Series (Special thread)

Series (Special thread)

Ah yule demu wa Condor, Leem Lubany yupo humu kumbe? Namuona na mchizi wa kati kati hapo alikuwepo kwenye series ya The Strain..
Hii si ya kukosa kabisa!
Uyo demu ni hatar kwenye condor, anaua kitaalam sana, kweenye seasson 2 yule deputy director wa cia kaibukiwa mwenyewe kasema sitopigaa kelele kauliwa taratibu
 
Godfather of Harlem...nimeitizama yote, ni series nzuri,kuna muda imepoa sana, nafikiri ni kutokana na kuifanya iwe na madhari ya miaka ya nyuma sana ndio maana imechangia...
Utamu wa Godfather of Harlem, unakolezwa na story ya Malcom X, harakati zake zile za dini, bado pia humo ndani tunamuona bondia gwiji Mohammed Ali...

Kwangu mimi niliipenda, ila haihitaji haraka...habari nzuri ni kuwa imepewa tena msimu ujao, tutegemee kuiona ikirudi msimu wa pili, kwan ilipoishi ni kama ndio imeanza sasa, Bumpy Jonson kaungana tena Malcom X, na hii ni baada ya Malcom X kuona harakat za Kiislamu hazipo poa kama alivyokuwa anafikiria hapo mwanzo.View attachment 1527901
Ndo maana sijaifuta mzee cz naamini Kuna kitu na kuhusu imepoa cz imetengenezwa kizamani sio kweli cz Kuna series moja inaitwa black sails, Narcos Mexico, snowfall na peaky blinders zina mandhari ya zamani lkni zinakinukisha kimoja
 
Ndo maana sijaifuta mzee cz naamini Kuna kitu na kuhusu imepoa cz imetengenezwa kizamani sio kweli cz Kuna series moja inaitwa black sails, Narcos Mexico, snowfall na peaky blinders zina mandhari ya zamani lkni zinakinukisha kimoja
Ni kweli mzee, hizo series ulizosema hapo zote mazingira yake ni ya kizamani ila ziko poa... Ipe muda tena mzee
 
MOST DANGEROUS GAME

Series - (Complete season 1)
Genre: Action | Thriller
Duration: 7 minutes
Rate: 7.9/10


Hii series ni ya moto mno, kama unavyoliona jina lake!

Dodge, baada ya kukumbwa na ukata wa kifedha huku mkewe akiwa na mimba na yeye baadae anakuja kugundulika kuwa ana uvimbe (cancer) kwenye ubongo, anaamua kwenda kuomba msaada kwenye kampuni ya TF ambayo ina kitengo cha kuwasaidia wahitaji.
Kwa bahati mbaya, kwake yeye inakuwa tofauti.

Mchizi analazimishwa acheze game la msako, yeye akiwa kama prey (anaewindwa) na kikundi cha watu ambao hawafahamu.

Jamaa inabidi acheze tu kwa maana hakuna njia nyingine ya kumsaidia mkewe mjamzito na ukizingatia yeye anao muda mchache tu wa kuishi kutokana na kuwa na uvimbe kichwani.

Dili ipo hivi, jamaa atakiwa aingie kwenye game (hunt), kila anapokamilisha lisaa moja kwenye msako kama bado atakuwa yupo hai basi zitakuwa zinaingizwa pesa kwenye benki akaunti anayotumia na mke wake kiasi cha $50,000/=

Humo kuna sheria za mchezo, jamaa anaambiwa asimjulishe mtu yeyote kuhusu hiyo game na wala asikimbie mji, akifanya hivyo atakuwa amekiuka masharti ya mchezo na hivyo mchezo hautoisha.
Pia wauwaji wanaruhusiwa kutumia silaha zote kuua isipokuwa bunduki.

Humo ndani kinawaka vibaya vibaya!

Kuna muda jamaa anaingia kanisani kwa padri kuungama, kumbe huyo padri mwenyewe yupo kwenye game anamuwinda!

Ni series fupi tu, kila episode haizidi dakika 8 na ina jumla ya episode 15. Siku haiishi ushaimaliza.
Kuna muda unaona kama inaisha haraka haraka, unatamani hata ingekuwa na dk 60!

Fanyeni kuitafuta haraka sana!

Ninauhakika kabla hujaimaliza utakuwa tayari ushanishukuru.
_20200812_153840.JPG
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom