Serikali itenge siku maalum ya kuwapa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari vidonge vya minyoo na kichocho

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
388
772
Kwa heshima na taadhima ninaiomba Serikali itenge siku maalum ya kuwapa wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari vidonge vya minyoo na kichocho. Leo nilikuwa nafanya mazoezi asubuhi nimekutana na wanafunzi wengi wakienda shuleni wengi niliowaona kwa kweli hawakuwa na afya nzuri.

Ikumbukwe pia familia tunatofautiana kwa masuala ya malezi ya watoto wetu. Sisi tulipokuwa tunasoma shule za msingi Serikali ilikuwa inatenga siku moja baada ya miezi sita kwa ajili ya kupewa vidonge vya minyoo na kichocho.

Mhe. Ummy Mwalimu haya ni mawazo yangu na hivyo tunataka Taifa lenye watoto walio na afya nzuri pindi wakiwa shuleni. Utaratibu mzuri unaweza kuwekwa na Wizara ya Afya kutekeleza mpango huu.
 
Back
Top Bottom