MOST DANGEROUS GAME
Series - (Complete season 1)
Genre: Action | Thriller
Duration: 7 minutes
Rate: 7.9/10
Hii series ni ya moto mno, kama unavyoliona jina lake!
Dodge, baada ya kukumbwa na ukata wa kifedha huku mkewe akiwa na mimba na yeye baadae anakuja kugundulika kuwa ana uvimbe (cancer) kwenye ubongo, anaamua kwenda kuomba msaada kwenye kampuni ya TF ambayo ina kitengo cha kuwasaidia wahitaji.
Kwa bahati mbaya, kwake yeye inakuwa tofauti.
Mchizi analazimishwa acheze game la msako, yeye akiwa kama prey (anaewindwa) na kikundi cha watu ambao hawafahamu.
Jamaa inabidi acheze tu kwa maana hakuna njia nyingine ya kumsaidia mkewe mjamzito na ukizingatia yeye anao muda mchache tu wa kuishi kutokana na kuwa na uvimbe kichwani.
Dili ipo hivi, jamaa atakiwa aingie kwenye game (hunt), kila anapokamilisha lisaa moja kwenye msako kama bado atakuwa yupo hai basi zitakuwa zinaingizwa pesa kwenye benki akaunti anayotumia na mke wake kiasi cha $50,000/=
Humo kuna sheria za mchezo, jamaa anaambiwa asimjulishe mtu yeyote kuhusu hiyo game na wala asikimbie mji, akifanya hivyo atakuwa amekiuka masharti ya mchezo na hivyo mchezo hautoisha.
Pia wauwaji wanaruhusiwa kutumia silaha zote kuua isipokuwa bunduki.
Humo ndani kinawaka vibaya vibaya!
Kuna muda jamaa anaingia kanisani kwa padri kuungama, kumbe huyo padri mwenyewe yupo kwenye game anamuwinda!

Ni series fupi tu, kila episode haizidi dakika 8 na ina jumla ya episode 15. Siku haiishi ushaimaliza.
Kuna muda unaona kama inaisha haraka haraka, unatamani hata ingekuwa na dk 60!
Fanyeni kuitafuta haraka sana!
Ninauhakika kabla hujaimaliza utakuwa tayari ushanishukuru.
View attachment 1535128