Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,660
- 46,350
Wazungu wamekuwa wakitupiwa lawama kwa kiasi kikubwa kwamba wanafanya njama za kuinyonya na kuididimiza Africa lakini uhalisia unakataa kwa kuangalia mambo kadhaa.
1. Uagizaji wa magari kutoka nje ndio manunuzi makubwa zaidi katika biashara ya Africa na Serikali za Africa ndizo waagizaji wakubwa zaidi wa magari ya kifahari muuzaji mkubwa wa magari hayo akiwa Japan.
2. Silaha inayotumika zaidi katika vita, migogoro, ugaidi, uasi na mauaji barani Africa ni AK-47 ambayo ni bunduki inayouzwa na Urusi.
3. Muuzaji mkubwa wa nguo japo nyingi ni hafifu kwa ubora hapa Africa kwa sasa ni China. Wakulima wa Bariadi wanaozalisha pamba wanauza kg 1200 ambapo shati moja kutengenezwa halimalizi hata Kg1 halafu wanakuja kuuziwa hilo shati kwa 10,000. Hapo bado hatujazungumiza viwanda vyetu vya nguo kuuwawa kifo cha mende na bidhaa hizo za mchina.
6. Afrika Chakula kingi tunachoagiza ni ngano, sukari na mafuta kutoka Russia, India, Brazil na China.
7. Wajenzi wakubwa waliochukua kandarasi muhimu za ujenzi wa Africa kwa Sasa katika kila sekta ni Wachina. Kama ni 10% za miradi, ubora hafifu wa miondombinu au kudumaa kwa makandarasi wa ndani wao Wachina ndio wa kulaumiwa.
8. Sehemu kubwa ya dawa za Africa kwa sasa zinatoka India. Hata dawa ambazo zingewezwa kutengenezwa Africa zinatoka huko.
9. Biashara kubwa za madawa ya kulevya Africa zinahusisha zaidi nchi za Asia kama China, India, Iran na Pakistan. Pia biashara haramu za ujangili zinahusisha watu kutoka maeneo hayo.
10. Muendeshaji bandari mkubwa zaidi na katika nchi nyingi kwa sasa Africa ni DP World ambao ni Waarabu.
Mataifa ambayo yanalaumiwa sana na kushitumiwa kwa conspiracies za kuikandamiza Africa wanachimba madini tu ambayo angalau hata yanatoa ajira za kueleweka na yana uwazi kiasi. Pia sehemu kubwa ya mapato kupitia Utalii na misaada ni kutoka hayo mataifa na zaidi sana hayo mataifa hata husomesha raia wa kiAfrica katika elimu bora zaidi.