Serengeti fiesta 2014 special thread

Nashangazwa sana na wanaosema Diamond anapiga tour eti.. Honestly Mimi simchukii diamond na nafurahia mafanikio yake nje ya maisha yake ya kipumbavu.

Sasa, naomba nijuzwe Diamond kapiga tour wapi?? Kwa Africa amefanya show wapi ukiacha hapa nyumbani na ile show moja ya
Kenya?? Alishawahi fanya show Uganda?? Alishawai Fanya show South Africa (siongelei zile za big brother).. Alishawai fanya show yeyote west Africa?? Ukweli ni kwamba tunajidanganya tu kuwa diamond yupo international lakini si kweli. Yule anatumiwa tu na media mbalimbali ili tu wapate soko hapa East Africa, hata akina Davido na Mafikizolo wanamtumia tu ili washike soko letu.. Hivi huko Nigeria, South, na kwingine hakuna open show kama fiesta?? Mbona haitwi kuperform huko kama sisi tunavyowaita international artists??
 

Mi sio mshabiki wa dogo, ila ninamtetea pia. Kiba naye ajiandae, akifika juu ataundiwa zengwe, ndo waTz wengi tulivyo. Umeongea point, kula 'like' ulipo.
 

Mkuu lakini mbona mna haraka sana??? Mwahitaji mtoto azaliwe akae atambae atembee akimbie ndani ya week?? Ni taratibu atajulikana mpk ataitwa leo yupo na davido kesho na mafikizolo keshokutwa kaitwa bigbrother ni hivyo mpk atainuka muhimu km watanzania tuwape sapoti vijana wetu si kuwakatisha tamaa...
Vivyo hivyo kwa kiba aangalie alikosea wapi mpk si msanii mkubwa ndani na nje ya tz wakati alishapiga mpk collabo na r kelly...kwangu naamini laiti huyu diamond angepata ile nafasi leo hii tungeongea mengine... Kiba alibweteka na anaendeshwa na ujamaa wa kufanya mziki burudani na si kazi... Hao mashabiki wanaompa kick kwa nyimbo moja sidhani km watamsaidia km asipojipanga ye mwenyewe'!! Ajitengeneze aongeze thamani yake afanikiwe na muziki wake!!' kiba si wakutegemea sapoti ya kulazimisha na ya kumzomea mwngne kiba asimame yeye km yeye....

Namsikitikia sana diamond kwa anayayopitia ila namsikitikia zaidi kiba kwa anapopitishwa na aliyopitia kale kutokutumia nafasi (ufinyu wa mawazo)
TUWAPENI SAPOTI WOTE TANZANIA NI YETU SOTE
 
So Jana mwanafa,weusi na kiba ndo walifunika,si ndio!

Jana waliofunika ni mabinti wote wa Tz. Mdee, Recho, Shaa, Lina walikuwa ni shiiidah. Good performance. Fa steji lote kuuubwa anajaribu kulitawala mwenyewe, lilimtawala. Weusi nao badala ya kupagawisha mashabiki, wanatumia muda mwingi kuimbiana wao wenyewe (yaani wanatengeneza kaduara kao na kuanza kuimbiana), kwa mimi perfomance nzuri ya wanaume ilikuwa ni Kiba na Diamond na Ommy. T.I mitusi tuuu.
 
Sio bure watu kupandishwa mabasi ya bure kwenda leaders kuombwa wamshangilie kiba promo ya clouds ili wale pesa toka kwake

Eehh na alivyo na uchu wa pesa now watamla sana tu
 
Sijui why wameunganisha thread ya before na after the show ndio maana jf inaboa mara nyingi

Sasa mnategemea watu watakaa chini wasome yote haya yote wanaficha maovu ya clouds fm.

Boring
 

Mkuu hayo maswali yako mbona magumu hivyo.
 
Ndugu sina Uteam wanamuziki wote wa Tanzania nawakubali , Kiba namkubali kuliko unavyofikiria ila siwezi kukaa kimya eti nitaonekana Team , Team maana yake nini , am too old for this nonsense !

poa dada kila la heri ila kauli zake zinamponza
 

Mi nawapenda hawa vijana wote wawili. Sina tatizo na Kiba kushangiliwa wala Diamond kuzomewa. Nilijibu aliyeniquote/ niliyemquote. Aliyekwambia kama mtu alikupandisha unatakiwa uendelee kuishi kutokana na anavyotaka yeye ni nani?? It's a dog eats dog world, utapoteza muda wako kama mtataka Diamond awanyonye cocks zenu kisa eti mlimsaidia kupanda. Yaonyesha wewe ndo una wivu wa kuku dume.
 
Wana wivu hela ya kuingia kule umewalipia wewe mpaka uwachagulie mtu wa kumshangilia na yupi wa kumzomea kama vipi ungeenda we kumshangilia basi

Punguza hasira. Ukweli unabaki dogo anapiga pesa ndefu na ndio tatizo la watanzania wengi.
 
wadau naomba niulize eti Jay Z amewah kufanya showa Tanzania?iilikuwa mwaka gani?
 
kumbe hiyo ndo moja ya sababu, dah!
 
Pigeni kelele wakat mnaendelea kumsikiliza chibu chibu, natumaini chibu atafocus kwenye mziki na sio kumrudisha tena kwenye ramani kiba! Alishapotea na atapotea tena baada ya fiesta!
 
Wiz Khalifa kama kuna watu wa heshima usisikilize miziki yake. Ila bana, kama ni mwanamziki wa kibongo ndo ana makosa kama hayo Marekani hawampi visa. Sisi tunapokea tu...Ha haaa!.

Kuna haja ya kuchagua wanamuziki wa kuja. Huyu hafai,alikuwa too much matusi na hata akiongea kawaida hasomeki. Nadhani alipiga ganja au unga kabla ya show. Matusi mengi sana. Ila pia kuna mbongo mmoja alitukana 'kumamazao' live.
 
Kama anaubavu aanze life lake, clouds wanazingua

BTW hivi kule uingereza na ujerumani ni clouds pia???
Uk na ujerumani ilikuwa ni mapromota wanamzingua, ila mwisho wa siku yeye kama msanii ndo alionekana mbaya. Ila kiukweli ni mapromota ndo waliharibu, washabiki hawaoni hilo.
 
Mr Blue kafunika vibaya sana jana, naona wabongo wanamkubali sidhani hata kama TI alishangiliwa vile, ila southern accent ya TI nayo iliwachanganya wengi inaelekea hitilafu ya sauti nayo iliua flava.
Kuzomewa kwa Diamond ilikuwa sio ustaarabu kabisa, hata kama kuzomea wangezomea wimbo wa kwanza tuendelee na show ujumbe ungefika, mashabiki wa kibongo wanafiki sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…