Series (Special thread)

Series (Special thread)

Mkuu yule siyo jack proad, yule anaitwa nicholas brody kwenye season ya tatu mkuu.

Na jamaa hakunyongwa waraabu waliwahadaa wamarekani tu, kwenye season ya 4 episode ya 7 Pakistan intelligence services (ISI) waliwakutanisha carrie na brody kwenye self house yaliokuwa makazi ya general wa jeshi la Pakistan.

Season ya 4 carrie anakuwa ni station chief kabul, Afghanistan, alipewa information ambazo hazikuwa sahihi na CIA station chief wa Pakistan Sandy Bachman, kuhusu uwepo wa gaidi aliyekuwa anawindwa na wamarekani kwa udi na uvumba Haissam Haqqani kwenye eneo ambalo halikuwa sahihi anaua innocent people waliokuwa kwenye harusi kwa drone. (Anafahamika kama drone queen)

Haissam Haqqani alikuwa ni mtu ambaye alitengenezwa Saul na Dar Adal kwa lengo la kumuyumbisha head wa CIA pale Langley,senator aliteuliwa na rais kuiongoza CIA. Hivyo Saul na Mwanae Dar Adal hawakuwa na kazi zaidi ya kupiga fitina.

ISI wanamtengeneza mme wa balozi wa USA pale Pakistan kuwa informer wa kuwapa taarifa nyeti juu ya mipango ya CIA pale Pakistan na alifanikiwa kuwaonyesha safe house za CIA.

Quin alipewa mission ya syria, carrie alifanikiwa kutega bomu la kumuua Hissam kwenye mlango wa gate lake, ile anataka kulipua general akamwambia usilipue angalia kwenye gari amekaa nani, kuangalia anamkuta Dar Adal amekaa siti ya nyuma wanapiga story. Carrie alibaki mdomo wazi.

Season ya 5 na ilikuwa ni Berlin, nimeshaielezea mkuu na 06 nayo nimeshaigusia.

Season ya 07 iliyoisha juzi. Warusi wamemfanya mbaya carrie kawa kichaaa. Lakini pia wamemchafua rais wa marekani ambavyo ameamua kuresign kwenye hiyo nafasi yake. Dar Adal bado yuko kwenye federal prison.

Homeland is my favorite show all the time.
Gideon Raff huyu mwiziraiel anajua kuandika story na kudirect.
uko vzr mkuu umeichambua kama edo kumwembe na mpira, yaa nimechanganya jamaa ni Nicolaus proady, katisha sana kwenye hii kitu, ngoja niisake mm nilijua ameshany'ongwa na ndio mwisho kumbe ndo kwanza kumekucha. NISAIDIE LINK KAMA UNAYO, TERREIUM NAONA WANASUMBUA KWENYE HOMELAND
 
uko vzr mkuu umeichambua kama edo kumwembe na mpira, yaa nimechanganya jamaa ni Nicolaus proady, katisha sana kwenye hii kitu, ngoja niisake mm nilijua ameshany'ongwa na ndio mwisho kumbe ndo kwanza kumekucha. NISAIDIE LINK KAMA UNAYO, TERREIUM NAONA WANASUMBUA KWENYE HOMELAND

Naona bado unaendelea kuchemka, anaitwa Nicholas Brody siyo proady.

Link mkuu ni torrents site tu unashusha mizigo tan yako.
 
kwa wale wapenzi wa SIREN, hii kitu ni hatari
Napenda kujua latest series ambayo iko walau episode ya 2 au 3.
Napata shida kufatilia series ambayo iko mbali naona kero kuishusha.
Recently nafatilia The Crossing,kila jumanne naishusha mwenyewe nipo episode ya 5.
Any other series?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom