Wameniudhi sana hawa watu kwa kumuua Bianca. Isitoshe, wamemuua na Vince pia. Bianca alikuwa anaelekea kuliwa kimasihara na mwamba, mara wakamrudisha tena kwa Paul. Hawa waandishi wana mambo mengi mno.
Wameboa sana hawa writers kama wae waliomuua Ned Stark kwenye season ya kwanza ya GoT. Plot twists ni nyingi, episodes ni chache. Ila wamejua kucheza na hisia za watazamaji. Leo unakuwa upande wa Bianca na unataka amdake Jackal, kesho unakuwa upande wa Jackal na unataka awashughulikie wale wahuni wanaomdulumu mshiko wake kirahisi rahisi tu baada ya kutumia nguvu na akili zote zile kutekeleza mauaji yao. Sasa Tywin Lannister nae atapata alichokitafuta kwa Jackal. Angemlipa tu yaishe. Sasa amewaudhi Jackal na Zina kwa pamoja...
Na wamempa The Jackal likeability kubwa. Unaona kabisa jamaa ana maadili fulani licha ya kulazimika saa zingine kufanya maamuzi asiyopenda ili aokoe maisha yake au atimize lengo lake, ila hauwi tu bila sababu ya msingi.
Theory yangu ni kuwa Osita atabeba mikoba ya Bianca sasa. Ni kama wanataka kila season iwe na protagonist mpya wa kupambana na The Jackal, na Jackal atakuwa anabadilika badilika kuwa steringi na adui ndani ya msimu kama msimu wa kwanza, ila sioni kama hii style itaweza kukaa zaidi ya misimu miwili.