JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Shaka Hamdu Shaka Jumanne
26 Oktoba, 2021 ametembelea Ofisi za Bodi ya Mikopo ya wanafunzi elimu ya Juu zilizopo maeneo ya Tazara Wilaya Temeke Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na viongozi na watendaji wa bodi hiyo.

#ChamaImara
#KaziIendee

IMG-20211026-WA0196.jpg

IMG-20211026-WA0190.jpg
 
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA, ITIKADI NA UENEZI SHAKA HAMDU SHAKA, ATUA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Shaka Hamdu Shaka Jumanne
26 Oktoba, 2021 ametembelea Ofisi za Bodi ya Mikopo ya wanafunzi elimu ya Juu zilizopo maeneo ya Tazara Wilaya Temeke Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na viongozi na watendaji wa bodi hiyo.

#ChamaImara
#KaziIendee

View attachment 1987465

View attachment 1987470

View attachment 1987471

View attachment 1987472
Hii m!j!ng@ ya bodi ya mkopo full uoga. Ndio maana ilikua batch ya nne wapewe actually imeandikwa wacheki ijumaa hii tarehe 29 October.

All of a sudden Leo wamerelease mikopo.

Bila punda kupigwa mijeled haendi.

Body language explains it all in the photos.
 
Hao HESLB nikikundi cha wasiotenda haki. Hebu fikiria mtu amesoma private tangu nursery mpaka kidato cha sita wazazi wake wapo na wanauwezo na anapewa mkopo kisha wananyimwa yatima na wengine wanaachia vyuo katikati.

Mh.Rais anatakiwa asafishe hilo jengo kuanzia huyo Mkurugenzi mpaka wapanga mafaili.
 
shaka na bodi za mikopo kuna muhusu nini kuleta siasa ccm ili kupata wapiga kura 2025 ndani ya ccm
 
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA, ITIKADI NA UENEZI SHAKA HAMDU SHAKA, ATUA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Shaka Hamdu Shaka Jumanne
26 Oktoba, 2021 ametembelea Ofisi za Bodi ya Mikopo ya wanafunzi elimu ya Juu zilizopo maeneo ya Tazara Wilaya Temeke Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na viongozi na watendaji wa bodi hiyo.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeielekeza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuendelea kutoa kipaumbele kwa kundi la watoto masikini na wenye mahitaji maalumu wenye vigezo vya kunufaika.

Pia, kimeipongeza bodi hiyo kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuwafikia wanafunzi, huku ikisema ongzeko la marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika kulikotokana na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kufuta Kodi ya ongezeko la zuio kwenye Mikopo ya elimu ya Juu (Retention fee), ni kielelezo cha ufanisi.

Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, alipotembelea HESLB kuona jinsi inavyofanya kazi.

Shaka alieleza kuwa, Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ibara ya 80 (h) inasema serikali itaimarisha na kuboresha mfumo wa ugharimiaji wa elimu ya juu ikiwemo bodi ya mikopo ya Juu, ili kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wenye uhitaji na sifa stahiki wanapata fursa ya kujiunga na elimu ya juu.

Alisema Rais Samia ameonyesha dhamira ya dhati kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa ya kusoma ambapo, ameongeza mkopo wa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka sh bilioni 464 hadi sh. bilioni 570.

#ChamaImara
#KaziIendee

IMG-20211026-WA0029.jpg

IMG-20211026-WA0030.jpg

IMG-20211026-WA0036.jpg
 
Je, umewauliza kwa nini hadi leo hii wanafunzi wengi walioomba mikopo hawajapatiwa na wamechelewa kuripoti au kukamilisha usajli wao?

Usiende tu kupiga picha huku wazazi wako hoi wanawaza na kuwazua.
 
Wakimaliza mnawasihi wajiajiri, wakijiajiri kama wamachinga, mnawazingua.
 
Bodi hii ina wafanyakazi wa hovyo sana, unamaliza makato ya marejesho ya mkopo wanapumzika makato mwezi mmoja mwezi unaofuata wanaanza kukukata tena, kupata clearance ya kumaliza marejesho ya deni au statement mpaka uwafuate Temeke na uwape rushwa.
 
Lakini Huyu Jamaa anajitahidi kufanya Mambo yenye Mashiko

Sio Kama Kale Kazee Kachawi ka Chakubanga
 
Napenda sana viongozi wanaofuatilia maisha ya wananchi, hasa wanyonge na kutoa maamuzi yenye kuleta matokeo chanya. Hongera ndugu Shaka.
 
Hao HESLB nikikundi cha wasiotenda haki. Hebu fikiria mtu amesoma private tangu nursery mpaka kidato cha sita wazazi wake wapo na wanauwezo na anapewa mkopo kisha wananyimwa yatima na wengine wanaachia vyuo katikati.

Mh.Rais anatakiwa asafishe hilo jengo kuanzia huyo Mkurugenzi mpaka wapanga mafaili.
Wakati mwingine nawalaumu hao Bodi ya Mikopo. Kuna baadhi yenu mnatoa taarifa za uongo ili mpata kikubwa. Mnapobainika na kushughulikiwa ndio mnakuja humu JF na mitandao mingine kulia lia. Kuweni waaminifu!
 
Kawapelekea ilani ya chama na majina ya tu uvccm tudogo tudogo kupate mkopo, badala ya kuacha heslb kufanya kazi kwa KPI zao
 
Ule ni mkopo na unatokana na kodi za wenye pesa na wasio nazo,
Unapaswa kupigania wote mmpate sio kutaka wenzio wakose upate wewe

Inawezekana kote kasoma Wazazi wakiwa na pesa na kafika chuo kikuu wazazi hawana pesa au wanasogeza wadogo zake ambao nao wamefikia kiwango cha kwe da Shule

Umaskini na unyonge sio tiketi ya kutaka kila haki ya Serikali kwa Raia ianzie kwako

Back
Top Bottom