Serikali ya Tanzania itoe VISA free kwa wahindi, wachina, wakorea, wajapan katika hatua za mwanzo

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,017
12,306
Napendekeza serikali ya Tanzania ichukue hatua katika haya mapendekezo yangu.

1. Napendekeza serikali ya JMT itoe visa free kwa raia kutoka India, China, Japan na Korea

- katika mchakato wa visa free kwa mataifa mbalimbali tuanze na hayo mataifa manne kwanza kwa miaka 20 ya mwanzo.

2. Napendekeza serikali itoe uraia wa hadhi maalum kwa raia kutoka katika hizo nchi nne ( India, China, Korea, Japan )

- Hapa kutakuwa na vigezo vya kupata huo uraia wa hadhi maalum ambae raia kutoka katika hayo mataifa aliye kidhi vigezo fulani ambavyo serikali itaweka ikiwemo kiwango cha fedha alicho nacho, umuhimu kiasi gani alio nao kwa Tanzania n.k

- Hapa huyu raia atakuwa na uwezo wa kuwa na uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na hiyo nchi aliyotoka( India, China, Japan, Korea )

Mapendekezo yangu yamejikita zaidi katika kupewa uraia wa hadhi maalum na visa free kwa raia kutoka China, India, Japan na Korea
 
Hapana hiyo sio sawa, wao huwa wanakupatia free visa? Tuache kujishusha hata kama tunawavutia. Watoe pesa walipe VISA.
 
Katika Nyanja ya diplomasia kuna kitu kinaitwa reciprocity.
Je na hizo nchi tajwa hapo juu ziko tayari kufanya kitendo hicho kwa raia wa Tanzania?
Au sisi tu wawe Visa free kwetu alafu tukitaka kwenda kwao tukapange mstari kuomba Visa ubalozi wao?
 
Hizi hatua za mwanzo kwetu sisi tutakazo chukua zita warahisishia nao kuchukua maamuzi bora juu yetu pia
 
PIA TUNAWEZA KUOMBA USHIRIKI NA KWA PAMOJA TUKAANZISHA INDIAN OCEAN ECONOMIC COOPERATION ( IOEC )

Members wa mwanzo wakawa
  • Tanzania
  • India
  • Korea
  • China
  • Japan
Hili ni pendekezo langu pia
 
Hizi hatua za mwanzo kwetu sisi tutakazo chukua zita warahisishia nao kuchukua maamuzi bora juu yetu pia
Japan na Korea zinafaa sana, lakini siyo China na India.
Lakini sioni Japan akijitia doa katika hili kirahisi hivyo, japokuwa tuna ushirikiano mzuri sana nao na pia tuna watu wetu wengi kule ila silioni hili likitimia siku za karibuni.
 
Why not India na China ? Na kwa nini uhisi kuwa Japan atajitia doa ?
 
Back
Top Bottom