Sherehe za Uhuru: Mkapa hakutokea tena

JK kasalimiana na waliokaa Jukwaani baada ya kupigiwa mizinga 21 pamoja na wimbo wa taifa kuimbwa lakini kilichowafurahisha wengi ni yeye kusalimiana na Mama Salma Kikwete.

Gwaride linaanza
Wamefurahi kwa nini?

Huyo rahisi haoni aibu kwa serikali yake ya kifisadi.
 
Namna ambavyo watoto wamejipanga haraka na kuitengeneza ramani ya Tanzania wamenifanya nijisikie faraja. Pamoja na kulala na kuamka wamependeza sana. Zanzibar imeonekna vema kabisa, maziwa yetu vema kabisa.

Ni ITV ambapo mpangilio huo umeonekana vema. Next time StarTv na TBC1 wawe makini sehemu za kuweka cameras
 
Imenifurahisha kumwona Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiimba pamoja na wanafunzi wa shule za msingi wimbo wa "Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote" (japo Mheshimiwa Karume hakuonekana kuimba kabisa). Naamini maneno yaliyo katika wimbo huo hakuwa anayaimba hivihivi bali yanatoka moyoni.
 
Kuhusu uhuru wetu,ni jambo zuri kwamba leo tunasherehkea miaka 47 ya uhuru.
Lakini nadhani statement ya Daily News ya kusema kwamba Ndugu Rais alisema juzi alipokuwa Mvomero,kwamba ,the government does have a monopoly to violence,nadhani this statement is very provocative.Kwa sababu hii ni sawa na kusema kwamba Ndugu Rais aliyetangaza vita dhidi ya ufisadi,sasa ametoa ruhusa kwa mafisadi kuwashambulia wananchi. Haya maneno yalizungumzwa kiswahili,na ningependa sana kufahamu ni nini hasa alichosema Ndugu Rais.
Lakini,ina maana kwamba Daily News ambacho ni chombo cha Serikali,linachochea fujo. Sasa uhuru uko wapi?Hata Freeman Mbowe jana alikuwa anaongea khusu mawaziri wanaoleta vitisho.
Mafisadi ambao wameliibia Taifa wanazungumza maneno haya,adding insult to injury.
Wao wanagombana na Serikali,na ni gari za Polisi ndizo zinazopiga hodi nyumbani kwao kuwapeleka Mahakamani. Kwa hiyo hawana sababu ya kugombana na raia wa kawaida.
 
Uhuru wa Mtanganyika bado uko shakani.

Wazee wetu walipambana kwa namna mbali mbali kupinga kutawaliwa na mkoloni mwishowe tukapata/kutwaa uhuru kama tunavyojua. Wazee wetu wakajaribu kuiinua nchi ikiwa mtoto ikue na kufikia utu uzima, kazi haikuwa ndogo, ilichosha na kukatisha tamaa.

Kwa jinsi ile ile ambayo zamani za mababu tulikuwa na kina Sultani Mangungo wa Msovero na Bwana Carl Peters, zama hizi zimerudi kwa staili ya tofauti japo mwisho wote wanafanya kile kile. Ninaona karaha kusikia kuwa Tanzania inasifika kwa kuwa na madini kwa wingi duniani. Zaidi ya hao wachache (kina Mangungo) makampuni ya kigeni yananufaika na rsilimali zetu. Mpaka leo huwa najiuliza hivi kweli naweza kufanya kazi BARRICK kwa amani kabisa toka moyoni (japo siwalaumu Watz wenzangu wanaofanya kazi pale). Mara ya mwisho kumsikia Mwanyika (wa Barrick) akiitetea hiyo kampuni kidogo machozi yanitoke.

Bwana utuhurumie Watanzania/Watanganyika.

Hongereeni kwa "uhuru" wetu kutimiza miaka 47.
 
Companero said:
Uhuru hatukuutwaa/pata/pewa/nyakua 1961 maana bado Malkia alikuwa ndio Mkuu wa Nchi yetu na Nyerere alikuwa ni mwakilishi wake!

..hoja hii kwa kweli ni kwa history-geeks.

..kuna wengine wanaweza kuhoji kwamba hata Malkia naye kwa jina la League of Nations/United Nations. kwamba Nyerere hakwenda kudai Uhuru kwa London kwa Malkia bali New York.

NB:

..hata wakina Japhet Kirilo walipokuwa na madai ya ardhi kule Meru walipeleka malalamiko yao League of Nations.
 
Date::12/9/2008
Mama Maria, Mwinyi wang'ara sherehe za Uhuru

mamanyerere.jpg

Mama Maria Nyerere akitoka nje ya Uwanja wa Taifa baada ya sherehe za miaka 47 ya Uhuru.

Jackson Odoyo na Exuper Kachenje
Mwananchi

MAMA Maria Nyerere na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, jana walikuwa kivutio katika maadhimisho ya Sherehe za Uhuru yaliyofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam baada ya kushangiliwa na umati wa watu waliohururia sherehe hizo huku viongozi wengine wakiingia kimya kimya.

Kitendo cha wananchi kuwashangilia viongozi hao kwa nderemo na vifijo bila hata kuhamasishwa ilileta utafauti mkubwa kati yao na Rais Jakaya Kikwete ambaye alishangiliwa na baadhi ya makundi hasa baada ya kutangaziwa na mwongoza sherehe.

Akitangaza wakati msafara wa rais unakaribia kuingia uwanjani huku watu wakiwa kimya, mwongoza sherehe huyo alisema: “Mabibi na mabwana tunayemtarajia kuingia uwanjani hivi sasa ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Kikwete, hivyo atakapo ingia uwanjani ninaomba tumshangilie kwa nguvu zetu zote”.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya tangazo hilo Rais Kikwete akaingia uwanjani kwa kutumia geti kubwa na kuzunguka uwanja akiwa katika gari la wazi la Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) ndipo makundi hayo yakijaribu kushangilia kwa sauti ya chini huku baadhi yao wakipeperusha bendera ya Taifa.

Viongozi ambao hawakushangiliwa hata kidogo na wananchi hao licha ya kwamba ujio wao katika uwanja huo ulitangazwa dakika chache kabla hawajawasili ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Amani Abedi Karume, Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa.

Viongozi wengine waliongia uwanjani hapo kimya kimya ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye, mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombare Mwiru na baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu ya nne wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Utawala Bora, Sophia Simba.

Kitendo cha Mama Maria Nyerere na Mwinyi kushangiliwa kilitafsiriwa na baadhi ya wananchi kwamba ni ishara ya uongozi wao mzuri ikilinganishwa na baadhi ya viongozi walioko madarakani na waliostaafu.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kitendo cha miaka ya Uhuru wa Tanzania kuzidi kuongezeka wakati uchumi wa nchi unazidi kuporomoka ni matokeo ya mikataba ya kifisadi.

“Takwimu za serikali kuanzia mwaka 2001 hadi 2007 unaonyesha kwamba wastani wa wananchi milioni mbili hawana ajira na idadi hiyo ni sawa na asilimia 30 ya watanzania wote na hii inatokana na mikataba ya kifisadi ambayo serikali imekuwa ikiingia,” alisema Profesa Lipumba.

Lipumba alisema hata hivyo maadhimisho hayo yanafanyika kukiwa na mambo ya kujivunia kama utulivu wa kisiasa pamoja na kuwa na serikali ya kiraia ni wakati muafaka wa kupima malengo ya uhuru.

"Ni siku ya nzuri ya kusherehekea uhuru wetu tukijivunia kuwa na serikali ya kiraia na utulivu wa kisiasa, lakini ni wakati muafaka wa kupima malengo yake," alisema Lipumba.

Alifafanua kuwa wakati wa uhuru malengo ilikuwa kupambana na madui watatui wakubwa aliowataja kuwa ni umasikini, maradhi na ujinga na kueleza kuwa uhuru haujatumika vya kutosha kukabiliana na maadui hao.

Alisema pamoja na hali hiyo, bado serikali haijajipanga vema katika sera zake na kuweka mipango mizuri ya kiuchumi itakayolikomboa taifa.

Naye John Momose Cheyo alisema katika miaka 47 ya uhuru wa Tanzania Bara, viongozi wana changamoto kubwa kuhakikisha wanatumia rasilimali zao kwa ajili maendeleo ya taifa.

Alisema siku ya uhuru si ya chama fulani bali ni ya watanzania wote kujenga utaifa na kwamba, sasa umefika wakati wa serikali kujijengea uwezo na kuwa na bajeti ya kujitegemea.

"Ni vizuri kujijenga, kujenga uwezo wa bajeti ya kujitegemea ili tuweze kugharamia maendeleo yetu wenyewe na kuachana na wafadhili kwani wanatupa masharti ambayo yanaweza kutukwamisha," alisema Cheyo.

Alisema inafaa kuiga mfano wa nchi jirani ya Kenya ambayo bajeti na uchumi wake kwa kiasi kikubwa hutokana na mapato yake.

Naye Mbunge wa Nkasi, Ponsiani Nyami (CCM), alisema kuwa katika kipindi chote tangu uhuru mpaka sasa kumekuwa na mafanikio makumbwa katika nyanya mbalimbali.

Alisema umoja, amani, utulivu na muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni moja ya mafanikio ya uhuru wa Tanzania Bara.

Alibainisha mbali na matatizo yaliyoikumba Tanzania kutokana na kushiriki kikamilifu harakati za ukombozi wa nchi za Afrika, bado taifa limeendelea kuwa imara.
 
Najua watu wanapenda headlines za namna hiyo.

Lakini Mkapa hajambo tu anakula pensheni tunayomlipa pole pole ingawa alishindwa kuonyesha heshima kwa taifa aliloliongoza kwa miaka kumi na kuendelea na miradi yake ya ANBEN wakati wa sherehe za uhuru
 
Najua watu wanapenda headlines za namna hiyo.

Lakini Mkapa hajambo tu anakula pensheni tunayomlipa pole pole ingawa alishindwa kuonyesha heshima kwa taifa aliloliongoza kwa miaka kumi na kuendelea na miradi yake ya ANBEN wakati wa sherehe za uhuru
Huyu 'mzee wetu' si hayupo Tanzania kwa sasa? Labda kama nasahau, ila nakumbuka kuna sehemu alienda kusuluhisha.
 
Kila binadam ameumbwa na aibu/haya ... sishangai kusikia kwamba Che Nkapa hakuonekana kwenye sherehe za Uhuru. Anaona noma sana kutokea mbele za watu na si ajabu anaogopa fasheni ya sasa hivi za kuzomea ama kuwaita fisadi viongozi wote waliotufisadi. Kuzomewa National Stadium mbele ya mabalozi ni aibu kubwa sana, na hiyo nadhani ni dawa nzuri sana hasa kama serikali inaogopa kuwaburuza mahakamani.

Kwa mwendo huo hata utamu wa mapesa aliyotufisadi walalahoi siuoni, maana huwezi kuyatumbua kwa nafasi bali kwa kujificha ficha huku ukiogopa kwamba walalahoi wanaweza kukuona na kuamua kukuzukia! Iko siku wananchi wakichoshwa watakuja kuvamia mali za mafisadi na kuziharibu!
 
Kesho kutwa tunatimiza miaka 47 toka Tanganyika ilipopata uhuru wake na baadae kuungana na kuwa Tanzania. Hapa kuna watu wenye elimu,ufahamu,ujuzi na kumbu kumbu za kila aina. Naona ni vyema,ukiona inafaa,ukachangia tuna kipi cha kijivunia na unawashauri nini wakuu wetu mpaka hapa tulipofikia? Unapongeza nini na unaona nini kifanyike ili kuboresha uhuru wetu?Wapi parekebiswe?


Najivunia:
1. Umoja wetu umerahisisha kuepuka vita vya kikabila, na tumeunganika kutambuliwa ka "WaTanzania"
2. Lugha yetu - kiSwahili. Inaenea ikiendelea kutuunganisha nchini na nje ya mipaka. Inakuza jumuiya ya 'WaSwahili'. Ni ya kiBantu, kwa hiyo waBantu wanaielewa na kutamka kirahisi.

Ningependa tuboreshe:
1. Elimu. Wengi wanakwamishwa na lugha ya kiingereza wanapobadilisha lugha za mafunzo wakimaliza primary school. Miaka ya primary schools ni miaka ambayo watoto wana uwezo mkuu wa kujifunza lugha. Naamini, kwa mfano, tukianza kufundisha kutumia kiingereza tokea darasa la nne, tutaboresha uwezo wa wanafunzi wetu kusoma (secondary schools na vyuoni nk) na kushindana na wanafunzi wa nchi nyinginezo vizuri. Alternative, ni kutumia kiswahili hata vyuoni, hii itamaanisha tuwe na vyuo vingi vyenye uwezo wa kisasa kutupa wanasayansi na madaktari wenye uwezo bora na wa kisasa. I don't stress on the latter, rather pointing out alternative ... otherwise, we at this economical stage, we will continue to have us and our children be educated abroad. Kwa hiyo, basi tuwape uwezo wa kusoma abroad, ama?

2. Wananchi wengi hatujui Katiba ya nchi yetu vizuri ama hata kidogo. Inamaanisha elimu na vyombo vya habari vinavofundisha wananchi havijafanya kazi nzuri ndani ya miaka hii 47. Tanzania imeacha ujamaa miaka mingi sasa, lakini bado tunatawaliwa tukitumia katiba ya zamani ya enzi za ujamaa. Ni kwa sababu elimu yetu ya katiba, sheria, na haki zetu ipo gizani.

3. Viongozi wetu bado wanatumia SIRIKALI kuongoza. Wananchi tunahitaji na tuna haki za kujua kazi za viongozi tuliowaajiri. Vyombo vya habari vinahitaji na vina haki ya kuchambua hizi kazi za viongozi wetu na ka vile wanatimiza ahadi zao zilizorekodiwa na kutupasha bila ubaguzi. Viongozi (Raisi na wale wa vijijini) wanahitaji kutumia vyombo vya habari, ama mikutano vijijini - labda mara moja kila mwezi - kutupasha vile walivotumia pesa shs x tulizowapa, ama walizopewa na wazungu... vile wanavotarajia kutumia ama kutenda kazi zipi... nk


tz%20flag%20final.gif
Mungu%20ibariki%20tz3.gif
 
wabongo bana????kuweni na uhakika wa facts mnazoandika sio kuandika tu for the sake of kuandika n at de end kushusha hadhi yenu..

huyo che nkapa si juzi sijui jana nimemuona cnn na bcc akiwa na obasanjo kusuluhisha matatizo ya congo huko? ama wako nkapa wawili?eti anakula miradi yake ya anben....loh
 
Sherehe za Uhuru: Mkapa hakutokea tena

kWANI LAZIMA AENDE, MTU ANISAIDIE JAMANI

Halafu kuba askari wangewekwa kuzuia asizomewe?? au yeye unafikiri hana mshipa wa aibu!
 
wabongo bana????kuweni na uhakika wa facts mnazoandika sio kuandika tu for the sake of kuandika n at de end kushusha hadhi yenu..

huyo che nkapa si juzi sijui jana nimemuona cnn na bcc akiwa na obasanjo kusuluhisha matatizo ya congo huko? ama wako nkapa wawili?eti anakula miradi yake ya anben....loh


Najua watu wanapenda headlines za namna hiyo.

Lakini Mkapa hajambo tu anakula pensheni tunayomlipa pole pole ingawa alishindwa kuonyesha heshima kwa taifa aliloliongoza kwa miaka kumi na kuendelea na miradi yake ya ANBEN wakati wa sherehe za uhuru

Mtaalam
Pole sana na kuhadaika; uwe unasoma posts mbalimbali kwa makini.
 
Hivi kwenye Sherehe za uhuru na nyinyi mnafanya BBQ kama huku mtoni? Labda Mkapa alikwenda kupasua kuni za BBQ.
 
Tangu kuibuka kwa kashfa za kufanya biashara akiwa Ikulu, ununuzi wa rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi na kutupora mgodi wa Kiwira amekuwa akizikacha dhifa za kitaifa mbali mbali. Kuanzia muungano na uhuru mwaka 2007 na mwaka huu pia. Anajua fika akifika pale uwanjani watu watampokea kwa vifijo vya fisadi fisadi fisadi ndiyo maana anaingia mitini anajua haya mambo ya kufanya biashara akiwa Ikulu, kashfa y rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi na kupora mgodi wa Kiwira yatanyamaza ili arudi tena ulingono na kuhudhuria sherehe mbali mbali za Kitaifa. Bado tunamkoromea mpaka atueleze Ikulu alikuwa anafanya biashara gani na alifanya na nani biashara hiyo na kuturudishia mgodi wetu wa Kiwira.
 
Back
Top Bottom