Series (Special thread)

Series (Special thread)

Habari.Wadau mwenye link ya kudownload MacGraw Avenue tafadhali.Nimejaribu kuitafuta kila kona nimechemka
 
Vip Tehran nzuri na inahusu nn ?
Anhaa! See ni series ambayo imenifanya kila series inayotolewa na Apple TV+ niwe naziangalia ukianzia Tehran mpaka The mosquito coast zote ni kali kwa upande wangu.
So Tehran ni series inayohusu uhasama unaoendelea baina ya Israel and Iran. Sasa hii Israel kupitia Intelligence agency yake ya Mossad kama unavyoona USA wana CIA wanataka kulipua nuclear reactor ya Iran kwa kutumia ndege za kivita ila ubaya hawawezi kutuma ndege za kivita kwasababu Iran wana system ya kudetect ndege za kivita zozote kwenye anga lao ambazo zinakuja kuvamia na automatically zinalipua izo ndege za kivita. So Mossad wanamtuma shushushu wao wa kike ambaye alizaliwa Iran ila akakulia Israel ambaye ndugu zake bado wapo Iran.
Sasa huyo dada ambaye ni hacker anatakiwa akazime iyo system ya kudetect ndege za kivita ili Israel watume ndege zao za kivita kulipua nuclear reactor sasa huyo shushushu wao ataingiaje hapo na pia ndio mission yake ya kwanza?.... kumbe hao Mossad waligundua kuna mfanyakazi wa kike anafanya kazi kwenye kampuni ya umeme ambaye anafanana na shushushu wao ila uyo mfanyakazi anaomba kuhama nchi so wakabadilisha identies na huyo shushushu wa Israel Airport.
Sasa huyo shushushu katinga Iran na anaenda kazini kama Kawa so wakati anaingia kwenye mitambo na kuanza kuhack kuna kitu hawakugundua yule mwanamke aliyebadilishana naye identies moja ya kitu kilichomfanya ahame ni kuwa alikuwa akilazimishwa kufanya mapenzi kinguvu na mmoja wa wasimamizi wa kituo iko. So huyo shushushu wakati anahack jamaa alikuja kutaka abake sasa demu katika kupambana akamuua huyo jamaa so mission ikaingia mdudu na polisi katika kuchunguza wakagundua ni shushushu so demu inabidi aanze kusurvive asikamatwe na wapelelezi wa Iran na pia katika waongozaji wa mission iyo kutoka Mossad kuna mtu ni wa Iran kapandikizwa atoe siri zozote za Israel kwao.

So bonge la series mzee na ina episodes chache kama series zingine za Apple TV+ na mwaka huu watatoa season 2
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom