WHAAAAAAAT? Tuanze na la huyo jamaa yako kwanza! Ni Empire ipi hiyo unayoizungumzia kwamba mshikaji wako haipendi? Ni hii hii ya akina Lucious na Cookie au nyingine? Kama ndo yenyewe basi kweli issue ya TASTE ni kitu cha ajabu sana manake, ni kv tu nafahamu taste ya mtu ina mchango mkubwa sana ktk kupenda hiki au kile otherwise wala nisingemuelewa mtu akisema Empire ni mbovu!
Kuhusu kufahamu kwanza stori za vitabuni nakubaliana na wewe kwa 100% na hii ndio sababu series na filamu za vampires, zombies, batman stuff na hata GOT stuff zinafanya vizuri sana USA manake majority origin yake ni comic books kv Marvel Comics (for Spiderman stuffs). Na majority ya Wamarekani wamevisoma hivi vitabu tangia utotoni hadi ukubwani depending na rating manake vingi vinakuwa kwenye graphics. Is like sisi watoto wa zamani utuambie kuna series ya akina Lord Lofa na Pimbi (Sani), obvious lazima tutazipenda tu manake ikiwa tulizipenda zikiwa kwenye mfumo wa picha seuze motion picture!