo kuwa mwazi, kukosoa na kushauri, huko ndiko kujenga chama.
   
 6. R

  Red one Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kamanda hii siyo ccm kila kitu kilichopo lazima kiwekwe wazi mimi naungana na mtoa mada anajua kueleza vizuri tena kwakifupi sana na mada kukaa mkao wa kusomeka kwa urahisi
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wanajamii Forums, kweli John Shibuda kadiri ya msimamo wake alioonyesha tangu awe mbunge wa Chadema hamuoni kama Kaingia Chadema kwa ajili ya ubunge na wala si kwa mapenzi ya chama. Yeye hata alivyojieleza bungeni bado ni mpenzi wa CCM.

  Zito Kabwe naye ni ndumila kuwili na kila inapotokea jukumu la viongozi wa Chadema kwenye mikutano au maandamano haishiwi visingizio, lakini kwenye kamati za bunge anakolipwa posho matatizo yote ya kifamilia huisha.

  Shibuda si muafaka kwa sasa kuwa mwenyekiti wa mkoa, anahitaji kubaki chini ya uangalizi maalum kwa manufaa ya Chadema na wananchi.
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  HEKO WAHESHIMIWA ZITTO NA LEMA KWA UKOMAVU WENU KIDEMOKRASIA:
  HATA SIKU MOJA WALA MSIOGOPE KUKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA KATIKA HOJA BILA CHUKI WALA MIZENGWE


  Waheshimiwa Zitto, Lema na kamati kuu zima, napenda niwapongeze tena saaana kwa jinsi mnavyohakikisha kwamba NEMBO YETU YA 'DEMOKRASIA' kweli inafanya kazi kiukweli ndani ya chama katika vyombo vyetu vyote vya maamuzi.

  Huo ndio ukomavu wa kidemokrasia, uwazi wa kuendesha mambo kuonyesha utayari wa CDM kuongoza taifa bila kwepo TABAKA LA WATEULE ndani ya chama ambao kauli zao hazipingwi. Nawapongeza pia kukataa kubariki maamuzi ya barabarani katika kuteuana ukaimu mwenyekiti huko Shinyanga. Mhe Shibuda sasa ajindae tu kuingia kwenye kinyang'anyiro katika kukijenga chama huku kwa ushirikiano zaidi.

  Ndio demokrasia ndani ya vyama inapokomaa na baada ya hapo wote wawili kuendelea kusalimiana na kuendeleza harakati za kufanya kazi kwa pamoja zaidi kutetea maslahi ya umma wa Tanzania.

  Nasema ni ndani ya CHADEMA tu ndimo kulimo kiwango hicho cha juu cha demokrasia na misingi ya maadili ya vipi kushika uongozi KWA KUZINGATIA ITIKADI YETU YA 'NGUVU NA MAMLAKA YA UMMA' katika kila tulitendalo na maamuzi tunayoingia.

  Mwisho, chama bila mikiki mikiki ya ndani lakini kwa misingi ya disciplined democratic space exercising tayari ni marehemu mtarajiwa kama kilivyo CCM ambako tofauti tu ya maoni kesho yake mtu anakolimbwa kwa kile anachokiamini.

   
 9. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Alitumia uhuru wa kutoa mawazo yake hivyo si vema kulaamu, mbona ya CCM huwa inaandikwa kwa utaratibu kama huu na kujadiliwa tena kwa kicheko.
  Kikubwa ninahokiona ni kwamba ndani ya Chadema kuna watu wanajiona wao ndiyo wao na baadhi ya wengine kila wakisemaau kufanya kitu wanaonekana kama wasaliti / wamekosea kama ambavyo comrade Zitto anavyoandamwa na hasa kwa kuwa kwa kiasi fulani haelewani na Slaa na Mbowe kifikra, maana Zitto ana vision kubwa hivyo anaangalia na kuchambua mambo kwa mtazamo wa hali ya juu na kuona miaka kumi mpaka ishirini ijayo.
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,850
  Likes Received: 11,973
  Trophy Points: 280
  Too much exaggretion achambue lakini asivunje katiba ya chama kwa malengo binafsi.
   
 11. K

  Kaseko Senior Member

  #11
  May 1, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  si kweli kwa hilo jambo kwa sasa, ninavyomfahamu shibuda akiwa anataka kitu huwa nimnyenyevu sana. Yeye alikuwa anaona aibu tu sabab amekikuta chama kina watu makin, sidhan kama maamuz yanaweza kutenguliwa na kamati kuu wakati katiba ya chama ilifuatwa nadhan bwana shibuda kapewa baraka zote za kuingia cc, baada ya kupewa uongozi bwana shibuda kishatoa mikakati mingi.
   
 12. K

  Kaseko Senior Member

  #12
  May 1, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwa sababu za kinafiki hizo sidhani kamati kuu wali consider sana mtoa mada amekurupuka tu, nadhan maamuzi ya suala hilo si hayo.
   
 13. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hayo waweza kuwadanganya wenzako mnapokuwa kwenye vijiwe vya kahawa/tangawizi au mnapocheza bao lakini si hapa.

  Too low!!

  Grooaaaan!!
   
 14. h

  hoyce JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nilishangaa kilichomkimbiza Zitto kusimamia uteuzi wa Shibuda hata habla Magadullah hajazikwa! Lazima ana maslahi binafsi, ndio maana Lema kasema anatumiwa
   
 15. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tujuzeni yaliyojiri baada ya Zitto na Lema kutoleana uvivu! Kuna hatua zozote zilizochukuliwa?
   
 16. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  wala hatukuhitaji upofu huu wa mawazo,wewe unamwona Zitto haeleweki na wenzake kwa sababu tu eti ana vision ya miaka10 mbele,yawezekana ila anatakiwa awe bayana ili vision yake ieleweke ama la hatuitaji vision private ya mtu mmoja tunahitaji vision moja ya chama kimoja inayoeleweka

  alafu kabla haujaandika hebu tumia akili yako ndogo kujihoji,ni nani alikwambia kweli Dr.na Mbowe hawamtaki Zitto?ulitegemea ni nani atamwamini katika baadhi ya matendo yake yanayofahamika bayana?

  Acha utoto,hata angelikuwa ni ndugu yako wa kuzaliwa hauwezi kumwamini tena kama mwanzo mpaka pale atakapo omba msamaha na kubadilika,na labda tu unadhani ni kwa nini mara hii Zitto alikabiliwa na upinzani pale jimboni kwake tofauti na ilivyokuwa awali,go and have a research,NYAMBAFUUUUUUUUUUUUUUU
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  May 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu hutaki watu tuambiwe ukweli? Suala hapa ni kama kweli kilichotokea ndicho hicho ama jamaa ameongeza chumvi. Kama alichoandika ndicho kilichotokea basi ni vema na haki nasi humu kujulishwa kilichotokea nyuma ya pazia. Mbona tulikuwa tunashangilia yaliyokuwa yakitokea nyuma ya pazia wakati CCM wanalumbana kuvuana magamba?
   
 18. p

  pondamali Member

  #18
  May 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa kweli Huyu Zitto haeleweki, kila controversial ya CDM lazima ahusike. Isije ikawa amepandikizwa kuiua CDM.
   
 19. R

  Red one Member

  #19
  May 1, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Baada ya hapo busara za mwenyekiti zikatumika na ndipo lema akasema na heshimu tu meza kuu isingekuwa hivyo leo zitto ungetuambia usaliti huu unautoa kwanani na ni kwanini? Ndipo ikafika mahala pa kupiga kura, wanaotaka shibuda awepo alikuwa mmoja wasiyo taka walikuwa 18 na zitto, mama yake, mkumbo hawakupiga kura upande wowote ule. Acha ni seme ukweli nimefurahi sana kwa lema kujiunga na sisi kwenye kamati kuu ametutoa uoga wa kumuona fulani kama mungu hivi...
   
 20. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  TAARIFA HII SIO YAKWELI, IPO KICHONGANISHI, haya mambo sio rasmi, tuweni makini. Jf itakuwa sasa kibanda cha kahawa!
   
Loading...