Rais Samia ameongeza Bilioni 654 bajeti Mikopo Elimu ya Juu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
"Mikopo ni fedha. Tangu shughuli ya kukopesha fedha imeanza miaka 19-20 takriban Tril.7. 3 zimewekezwa. Huu unaitwa ni uwekezaji wa Serikali katika rasilimali watu. Na wanufaika Laki Saba wamepata mikopo.

"Katika miaka Mitano au Sita kuanzia 2020-21 kiasi cha bajeti kilichopitishwa ni Bil. 464 na wanufaika walikuwa Laki na Nusu. Mwaka uliofuata ni Bil. 570

"Wakati Mama, Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia mwaka 2021-22 ameongeza kwa kiasi kikubwa sana kutoka Bil. 464 hadi 570 ni ongezeko kubwa sana na halijafanyika kwa miaka mingi wakanufaika wanafunzi Laki moja na sabini na saba.

"Na mwaka Jana ilikuwa Bil. 654 wanufaika Laki moja na tisini na huu mwaka wanufaika watakuwa Laki mbili na ishirini na bajeti ni Bil.786." Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru

#PBCloudsFM
 
Acheni kutia watu hasira Mimi sioni kuwa wameongeza,binafsi naona ni siasa zinatumika kutudanganya hamna huhalisia wowote, Kuna watu kibao wako nyumbani wamenyimwa alafu mnaleta mapambiao yasio na tija ,nenda vyuoni kuna wanafunzi kibao hususani mwaka wa Kwanza hawaamini walichokutana nacho na ZAIDI WENGI WAMEAMUA KUSITISHA MASOMO
 
Dhana ya mikopo ni dhana ambayo binafsi siikubali kwa kuwa 80% ya fedha hazitaweza kurudishwa,
Dhana yangu ni mfaulu na mwenye uwezo kimasoma, asonge mbele mpaka kikomo, chake, kwa facilitation zote, vitabu viwepo, chakula safi kiwepo, na malazi safi yawepo, mifumo ya elimu ya veta iimarishwe,pass mark zipandishwe, ili atakayestahili awe kweli amestahili favour ya serekali,huu ndio mfumo utakaotuondolea viongozi wabovu na wajinga hapo baadae.
 
Utaratibu awali ndo ulivyokuwa, serikali ilikuwa inatoa ufadhili kwenye vyuo vikuu vya umma ambako wanafunzi wote waliofaulu vizuri walikuwa wanadahiliwa huko........baadaye wajanja wakachomeka hoja kwamba serikali ianze kufadhili wanafunzi hadi vyuo binafsi, ndo hapo utitiri wa vyuo na kozi vikaanzishwa na serikali kuanza kuzidiwa na idadi ya wanafunzi.

Utaratibu wa awali ulikuwa mzuri kwani serikali ilikuwa na uwezo wa kupanua vyuo vyake au kuongeza udahili kulingana na bajeti waliyo nayo.

Mwisho wa siku wameishia kuharibu elimu na future ya watoto wa watanzania walio wengi ambao watoto wao wamefaulu na kuchaguliwa vyuo vikuu vya umma na serikali kuwanyima ufadhili wa masomo yao, ni jambo linalosikitisha sana.​
 
Serikali inajukumu la kiwasomesha watu wake!
Na kama ni mkopo wapewe wanaostahiki bila masharti kuwawezesha kusoma!
Baada ya kuhitimu wapewe ajira ili waweze kurejesha mikopo yao!
Kuhusu idadi ya vyuo vikuu... Ikiwezekana viongezwe viwe vingi! Kila mkoa kuwepo chuo!
Elimu si anasa!
 
Utaratibu awali ndo ulivyokuwa, serikali ilikuwa inatoa ufadhili kwenye vyuo vikuu vya umma ambako wanafunzi wote waliofaulu vizuri walikuwa wanadahiliwa huko........baadaye wajanja wakachomeka hoja kwamba serikali ianze kufadhili wanafunzi hadi vyuo binafsi, ndo hapo utitiri wa vyuo na kozi vikaanzishwa na serikali kuanza kuzidiwa na idadi ya wanafunzi.

Utaratibu wa awali ulikuwa mzuri kwani serikali ilikuwa na uwezo wa kupanua vyuo vyake au kuongeza udahili kulingana na bajeti waliyo nayo.

Mwisho wa siku wameishia kuharibu elimu na future ya watoto wa watanzania walio wengi ambao watoto wao wamefaulu na kuchaguliwa vyuo vikuu vya umma na serikali kuwanyima ufadhili wa masomo yao, ni jambo linalosikitisha sana.​
Elimu haiharibiwi chuo kikuu,mwanafunzi wa chuo hafundishwi kama form 3,hukuwepo pengine kabla ya utaratibu wa mikopo,udsm ilikua ikichukua wanafunzi elfu nne,mtu una division two hupati nafasi chuoni,leo kwenye kampuni nyingi na nafasi nyingi serikalini kuna vijana waliopata elimu ya juu kupitia mikopo,kama ulipata mikopo na ipo ofisini basi jus utaulipa tu,wengi wa mwanzo wamemaliza julio's mikopo yao,rundo la watu wanaohitaji kuingia chuo linalotokana na ongezeko la watu,serikali haiwezi midi kulifadhili
 
"Mikopo ni fedha. Tangu shughuli ya kukopesha fedha imeanza miaka 19-20 takriban Tril.7. 3 zimewekezwa. Huu unaitwa ni uwekezaji wa Serikali katika rasilimali watu. Na wanufaika Laki Saba wamepata mikopo.

"Katika miaka Mitano au Sita kuanzia 2020-21 kiasi cha bajeti kilichopitishwa ni Bil. 464 na wanufaika walikuwa Laki na Nusu. Mwaka uliofuata ni Bil. 570

"Wakati Mama, Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia mwaka 2021-22 ameongeza kwa kiasi kikubwa sana kutoka Bil. 464 hadi 570 ni ongezeko kubwa sana na halijafanyika kwa miaka mingi wakanufaika wanafunzi Laki moja na sabini na saba.

"Na mwaka Jana ilikuwa Bil. 654 wanufaika Laki moja na tisini na huu mwaka wanufaika watakuwa Laki mbili na ishirini na bajeti ni Bil.786." Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru

#PBCloudsFM
Utapeli wa kijinga Bado hamjaacha? Hizi story za kupika kawaambieni wale mnaowabeba na Malory maana ndio hawana ufahamu wowote.
 
Acheni kutia watu hasira Mimi sioni kuwa wameongeza,binafsi naona ni siasa zinatumika kutudanganya hamna huhalisia wowote ,Kuna watu kibao wako nyumbani wamenyimwa alafu mnaleta mapambiao yasio na tija ,nenda vyuoni kuna wanafunzi kibao hususani mwaka wa Kwanza hawaamini walichokutana nacho na ZAIDI WENGI WAMEAMUA KUSITISHA MASOMO
Sasa hapa anayeongelea hisia ni nani kama sio wewe?
 
Utapeli wa kijinga Bado hamjaacha? Hizi story za kupika kawaambieni wale mnaowabeba na Malory maana ndio hawana ufahamu wowote.
Ndio na wewe ushaambiwa sasa na unashiriki mjadala hapa
 
Tumekutana na wanafunzi kibao wanalalamika wamekosa mikopo Tena Wana div 1.7 ingawa wapo waliopewa Hadi wa diploma.
I hope unafahamu kuwa ufaulu sio kigezo pekee cha kupata mkopo na pia sio wanafunzi wote watapata mkopo
 
Back
Top Bottom