Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,325
Barubaru maendeleo ya nchi yanapangwa kwa kuangalia dini?
kama mnataka kujua mko wangapi jihesabuni wenyewe kama wakristo wanavofanya ktk jumuia,parokia,usharika nk... waziri wa fedha anavosoma bajeti huwa anasema bejti hii ni ya waislamu na hii ni ya wakristo au inamlenga kila Mtanzania?
Labda nikuulize. Kipengele cha Jinsia kina maana gani wakati wote ni watu? kinasaidia nini katika mipango ya nchi?
Lakin kwa kukusaidia unahitaji sana kufikiri nje ya box. Unapotaka kupanga maendeleo ya nchi ni lazima uangalie jamii husika kuna kitu kinaitwa mila na desturi na sirka za jamii husika ndanimwe utaangalia hata dini yao ili kuweka kitu ambacho kitaendana na jamii husika bila kukiuka maadili ya mila na desturi zao.
Lakin pia hata hivi sasa mnazungumzia kuwawezeha wanawake katika uongozi na utawala na elimu hususan masomo ya science. Inakubidi ujue idadi yao na kupanga mikakati. lakin hata pale mnaposema waislam hawajasoma ni vizuri kupanga mikakati ya kuwaendeleza kama inavyofanywa kwa kabila la wahazabe au wabarbaidi. Hiyo ni mifano tu ya kuendeleza makundi fulani ya jamii kwa kuyapa kipaumbele katika maendeleo.
katika kupanga maendeleo siku zote tunaangalia maeneo duni na kuyapa pesa nyingi za maendeleo kulinganisha na sehemu zilizoinuka.
Funguka utayaona mengi. Sioni sababu mpaka sasa kuondoa kipengele cha DINI. labda tu sababu ya msingi.