Tuzungumze kwa reasoning. Hivi kama ingekuwa ni kweli kuna ubaguzi au hila za wakristo dhidi ya Uislam, wasomi wote wa kiislam na viongozi wote wa kiislam wameshindwa kuliona hilo mpaka walione akina Ponda wasio na upeo wowote? Hivi akina Kawawa, Aboud Jumbe, Rais Mwinyi, Salim Ahmed Salim, Rais Kikwete, Jaji Mkuu, Makamba (former katibu mkuu wa CCM), IGP, n.k. wote hawa wameshindwa kuuona huo mfumo gandamizi dhidi ya Uislam kiasi kwamba pamoja na kushikilia nafasi za juu kabisa za maamuzi wameshindwa kuuvunja? Huo mfumo unashikiliwa na nani hasa kiasi kwamba mawaziri wakuu, wakuu wa polisi, marais, wote washindwe kuugundua na kuuvunja? Yaani mnataka kutuaminisha kuwa Kikwete, Mwinyi, Said Mwema, Salim, hawakuwa waislam bali nao walikuwa wanatumikia mfumo wa kuwagandamiza waislam? Ukifika hapo ndipo unapoona watu wanaopiga hizi propoganda ni watupu wa dhamira na fikra. Mimi ni mkristo, nilisoma shule ya serikali, nikihudumiwa na mzazi mmoja baada ya kufariki baba yangu, nilipofika, najua hatua za taabu nilizopitia, sijawahi kufanya kazi ya serikali wala shirika la umma, watoto wangu wote hawajawahi kusoma shule ya serikali, wapo ndugu zangu ambao hawakumaliza hata darasa la saba, mbona huo 'mfumo wa Ukristo' sikuuona ukinisaidia wakati nikihangaika au kuwasaidia wale ndugu zangu ambao wengine hawakuweza kumaliza elimu ya msingi? Msaada pekee nilioupata kanisani ni mahubiri kuwa 'asiye fanya kazi na asile', na kwa lolote ulitendalo mtegemee Mungu, usikate tamaa maana Mungu humwinua yeye asiyekata tamaa. Maneno haya ndiyo wimbo wangu kwa watoto wangu leo. Mtoto wangu wa kwanza anasoma pale Feza, shule inayomilikiwa na Uturuki ambao 98% ya wakazi wake ni waislam, lakini kila mara ameweza kuwa wa kwanza darasani hadi kuzawadiwa U$1,000. Je, na pale Feza anapendelewa kwaajili ya Ukristo wake? Mnaozusha hizi tuhuma za kipuuzi mfikirie kwa makini. Tufanye kazi kwa bidii, daima tuwaambie watoto wetu umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii, kusoma kwa bidii kuliko kuwajaza ujinga wa kuwa wanaonewa. Matokeo yake wanajibweteka wakiamini kuwa kutofanikiwa kwao ni kwa sababu wanabaguliwa.