Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Shaka Hamdu Shaka Jumanne
26 Oktoba, 2021 ametembelea Ofisi za Bodi ya Mikopo ya wanafunzi elimu ya Juu zilizopo maeneo ya Tazara Wilaya Temeke Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na viongozi na watendaji wa bodi hiyo.

#ChamaImara
#KaziIendee

View attachment 1987465

View attachment 1987470
Good boss, Shaka amekuwa mtulivu sana na mtu mfikiri masikini wakati wote,

Hongera Crde Shaka
 
Ule ni mkopo na unatokana na kodi za wenye pesa na wasio nazo,
Unapaswa kupigania wote mmpate sio kutaka wenzio wakose upate wewe

Inawezekana kote kasoma Wazazi wakiwa na pesa na kafika chuo kikuu wazazi hawana pesa au wanasogeza wadogo zake ambao nao wamefikia kiwango cha kwe da Shule

Umaskini na unyonge sio tiketi ya kutaka kila haki ya Serikali kwa Raia ianzie kwako
Kwanza wazazi wenye pesa ndio walipa kodi. Mkopo ni haki ya kila mwanafunzi wa elimu ya juu.
 
Ule ni mkopo na unatokana na kodi za wenye pesa na wasio nazo,
Unapaswa kupigania wote mmpate sio kutaka wenzio wakose upate wewe

Inawezekana kote kasoma Wazazi wakiwa na pesa na kafika chuo kikuu wazazi hawana pesa au wanasogeza wadogo zake ambao nao wamefikia kiwango cha kwe da Shule

Umaskini na unyonge sio tiketi ya kutaka kila haki ya Serikali kwa Raia ianzie kwako
Hapa ndio wengi hukosea. Kigezo cha kutompa mtu mkopo kisiwe alisomaje huko nyuma bali kama kwa sasa damilia yake inajiweza kumsomesha.

Imagine una baba director wa kampuni kubwa kwa miaka mingi. Ina maana shule utakazosoma zitakuwa ghali. Now imagine same baba akaugua kwa muda mrefu mkatumia resources kumuuguza mpaka kupona, then akawa hawezi tena kufanya ile kazi.

Kumnyima mkopo mtoto itakuwa ni kumwonea. Kama ambavyo mtoto amesoma kayumba kwa sababu mzee alikuwa anatafuta ilq by the time anaingia chuo baba ni alwatan bilionea. Huyo anapaswa kuwa chini kwenye priority regardless ya historia
 
Kama vile aliendatu kupiga nao picha maana wanadai hawaendeshwi na CCM wao nitaasisi huru.
 
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA, ITIKADI NA UENEZI SHAKA HAMDU SHAKA, ATUA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Shaka Hamdu Shaka Jumanne
26 Oktoba, 2021 ametembelea Ofisi za Bodi ya Mikopo ya wanafunzi elimu ya Juu zilizopo maeneo ya Tazara Wilaya Temeke Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na viongozi na watendaji wa bodi hiyo.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeielekeza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuendelea kutoa kipaumbele kwa kundi la watoto masikini na wenye mahitaji maalumu wenye vigezo vya kunufaika.

Pia, kimeipongeza bodi hiyo kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuwafikia wanafunzi, huku ikisema ongzeko la marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika kulikotokana na uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kufuta Kodi ya ongezeko la zuio kwenye Mikopo ya elimu ya Juu (Retention fee), ni kielelezo cha ufanisi.

Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, alipotembelea HESLB kuona jinsi inavyofanya kazi.

Shaka alieleza kuwa, Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ibara ya 80 (h) inasema serikali itaimarisha na kuboresha mfumo wa ugharimiaji wa elimu ya juu ikiwemo bodi ya mikopo ya Juu, ili kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wenye uhitaji na sifa stahiki wanapata fursa ya kujiunga na elimu ya juu.

Alisema Rais Samia ameonyesha dhamira ya dhati kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa ya kusoma ambapo, ameongeza mkopo wa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka sh bilioni 464 hadi sh. bilioni 570.

#ChamaImara
#KaziIendee

View attachment 1987798

View attachment 1987799

View attachment 1987801
Maboss hao wa mikopo wamenonaa kweri kweri

Ova
 
Back
Top Bottom