Series (Special thread)

Kama ttcl inashika vizuri huko unga tu hio kwa simu ya mdogo wako maana airtel watakupa hasara nyingine japo ttcl gb 10 ni 2500 sijui kama weshashusha bei. Halotel wametukomoa wengi.
 
airtel gb 10 kwa 1500 kuanzia saa sita usiku menu ile ile *149*99# kisha internet halafu siku utaona bando la usiku
Ngoja nitaitafuta line ya Airtel, sikuwa nayo, hii halotel sion faida yake kila nikiunga hicho kifurushi cha usiku, asubuh nakuta kama nilivyo acha jana, hasara tu, imebidi nipotezee hiyo line...

Natumia TTCL, wako na speed poa tu
 
hao ttcl au airtel ukipata simu ya 4G utawapenda kasi nzuri. Japo sijajaribu kasi 4G ya ttcl.

ila ninge akina popo hawalali mpaka mzigo wote ufike. kumbe huwa unategesha kisha unalala hapo ndipo hasara inapotokea maana halotel wana katabia ka kuzima data kwa sekunde kadhaa
Ngoja nitaitafuta line ya Airtel, sikuwa nayo, hii halotel sion faida yake kila nikiunga hicho kifurushi cha usiku, asubuh nakuta kama nilivyo acha jana, hasara tu, imebidi nipotezee hiyo line...

Natumia TTCL, wako na speed poa tu
 
Hahah nilikuwa nategesha halafu nalala, nikiamka kula daku, nakuta kama nilivyoacha aisee, nmerudia mara nne buku jero langu linaenda tu, dah nilikuwa napata hasira basi tu...

Hapo kwenye upopo ndio mtihani, na mausingizi ya kifala sana siwezagi kutoboa kabsa hata kama nmepania hiyo siku nitoboe, itafika mida mida tu naanza kuona wenge la usingiz
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚usingizi shuain zake. Jana nikasema ngoja nishushe vitu imefika muda wa saa sita kasoro kumi hali ikabadilika usingizi sio usingizi kizunguzungu sio kizunguzungu ikabidi nilale tu hapo nilikua sijaunga maana waunga bando la usiku tuna mengi ya kusimulia

nilishawahi unga bando kabla ya saa sita wakalibeba na kifurushi sijui walimpa nani. Siku hizi naunga ikifika saa sita yenyewe
 
yale huwa ni mateso makali sana tunapitia, hasa hasa hizi za kikorea kwa upande wangu huwa naona zina kazi kidogo wakati wa kuzishusha tofauti na hizi za kizungu, ukishaiweka kwenye Torrent tu kazi inaisha..
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚mateso sana halafu kanakuja ka mtu kanaleta flash kirahisi rahisi eti niwekee,kakiangalia kasipoipenda kanakulaumu una machaguo mabovu
yale huwa ni mateso makali sana tunapitia, hasa hasa hizi za kikorea kwa upande wangu huwa naona zina kazi kidogo wakati wa kuzishusha tofauti na hizi za kizungu, ukishaiweka kwenye Torrent tu kazi inaisha..
 
Issue sio mtandao kama hawa wabaya au hawa wazuri bali angalia uwo mtandao wako na sehemu unayoishi unasupport vizuri maana mitandao yote kuna sehemu inafanya vizuri kwingine unakuwa utopolo. kwamfano mimi huku napoishi Halotel haifanyi vizuri kwasababu ina support 3G tu na sio 4G So wakati wa usiku ndio natumia kushusha series ila sijui Airtel haifanyi vizuri ila mitandao ipo poa Sema ndio ivo haina vifurushi vya offer kama Halotel na Airtel
 
mateso sana halafu kanakuja ka mtu kanaleta flash kirahisi rahisi eti niwekee,kakiangalia kasipoipenda kanakulaumu una machaguo mabovu
hakajui mziki unaopitia usiku mnene, utasikia mimi napendaga zile za kijijini, naona ww umejaza za mjini tupu
 
wapenzi wa queen of the south naona season 5 imeshaanza kuachiwa
 
Shadow and bone series moja nzuri imeachiwa wiki iliyopita iko full season 1
 
Hivi Breaking Bad imeandikwa vizuri kiasi hiko !?maana naona wanautoleaga mfano sana kwenye series amazing storyline & scripts
 
Wale wapenzi wa series za beef Kati ya waarabu na israel ambao mliofuatilia pia Fauda Basi mzigo mwingine huu unaenda kwa jina la TEHRAN unaonyeshwa na apple tv plus ambao this time ni ujasusi kati ya Israel na Iran.
Hii series ni kali sana aisee, nmeianza jana baada ya kufuturu,nmeenda nayo hadi muda wa daku...najiuliza sijui kwanini waliweka episodes chache vile dah...ujasusi wa humu ndani sio wa mchezo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…