BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Dar yaombwa kujitokeza sherehe za Uhuru
Godwin Myovela
Daily News; Saturday,December 06, 2008 @00:03
Wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Uhuru wa Tanganyika zitakazofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa zamani Dar es Salaam, Jumanne ijayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, alitoa mwito huo jana, ambapo alisema milango ya Uwanja wa Taifa itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi, na mgeni katika sherehe hizo atakuwa ni Rais Jakaya Kikwete.
Nachukua nafasi hii kuwaalikeni mhudhurie kwa wingi kwenye sherehe hizi, ambazo safari hii zitapambwa na gwaride maalumu la majeshi yetu ya ulinzi na usalama, ambayo Rais atapata fursa ya kuyakagua, alisema.
Aidha, alisema kutakuwa na halaiki iliyoandaliwa na wanafunzi takribani 2,000, ngoma za asili na michezo mingine mbalimbali. Aliwataka pia wamiliki wa vyombo vya usafiri hasa daladala, kuyaelekeza mabasi yao njia ya kwenda Uwanja wa Taifa ili kufanikisha maadhimisho hayo pamoja na kuwawezesha wananchi kushiriki katika tukio hili maalumu na la kihistoria.
Aidha, alitoa mwito kwa viongozi wa madhehebu ya dini, wazee, viongozi wa serikali, wakuu wa idara za serikali, taasisi, mashirika ya umma na viwanda, kuhamasisha waumini wao kuhudhuria kwenye maadhimisho hayo. Tanganyika ilipata Uhuru wake Desemba 9, 1961 kutoka kwa wakoloni wa Uingereza.

Last edited by a moderator: