Madereva wa Tanzania wanalipishwa zaidi ya milioni moja kwa siku 90 wawapo Zambia; Watanzania wanalipa Visa kuingia DR Congo. Majirani zetu si wema

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Madereva wa Tanzania wanalalamika kwamba Zambia imewakataaa badala yake wanataka madereva wote wanaoingiza magari Zambia wawe RAIA wa Zambia. Dreva mmoja anatakiwa kuwa na siku 90 kwa mwaka, akizidisha siku 90 kwa mwaka anatakiwa kulipia si chini ya milioni moja na laki mbili ndipo aingize gari Zambia.

Haya ni maumivu makubwa sana kwa Watanzania hasa ikizingatiwa Mhe. Rais aliwaruhusu Wazambia kuingia na kukaa nchini miezi sita mfululizo bila kuchajiwa chochote. Kwanini serikali yetu imekaa kimya wakati watanzania wakitishiwa kutoruhusiwa kuingia Zambia? Kwanini madereva wetu wamekuwa wanyonge wanaandika DM badala ya kupaza sauti? Endapo Tanzania itaendelea kuwa mnyonge watanzania watawachukuliaje wageni?

Ipo wapi reciprocity kati yetu na Zambia? Madereva wakilalamika wanakamatwa tena na askari wa Tanzania kuwazuia wasilalamikie kadhia hizi. Matajiri wamiliki wa magari wameanza kupunguza kazi Watanzania na kuongeza ajira za wageni. Sijui kama serikali imefanya utafiti.

Tukiachana na Zambia twende DRC Congo, huku ndipo wanapotoka wanamziki wengi wa bendi hapa nchni, wafanyakazi wa saluni na vibarua mbalimbali. Lakini pia huku wanatoka wafanyabishara wengi wanaoingia nchini kutafuta riziki. Taarifa za wadau zinasema RAIA wa Congo wanakuja Tanzania bila kulipa visa toka walipokubaliwa kuingia jumuia ya Afrika Mashariki. Lakini kinyume chake RAIA wa Tanzania wakiwemo madereva wanalazimishwa walipe visa kuingia Kongo na sometimes wanateseka wawapo kwenye ardhi hiyo. Serikali ipo kimya na kama haitoshi wakongo wanaendelea kula Bata hapa nchini.

Kwa muktadha huu ipo wapi reciprocity kati ya Tanzania na Congo? Kwanini tunaabudu sana unyonge? Leo hii kama Congo wamegoma kuondoa visa sisi kwanini tumeondoa? Kwanini tusingewasubiri wawe tayari?

Hizi ni nchi mbili ambazo naamini Makamba anafahamu changamoto zake lakini hawezi kuchukua hatua hadi aone mabango ndipo aseme tunaingia kwenye majadiliano.

Tanzania lazima tukubali kwamba hatupo tena kwenye kipindi cha ukombozi wa bara la Afrika, lazima tutambue kwamba tupo kwenye vita ya kiuchumi ambayo inaongozwa na principle moja tu SCRATCH MY BACK AND ILL DO SO ALSO. RECIPROCITY PRINCIPLES NI MUHIMU SANA KWA SOVEREIGNITY YETU.

Madereva na matajiri wa kimataifa amkeni mpige kelele. Mtalaza watoto njaa mkikaa kimya.
 
Hao Zambia si watakuwa wanavunja makubaliano ya EAC na Zambia ya SADC kama wanafanya hivyo.
 
Hapana watz ndio wajinga atuna wivu kwenye uchumi wetu. Kuna jamaa leo kaweka uzi kuuliza kuhusu magari ya watalii ya tz hayaruhusiwi kuingia mbuga za Kenya kwanini? Ila ya Kenya yakija mbuga za tz yanaingia.
 
Back
Top Bottom