Tunahangaika sana na matokeo ya Sekondari lakini msingi mzuri unaanzia shule za msingi

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,726
2,082
Niende tu kwenye mada salamu zenu.

Elimu ya msingi ndio mambo yote, ndio kila kitu hapo hayo mengine ni muendelezo tu wa kumuandaa mtoto kuwa professional ndio maana imeitwa elimu ya msingi.

Sasa kama mtoto hatapata msingi mzuri wa elimu basi huko mbele itakuwa shida kwake.

Nimeona tunafuatilia sana matokeo ya international School, kifupi ni kwamba hizi shule zinapokea wanafunzi ambao tayari wako vizuri toka shule za msingi na pia kama wapo ambao wanasuasua basi sidhani kama wanafika nao kwenye mtihani wa Necta.

Nadhani watawaacha njiani ili shule ionekane iko vizuri. Yaani hao wanafunzi wanaosuasua wasije wakaharibu jina la shule.

Kwa hiyo kifupi ni kwamba wazazi ndio wanatakiwa kupewa pongezi na sio hizo shule za international English nn sijui.

Hizo shule za za international ni kwamba mwanafunzi au walimu wanaenda kuteleza tu kwenye ganda la ndizi tayari kazi yote anakuwa kaimaliza mzazi.

Shule zetu za msingi zingekuwa na mazingira mazuri ya elimu kuanzia madarasa, walimu mitaala na idadi pia ya wanafunzi darasani ingekuwa ya nzuri, huko sekondari watoto wetu wangekuwa wanateleza tu.

Secondary school ni elimu sasa ya kumuandaa mtoto kwa masomo ya kitaalamu baada ya kupata msingi Bora.

Kwa hiyo kifupi international School hawana kazi kubwa ya kufanya wanawashukuru tu wazazi kisirisiri kwa kuwapa kazi rahisi ya kufanya.

Asante.
 
Unaposema international unaelewa maana yake? Au ulitaka maanisha medium schools

Maana huko Unapozungumzia nahisi umepotea venue hizo shule za international ni wazazi wachache sana wanaopeleka watoto huko .
 
Unaposema international unaelewa maana yake? Au ulitaka maanisha medium schools

Maana huko Unapozungumzia nahisi umepotea venue hizo shule za international ni wazazi wachache sana wanaopeleka watoto huko .
Ni hizi shule zetu za private hili neno international ni kama la kuziremba tu.
 
Back
Top Bottom