Sheikh Ponda yuko sahihi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Ponda yuko sahihi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwongozo, Jun 12, 2012.

 1. m

  mwongozo Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi Sheikh Ponda Issa ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Kutetea Haki za Waislamu alitanabahisha kuwa iwapo serikali haitoweka kipengele cha dini katika fomu za sensa ya mwaka, jumuiya yao itahamasisha Waislamu wasishiriki katika zoezi la sensa.Alisema kuwa nchi hii siyo ya Kikristo lakini INATAWALIWA NA MFUMO KRISTO.

  Alisema kutokana na mazoea, Waislamu wanabaguliwa katika mgawanyo wa keki ya taifa khasa upande wa ajira. ofisi na idara za serikali zinaongozwa na Wakristo kwa asilimia kubwa kulinganishwa na waislamu. alitoa mfano wa TRA, NECTA, Wizara ya Eimu, Wizara ya Ujenzi, Afya, Mahakama nk........... kwa mujibu wa Sheikh Ponda, wastani wa ajira ni karibu Wakristo 77% na Waisalmu siyo zaidi ya asilimia 20%. Licha ya hoja inayojengwa kuwa Waislamu hawajasoma lakini akasema waliosoma wapo.

  Akatanabahisha kuwa kwa maslahi na umoja wa kitaifa, kupuuza watu ambao ni sehemu ya jamii ktk keki ya taifa ni jambo hatari sana! Kwa kuwa wtu wanadai waislamu ni chini ya 20% katika nchi hii, akapendekeza sensa ya mwaka huu kiwekwe kipengele cha dini ili idadi ya watanzania kidini ijulikane. Kwa mujibu wa Sheihk Ponda, anaamini kuwa waislamu ni takriban 64% ya rais wa Tanzania.

  "SIYO SAHIHI WATU WENYE IDADI HII KUPUUZWA KATIKA UWIANO WA AJIRA SERIKALINI", alisema Sheikh Ponda.Alitoa mifano wa nchi karibia zote za Ulaya, Marekani, asia pamoja na Afrika, kipengele cha dili kipo kwenye fomu za sensa zao. "Ukisoma country profile au fact file uingiapo katika nchi mbalimbali, utakuta wameandika wastani wa idada ya raia kidini" alisisitiza Ponda. "Mbona mnajifanya kama hamtembei au hamjui kinacho endelea ulimwengunu jamani!" alilalama Ponda.

  HOJA YANGU Ndugu znaguni Watanzania, tufike sehemu tuache ukweli udhihiri. kama Waislamu wanalalamika kuwa wanabaguliwa katika ajira labda kutokana na uchache wao, kwa nini suala la dini lisiwekwe wazi? au utakua udini? au uchochezi? au uvunjifu wa amani? Kama ni hivyo, mbona karibu 98% ya sensa zote duniani zina kipengele cha dini!? je huko wameuana kutoakana na kipengele hicho? TUBADILIKE!!!

  Naomba kuwasilisha!
   
 2. S

  Starr Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waambie wafanye sensa yao wajue idadi ya waumini wa kiislam
   
 3. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Nadhani hii ni busara kwani muanisho huu wa kipengele cha dini ni muhimu hasa kukiwa na mipango inayohusu dini.. kama kujua tunahitaji kutenga ardhi kiasi gani kwa ajili ya misikiti/makanisa... au makaburi
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sheikh Ponda amejipa kazi ya kuenesha shari nchi hii. Pengine ni kwa sababu ya tatizo la ajira, lakini sioni ni kwa vipi waislam watakaa chini na kumsikiliza huyu semi-illiterate!<BR><BR>Week chache zilizopita alikuwa anapiga debe kuwaunga UAMSHO, sasa makanisha yamechomwa kakimbilia kwenye sensa! UAMSHO kawaacha kwenye mataa! Ni aina ya ma-sheikh kama hawa wanaoudhalilisha uislam. Hana la maana alilofanyia hii nchi zaidi ya kugawa watu.
   
 5. i

  isotope JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mi naona mnatafuta sababu nyingine ya kuandamana. Mtaandamana kupinga matokeo ya sensa, mtaandamana kutaka mkurugenzi wa Takwimu naye ajiuzulu. Mi nawajua, sensa ikitoa matokeo kinyume na matarajio yenu, kesho yake wote mko barabarani. Hebu jihesabuni wenyewe tu, maana mfumo wa sensa wa sasa hauwezi kutupa majibu ya contraversial issue kama hiyo ya idadi ya waislamu.
   
 6. nundaz

  nundaz JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  mwaka 2005 wakat kikwete anagombea askof mmoja alisema kik ete ni chaguo la mungu hawakulalamika! mwaka juz bakwata wakasema docta slaa hawez kuwa rais kisa mkristo! uchaguz igunga bakwata wakatoa tamko kuwa waislam kutopigia kura chadema! mwaka jana vuguvugu la maandamano ya chadema waislam wakasewa serikali inaandamwa sababu rais ni muislamu...! wametoka hapo wameandamana bla kbali, sasa wanakuja na ajenda za ajira na sensa...? ivii wao tu wanamatizo? wakristo hawana?
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Alonena ni suala zuri sana. vipengele muhimu va kuzingatiwa katika sensa ni pamoja na Umri, Dini, jinsia, hali za watu (ulemavu n.k) kwa ajili ya mipango ya nchi kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

  Ni vizuri kulijadili kwa kina kwa mustakabali bora wa nchi yenu katika mipango ya baadae.
   
 8. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Fanyeni sensa misikitini acheni lalama kila leo utadhani bi mdogo mnakera
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Wasukukuma tuko kama 8m ambayo ni 20% ya Watanzania. Vipi hilo Sheikh Ponda from Burundi?
   
 10. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi mwenyewe nataka hicho kipengele cha dini kiwepo kina faida zake jamani
   
 11. i

  isotope JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hapo matokeo lazima yatolewe kila kituo, halafu kuwe na mawakala wa dini zote ili kuhakikikisha hakuna uchakachuaji. Vinginevyo itakuwa ni chazo cha vurugu nchini.
   
 12. papason

  papason JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Kusema kweli kuna umuhimu kwa kipengele cha dini kuongezwa kwenye zoezi zima la sensa ya wa TZ
   
 13. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  mbona nyie wagala mnaogopa sana hiki kipengele? Kuna nini kimejificha?
   
 14. m

  mfumo JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ahsante mwongozo kwa taarifa hii.
  Nakufagilia sheikh ponda, hayo uliyosema ni kweli tupu. Nafurahi pia kusikia mkutano wa jana wa sensa dodoma waislamu wote pamoja na bakwata wamekubaliana kususia sensa ya mwaka august 2012 kama kipendele cha dini hakitakuwepo kwenye fomu ya sensa. Cha kushangaza zaidi maaskofu wao wanataka kipengele hicho kisiwepo ati kitahatarisha amani. Amani itaharibika vipi ikiwa tutajua idadi ya waislamu wangapi na wakristo wangapi? Maaskofu walishindwa kujibu swali hili!!!!!! What is behind the scene maaskofu??? Kuna jambo gani limejificha hapa mpaka hamtaki tujue idadi yetu kutokana na dini zetu?!!
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0

  Kuna kitu kimejificha hapo.

  Mbona mkiwa mnatoa maelezo Polisi mnaandika sio tu kabila mpaka dini mnabainisha. Kwenye vitabu vya wageni hotelini na nyumba za kulala wageni mbona kunakipengele cha dini na kabila. Kwanini msikiweke hata kwenye sensa zenu.

  Nafikiri kiuchumi wanazuia kuona ni misada au misamaha ya kodi kiasi gani wanayopata dini moja dhidi ya zingine na kunufaika kwa namna gani kiuchumi dhidi ya wengine.

  Kuna mengi sana . Lakin msingi mkuu ni mipango ya nchi yenu kuweka usawa wa kitabaka na kijamii kwa kupata taarifa sahihi ndani ya sensa.
   
 16. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hivi kuwa shekhe inabidi uwe na elimu gani...?
  maana reasoning lazima iwepo eb nisaidieni jamani....!
   
 17. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hivi akijua waislam ni asilimia 70 ndiyo itamsaidia nini? watu wanafikiria namna ya kuitoa nchi katika umaskini yeye anafikria kuzaa ili idadi ya waislam iwe kubwa kuliko dini nyingine, bila kujiuliza ili hao watoto wengi wanahitaji kupelekwa shule ili waweze kujikwamua katika maisha yao ya baadaye. Kama lengo ni kufahamu Waislam wako wa ngapi katika kila msikiti au mtaa kuna jumuiya ya kidini watumie hizo jumuiya kujihesabu kama lengo ni kujua idadi yao. Unajua inachosha mara mahakama mnataka, mara ajira, ni kweli kuwa hajui ajira zinatolewa kwa ushindani? Si ajabu Tanzania hatuendelei leo mtu kama huyo apewe nafasi ya kuwa Waziri wa Utumishi wa Umma sijui nini kitatokea. Shuleni tunaonewa, mtaani tunaonewa, kazini tunaonewa bado kwenye familia nako mtakuja hapa na kusema tumeingiliwa. Tutumie muda wetu kufikiria maendeleo ya nchi badala ya kuendekeza ubinafsi wa kidini. Nchi haijengwi kwa kujua idadi ya waislam kwenye mji au mtaa fulani.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Barubaru,
  Kwani namba ya waamini wa dini yako, hata kama ni kubwa ina faida gani kwa uwepo na ustawi wa Taifa hili? Kama namba ni tija, waafrika tulivyo, tunaweza kuanzisha mashindano ya kuzaana bila utaratibu, bila kujua kwamba anayeongoza dunia ya leo sio kwamba ana namba kubwa, la hasha!!! Ana elimu, uwezo na ujuzi mkubwa.
  Ndio maana waisrael kwa idadi ni wadogo lakini pale walipo waliwahi kupigana na mataifa karibu yote yaliowazunguka kwa wakati mmoja na kuwashinda. It was not by chance....it was by design and intelligence to come with victory. So hoja hapa kwetu sisi wengine ni kuhakikisha generations zetu zina aim higher kwa kutafuta mambo ya msingi yatakayotusukuma huko. Sio haya mambo ya kujua nani ni dini gani! So what?
   
 19. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #19
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Halafu wakokotoe kwenye idadi itakayopatikana ya watanzania wote ili wajue waislam ni roughly asilimia ngapi ya population ya tzii
   
 20. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  ha ha ha mkuu umenichekesha sana....... kwani kusudi la sensa ni kujua kati ya wakristo na waislam wepi ni wengi??? ha ha ha ha hata hivyo suala la dini sio la kudumu sana.... vijana wa siku hizi wanabadili dini kama vyama vya siasa vile
   
Loading...