Series (Special thread)

Series (Special thread)

Hii hapa ndugu yangu inaitwa THE PUNISHER, imezalishwa na MARVEL nadhani unajuaga MARVEL mambo yao pia imetoka under NETFLIX so unapata episodes 13 zote ambazo ni complete season 1.

Hii series niliona juzi inatrend huko Twitter ndipo nikaipa concentration kidogo nimekuja kugundua sasa ni series Bora kabisa, hapo chini Kuna picha inaonyesha ratings zake zimematch na GAME OF THRONES na BREAKING BAD ya 9.5

0fa5566cb51de163efb4b4da07246ca1.jpg


Episodes guide: mnaona hapo chini episodes zina ratings za 9 out of 10,haya mambo hutokea kwenye GAME OF THRONES, STRANGER THINGS labda na HOUSE OF CARDS kwa series ambazo zinarushwa kwenye kizazi hiki nawashauri wote hii kitu ni tatizo itafteni alafu mtarudi na mrejesho hapa.

06ce2477eefbc8b8f4c139770401f29b.jpg
The Punisher nimeikubali..marvel nawakubali sana.
 
Nimeangalia season nyingi ila hizi za ki intelligence ndo kiboko..
>>>Prison Break
>>>24 Hours, hii imebidi nianze mwanzo ndo nipo Season 4
Huyu Chloe O'Brian nampenda sana Hasa akiwa kanuna.

>>>3Days hii nayo kiboko Han Tae Kyong alinikosha sana alivyokua anamlinda Raisi..
 
Vikings season 5 returns Tomorrow

a341f964a3e6aa1a5941cdb975164969.jpg
Kati Ya Series Ambayo Kila Nikiangalia Huwa Natabasamu Na Sijajua Kwa Nini,Ilifikia Hatua Mpaka Niliimisi, Nilivyosikia Inarejea Tena Nikajikuta Natoa Tabasamu La Nguvu Yaaani, Kati Ya Series Ninazo Zikubari Sana Sana..
 
Chige, kazi ya producer ni kuhakikisha anatengeneza script ya tukio huu ndo msingi mkuu wa maproducer wote,ndo maana nimekutolea mfano wa JJ Abram ambaye mm namkubali kuliko hata wale waliotengeneza 24 na Prison break maana ni km waliziotea zile na hawakuproduce series angalau zilizoendana na zile za awali.

Producer .. Anasimamia na kuongoza uzalishaji wa fulamu. Ndio tuseme CEO wa production.. Anajua nani atafaa kuwa Director.. Nani atatafuta waigizaji fedha zitatoka wapi..mauzo na matangazo yatafanyikaje nk

Mara nyingi wanakuwa na Ass. Producers katika miradi inayokuwa mikubwa sana.

Story+scripting hii inafanywa na kundi la watu.. Wanaoangalia mambo mengi madogo madogo ila muhimu katika filamu.. Vitu kama dialogue, monologue, portrayal of characters (Tabia zao) no hapa kunakuwa na director, mtunzi wa story au hadithi(kwa sehemu ambayo kitabu kinatumika). Kwa sehemu zingine watunzi sio lazima wawepo ila jopo la wataalamu wanaweza kuja na script has a kwa movie za genre ya Documentary.

Director:- huyu ndio mpishi.. Huyu anajua lengo kuu lafilamu na anakuwa na uwezo wa kuiamuru kwa vipande vipande iletwe kupitia camera movements, mwanga, uigizaji na maelezo. Hutu anaijua filamu ikiwa kichwani mwake na anajitahidi kuzielekeza element nyingine za uzalishaji ili zifikie lengo alilonalo kichwani.
 
Mkuu chuma cha reli... hili la waigizaji hata mimi nimeshalisema mara kadhaa hapa jamvini... tatizo la msingi la filamu zetu ni kweli sio waigizaji. Tukiacha technical issues ambazo ni zipo juu ya uwezo wa wengi lakini tatizo la msingi... la kwanza ni story/script na pili ni directors. Na kama tutataka kwenda mbali zaidi kufahamu tatizo kuu ni nani hapo kati ya Director na Mwandishi, wala sitasita kusema kwamba tatizo kuu kati ya hao wawili ni mwandishi. Story ndie base ya filamu... nimekuwa nikisema hili mara kwa mara kwamba, ukishakuwa na stori mbaya basi hata ukichukua A-List Actors kutoka Hollywood bado filamu itakuwa mbaya tu kwa kuwa wao watacheza according to story! Kwenye movie kuna kitu kinaitwa Characterization... hii characterization ndiyo inamtofautisha kati ya msanii mmoja na mwingine! Tunapoangalia tabia zisizotabirika na maamuzi yenye utata ya Jack Baeur lakini yakiwa constant hii ni part of characterization. Hata hivyo muigizaji anaivaa characterization kama ilivyo kwenye stori... hapa kazi ya muigizaji ni kuuvaa uhusika huku Director akihakikisha kwamba Mwigizaji anauvaa uhusika lakini msingi wa yote hayo ni stori! Tunapoangalia movie huku tukiwa hatufahamu what will happen next ni kwavile stori yenyewe haiku-reveal nini kitatokea! Kazi ya muigizaji ni kuhakikisha kwamba hata kama sekunde kumi zijazo kuna kitu cha hatari kitatokea kwenye scene husika lakini asianze kuivaa hofu kama maandalizi ya tukio linalokuja hivi punde na Director anahakikisha kwamba Muigizaji anakuwa kwenye mood ya kawaida lakini msingi wa yote haya upo kwenye stori!

So, to make story short... kwa waigizaji hawa hawa tulionao endapo wanapata story bora na directors wanaoweza kufanya coordination kati ya story na waigizaji, basi unaweza kushangaa unapata filamu bora kabisa kwa kuangalia. Technical issues ni secondary problem lakini kama stori imesukwa vizuri na ikasukika... director akatengeneza coordination mzuri basi suala la technical issues wala huwezi kuliona! Isitoshe, technical issues/problems ni suala la kitaalamu zaidi ambalo mtazamaji wa kawaida wala hawezi kuligundua kama filamu inavutia! If you're above 25 years then I bet umeshawahi kuangalia movie kupitia VHS! Pamoja na kwamba quality ilikuwa very poor huku kunasa nasa ilikuwa ni jambo la kawaida lakini watu walikuwa wanakuwa excited na movie... unakuta mtu anakusimulia movie ya Rambo ya kwenye VHS kuliko unavyoweza kuisimulia Bongo Movie iliyo kwenye DVD!
Ukweli kabisa.. Waongozaji, waandishi ..na cinematographers wakibadilika..hasa waongozaji kunauwezekano filamu zikakua. Itabidi nijitose some day..tusijeonekana tunaongea tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom