Kenya Yaondoa Visa Kwa Raia Wa Afrika. Je, Tanzania na sisi tufuate njia hiyo?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,812
Kenya Imetanga kuondoa hitaji la kuwa na Visa Kwa raia kutoka Mataifa ya Afrika wanaotaka kuingia na kuishi Nchini humo.

Je Tanzania tufuate Mkondo Kwa kuondoa visa Kwa Nchi zote za Afrika Ili kukuza biashara na Utalii?

View: https://twitter.com/swahilitimes/status/1699379341921067312?t=IdqqqfHxlFQX57a_Q_M_JA&s=19

Binafsi naunga mkono Tanzania kuondoa visa na ikibidi AU wapitishe azimio la kuondoa Visa baina ya Mataifa japo najua Afrika Kusini watakataa.

Rais wa Kenya William Ruto amesema kwamba serikali yake itaondoa viza kwa Waafrika wanaokwenda nchini humo ikiwa na maana ya kwamba raia yeyote wa Kiafrika anayetembea Kenya hatahitaji kuwa na viza.

Hayo ameyabainisha hii leo Septemba 4, 2023, wakati akihutubia kwenye uzinduzi rasmi wa Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi Afrika 2023 katika Ukumbi wa KICC, Nairobi, kiongozi wa nchi alisema.

"Miezi isiyo mbali kutoka sasa, tutaondoa hitaji la visa kwa Waafrika wanaotembelea Kenya, sio haki unapotembelea nyumbani hadi uwe na viza," amesema Rais Ruto

Hatua hiyo ya kufungua mipaka ya Kenya kwa nchi zote za Bara Afrika, inawiana na mikakati ya Afrika Mashariki ambapo raia wa ukanda huu hawahitaji kuwa na visa kuzuru nchi yoyote Afrika Mashariki.

View: https://twitter.com/MwananchiNews/status/1699009966755983785?t=c5P6z8dJXGUqu6STwveQNg&s=19
 
Angetamani sana visa free ila Sasa nyie nyumbu wa danganyika mtasema anapiganada Nchi
Kwani kaanza lini kutusikiliza sisi tunachoshauri au kutaka? Mambo mengi tu kayazibia masikio tena anasema wazi kabisa hivyo hata hilo afanye tu, binafsi mie namtambua kama mtawala hivyo anaweza kufanya lolote analojisikia kwenye utawala wake.
 
Kaam yapi?
 
Kaam yapi?
Katika mambo yanayo endelea nchini na malalamiko yaliyojaa ila ndio kwanza kauli unazozisikia kutoka kwake kwa Rais ni kwamba kaziba masikio mara kaamua kukaa kimya, maana yake hana time ya kuwasikiliza wananchi kama hilo la bandari ndio aliweka wazi kabisa kuwa ameamua kukaa kimya.
 
Watu wanaoenda Kenya Kwa kiasi kikubwa huenda kuifaidisha Kenya.

Watu wanaokuja Tanzania Kwa kiasi kikubwa huja kuifaidi Tanzania.
Fact...
Tukiwaiga Kenya tutapotea..fursa nyingi zinaenda kishikwa na wageni.

Sasa hivi tu kuna visa angalia idadi ya wageni walivyojazana Zanzibar.

Michamvi,paje,nungwi tunagombania nao daladala na mishikaki ya jero jero. Wamekua wengi mpaka kero mpaka bar za uswahilini tuko nao

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
 
Katika mambo yanayo endelea nchini na malalamiko yaliyojaa ila ndio kwanza kauli unazozisikia kutoka kwake kwa Rais ni kwamba kaziba masikio mara kaamua kukaa kimya, maana yake hana time ya kuwasikiliza wananchi kama hilo la bandari ndio aliweka wazi kabisa kuwa ameamua kukaa kimya.
Rais hana mda wa kujibu individual cases
 
Fact...
Tukiwaiga Kenya tutapotea..fursa nyingi zinaenda kishikwa na wageni.

Sasa hivi tu kuna visa angalia idadi ya wageni walivyojazana Zanzibar.

Michamvi,paje,nungwi tunagombania nao daladala na mishikaki ya jero jero. Wamekua wengi mpaka kero mpaka bar za uswahilini tuko nao

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
Saizi hizo fursa mnazo? Mumezishika au kutwa kucha kulalamika?
 
Kenya Imetanga kuondoa hitaji la kuwa na Visa Kwa raia kutoka Mataifa ya Afrika wanaotaka kuingia na kuishi Nchini humo.

Je Tanzania tufuate Mkondo huo Ili kukuza biashara na Utalii?

Binafsi naunga mkono Tanzania kuondoa visa na ikibidi AU wapitishe azimio la kuondoa Visa baina ya Mataifa japo najua Afrika Kusini watakataa.

--
Rais wa Kenya William Ruto amesema kwamba serikali yake itaondoa viza kwa Waafrika wanaokwenda nchini humo ikiwa na maana ya kwamba raia yeyote wa Kiafrika anayetembea Kenya hatahitaji kuwa na viza.

Hayo ameyabainisha hii leo Septemba 4, 2023, wakati akihutubia kwenye uzinduzi rasmi wa Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi Afrika 2023 katika Ukumbi wa KICC, Nairobi, kiongozi wa nchi alisema.

"Miezi isiyo mbali kutoka sasa, tutaondoa hitaji la visa kwa Waafrika wanaotembelea Kenya, sio haki unapotembelea nyumbani hadi uwe na viza," amesema Rais Ruto

Hatua hiyo ya kufungua mipaka ya Kenya kwa nchi zote za Bara Afrika, inawiana na mikakati ya Afrika Mashariki ambapo raia wa ukanda huu hawahitaji kuwa na visa kuzuru nchi yoyote Afrika Mashariki.
Huu ni mtego kwa Tanzania pekee! Majamaa yameisha kausha fursa zote sasa yanategea kwingine! Hasa Tanzania.
Kenya ni koloni! mabepari wa kila aina waweishaikausha kila kitu! wazungu na wakikuyu wanamiliki 70% ya ardhi yote!! sasa yWewe SSH ukiingia mkenge wa kutangaza kama ulivyo mzembe hiyo itakuwa yako! Ni lazima tufuate mfumo wa kiuchumi tuliojichagulia!
 
Ila we Jamaa ,daa fursa ni akili sio mashamba and such blaa blaa
 
Back
Top Bottom