Mbona nimeshasema PLOT TWIST ZA KIBOYA ndio sababu au haukusoma maandishi yote niliyoandika?
Poa, ngoja nikuambie kwanini ninaona mchongo umepoteza mvuto.
Lakini zingatia huu ni mtazamo wangu binafsi chief, kwangu mimi season 2 ya huu mchongo imekuja kuvuruga motion nzima ya series:
1. Sean kutoka kuwa muhuni katili hadi kuwa pussy ni plot twist ya kiboya, bora wasingemrudisha kwenye season 2, baada ya kupigwa ile shaba ingebakia tu kuwa mwamba amedanja.
2. Yule Bi Mkubwa wake Sean kuungana na maadui kuangamiza familia yake kwangu mimi ni plot twist ya kiboya, hivi alikuwa anapigania nini kiasi kwamba alikuwa yupo tayari kupoteza vijana wake wawili wa kiume?
3. Asif na Lale kuungana ni plot twist ya kulazimisha, haimake sense, kama umefuatilia vyema season 1 basi utakuwa unajua kuwa uadui wa hao watu wawili upoje.
Ningeendelea, ila nitakuchosha tu.
Pia mkongwe, sisi watu wengine tukicheki series huwa tunafuatilia mtiririko wa matukio yote, huwa sipeleki mbele ili kuangalia scene ambayo shaba zinapigwa au mikono inachapwa, huwa nacheki mchongo kutoka sekunde ya kwanza mpaka ya mwisho, hivyo ikitokea nimekutana na plot twist isiyokuwa na mashiko ndani yake mzuka huwa unakata, haijalishi series ina action kiasi gani.