Mikopo Kwa Wanafunzi Wa Elimu ya Juu (Vyuo vya Kati na Vikuu)

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
8,293
8,855
Habari Watanzania wenzangu

Napenda nami nitoa mchango wa mawazo katika hiki kilio wanacho kutana nacho wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania bara

Pia mnivumilie kwa kuwa sio muandishi mzuri sana japo nimewiwa kuandika na Nina imani wapo watao nielewe japo kwa uchache wake na watakao kuwa na mawazo ya kuongezea au kujadili ili kunogesha mnakasha huu, basi litakuwa jambo jema na zuri

Nimeona manung’uniko mengi sana hapa JF toka kwa wazazi, ndugu, jamaa, marafiki na wazazi kwa ujumla kwa jinsi ambavyo hawa kulizishwa na zoezi linalo endelea la utoaji wa mikopo na kupelekea wanafunzi wengi kukosa mikopo na wengine kupata katika kiwango ambacho hakitoi faraja kwa wahusika kuweza kufikia malengo yao,

Bodi ya mikopo imekuwa mkombozi kwa familia nyingi za watanzania kwa kusaidia kiuchumi wanafunzi pamoja na kundi kubwa lilonyuma ya wanafunzi hao pia, Tuna ipongeza sana kwa utendaji wao pamoja na kuwa na changamoto mbili tatu hasa baada ya kuwa na mzigo mkubwa sana wa kutoa mikopo kwa hivi sasa kuanzia ngazi ya cheti mpaka PG kama sikosei, wakati huko nyuma walikuwa na wanufaika wachache tu wa ngazi ya digrii tofauti na ilivyo sasa

Changamoto ni nyingi sana pamoja na wanufaika kutoweza kulipa mikopo yao kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali, hivyo kupelekea ufanisi wa utoaji mikopo kushuka

Lakini pia pamoja na yote kuwa tuna changamoto nyingi katika bodi yetu hii ambayo imefanya mazuri mengi na inaendelea kufanya, bado wadau wote wa elimu nchini tuna wajibu wa kufanya jambo kupunguza huu mzigo walio nao Bodi ya mikopo ya elimu ya juu, na ni kwa nia njema ya kusaidia jamii yetu

Ni vyema kila mdau wa elimu aweze kuwajibika kusaidia maendeleo ya taifa letu, iwe kwa mawazo jinsi ya kuboresha utendaji, jinsi wanufaika wanavyo paswa kuwajibika, wazazi au walezi na taasisi nyingine

Kuna mikopo mingi ya aina mbalimbali inatolewa na taasisi mbalimbali kama:-

1. Mikopo ya Mama samia
2. Mikopo toka BOT
3. Mikopo ya MO foundation
4. Mikopo toka UDSM
5. Mikopo nazani toka NMB
6. Mikopo nazani toka CRDB

Hii ni mikopo kwa uchache ninayo ifahamu, inaweza ikawa ipo zaidi ya hii au kuna mingine haipo

Maoni/ushauri
1. Kwanza wanafunzi wachangamkie mikopo ya aina mbalimbali iliyopo mbele yao ili kuongeza wigo wa kupata kunufaika na mikopo inayotolewa na taasisi mbalimbali nchini

2. Walio pata kunufaika na mikopo ya elimu ya juu, warejesho mikopo hiyo ili iweze kunufaisha na wengine wenye uhitaji ili tusije pelekea kuvunja kwa bodi husika kwa kushindwa kujiendesha

3. Serikali ione umuhimu wa kufuta ada kwa elimu ya chuo Au vyuo vikuu vya serikali pekee kama walivyofanya kwa ngazi zingine za elimu (Msingi na Sekondari) ikishindwa kabisa basi watoe ruzuku ambayo itasaidia kupunguza ada angalau kwa hadi 50%

4. Vyuo vyote nchini vione umuhimu wa kujifunza toka chuo kikongwe UDSM kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wake

5. Serikali za wanafunzi pia zione umuhimu wa kutoa mikopo Au ufadhiri kwa wanafunzi kupitia pesa wanazo kusanya kwa kila mwanafunzi (mara nyingi wanufaika huwa ni marais wa Vyuo na viongozi wengine wa juu kwa kujilipa nk)

Nilitegemea wanafunzi ambao ndio wahanga na tunao wategemea ktk mustakhabari wa taifa letu, basi wangeweza kuja na mawazo mazuri ata kutoa ufadhiri wa ada 50% mpaka 80% kwa wanafunzi wenye uhitaji, na hili wakalitizame wakashauriane na Vyuo vyao kuweza kufanya kitu kizuri

6. Halmashauri za wilaya, manspaa, majiji; wana makusanyo mengi sana ambayo wanapata kutoka ktika vyanzo mbalimbali walivyo navyo, wana weza kutumia ata asilimia kadhaa toka ktk makusanyo yao kuweza kusomesha vijana 10 hadi 20 kwa kila mwaka, vijana toka ktk maeneo yao ya kiutendaji na kiutawala maana wao ndio wapo karibu zaidi na vijana husika

7. Taasisi mbalimbali; kuna NGO ambazo zipo kusaidia jamii mbalimbali mfano watu walio kwenye mazingira magumu, wanawake, kuinua vijana nk nazani na zenyewe zitenge fungu kusaidia wanufaika wao ktk maswala ya kielimu

8. Tutengeneze sheria nzuri ambazo zitawabana wadau mbalimbali kama makampuni, mashirika mbalimbali waweze kusomesha walau vijana wawili mpaka watano kila mwaka

Tuna makampuni ya migodi, usafirishaji, utalii, tumbaku (kilimo) nk

Tuna mashirika mbalimbali ya misaada ya kimataifa na kitaifa yaweze kuchangia zaidi ktk nyanja Au eneo hili

Ikitupendeza ata vyama vya siasa navyo ktk vyanzo vyao vya mapato, iwe ruzuku au vinginevyo basi waweze kuona umuhimu wa kusaidia eneo hili

Tuamshane tuweze kujenga Tanzania yetu, tusiwe wepesi wa kutupiana mpira na kutafuta mtu wa kumbebesha mzigo huu

NB:
Mtanisamehe kwa ambao nime wakwaza kwa uandishi wangu, sio muandishi mzuri sana, japo nimeona niandike kutokana na wimbi linalo endelea la wazazi/walezi, vijana/wanafunzi na wadau wengine wakiwa hawana furaha kwa kinacho endelea juu ya utoaji mikopo hii ya elimu ya juu

Mods mkiona kuna umuhimu wa kurekebisha au kuboresha ni (kufuta Au kuongeza) ruksa

ChoiceVariable Mohamed Said FaizaFoxy Wadiz Mwifwa Pascal Mayalla johnthebaptist Magonjwa Mtambuka Dkt. Gwajima D Donatila cocochanel Salary Slip Maghayo makaveli10 Retired Herbalist Dr MziziMkavu Mwl.RCT Mhaya
RR Mshana Jr Tate Mkuu Victor Mlaki grand millenial Objective football Voice of Tanzania hatedthemost GERRY12 NAMBA MOJA AJAYE NCHINI cmp leoleo-tu Mywangu Mpwayungu Village RealixT Redor Depal Shadow7 Shadeeya Michaeljoas The thinker27 Robert Heriel Mtibeli
 
Nijuavyo, wale wanaofanya vizuri kuna "scholarship" mama Samia kaianzisha.

Ushauri wangu, taasisi, idara na mashirika binafasi yaanzishe "scholarships" kwa vigezo vyao na masharti ya hao wanao "qualify" kuja kuwafanyia kazi wamalizapo masomo.
 
Back
Top Bottom