Sherehe za Uhuru: Mkapa hakutokea tena

anajua hakuna jipya.saaana JK ataanza kuwaimbisha nyimbo za kitoto za "happy birthday Tanganyika" na mtu principled kama mkapa hana sauti ya kuimbia nyimbo hizo
 
ujasiri wa kutokea mbele ya umati mkubwa wa watu aliowafisadi ataupata wapi? Mkapa hana huo ujasiri alitakiwa awe keko. Asherehekee uhuru upi wakati ali abuse ofisi
 
Jamani tuwe fair, Mkapa yupo Kenya akishughulikia mgogoro wa DRC na jana ndo kikao mhimu kilikuwa kinafanyika. Ni sahihi kumshutumu Bw. Mkapa kwa makosa aliyoyafanya lakini si haki kufanya hivyo pasipo sababu.
 
Uhuru hatukuutwaa/pata/pewa/nyakua 1961 maana bado Malkia alikuwa ndio Mkuu wa Nchi yetu na Nyerere alikuwa ni mwakilishi wake!

Yaani tulitwaa UHURU tulipokuwa JAMHURI? Mbona nchi za Jumuiya ya Madola zina Malkia kama mkuu wao, na bado zinasema zina UHURU? Wanadanganyana?

Tuna UHURU wa kujiamulia mambo yetu wenyewe? Mbona wahisani bado wanatuamulia?

Na tusisahau Madaraka ya Ndani ambayo tulipta mwaka 1960. Vipi, mbona hatuyashangilii. Maana zilikuwepo hatua tatu: Madaraka ya Ndani, Uhuru Kamili, na Jamhuri.

Kenyatta kaandika kitabu: "Not Yet UHURU". Is it not applicable to us?
 
JK kasalimiana na waliokaa Jukwaani baada ya kupigiwa mizinga 21 pamoja na wimbo wa taifa kuimbwa lakini kilichowafurahisha wengi ni yeye kusalimiana na Mama Salma Kikwete.

Picha walioipata Wabongo wengi walipomwona Muungwana anasalimiana na mkewe ni kwamba labda muungwana hakuamka kitanda kimoja na mkewe, kitu ambacho nadhani si kweli.

Katika hali ya kawaida asingeweza kuwasalimia watu wengine na kumruka mkewe kisa eti wameamka kitanda kimoja wakati pale wapo kwenye shughuli ya kitaifa hivyo suala la U'mke na U'mme havipo
 
Kenyatta kaandika kitabu: "Not Yet UHURU". Is it not applicable to us?

Heshima yako mkuu. Weka kumbukumbu zako vizuri. Not Yet UHURU kimetungwa na Oginga Odinga, siyo Jomo Kenyatta. Nimekisoma sana kitabu hicho mzee.
 
Jamani tuwe fair, Mkapa yupo Kenya akishughulikia mgogoro wa DRC na jana ndo kikao mhimu kilikuwa kinafanyika. Ni sahihi kumshutumu Bw. Mkapa kwa makosa aliyoyafanya lakini si haki kufanya hivyo pasipo sababu.

Shukrani mkuu kutupa habari hiyo. Binafsi nilijiuliza sana huyu mzee yupo wapi hata akaminya kujitokeza uwanjani! Hata hivyo, nadhani chenkapa kafurahi kuwepo huko kwenye kikao siku ya jana maana yale yaliyojiri jana pale uwanjani sidhani kama ANGEPONA. Watanzania walionyesha waziwazi kuwa wamechoka na ufisadi. Ni kwa sababu hiyo Mama Nyerere na mzee Mwinyi walishangiliwa sana walipoiingia uwanjani kuliko hata alivyopokelewa rais! Kwa kweli rais alipata " cold reception" japo MC alijitahidi sana kuwahamasisha watu wamshangilie mkuu wa kaya. Sasa nahisi cheNkapa angejitokeza tu wakati wananchi wana bifu zito naye na huyo Yona wake, Mramba nk, basi, shughuli ingekuwa pevu. " huyoooooo, huyoooooo, huyooooo, fisadi " tungevitarajia - hata kwa minong'ono ya chinichini tu (sababu ya kuogopa ulinzi).
 
Mkuu share nakubaliana nawe kabisa, lakini sijui kama picha hiyo itakuwa imemfikia Mkuu wa kaya maana washauri wake na wapasha habari wake bila shaka wanamdanganya kila siku. Wananchi wa Tanzania siyo wale wa enzi za zidumu fikra za Mwenyekiti, sasa hivi tunatumia ubongo wetu japo kwa kiasi kidogo.
 
Nadhani ujumbe kaupata wa cold reception kwani hata magazeti yameandika habari hiyo!
Ukweli ni kwamba wabongo tumepigika na tumechoshwa na serikali ya ki 'ze comedy'!
 
Angekuwa kenya akishughulikia hiyo migogoro yao bila uhuru wa tanganyika kuwepo? nini kimempa hata hako kanafasi kama sio uhuru wa tanganyika? maelezo mazuri ila bado hayajitoshelezi kutete hoja i li hapa jamvini
 
Ha..ha..habari ndio hiyo
 
Back
Top Bottom