Shibuda out

Shibuda out

People,cant we argue objectively?Mbona kila kitu siku hizi ukabila unawekwa Mbele?Sidhani kwa mwanasiasa yeyoteMakini wa upinzani itakuwa ni busara kusimamia Propaganda za CCM,mtu anaongelea ukabila na kuiweka centre stage ya discussion.Jamani let us move forward as Tanzanians.Some people are suffering from a serious Identity crisis.Hizi propaganda za CCM against CHADEMA zitakuja kutuletea madhara makubwa huko baadae as a Nation na si kama Chadema.Itafikia hatua makabila fulani yataanza kuchukiana,Hizi mbinu za Ki-NAZI za CCM tuachane nazo. Kama mtu una hoja za msingi jadili,tusikimbilie umbrella ya Tribalism,hii ni old school political weapon.It sucks!
Pia,hoja za kupigana au matusi hayawezi kuleta Unity katika jambo lolote zaidi ya kujenga ukuta.Najua Chadema inapigwa kila angle kwa sababu ya husda,mamabo mengine ni madogo tu ya ku-correct.Sio big Issue.
 
Hayo waweza kuwadanganya wenzako mnapokuwa kwenye vijiwe vya kahawa/tangawizi au mnapocheza bao lakini si hapa.

Too low!!

Grooaaaan!!


hahahahaaa umenichekesha sana aisee eti "groan",
lakini ndio ivo kwani alokwambia nao cdm hawapishani kimtizamo!!
lazima vitu vichongwe viwe bora ata ccm imepitia uko,,,poa tu ata wakichapana makonde



 
Binafsi nimeipenda tabia ya Lema kwasababu zifuatazo:_
1.Kwanza anauwezo wa kukisimamia anachokiamini.
2.kile anachokiahidi ndicho anachokitekeleza haijalishi itamgharimu kiasi gani .
3.Nimtu asiyependa blah blah kwenye seriously issue
4.Ni mtu anaeumia kwa dhati kuona rasilimali za inji yetu hazimnufaishi mzawa.
5.Ni mtu anaewachukia vigeugeu yaani hapa mnakubaliana hivi na kule wanatenda vile.
6.Lema hayupo kimaslahi binafsi na hafanyi ubunge kama chanzo chake cha mapato.

Mimi niseme neno moja kwako mbunge wangu kazi unayoifanya ndio tulio kutuma wana Arusha usisikilize maupupu yao.

Statistic Duniani kote zinaonyesha watetezi wa wanyonge ndio huonekana wabaya kuliko wale wauwaji wanaojivisha ngozi za kondoo.

Hebu kwanza tujiulize swali dogo tu wakuu hivi hizo siasa tunazoziita eti za kistaarabu tuanufaika nazo vipi kama Taifa?

Lema na ZITTO nawafananisha kama na ndugu wawili wanaosimamia mali za familia kwakua wao ni wakubwa sasa shida inakua mmoja anajitahidi sana kutafuta vyanzo vipya vya mapato kushawishi wateja ,kuimarisha masoko na kuleta bidhaa mpya kadri awezavyo na ndugu mwingine yeye kwakua alikua hapo kabla basi amepunguza kasi kabisa ila ukimwangalia kwa kwamacho anapretend kama na yeye anawajibika vilivyo kumbe yeye yupo kwa ajili ya kutapanya kilichokusanywa na mwenzake kwa maslahi yake binafsi hii inauma sana wakati fulani hali kama hii ikikukuta unaweza kumfanya mtu kitu mbaya nahisi hii ndo hali ilivyo kati ya wabunge wa CCM na Mh_Lema au Mh:_Zitto na Mh:_Lema

Mh:_ LEMA usivunjike moyo wananchi wako tupo pamoja nawe.
 
wanaJF

kamati kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) iliyokutana tarehe 30/4/2011 imeamua kumtoa Shibuda kwenye nafasi ya kukaimu nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, lakini kwnye kikao hicho nusura zichapwe kati ya Lema na Zitto baada ya Lema, kumjia juu Zitto ya kuwa mambo yote hayo ya shibuda kayasababisha yeye pale Shinyanga kwa kuwaambia baraza la uongozi la mkoa kumteua Shibuda kuwa Kaimu Mwenyekiti wakati katiba ya chama inasema Kaimu Mwenyekiti anapaswa kutokana na Baraza la Uongozi la Mkoa,

huku Shibuda akiwa si mjumbe wa Baraza hilo, ndipo aliposimama Zitto na kupinga kauli hizo ndipo wabunge na wajumbe wa kamati kuu walipo kuja juu na kumkumbusha zitto juu ya Shibuda ya kuwa aliwatukana wabunge na akaambiwa aombe radhi akakataa na mpaka sasa hajaomba kwanini zitto unamtetea huyu jamaa, aliuza mjumbe huyo ambaye ni swahiba wa zitto bwana Msafiri Mtemelwa

Hili la Lema kutaka kupigana ni tatizo maana hata Bungeni alisema wafunge milango. Kuna bwana mmoja anaitwa Ngogo pamoja ushabiki wake kwa TLP aliandika kwa makini hasa juu ya tabia ya Lema. Hii si namna njema ya kutatua matatizo.
Lakini pia suala la kuteua watu, Zitto si wa kwanza, kuna siku hapa huko Nzega mtu alisimamishwa uongozi na Dr Slaa, watu wakasema saana hapa haja ya kuheshimu taratibu za CHAMA. Kwahiyo kuna tatizo CDM la kila mtu kufanya anachoona kinafaa ili mradi tu atapata umaarufu.
Mwisho kuhusu Shibuda, wengi walisema yaani mtu akihamia CDM anapata na cheo haraka saana. Muangalieni Marando na kesi anazoendesha zipo tofauti na falsafa ya CDM lakini kabambikwa cheo na leo hii Pro Safari. Tutaona na kusikia mengi.
 
Being in a team means giving up our individuality.......
a mwenye masikio na alisikie neno hili.
 
Hili la Lema kutaka kupigana ni tatizo maana hata Bungeni alisema wafunge milango. Kuna bwana mmoja anaitwa Ngogo pamoja ushabiki wake kwa TLP aliandika kwa makini hasa juu ya tabia ya Lema. Hii si namna njema ya kutatua matatizo.
Lakini pia suala la kuteua watu, Zitto si wa kwanza, kuna siku hapa huko Nzega mtu alisimamishwa uongozi na Dr Slaa, watu wakasema saana hapa haja ya kuheshimu taratibu za CHAMA. Kwahiyo kuna tatizo CDM la kila mtu kufanya anachoona kinafaa ili mradi tu atapata umaarufu.
Mwisho kuhusu Shibuda, wengi walisema yaani mtu akihamia CDM anapata na cheo haraka saana. Muangalieni Marando na kesi anazoendesha zipo tofauti na falsafa ya CDM lakini kabambikwa cheo na leo hii Pro Safari. Tutaona na kusikia mengi.
Usifikiri kila anayehamia CDM lazima apate cheo vigezo vinaangaliwa na loyality yake kwa chama.
Kuhusu maamuzi ya kuteua, kuna viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa wale wa kuchaguliwa wanahitaji vikao rasmi kutengua au kujazwa kama hiki cha m/kiti wa mkoa ambacho Zitto amejichukulia madaraka mkononi yasiyo yake kwa kumpachika Shibuda, lakini wale wa kuteuliwa kama cheo cha Naibu Katibu mkuu na makatibu wote akiwemo yule wa Nzega haihitaji kikao chochote.
 
who is LEMA by the way?


lema.jpg
 
Zitto katika Chadema ni kama Lowassa katika CCM. Chadema wawe makini kwani Zitto ana tamaa ya madaraka na fedha hivyo huweza kutumiwa na yeyote ilimradi atimize lengo la kukidhi tamaa zake. Tamaa ya Zittoo ni kama Lowassa anayeponswa na tamaa zake sasa katika CCM.
 
Sunday, 01 May 2011 22:56

NI VITA YA KAMBI ZA MBOWE, ZITTO, SHIBUDA ANG'OLEWA KAIMU M/KITI SHY

Ramadhan Semtawa

VITA vya makundi vimezidi kuviandama vyama vikubwa vya siasa nchini, ambapo sasa hali si shwari ndani Chadema, ambako kunadaiwa kuwepo mkakati wa kumng'oa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, anadaiwa kuponzwa na msimamo wake kupinga ununuzi wa magari mitumba yenye thamani ya Sh480 milioni ya Chadema.

Hali hiyo ilijitokeza katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi juzi Jumamosi chini ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kikao ambacho pia kilimg'oa John Shibuda katika nafasi ya kukaimu uenyekiti mkoa wa Shinyanga.Shibuda ambaye ni mbunge wa Maswa Magharibi ameondolewa baada ya kukalia nafasi hiyo takriban kwa siku nne tu tangu ateuliwe, kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Shinyanga Philip Shelembi ambaye alizikwa April 27, 2011.

Chanzo cha mvutano
Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa kikao hicho zinasema kuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, ndiye alianzisha mvutano wa kutaka Zitto ang'olewe kutokana na kupinga wazo la kununua magari chakavu kutoka India.

Chanzo chetu cha uhakika kilidokeza kuwa mashambulizi dhidi ya Zitto yalianza pale alipounga mkono hoja ya Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo ambao walinukuliwa wakisema kwamba, isingekuwa sahihi kwa chama hicho kinachopinga ufisadi kufanya ufisadi kwa kununua magari chakavu wakati wamekuwa wakiibana serikali isifanye hivyo.

Baada ya Zitto kuunga mkono hoja hiyo, vyanzo hivyo nifafanua kuwa ndipo vurugu zilipoanza kwani Lema alianza kumrushia vijembe akisema kwamba Zitto ni tatizo na kwamba amekuwa akimtetea Shibuda.

Habari zinasema baadhi ya wajumbe walisema hoja ya Lema haikuwa na nguvu ya kumshutumu Zitto kwani Shibuda ni mbunge halali wa Chadema.

Duru zaidi za kisiasa kutoka ndani ya kikao hicho zinasema wakati mvutano huo ukiendelea, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alikuwa kimya huku kwa mara ya kwanza Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akiwa mmoja wa wajumbe waliomtetea Zitto.

"Wakati Lema akisema hivyo, Dk Slaa wakati wote alikuwa kimya na hakusema chochote. Mnyika alisimama na kumtetea Zitto kwa mara ya kwanza, na katika utetezi pia alikuwepo Grace Kiwelu," kiliweka bayana chanzo hicho.

Katika majibizano hayo inadaiwa ulifika wakati Zitto alisimama na kumwambia mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwamba mpango mkakati wake huo wa kujenga mtandao utakuja kumgharimu katika siku za usoni."Zitto alimwambia Mbowe mpango wake huo wa kujenga mtandao ungekuja kumletea matatizo hapo baadaye, "kilisema chanzo hicho kikimnukuu Zitto ndani ya kikao.

Kung'olewa kwa Shibuda
Mbali ya Zitto, Kamati Kuu hiyo pia iliazimia kutengua nafasi ya Shibuda, kukaimu nafasi ya uenyekiti ya Chadema mkoa wa Shinyanga.Vyanzo hivyo viliongeza kwamba, kabla ya mpango huo genge linalompinga Zitto lilimshutumu kwamba alikwenda Shinyanga na kushirikiana na baadhi ya wanachama kumweka Shibuda ili kutimiza ajenda zao.

Mvutano huo unaondelea ndani ya Chadema unazidi kukiweka chama hicho kinachokua na kuwa na malengo ya kukamata dola katika wakati mgumu kutokana na makundi mawili, huku moja likimuunga mkono Zitto na jingine Mbowe.

Zitto na Shibuda ni viongozi ambao wamekuwa wakikumbwa na misukosuko ndani ya Chadema na mara kadhaa Zitto amenusurika kung'olewa katika nafasi zake za uongozi kutokana na kile kinachodaiwa ni hulka yake ya kutofautina na wenzake hata katika mambo yenye maslahi kwa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Kauli za Zitto, Shibuda
Zitto alipoulizwa na Mwananchi jana jioni kuhusu tafrani hiyo alisema "….tafadhali sana, naomba nisiongee chochote kwa sasa, hiki ni kipindi cha kukijenga chama, si kipindi cha kuonyesha umma kwamba Chadema kuna mgogoro".

Pale mwandishi alipomhoji zaidi alisema "…tafadhali naomba nikupigie baadaye" kisha kukata simuKwa upande wake Shibuda alikiri kusikia taarifa hizo na kuongeza kwamba, anasubiri apate taarifa rasmi kwani yeye alipewa heshima hiyo na wanachama wa Shinyanga kupitia vyombo vyao vya maamuzi.
 
Duuh, watu mliozoea mfumo wa 'ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI' mnavyoweweseka pindi mnapoona DEMOKRASIA ya kweli ndani ya Chama Cha kisasa CDM inavyofanya kazi!!!!

Ehe, ndio mwisho wa uelewa wako unavyokueleza kwamba demokrasia ndani ya mijadala ndani ya vikao rasmi ya chama ni migogoro sio??????????

Laiti kama ingalikua ni kwamba watu siku zote hukubaliana kwa kila kitu asilimia mia kwa mia basi kusingekwepo na haja yoyote ya kuitisha VIKAO ambamo kimsingi watu hutegemewa kuleta mawazo tofauti juu ya jambo moja kabla ya wote hatimaye kukubaliana mwelekeo wa mambo.
 
Hivi hili suala la Shibuda limekaaje? Jamani kama alichaguliwa na wananchi au vikao vya maamuzi ya Shinyanga naomba CDM msivuruge utaratibu maana anakaimu tu na wakati wa uchaguzi basi itajulikana kama alikuwa mchapa kazi au la!!

Epukeni migogoro kwa kutomwondoa Shibuda kinyemela hata kama hafai.
 
Tofauti ya Chadema na CCM ni kubwa ndani ya CDM hakuna kitu kinachoitwa ndiyo mzee hata kama m/kiti ana hoja lazima aitetee hakuna kupita hivihivi tu kwa vile imetolewa na m/kiti. Ila kwenye ajali yeyote ile tahadhali lazima iwepo majeruhi huwa hawakosekani.
 
Hivi hili suala la Shibuda limekaaje? Jamani kama alichaguliwa na wananchi au vikao vya maamuzi ya Shinyanga naomba CDM msivuruge utaratibu maana anakaimu tu na wakati wa uchaguzi basi itajulikana kama alikuwa mchapa kazi au la!!

Epukeni migogoro kwa kutomwondoa Shibuda kinyemela hata kama hafai.
Shibuda is not a big deal in Chadema kwani aliambiwa anakaimu kwa siku ngapi hizo siku 4 zinamtosha kwa taarifa yako ameshaondolewa.
 
Usifikiri kila anayehamia CDM lazima apate cheo vigezo vinaangaliwa na loyality yake kwa chama.<br />
Kuhusu maamuzi ya kuteua, kuna viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa wale wa kuchaguliwa wanahitaji vikao rasmi kutengua au kujazwa kama hiki cha m/kiti wa mkoa ambacho Zitto amejichukulia madaraka mkononi yasiyo yake kwa kumpachika Shibuda, lakini wale wa kuteuliwa kama cheo cha Naibu Katibu mkuu na makatibu wote akiwemo yule wa Nzega haihitaji kikao chochote.
<br />
<br />
hebu taja mtu mmoja mwenye jina ambaye hakupewa cheo chadema. Taja kifungu cha katiba kinachoruhusu yule katibu wa Nzega kuvuliwa cheo!
 
pamoja kuwa wengine mnaona hii ni democrasia lakini mimi bado
naona kuna tatizo, hasa kutoka kwa huyo LEMA,
siwezi changia sana ila ili ni tatizo tena kubwa, kama hata dr wa ukweli alikuwa kimya!!!
kwanza hayo magari chakavu kwa nini watu LEMA anayatetea kwa nguvu kuna 10%
huyu ni wa kupiga chini atakitosa chama baharini tena kilindini kabisa
 
hii habari ilishajadiliwa hapa..kama vp iwe attached kuleee kwa mwanzo..i.e Shibuda out!!
 
Back
Top Bottom