Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 123,221
- 98,176
Kumekuwa na shutuma nyingi sana juu ya uongozi wa juu wa chama.
Shutuma za ubadhilifu wa rasilimali fedha ndani ya chama.
Huu ni ushuhuda kutoka kwa mmoja wa viongozi wa chama mkoa wa Kilimanjaro.
Tujadili wana Jf
---------------
Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mwanga, Mkoani Kilimanjaro Lembrus Mchome ametoa tuhuma dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, akidai kuwa amekuwa akikusanya fedha kutoka kwa wadau, wafanyabiashara na mashirika mbalimbali kwaajili ya shughuli za chama lakini fedha hizo hazijafikishwa kwenye mifuko rasmi ya chama.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mchome amedai kuwa suala hilo lilijadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema na kusababisha mvutano miongoni mwa viongozi, akimpongeza Godbless Lema kwa kile alichodai kuwa ni alisimama kidete kutaka fedha hizo ziwekwe wazi na kuwajibishwa kwa waliohusika.
"Tumekuwa na Makamu Mwenyekiti ambaye amekuwa akichukua fedha kutoka kwa wadau mbalimbali lakini zimekuwa hazifiki ndani ya chama. Ndio maana juzi kwenye Kamati Kuu wamegombana. Nimpongeze sana Godbless Lema kwani alisimama kidete kutaka fedha hizi zirudi, lakini haikuwezekana kwani Makamu Mwenyekiti alidai kuwa ameshazitumia na nyingine amenununulia vyombo vya muziki vya chama," alisema Mchome.
Mchome amebainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara waliowasiliana na Uongozi wa Chadema kupitia Kamati kuu iliyoketi Mkoani Kigoma walithibitisha kuwa walitoa michango kwa Heche kwaajili ya kukisaidia chama. Pia alidai Heche alisafiri hadi Afrika Kusini kwa lengo la kupokea fedha kutoka kwa wadau, akitoa rai ya wanachadema kumshinikiza Heche kujiondoa kwenye uongozi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.
"Sasa niwaombe wanachama wa Chadema tushikamane kumtaka John Heche atupishe kwanza kwaajili ya uchunguzi. Chama hiki kinaamini katika misingi ya haki na kupinga ufisadi, kwa hiyo kwanini leo tumfumbie macho Heche?" alisema Mchome.
Katika hatua nyingine Mchome amemtuhumu Heche kunufaika kisiasa na hali ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kuwa gerezani, akisema amekuwa akijijenga kisiasa pamoja na kutumia mwanya huo kuweza kufanya ubadhirifu kwa
Chanzo: Michuzi TV